Terjemahan makna Alquran Alkarim - Terjemahan Berbahasa Sawahili - Ali Muhsin Al-Barwani * - Daftar isi terjemahan

XML CSV Excel API
Please review the Terms and Policies

Terjemahan makna Ayah: (158) Surah: Surah Al-An'ām
هَلۡ يَنظُرُونَ إِلَّآ أَن تَأۡتِيَهُمُ ٱلۡمَلَٰٓئِكَةُ أَوۡ يَأۡتِيَ رَبُّكَ أَوۡ يَأۡتِيَ بَعۡضُ ءَايَٰتِ رَبِّكَۗ يَوۡمَ يَأۡتِي بَعۡضُ ءَايَٰتِ رَبِّكَ لَا يَنفَعُ نَفۡسًا إِيمَٰنُهَا لَمۡ تَكُنۡ ءَامَنَتۡ مِن قَبۡلُ أَوۡ كَسَبَتۡ فِيٓ إِيمَٰنِهَا خَيۡرٗاۗ قُلِ ٱنتَظِرُوٓاْ إِنَّا مُنتَظِرُونَ
Wanangoja jengine ila wawafikie Malaika, au awafikie Mola wako Mlezi, au zifike baadhi ya Ishara za Mola wako Mlezi? Siku zitakapo fika baadhi ya Ishara za Mola wako Mlezi, kuamini hapo hakutomfaa mtu kitu, ikiwa hakuwa ameamini kabla yake, au amefanya kheri katika Imani yake. Sema: Ngojeni, nasi pia tunangoja.
Hoja imekwisha simama ya kuwa kuamini ni waajibu. Na watu hawa hawakuamini. Basi wanangojea nini ndio waamini? Je, wanangojea wawajie Malaika wawe ni Mitume badala ya kuwa wanaadamu, au wawe ni mashahidi kushuhudia ukweli wako? Au aje Mwenyewe Mola wako Mlezi, wamwone, au ashuhudie ukweli wako? Au zije baadhi ya alama za Mola wako Mlezi zishuhudie ukweli wako? Na pindi zikija hizo alama za Mola wako Mlezi za kuwapelekea kuamini, basi Imani yao haitowafaa kitu. Kwani hiyo itakuwa ni Imani ya kahari, hawana hila. Na sasa tena haimfalii mwenye kuasi toba yake na ut'iifu wake. Kiwango cha kufanya waajibu kimekwisha pita! Waambie hawa wanao kataa na kukanusha: Ngojeni moja ya mambo hayo matatu, nanyi endeleeni katika kukanusha kwenu. Nasi pia tunangoja hukumu ya Mwenyezi Mungu juu yenu.
Tafsir berbahasa Arab:
 
Terjemahan makna Ayah: (158) Surah: Surah Al-An'ām
Daftar surah Nomor Halaman
 
Terjemahan makna Alquran Alkarim - Terjemahan Berbahasa Sawahili - Ali Muhsin Al-Barwani - Daftar isi terjemahan

Terjemahan Makna Al-Qur`ān Al-Karīm ke Bahasa Sawahili oleh Ali Muhsin Al-Barwani

Tutup