ការបកប្រែអត្ថន័យគួរអាន - ការបកប្រែជាភាសាស្វាហុីលី - មជ្ឈមណ្ឌលបកប្រែរ៉ូវ៉ាដ

លេខ​ទំព័រ:close

external-link copy
65 : 19

رَّبُّ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَمَا بَيۡنَهُمَا فَٱعۡبُدۡهُ وَٱصۡطَبِرۡ لِعِبَٰدَتِهِۦۚ هَلۡ تَعۡلَمُ لَهُۥ سَمِيّٗا

Mola Mlezi wa mbingu na ardhi na vilivyo baina yake. Basi muabudu Yeye tu, na usubiri katika kumuabudu. Je, unajua chochote kilicho sawa naye? info
التفاسير:

external-link copy
66 : 19

وَيَقُولُ ٱلۡإِنسَٰنُ أَءِذَا مَا مِتُّ لَسَوۡفَ أُخۡرَجُ حَيًّا

Na mwanadamu husema: Hivyo, nitakapokufa, ni kweli nitafufuliwa niwe hai tena? info
التفاسير:

external-link copy
67 : 19

أَوَلَا يَذۡكُرُ ٱلۡإِنسَٰنُ أَنَّا خَلَقۡنَٰهُ مِن قَبۡلُ وَلَمۡ يَكُ شَيۡـٔٗا

Je, hakumbuki mwanadamu ya kwamba hakika tulimuumba kabla, na wala hakuwa chochote? info
التفاسير:

external-link copy
68 : 19

فَوَرَبِّكَ لَنَحۡشُرَنَّهُمۡ وَٱلشَّيَٰطِينَ ثُمَّ لَنُحۡضِرَنَّهُمۡ حَوۡلَ جَهَنَّمَ جِثِيّٗا

Basi ninaapa kwa Mola wako Mlezi! Kwa yakini tutawakusanya wao pamoja na mashetani. Kisha tutawahudhurisha kuizunguka Jahannamu huku wamepiga magoti! info
التفاسير:

external-link copy
69 : 19

ثُمَّ لَنَنزِعَنَّ مِن كُلِّ شِيعَةٍ أَيُّهُمۡ أَشَدُّ عَلَى ٱلرَّحۡمَٰنِ عِتِيّٗا

Kisha kwa yakini tutaondoa katika kila kundi wale miongoni mwao waliozidi kumuasi Arrahmani (Mwingi wa rehema). info
التفاسير:

external-link copy
70 : 19

ثُمَّ لَنَحۡنُ أَعۡلَمُ بِٱلَّذِينَ هُمۡ أَوۡلَىٰ بِهَا صِلِيّٗا

Tena hakika Sisi tunawajua vyema zaidi wanaostahiki kuunguzwa humo. info
التفاسير:

external-link copy
71 : 19

وَإِن مِّنكُمۡ إِلَّا وَارِدُهَاۚ كَانَ عَلَىٰ رَبِّكَ حَتۡمٗا مَّقۡضِيّٗا

Wala hakuna yeyote katika nyinyi isipokuwa ataifikia. Hiyo ni hukumu ya Mola wako Mlezi ambayo lazima itimizwe. info
التفاسير:

external-link copy
72 : 19

ثُمَّ نُنَجِّي ٱلَّذِينَ ٱتَّقَواْ وَّنَذَرُ ٱلظَّٰلِمِينَ فِيهَا جِثِيّٗا

Kisha tutawaokoa sawasawa wale waliomcha Mungu; na tutawaacha madhalimu humo huku wamepiga magoti. info
التفاسير:

external-link copy
73 : 19

وَإِذَا تُتۡلَىٰ عَلَيۡهِمۡ ءَايَٰتُنَا بَيِّنَٰتٖ قَالَ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ لِلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ أَيُّ ٱلۡفَرِيقَيۡنِ خَيۡرٞ مَّقَامٗا وَأَحۡسَنُ نَدِيّٗا

Na wanaposomewa Aya zetu zilizo wazi, wale waliokufuru huwaambia wale walioamini: Ni lipi katika makundi mawili haya lenye cheo kizuri na lililo zuri zaidi barazani? info
التفاسير:

external-link copy
74 : 19

وَكَمۡ أَهۡلَكۡنَا قَبۡلَهُم مِّن قَرۡنٍ هُمۡ أَحۡسَنُ أَثَٰثٗا وَرِءۡيٗا

Na kaumu ngapi tuliziangamiza zilizokuwa na mapambo mazuri zaidi na wazuri zaidi katika muonekano! info
التفاسير:

external-link copy
75 : 19

قُلۡ مَن كَانَ فِي ٱلضَّلَٰلَةِ فَلۡيَمۡدُدۡ لَهُ ٱلرَّحۡمَٰنُ مَدًّاۚ حَتَّىٰٓ إِذَا رَأَوۡاْ مَا يُوعَدُونَ إِمَّا ٱلۡعَذَابَ وَإِمَّا ٱلسَّاعَةَ فَسَيَعۡلَمُونَ مَنۡ هُوَ شَرّٞ مَّكَانٗا وَأَضۡعَفُ جُندٗا

Sema: Yule aliye katika upotofu, basi Arrahmani (Mwingi wa rehema) na amuongezee (muda, mali na mengineyo) mpaka atakapoona yale waliyoahidiwa - ima ni adhabu au ni Saa, hapo ndipo watakapojua ni nani mwenye makao maovu zaidi na mwenye jeshi dhaifu zaidi. info
التفاسير:

external-link copy
76 : 19

وَيَزِيدُ ٱللَّهُ ٱلَّذِينَ ٱهۡتَدَوۡاْ هُدٗىۗ وَٱلۡبَٰقِيَٰتُ ٱلصَّٰلِحَٰتُ خَيۡرٌ عِندَ رَبِّكَ ثَوَابٗا وَخَيۡرٞ مَّرَدًّا

Na Mwenyezi Mungu huwazidishia wale walioongoka uongofu. Na mema yenye kubakia ni bora katika malipo mbele ya Mola wako Mlezi na yana marejeo mema. info
التفاسير: