Terjemahan makna Alquran Alkarim - Terjemahan Berbahasa Sawahili - Ali Muhsin Al-Barwani * - Daftar isi terjemahan

XML CSV Excel API
Please review the Terms and Policies

Terjemahan makna Ayah: (139) Surah: Surah Al-An'ām
وَقَالُواْ مَا فِي بُطُونِ هَٰذِهِ ٱلۡأَنۡعَٰمِ خَالِصَةٞ لِّذُكُورِنَا وَمُحَرَّمٌ عَلَىٰٓ أَزۡوَٰجِنَاۖ وَإِن يَكُن مَّيۡتَةٗ فَهُمۡ فِيهِ شُرَكَآءُۚ سَيَجۡزِيهِمۡ وَصۡفَهُمۡۚ إِنَّهُۥ حَكِيمٌ عَلِيمٞ
Na husema: Waliomo matumboni mwa wanyama hawa ni kwa ajili ya wanaume wetu tu, na wameharimishwa kwa wake zetu. Lakini ikiwa nyamafu basi wanashirikiana. Mwenyezi Mungu atawalipa kwa maelezo yao hayo. Hakika Yeye ni Mwenye hikima, Mwenye kujua.
Na katika mawazo yao ya uwongo hawa washirikina ni kuwa wanasema: Viliomo matumboni mwa wanyama walio watenga, walio zuwiwa wasichinjwe wala wasipandwe - viliomo matumboni mwao, yaani watoto, wanafaa kuliwa na wanaume, na haramu kwa wanawake. Na juu ya hivyo akizaliwa naye kesha kufa wote wanashirikiana wanakula! Mwenyezi Mungu Mtukufu atawalipa kwa uwongo wao walio mzulia kwa kitendo chao. Kwani wanadai kuwa kuharimishwa huku kunatokana na Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na hakika Mwenyezi Mungu anajua kila kitu, na ni Mwenye hikima. Vitendo vyake vyote ni kwa mujibu wa hikima. Naye atawalipa wenye dhambi kwa dhambi zao.
Tafsir berbahasa Arab:
 
Terjemahan makna Ayah: (139) Surah: Surah Al-An'ām
Daftar surah Nomor Halaman
 
Terjemahan makna Alquran Alkarim - Terjemahan Berbahasa Sawahili - Ali Muhsin Al-Barwani - Daftar isi terjemahan

Terjemahan Makna Al-Qur`ān Al-Karīm ke Bahasa Sawahili oleh Ali Muhsin Al-Barwani

Tutup