Check out the new design

Traduzione dei Significati del Sacro Corano - Traduzione swahili - Ali Muhsin Albirwany * - Indice Traduzioni

XML CSV Excel API
Please review the Terms and Policies

Traduzione dei significati Sura: Al-Hijr   Versetto:
قَالَ هَٰٓؤُلَآءِ بَنَاتِيٓ إِن كُنتُمۡ فَٰعِلِينَ
Akasema: Hawa binti zangu, ikiwa nyinyi ni watendaji. [71]
[71] Ili kuwanabihisha njia ya maumbile ya kisharia, Nabii wa Mwenyezi Mungu Luut'i akasema: Hawa mabinti wa mji huu, nao ni binti zangu, waoeni ikiwa mnataka kukidhi matamanio yenu.
Esegesi in lingua araba:
لَعَمۡرُكَ إِنَّهُمۡ لَفِي سَكۡرَتِهِمۡ يَعۡمَهُونَ
Naapa kwa umri wako! Hakika hao walikuwa katika ulevi wao, wakihangaika ovyo. [72]
[72] Ewe Nabii Muaminifu! Naapa kwa haki ya uhai wako! Hawa wamo katika mghafala, hawajui yatakayo wateremkia. Wamekuwa kama walio lewa! Hakika wao wamo katika upotovu, wanatapatapa, hawajui wapite wapi.
Esegesi in lingua araba:
فَأَخَذَتۡهُمُ ٱلصَّيۡحَةُ مُشۡرِقِينَ
Ukelele ukawatwaa wakipambaukiwa. [73]
[73] Na walipo kuwa wao wamo katika ulevi wao wa mghafala nyoyo zao na akili zao zikachotwa na ukelele mkali mno wa kutisha, wakati jua lilipo chomoza.
Esegesi in lingua araba:
فَجَعَلۡنَا عَٰلِيَهَا سَافِلَهَا وَأَمۡطَرۡنَا عَلَيۡهِمۡ حِجَارَةٗ مِّن سِجِّيلٍ
Na tukaigeuza nchi juu chini, na tukawanyeshea mvua ya mawe ya udongo wa Motoni. [74]
[74] Mwenyezi Mungu Aliye takasika katekeleza hukumu yake, akasema: Miji yao tukaifanya juu chini kwa kuivuruga, na tukawateremshia udongo ulio fanyika mawe ukiwateremkia kama mvua. Majumba yao yakaporomoka. Na wakitoka nje hukuta hiyo mvua ya mawe. Kwa hivyo wakawa wamezungukwa kila jiha. (upande)
Esegesi in lingua araba:
إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَٰتٖ لِّلۡمُتَوَسِّمِينَ
Hakika katika hayo zipo ishara kwa waaguzi. [75]
[75] Haya yaliyo washukia kaumu Luut'i ni alama wazi ya kuonyesha vipi Mwenyezi Mungu Mtukufu anavyo timiza ahadi yake. Wajuao mambo wanayatambua hayo, na wanayaelewa matokeo yake kwa alama zake, kwani kila kitendo chenye sifa ya ukosefu kina alama yake isiyo potea. Matokeo yake ni mfano wa haya, duniani na Akhera.
Esegesi in lingua araba:
وَإِنَّهَا لَبِسَبِيلٖ مُّقِيمٍ
Na miji hii ipo kwenye njia inayo pitiwa. [76]
[76] Na mabaki ya mji huu yapo yamesalia. Nayo yapo njiani katika njia inayo pitiwa na watu. Anaye taka kuwaidhika kwayo anaweza kuwaidhika.
Esegesi in lingua araba:
إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَةٗ لِّلۡمُؤۡمِنِينَ
Hakika katika hayo ipo ishara kwa Waumini. [77]
[77] Kwa kuwa mabaki yake yapo kwenye njia iliyo wazi ni dalili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kutimiza onyo lake, na Waumini wenye kut'ii Haki wanatambua hayo.
