Check out the new design

Terjemahan makna Alquran Alkarim - Terjemahan Berbahasa Sawahili - Pusat Terjemah Ruwwād * - Daftar isi terjemahan


Terjemahan makna Surah: Al-An'ām   Ayah:
وَمَا عَلَى ٱلَّذِينَ يَتَّقُونَ مِنۡ حِسَابِهِم مِّن شَيۡءٖ وَلَٰكِن ذِكۡرَىٰ لَعَلَّهُمۡ يَتَّقُونَ
Wala hakuna jukumu lolote kwa wale wamchao Mungu, lakini ni kukumbusha tu, asaa wapate kumcha Mwenyezi Mungu.
Tafsir berbahasa Arab:
وَذَرِ ٱلَّذِينَ ٱتَّخَذُواْ دِينَهُمۡ لَعِبٗا وَلَهۡوٗا وَغَرَّتۡهُمُ ٱلۡحَيَوٰةُ ٱلدُّنۡيَاۚ وَذَكِّرۡ بِهِۦٓ أَن تُبۡسَلَ نَفۡسُۢ بِمَا كَسَبَتۡ لَيۡسَ لَهَا مِن دُونِ ٱللَّهِ وَلِيّٞ وَلَا شَفِيعٞ وَإِن تَعۡدِلۡ كُلَّ عَدۡلٖ لَّا يُؤۡخَذۡ مِنۡهَآۗ أُوْلَٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ أُبۡسِلُواْ بِمَا كَسَبُواْۖ لَهُمۡ شَرَابٞ مِّنۡ حَمِيمٖ وَعَذَابٌ أَلِيمُۢ بِمَا كَانُواْ يَكۡفُرُونَ
Waachilie mbali walioifanya dini yao ni mchezo na pumbao, na uhai wa dunia ukawadanganya. Nawe kumbusha kwayo, isije nafsi ikaangamizwa kwa sababu ya iliyoyachuma, nayo haina mlinzi wala mwombezi ila Mwenyezi Mungu. Na ingetoa kila fidia, haitokubaliwa. Hao ndio walioangamizwa kwa sababu ya yale waliyoyachuma. Wao watapata kinywaji cha maji ya moto kabisa, na adhabu chungu.
Tafsir berbahasa Arab:
قُلۡ أَنَدۡعُواْ مِن دُونِ ٱللَّهِ مَا لَا يَنفَعُنَا وَلَا يَضُرُّنَا وَنُرَدُّ عَلَىٰٓ أَعۡقَابِنَا بَعۡدَ إِذۡ هَدَىٰنَا ٱللَّهُ كَٱلَّذِي ٱسۡتَهۡوَتۡهُ ٱلشَّيَٰطِينُ فِي ٱلۡأَرۡضِ حَيۡرَانَ لَهُۥٓ أَصۡحَٰبٞ يَدۡعُونَهُۥٓ إِلَى ٱلۡهُدَى ٱئۡتِنَاۗ قُلۡ إِنَّ هُدَى ٱللَّهِ هُوَ ٱلۡهُدَىٰۖ وَأُمِرۡنَا لِنُسۡلِمَ لِرَبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ
Sema: Je, tumuombe asiyekuwa Mwenyezi Mungu ambaye hatufai wala hatudhuru, na turejee nyuma baada ya Mwenyezi Mungu kwisha tuongoa? Tuwe kama ambao mashetani wamempumbaza katika ardhi, amechanganyikiwa? Anao marafiki wanaomwita aende kwenye uwongofu, wakimwambia: 'Njoo kwetu!' Sema: Hakika uongofu wa Mwenyezi Mungu ndio Uongofu. Nasi tumeamrishwa tusilimu kwa Mola Mlezi wa viumbe vyote.
Tafsir berbahasa Arab:
وَأَنۡ أَقِيمُواْ ٱلصَّلَوٰةَ وَٱتَّقُوهُۚ وَهُوَ ٱلَّذِيٓ إِلَيۡهِ تُحۡشَرُونَ
Na mshike Sala, na mcheni Yeye, na kwake Yeye ndiko mtakakokusanywa
Tafsir berbahasa Arab:
وَهُوَ ٱلَّذِي خَلَقَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ بِٱلۡحَقِّۖ وَيَوۡمَ يَقُولُ كُن فَيَكُونُۚ قَوۡلُهُ ٱلۡحَقُّۚ وَلَهُ ٱلۡمُلۡكُ يَوۡمَ يُنفَخُ فِي ٱلصُّورِۚ عَٰلِمُ ٱلۡغَيۡبِ وَٱلشَّهَٰدَةِۚ وَهُوَ ٱلۡحَكِيمُ ٱلۡخَبِيرُ
Naye ndiye aliyeziumba mbingu na ardhi kwa Haki. Siku atakaposema: "Kuwa!" Na yawe. Kauli yake ni Haki. Na ufalme wote ni wake Siku litakapopulizwa barugumu, Mjuzi wa yaliyofichikana na yanayoonekana. Naye ndiye Mwenye hekima, Mwenye habari zote.
Tafsir berbahasa Arab:
 
Terjemahan makna Surah: Al-An'ām
Daftar surah Nomor Halaman
 
Terjemahan makna Alquran Alkarim - Terjemahan Berbahasa Sawahili - Pusat Terjemah Ruwwād - Daftar isi terjemahan

Terjemahannya oleh Tim Markaz Ruwwād Terjemah bekerjasama dengan Perkumpulan Dakwah di Rabwah dan Perkumpulan Pelayanan Konten Islami dalam Bahasa.

Tutup