Check out the new design

Terjemahan makna Alquran Alkarim - Terjemahan Berbahasa Sawahili - Ali Muhsin Al-Barwani * - Daftar isi terjemahan

XML CSV Excel API
Please review the Terms and Policies

Terjemahan makna Surah: Al-Mujādilah   Ayah:

Al-Mujadilah

قَدۡ سَمِعَ ٱللَّهُ قَوۡلَ ٱلَّتِي تُجَٰدِلُكَ فِي زَوۡجِهَا وَتَشۡتَكِيٓ إِلَى ٱللَّهِ وَٱللَّهُ يَسۡمَعُ تَحَاوُرَكُمَآۚ إِنَّ ٱللَّهَ سَمِيعُۢ بَصِيرٌ
MWENYEZI MUNGU amekwisha sikia usemi wa mwanamke anaye jadiliana nawe juu ya mumewe, na anamshitakia Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu anayasikia majibizano yenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona.
Mwenyezi Mungu amekwisha sikia kauli ya huyo mwanamke anaye kurejea wewe kwa shauri ya mumewe aliye jitenga naye kwa kudai ati anamwona kama mgongo wa mama yake, na akamlalamikia Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu anayasikia hayo maneno mnayo jibizana. Hakika Mwenyezi Mungu anayasikia vyema yote ya kusikiwa, anayaona vyema yote ya kuonekana. Imepokelewa kuwa Sahaba mmoja, aitwaye Aus bin Ass'amit, aliudhika na mkewe aitwaye, Khola bint Tha'labah, akamwambia: "Wewe kwangu mimi kama mgongo wa mama yangu." Na katika siku za Ujahiliya ilikuwa ndio mwanamke kesha harimika kwa mumewe. Mwanamke akenda kumpa khabari Nabii s.a.w., na Mtume akamwambia: "Sijaamrishwa kitu katika kesi yako. Na sioni ila ni kuwa kweli umekwisha harimika kwake." Mwanamke akajadiliana na Mtume s.a.w. na akamrejea tena, na akawa anamshitakia Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kukhofu kufarikiana na mume na kupotea mwanawe. Haukupita muda ila ikateremka Aya hii na tatu zilizo baada yake.
Tafsir berbahasa Arab:
ٱلَّذِينَ يُظَٰهِرُونَ مِنكُم مِّن نِّسَآئِهِم مَّا هُنَّ أُمَّهَٰتِهِمۡۖ إِنۡ أُمَّهَٰتُهُمۡ إِلَّا ٱلَّٰٓـِٔي وَلَدۡنَهُمۡۚ وَإِنَّهُمۡ لَيَقُولُونَ مُنكَرٗا مِّنَ ٱلۡقَوۡلِ وَزُورٗاۚ وَإِنَّ ٱللَّهَ لَعَفُوٌّ غَفُورٞ
Wale miongoni mwenu wanao watenga wake zao, hao si mama zao. Hawakuwa mama zao ila wale walio wazaa. Na hakika hao wanasema neno linalo chusha, na la uwongo. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kughufiria, Mwenye kusamehe.
Enyi Waumini! Hao miongoni mwenu wanao jitenga na wake zao kwa kuwashabihisha katika kuharimikiana nao kuwa ati ni kama mama zao, ni wakosa. Wake zao sio mama zao. Ukitaka haki mama zao ni wale walio wazaa tu. Na hakika wanao watenga wake zao kwa kusema hivyo wanasema kauli inayo chusha, inayo udhi katika murwa mwema, na ni uwongo ulio tokana na haki. Na hakika Mwenyezi Mungu bila ya shaka ni Mkuu wa kusamehe na kughufiria kwa yaliyo kwisha pita kwenu.
Tafsir berbahasa Arab:
وَٱلَّذِينَ يُظَٰهِرُونَ مِن نِّسَآئِهِمۡ ثُمَّ يَعُودُونَ لِمَا قَالُواْ فَتَحۡرِيرُ رَقَبَةٖ مِّن قَبۡلِ أَن يَتَمَآسَّاۚ ذَٰلِكُمۡ تُوعَظُونَ بِهِۦۚ وَٱللَّهُ بِمَا تَعۡمَلُونَ خَبِيرٞ
Na wale wanao jitenga na wake zao, kisha wakarudia katika yale waliyo yasema, basi wamkomboe mtumwa kabla hawajagusana. Mnapewa maonyo kwa hayo. Na Mwenyezi Mungu anayajua yote mnayo yatenda.