Esegesi in lingua araba:
وَإِن كَانَ أَصۡحَٰبُ ٱلۡأَيۡكَةِ لَظَٰلِمِينَ
Na Hakika watu wa kichakani, walikuwa wenye kudhulumu [78]
[78] Kama kaumu ya Luut'i walivyo kadhibisha, kadhaalika wakaazi wa Kichakani kwenye msitu wenye matunda walimkanya Mtume wao. Wakawa madhaalimu wenye kudhulumu mno katika imani yao na maingiliano yao.
Esegesi in lingua araba:
فَٱنتَقَمۡنَا مِنۡهُمۡ وَإِنَّهُمَا لَبِإِمَامٖ مُّبِينٖ
Kwa hivyo tukawaadhibu. Na nchi mbili hizi ziko kwenye njia iliowazi. [79]
[79] Tukawateremshia nakama yetu. Na mabaki yao yapo njiani yanaonekana, na mpita njia akiwa ni mtu wa Imani basi anaweza kuzingatia kwayo.
Esegesi in lingua araba:
وَلَقَدۡ كَذَّبَ أَصۡحَٰبُ ٱلۡحِجۡرِ ٱلۡمُرۡسَلِينَ
Na bila ya shaka wakaazi wa Hijr waliwakanusha Mitume. [80]
[80] Na kama walio tangulia hali kadhaalika wakaazi wa Hijr walimkanusha Mtume wao aliye tumwa kwao, na kwa hivyo wakawa wamewakanusha Mitume wote. Kwani ujumbe wa Mwenyezi Mungu ni mmoja. Watu wa Hijr ndio Thamud. Na Hijr ni bonde baina ya Madina na Sham. Tazama maelezo juu ya Aya 73 ya Surat Al-Aa'raaf.
Esegesi in lingua araba:
وَءَاتَيۡنَٰهُمۡ ءَايَٰتِنَا فَكَانُواْ عَنۡهَا مُعۡرِضِينَ
Na tuliwapa ishara zetu, nao wakazipuuza. [81]
[81] Tuliwabainishia hoja zenye kuonyesha uwezo wetu, na Utume wa Mtume wetu, nao wakayapuuza, wala wasiyafikiri.
Esegesi in lingua araba:
وَكَانُواْ يَنۡحِتُونَ مِنَ ٱلۡجِبَالِ بُيُوتًا ءَامِنِينَ
Nao walikuwa wakichonga majumba katika milima kwa amani. [82]
[82] Nao walikuwa watu wenye nguvu na wajenzi. Walikuwa wakijenga majumba yao katika milima na wakiichonga hiyo hiyo milima. Na wao walikuwa wakijiamini kuwa wametua na nafsi zao na mali yao.
Esegesi in lingua araba:
فَأَخَذَتۡهُمُ ٱلصَّيۡحَةُ مُصۡبِحِينَ
Basi ukelele ukawatwaa asubuhi. [83]
[83] Walipo kufuru na wakakanya, zikawajia sauti za kutisha, za kuonya kuteketea kwao, wakahiliki wakati wa asubuhi.
Esegesi in lingua araba:
فَمَآ أَغۡنَىٰ عَنۡهُم مَّا كَانُواْ يَكۡسِبُونَ
Hayakuwafaa waliyo kuwa wakiyachuma. [84]
[84] Wala mali waliyo yachuma na majumba waliyo yajenga hayakuwalinda na hilaki iliyo wateremkia.
Esegesi in lingua araba:
وَمَا خَلَقۡنَا ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ وَمَا بَيۡنَهُمَآ إِلَّا بِٱلۡحَقِّۗ وَإِنَّ ٱلسَّاعَةَ لَأٓتِيَةٞۖ فَٱصۡفَحِ ٱلصَّفۡحَ ٱلۡجَمِيلَ
Na hatukuziumba mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake ila kwa ajili ya Haki. Na hakika Kiyama kitafika. Basi samehe msamaha mzuri. [85]
