Check out the new design

Terjemahan makna Alquran Alkarim - Terjemahan Berbahasa Sawahili - Ali Muhsin Al-Barwani * - Daftar isi terjemahan

XML CSV Excel API
Please review the Terms and Policies

Terjemahan makna Surah: Al-An'ām   Ayah:
ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَلَمۡ يَلۡبِسُوٓاْ إِيمَٰنَهُم بِظُلۡمٍ أُوْلَٰٓئِكَ لَهُمُ ٱلۡأَمۡنُ وَهُم مُّهۡتَدُونَ
Wale ambao wameamini, na hawakuchanganya imani yao na dhulma - hao ndio watakao pata amani na wao ndio walio ongoka. [82]
[82] Wanao muamini Allah, (Mwenyezi Mungu), na wasiichanganyishe imani yao hii na ibada ya yeyote asiye kuwa Yeye - hao tu ndio wenye haki ya kupata utulivu, na ni wao tu ndio walio ongoka kuishika Njia ya Haki na Kheri.
Tafsir berbahasa Arab:
وَتِلۡكَ حُجَّتُنَآ ءَاتَيۡنَٰهَآ إِبۡرَٰهِيمَ عَلَىٰ قَوۡمِهِۦۚ نَرۡفَعُ دَرَجَٰتٖ مَّن نَّشَآءُۗ إِنَّ رَبَّكَ حَكِيمٌ عَلِيمٞ
Na hizo ndizo hoja zetu tulizo mpa Ibrahim kuhojiana na watu wake. Tunamnyanyua kwa vyeo tumtakaye. Hakika Mola Mlezi wako ni Mwenye hikima na Mwenye ujuzi. [83]
[83] Na hiyo hoja kubwa ya Ungu wetu, na Umoja wetu, tulimpa Ibrahim aisimamishe kupambana na watu wake, naye kwa hiyo akatukuka juu yao. Na mtindo wetu kwa waja wetu ni kuwa tunamnyanyua madaraja kwa ujuzi na hikima tumpendaye katika wao. Hakika Mola Mlezi wako, ewe Nabii, ni Mwenye hikima. Huweka kila kitu pahala pake. Ni Mwenye kuwajua wepi wanastahiki kutukuzwa, na wepi hawastahiki.
Tafsir berbahasa Arab:
وَوَهَبۡنَا لَهُۥٓ إِسۡحَٰقَ وَيَعۡقُوبَۚ كُلًّا هَدَيۡنَاۚ وَنُوحًا هَدَيۡنَا مِن قَبۡلُۖ وَمِن ذُرِّيَّتِهِۦ دَاوُۥدَ وَسُلَيۡمَٰنَ وَأَيُّوبَ وَيُوسُفَ وَمُوسَىٰ وَهَٰرُونَۚ وَكَذَٰلِكَ نَجۡزِي ٱلۡمُحۡسِنِينَ
Na tukamtunukia (Ibrahim) Is-haq na Yaakub. Kila mmoja wao tulimwongoa. Na Nuhu tulimwongoa kabla. Na katika kizazi chake tulimwongoa Daud na Suleiman na Ayyub na Yusuf na Musa na Harun. Na hivi ndivyo tunavyo walipa wafanyao wema. [84]
[84] Na Sisi tulimpa Ibrahim, Is-haq na Yaaqub bin Is-haq. Na tukamwezesha kila mmoja wao kufikia Haki na Kheri, kama baba yao. Na kabla yake tulimwezesha Nuhu hivyo hivyo, na tukawaongoa katika wazao wa Nuhu, Daud, na Suleiman, na Ayyub, na Yusuf, na Musa, na Harun. Kama tulivyo walipa hawa, tunawalipa wafanyao wema kwa wanavyo stahiki.
Tafsir berbahasa Arab:
وَزَكَرِيَّا وَيَحۡيَىٰ وَعِيسَىٰ وَإِلۡيَاسَۖ كُلّٞ مِّنَ ٱلصَّٰلِحِينَ
Na Zakaria na Yahya na Isa na Ilyas. Wote walikuwa miongoni mwa watu wema. [85]
[85] Na tuliwaongoa Zakariya, na Yahya, na Isa, na Ilyas - kila mmoja wao katika hawa ni miongoni mwa waja wetu walio wema.
Tafsir berbahasa Arab:
وَإِسۡمَٰعِيلَ وَٱلۡيَسَعَ وَيُونُسَ وَلُوطٗاۚ وَكُلّٗا فَضَّلۡنَا عَلَى ٱلۡعَٰلَمِينَ
Na Ismail, na Al Yasaa, na Yunus, na Lut'. Na wote tuliwafadhilisha juu ya walimwengu wote. [86]
[86] Na tuliwaahidi Ismail, na Alyasaa, na Yunus, na Lut'; na tukawafadhilisha kila mmoja wa hawa wote kushinda walimwengu wote wa zama zao, kwa kuwapa uwongofu na Unabii.
