Terjemahan makna Alquran Alkarim - Terjemahan Berbahasa Sawahili - Ali Muhsin Al-Barwani * - Daftar isi terjemahan

XML CSV Excel API
Please review the Terms and Policies

Terjemahan makna Ayah: (94) Surah: Surah Al-An'ām
وَلَقَدۡ جِئۡتُمُونَا فُرَٰدَىٰ كَمَا خَلَقۡنَٰكُمۡ أَوَّلَ مَرَّةٖ وَتَرَكۡتُم مَّا خَوَّلۡنَٰكُمۡ وَرَآءَ ظُهُورِكُمۡۖ وَمَا نَرَىٰ مَعَكُمۡ شُفَعَآءَكُمُ ٱلَّذِينَ زَعَمۡتُمۡ أَنَّهُمۡ فِيكُمۡ شُرَكَٰٓؤُاْۚ لَقَد تَّقَطَّعَ بَيۡنَكُمۡ وَضَلَّ عَنكُم مَّا كُنتُمۡ تَزۡعُمُونَ
Nanyi mlitujia wapweke kama tulivyo kuumbeni mara ya kwanza. Na mkayaacha nyuma yenu yote tuliyo kupeni, na wala hatuwaoni hao waombezi wenu, ambao mlidai kuwa ni washirika wa Mwenyezi Mungu kwenu. Yamekatika makhusiano baina yenu, na yamekupoteeni mliyo kuwa mkidai.
Na Mwenyezi Mungu atawaambia Siku ya Kiyama: Sasa bila ya shaka mmekwisha yakinisha kwa nafsi zenu kuwa kweli mmefufuliwa kutoka makaburini kwenu, kama tulivyo kuumbeni mara ya kwanza. Na mmetujia hali ni wapweke, hamna mali, wala watoto, wala marafiki. Na mmeviacha nyuma yenu vyote tulivyo kupeni na mkaghurika navyo. Na wala Sisi hatuwaoni pamoja nanyi hao waombezi ambao mlidai kuwa watakunusuruni kwa Mwenyezi Mungu, na kuwa wao ati ni washirika wa Mwenyezi Mungu katika ibada! Makhusiano yote baina yenu na wao yamekwisha katika, na yamekupoteeni mliyo kuwa mkidai kuwa yatakufaeni.
Tafsir berbahasa Arab:
 
Terjemahan makna Ayah: (94) Surah: Surah Al-An'ām
Daftar surah Nomor Halaman
 
Terjemahan makna Alquran Alkarim - Terjemahan Berbahasa Sawahili - Ali Muhsin Al-Barwani - Daftar isi terjemahan

Terjemahan Makna Al-Qur`ān Al-Karīm ke Bahasa Sawahili oleh Ali Muhsin Al-Barwani

Tutup