Check out the new design

Terjemahan makna Alquran Alkarim - Terjemahan Berbahasa Sawahili - Pusat Terjemah Ruwwād * - Daftar isi terjemahan


Terjemahan makna Surah: Al-Baqarah   Ayah:
ٱلَّذِينَ ءَاتَيۡنَٰهُمُ ٱلۡكِتَٰبَ يَعۡرِفُونَهُۥ كَمَا يَعۡرِفُونَ أَبۡنَآءَهُمۡۖ وَإِنَّ فَرِيقٗا مِّنۡهُمۡ لَيَكۡتُمُونَ ٱلۡحَقَّ وَهُمۡ يَعۡلَمُونَ
Wale tuliowapa Kitabu, wanayajua haya kama wanavyowajua watoto wao. Na kuna kikundi katika wao huificha haki na hali wanajua.[1]
[1] Wao kwa hakika walikuwa wanajua katika sifa zake kabla ya kumuona, ambazo ziliingiliana na yeye mwenyewe walipomuona. (Tafsir Ibn Al-Qayyim)
Tafsir berbahasa Arab:
ٱلۡحَقُّ مِن رَّبِّكَ فَلَا تَكُونَنَّ مِنَ ٱلۡمُمۡتَرِينَ
Haki inatoka kwa Mola wako Mlezi. Basi usiwe kabisa miongoni mwa wenye shaka.
Tafsir berbahasa Arab:
وَلِكُلّٖ وِجۡهَةٌ هُوَ مُوَلِّيهَاۖ فَٱسۡتَبِقُواْ ٱلۡخَيۡرَٰتِۚ أَيۡنَ مَا تَكُونُواْ يَأۡتِ بِكُمُ ٱللَّهُ جَمِيعًاۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٞ
Na kila mmoja anao mwelekeo anaoelekea. Basi shindanieni mema. Popote mlipo, Mwenyezi Mungu atawaleta nyote pamoja. Hakika, Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu.
Tafsir berbahasa Arab:
وَمِنۡ حَيۡثُ خَرَجۡتَ فَوَلِّ وَجۡهَكَ شَطۡرَ ٱلۡمَسۡجِدِ ٱلۡحَرَامِۖ وَإِنَّهُۥ لَلۡحَقُّ مِن رَّبِّكَۗ وَمَا ٱللَّهُ بِغَٰفِلٍ عَمَّا تَعۡمَلُونَ
Na kokote uendako, uelekeze uso wako kwenye Msikiti Mtakatifu. Na hiyo kwa hakika ndiyo haki itokayo kwa Mola wako Mlezi. Na Mwenyezi Mungu si mwenye kughafilika na mnayoyatenda.
Tafsir berbahasa Arab:
وَمِنۡ حَيۡثُ خَرَجۡتَ فَوَلِّ وَجۡهَكَ شَطۡرَ ٱلۡمَسۡجِدِ ٱلۡحَرَامِۚ وَحَيۡثُ مَا كُنتُمۡ فَوَلُّواْ وُجُوهَكُمۡ شَطۡرَهُۥ لِئَلَّا يَكُونَ لِلنَّاسِ عَلَيۡكُمۡ حُجَّةٌ إِلَّا ٱلَّذِينَ ظَلَمُواْ مِنۡهُمۡ فَلَا تَخۡشَوۡهُمۡ وَٱخۡشَوۡنِي وَلِأُتِمَّ نِعۡمَتِي عَلَيۡكُمۡ وَلَعَلَّكُمۡ تَهۡتَدُونَ
Na kokote uendako, uelekeza uso wako kwenye Msikiti Mtakatifu. Na popote mlipo, zielekezeni nyuso zenu upande wake, ili watu wasiwe na hoja juu yenu; isipokuwa wale waliodhulumu miongoni mwao. Basi, msiwaogope wao, lakini niogopeni Mimi. Na ili niwatimizie neema yangu, na ili mpate kuongoka
Tafsir berbahasa Arab:
كَمَآ أَرۡسَلۡنَا فِيكُمۡ رَسُولٗا مِّنكُمۡ يَتۡلُواْ عَلَيۡكُمۡ ءَايَٰتِنَا وَيُزَكِّيكُمۡ وَيُعَلِّمُكُمُ ٱلۡكِتَٰبَ وَٱلۡحِكۡمَةَ وَيُعَلِّمُكُم مَّا لَمۡ تَكُونُواْ تَعۡلَمُونَ
Kama tulivyomtuma Mtume kwenu anayetokana na nyinyi, anawasomea Aya zetu na kuwatakasa na kuwafundisha Kitabu na hekima, na anawafundisha ambayo hamkuwa mnayajua.
Tafsir berbahasa Arab:
فَٱذۡكُرُونِيٓ أَذۡكُرۡكُمۡ وَٱشۡكُرُواْ لِي وَلَا تَكۡفُرُونِ
Basi nikumbukeni, nitawakumbuka. Na nishukuruni, wala msinikufuru.
Tafsir berbahasa Arab:
يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ ٱسۡتَعِينُواْ بِٱلصَّبۡرِ وَٱلصَّلَوٰةِۚ إِنَّ ٱللَّهَ مَعَ ٱلصَّٰبِرِينَ
Enyi mlioamini! Takeni msaada kwa subira na Swala. Hakika, Mwenyezi Mungu yu pamoja na wanaosubiri.
Tafsir berbahasa Arab:
 
Terjemahan makna Surah: Al-Baqarah
Daftar surah Nomor Halaman
 
Terjemahan makna Alquran Alkarim - Terjemahan Berbahasa Sawahili - Pusat Terjemah Ruwwād - Daftar isi terjemahan

Terjemahannya oleh Tim Markaz Ruwwād Terjemah bekerjasama dengan Perkumpulan Dakwah di Rabwah dan Perkumpulan Pelayanan Konten Islami dalam Bahasa.

Tutup