Tafsir berbahasa Arab:
وَمِنۡ ءَابَآئِهِمۡ وَذُرِّيَّٰتِهِمۡ وَإِخۡوَٰنِهِمۡۖ وَٱجۡتَبَيۡنَٰهُمۡ وَهَدَيۡنَٰهُمۡ إِلَىٰ صِرَٰطٖ مُّسۡتَقِيمٖ
Na kutokana na baba zao, na vizazi vyao na ndugu zao. Na tukawateuwa na tukawaongoa kwenye Njia iliyo nyooka. [87]
[87] Na tuliwateuwa baadhi ya mababa wa hao, na dhuriya zao, na ndugu zao, na tukawakhitari wao, na tukawawezesha waifuate Njia isiyo kwenda upogo.
Tafsir berbahasa Arab:
ذَٰلِكَ هُدَى ٱللَّهِ يَهۡدِي بِهِۦ مَن يَشَآءُ مِنۡ عِبَادِهِۦۚ وَلَوۡ أَشۡرَكُواْ لَحَبِطَ عَنۡهُم مَّا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ
Hiyo ni hidaya ya Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo humhidi amtakaye katika waja wake. Na lau wangeli mshirikisha yangeli waharibikia waliyo kuwa wakiyatenda. [88]
[88] Hiyo ndiyo tawfiqi kubwa waliyo ipata watu hawa, nayo ni tawfiqi (uwezesho) iliyo tokana na Mwenyezi Mungu, ambayo humwafiqia (humwezesha) amtakaye katika waja wake. Na lau wangeli shiriki watu hawa walio khitariwa zingeli potea a'mali zao za kheri zote walizo zifanya, na wasingeli pata thawabu.
Tafsir berbahasa Arab:
أُوْلَٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ ءَاتَيۡنَٰهُمُ ٱلۡكِتَٰبَ وَٱلۡحُكۡمَ وَٱلنُّبُوَّةَۚ فَإِن يَكۡفُرۡ بِهَا هَٰٓؤُلَآءِ فَقَدۡ وَكَّلۡنَا بِهَا قَوۡمٗا لَّيۡسُواْ بِهَا بِكَٰفِرِينَ
Hao ndio tulio wapa Vitabu na hukumu na Unabii. Ikiwa hawa watayakataa hayo, basi tumekwisha yawakilisha kwa watu wasio yakataa. [89]
[89] Hao ndio tulio wapa Vitabu vilivyo teremshwa, na ilimu zenye manufaa, na utukufu wa Unabii. Na washirikina wa Makka wakiyapinga mambo haya matatu, basi wamekwisha ahidiwa watu wengine wasiyo yakataa hayo wayachunge na wanafiike kwayo.
Tafsir berbahasa Arab:
أُوْلَٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ هَدَى ٱللَّهُۖ فَبِهُدَىٰهُمُ ٱقۡتَدِهۡۗ قُل لَّآ أَسۡـَٔلُكُمۡ عَلَيۡهِ أَجۡرًاۖ إِنۡ هُوَ إِلَّا ذِكۡرَىٰ لِلۡعَٰلَمِينَ
Hao ndio ambao Mwenyezi Mungu amewahidi. Basi fuata hidaya yao. Sema: Mimi sikuombeni ujira. Haya hayakuwa ila ni mawaidha kwa walimwengu wote. [90]
[90] Hao ndio Mwenyezi Mungu amewawezesha kuishika Njia ya Haki na kheri. Basi nyinyi wafuateni hao katika mambo waliyo wafikiana kwayo, nayo ni mambo ya misingi ya Dini, na misingi ya mwendo mwema, wala msifuate njia nyengine isiyo kuwa yao... Ewe Nabii! Waambie watu wako kama wao hawa walivyo waambia watu wao: Sitaki kwenu ujira kwa ajili ya kulifikisha Neno la Mwenyezi Mungu! Hii Qur'ani si chochote ila ni Ukumbusho kwa walimwengu wote, wala sina lengo mimi ila kuwa nyinyi mnafiike na hii Qur'ani.
Tafsir berbahasa Arab:
 
Terjemahan makna Surah: Al-An'ām
Daftar surah Nomor Halaman
 
Terjemahan makna Alquran Alkarim - Terjemahan Berbahasa Sawahili - Ali Muhsin Al-Barwani - Daftar isi terjemahan

Diterjemahkan oleh Ali Muhsin Al-Barwani.

Tutup