Na wale wanao watenga wake zao na kisha wakarejeza kauli yao, wakayaona makosa yao, na wakataka kubaki na wake zao, basi juu yao kumkomboa mtumwa kabla ya kugusana. Hayo aliyo yawajibisha Mwenyezi Mungu, ya kukomboa mtumwa, ni mawaidha kwenu mnawaidhiwa ili msirejee tena katika makosa hayo. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyajua vilivyo myatendayo.
Tafsir berbahasa Arab:
فَمَن لَّمۡ يَجِدۡ فَصِيَامُ شَهۡرَيۡنِ مُتَتَابِعَيۡنِ مِن قَبۡلِ أَن يَتَمَآسَّاۖ فَمَن لَّمۡ يَسۡتَطِعۡ فَإِطۡعَامُ سِتِّينَ مِسۡكِينٗاۚ ذَٰلِكَ لِتُؤۡمِنُواْ بِٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦۚ وَتِلۡكَ حُدُودُ ٱللَّهِۗ وَلِلۡكَٰفِرِينَ عَذَابٌ أَلِيمٌ
Na asiye pata mtumwa kumkomboa, basi na afunge miezi miwili mfululizo kabla hawajagusana. Na asiye weza hayo basi awalishe masikini sitini. Hayo ni hivyo ili mumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na hiyo ndiyo mipaka ya Mwenyezi Mungu. Na kwa makafiri iko adhabu chungu.
Na asiye pata mtumwa wa kumkomboa, basi yampasa afunge miezi miwili mfululizo kabla hawajagusana. Na asiye weza kufunga hivyo basi itampasa awalishe masikini sitini. Tumeyalazimisha hayo ili mpate kumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na mtende kwa mujibu wa Imani hiyo. Na hiyo ndiyo mipaka ya Mwenyezi Mungu, basi msiikiuke. Na makafiri watapata adhabu yenye machungu makali.
Tafsir berbahasa Arab:
إِنَّ ٱلَّذِينَ يُحَآدُّونَ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ كُبِتُواْ كَمَا كُبِتَ ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِمۡۚ وَقَدۡ أَنزَلۡنَآ ءَايَٰتِۭ بَيِّنَٰتٖۚ وَلِلۡكَٰفِرِينَ عَذَابٞ مُّهِينٞ
Hakika wanao pinzana na Mwenyezi Mungu na Mtume wake, watadhalilishwa kama walivyo dhalilishwa wale walio kuwa kabla yao. Na tulikwisha teremsha Ishara zilizo wazi. Na makafiri watapata adhabu ya kufedhehesha.
Hakika wanao mfanyia inda Mwenyezi Mungu na Mtume wake kwa kupingana nao watatupiliwa mbali kama walivyo tupiliwa mbali walio kuwa kabla yao. Na Sisi tumekwisha teremsha dalili zilizo wazi za kuonyesha Haki. Na hao wapinzani watapata adhabu ya kuwafedhehesha mno.
Tafsir berbahasa Arab:
يَوۡمَ يَبۡعَثُهُمُ ٱللَّهُ جَمِيعٗا فَيُنَبِّئُهُم بِمَا عَمِلُوٓاْۚ أَحۡصَىٰهُ ٱللَّهُ وَنَسُوهُۚ وَٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ شَهِيدٌ
Siku atapo wafufua Mwenyezi Mungu, na awaambie yale waliyo yatenda. Mwenyezi Mungu ameyadhibiti, na wao wameyasahau! Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kushuhudia kila kitu.
Siku Mwenyezi Mungu atapo wafufua wote baada ya kwisha kufa kwao, na awape khabari za yale waliyo yatenda. Mwenyezi Mungu amewawekea yote na ameyahifadhi, na wao wameyasahau. Na Mwenyezi Mungu ni Shahidi wa yote na anayajua yote.
Tafsir berbahasa Arab:
 
Terjemahan makna Surah: Al-Mujādilah
Daftar surah Nomor Halaman
 
Terjemahan makna Alquran Alkarim - Terjemahan Berbahasa Sawahili - Ali Muhsin Al-Barwani - Daftar isi terjemahan

Diterjemahkan oleh Ali Muhsin Al-Barwani.

Tutup