[85] Hatukuumba mbingu na ardhi na vilivyo kati yao katika anga, na viliomo ndani yake, watu na wanyama, na mimea na visio na uhai, na vinginevyo ambavyo mwanaadamu havijui, isipo kuwa kwa uadilifu, na hikima, na maslaha ambayo hayaambatani na fisadi ya kudumu isiyo na mwisho. Na kwa hivyo basi ni lazima siku ya kukomesha shari ifike bila ya shaka yoyote. Basi ewe Nabii Mtukufu! Wasamehe hao washirikina adhabu ya duniani, na ingiana nao kwa kuwastahamilia maudhi yao. Na kuwaita wito kwa hikima ni kuingiliana kwa usamehevu na upole.
Esegesi in lingua araba:
إِنَّ رَبَّكَ هُوَ ٱلۡخَلَّٰقُ ٱلۡعَلِيمُ
Hakika Mola wako Mlezi ndiye Muumbaji Mjuzi. [86]
[86] Ewe Nabii! Mwenyezi Mungu aliye kuumba na akakulea, ni Mwenye viumbe vyote, na anajua hali yako na yao. Yeye anastahiki umtegemezee mambo yako na yao. Naye anajua maslaha yako na yao.
Esegesi in lingua araba:
وَلَقَدۡ ءَاتَيۡنَٰكَ سَبۡعٗا مِّنَ ٱلۡمَثَانِي وَٱلۡقُرۡءَانَ ٱلۡعَظِيمَ
Na tumekupa Aya saba zinazo somwa mara kwa mara, na Qur'ani Tukufu. [87]
[87] Ewe Nabii Muaminifu, tumekupa Aya saba za Qur'ani, nazo ni Sura ya Al- Fatiha unayo ikariri katika kila Swala, na humo yamo ya kutunyenyekea na maombi ya uwongofu yaliyo kaamili. Na tumekupa Qur'ani Tukufu yote. Na ndani yake mna hoja, na miujiza. Kwa hivyo wewe una nguvu ambazo zinakufalia usamehe.
Esegesi in lingua araba:
لَا تَمُدَّنَّ عَيۡنَيۡكَ إِلَىٰ مَا مَتَّعۡنَا بِهِۦٓ أَزۡوَٰجٗا مِّنۡهُمۡ وَلَا تَحۡزَنۡ عَلَيۡهِمۡ وَٱخۡفِضۡ جَنَاحَكَ لِلۡمُؤۡمِنِينَ
Usivitumbulie macho yako vitu tulivyo waneemesha makundi fulani kati yao, wala usiwahuzunikie. Na wainamishie bawa lako (la huruma) Waumini. [88]
[88] Ewe Mtume! Usivitazame kwa kuvitamani na kuvitaka vitu vya starehe ya dunia tulivyo wapa makafiri wa kishirikina, na Kiyahudi, na Kikristo, na Kimajusi. Kwani hivyo ni duni kwa kulinganisha na ulio pewa wewe katika kuwasiliana nasi, na Qur'ani Tukufu. Wala usiwasikitikie kwa sababu ya kuendelea kwao na madhambi. Nawe tulia, na unyenyekee, na wachukue Waumini ulio nao kwa upole. Kwani hao ni nguvu za Haki, na watu wa Mwenyezi Mungu.
Esegesi in lingua araba:
وَقُلۡ إِنِّيٓ أَنَا ٱلنَّذِيرُ ٱلۡمُبِينُ
Na sema: Hakika mimi ni mwonyaji mwenye kubainisha. [89]
[89] Ewe Nabii! Waambie makafiri wote: Mimi nakuonyeni na adhabu kali, na nakubainishieni maonyo yangu kwa hoja za kukata.
Esegesi in lingua araba:
كَمَآ أَنزَلۡنَا عَلَى ٱلۡمُقۡتَسِمِينَ
Kama hivyo tuliwateremshia walio gawa, [90]
[90] Haya ni kama maonyo ya walio igawanya Qur'ani wakaifanya ati ni mashairi, na ukohani, na hadithi za kale na mengineyo. Nao wasiiamini juu ya kusimama hoja juu yao.
Esegesi in lingua araba:
 
Traduzione dei significati Sura: Al-Hijr
Indice delle Sure Numero di pagina
 
Traduzione dei Significati del Sacro Corano - Traduzione swahili - Ali Muhsin Albirwany - Indice Traduzioni

La sua traduzione di Ali Muhsin Albirwany.

Chiudi