Check out the new design

Terjemahan makna Alquran Alkarim - Terjemahan Berbahasa Sawahili - Pusat Terjemah Ruwwād * - Daftar isi terjemahan


Terjemahan makna Surah: Āli 'Imrān   Ayah:

Al-'Imran

الٓمٓ
Alif Laam Miim.
Tafsir berbahasa Arab:
ٱللَّهُ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ ٱلۡحَيُّ ٱلۡقَيُّومُ
Mwenyezi Mungu, hakuna mungu isipokuwa Yeye. Aliye hai, Msimamizi wa yote milele.
Tafsir berbahasa Arab:
نَزَّلَ عَلَيۡكَ ٱلۡكِتَٰبَ بِٱلۡحَقِّ مُصَدِّقٗا لِّمَا بَيۡنَ يَدَيۡهِ وَأَنزَلَ ٱلتَّوۡرَىٰةَ وَٱلۡإِنجِيلَ
Amekiteremsha Kitabu juu yako kwa haki, kinachosadikisha yaliyokuwa kabla yake. Na aliteremsha Taurati na Injili.
Tafsir berbahasa Arab:
مِن قَبۡلُ هُدٗى لِّلنَّاسِ وَأَنزَلَ ٱلۡفُرۡقَانَۗ إِنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ بِـَٔايَٰتِ ٱللَّهِ لَهُمۡ عَذَابٞ شَدِيدٞۗ وَٱللَّهُ عَزِيزٞ ذُو ٱنتِقَامٍ
Kabla yake, viwe uwongofu kwa watu. Na akateremsha Furqani (Upambanuo). Hakika, wale waliozikufuru Ishara za Mwenyezi Mungu wana adhabu kali. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, na Mwenye kulipiza.
Tafsir berbahasa Arab:
إِنَّ ٱللَّهَ لَا يَخۡفَىٰ عَلَيۡهِ شَيۡءٞ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَلَا فِي ٱلسَّمَآءِ
Hakika, Mwenyezi Mungu hakifichiki chochote kwake, katika dunia wala katika mbingu.
Tafsir berbahasa Arab:
هُوَ ٱلَّذِي يُصَوِّرُكُمۡ فِي ٱلۡأَرۡحَامِ كَيۡفَ يَشَآءُۚ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡحَكِيمُ
Yeye ndiye anayewaunda ndani ya matumbo ya uzazi kwa namna apendavyo. Hapana mungu isipokuwa Yeye, Mwenye nguvu, Mwenye hekima.
Tafsir berbahasa Arab:
هُوَ ٱلَّذِيٓ أَنزَلَ عَلَيۡكَ ٱلۡكِتَٰبَ مِنۡهُ ءَايَٰتٞ مُّحۡكَمَٰتٌ هُنَّ أُمُّ ٱلۡكِتَٰبِ وَأُخَرُ مُتَشَٰبِهَٰتٞۖ فَأَمَّا ٱلَّذِينَ فِي قُلُوبِهِمۡ زَيۡغٞ فَيَتَّبِعُونَ مَا تَشَٰبَهَ مِنۡهُ ٱبۡتِغَآءَ ٱلۡفِتۡنَةِ وَٱبۡتِغَآءَ تَأۡوِيلِهِۦۖ وَمَا يَعۡلَمُ تَأۡوِيلَهُۥٓ إِلَّا ٱللَّهُۗ وَٱلرَّٰسِخُونَ فِي ٱلۡعِلۡمِ يَقُولُونَ ءَامَنَّا بِهِۦ كُلّٞ مِّنۡ عِندِ رَبِّنَاۗ وَمَا يَذَّكَّرُ إِلَّآ أُوْلُواْ ٱلۡأَلۡبَٰبِ
eye ndiye aliyeteremsha juu yako Kitabu hiki. Ndani yake zimo Aya muhkam (zenye maana wazi). Hizo ndizo msingi wa Kitabu hiki. Na zimo nyingine Mutashabihat (zenye maana zisizo wazi). Ama wale ambao katika nyoyo zao umo upotovu, wao wanafuata zile zenye maana zisizo wazi kwa kutafuta fitina, na kutafuta maana yake. Na wala hapana ajuaye maana yake isipokuwa Mwenyezi Mungu. Na wale waliokita katika elimu husema: Sisi tumeziamini, zote zimetoka kwa Mola wetu Mlezi. Lakini hawakumbuki (hayo) isipokuwa wenye akili.
Tafsir berbahasa Arab:
رَبَّنَا لَا تُزِغۡ قُلُوبَنَا بَعۡدَ إِذۡ هَدَيۡتَنَا وَهَبۡ لَنَا مِن لَّدُنكَ رَحۡمَةًۚ إِنَّكَ أَنتَ ٱلۡوَهَّابُ
(Na wao husema) Mola wetu Mlezi! Usizipotoe nyoyo zetu baada ya kutuongoa, na tutunuku rehema itokayo kwako. Hakika, Wewe ndiye Mwenye kutunuku.
Tafsir berbahasa Arab:
رَبَّنَآ إِنَّكَ جَامِعُ ٱلنَّاسِ لِيَوۡمٖ لَّا رَيۡبَ فِيهِۚ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يُخۡلِفُ ٱلۡمِيعَادَ
Mola wetu Mlezi! Hakika, Wewe ndiye utakayewakusanya watu kwa Siku isiyo na shaka ndani yake. Hakika, Mwenyezi Mungu havunji miadi yake.
Tafsir berbahasa Arab:
 
Terjemahan makna Surah: Āli 'Imrān
Daftar surah Nomor Halaman
 
Terjemahan makna Alquran Alkarim - Terjemahan Berbahasa Sawahili - Pusat Terjemah Ruwwād - Daftar isi terjemahan

Terjemahannya oleh Tim Markaz Ruwwād Terjemah bekerjasama dengan Perkumpulan Dakwah di Rabwah dan Perkumpulan Pelayanan Konten Islami dalam Bahasa.

Tutup