លេខ​ទំព័រ:close

external-link copy
33 : 45

وَبَدَا لَهُمۡ سَيِّـَٔاتُ مَا عَمِلُواْ وَحَاقَ بِهِم مَّا كَانُواْ بِهِۦ يَسۡتَهۡزِءُونَ

Basi ubaya wa yale waliyoyatenda utawadhihirikia, na yatawafika yale waliyokuwa wakiyafanyia masihara. info
التفاسير: |

external-link copy
34 : 45

وَقِيلَ ٱلۡيَوۡمَ نَنسَىٰكُمۡ كَمَا نَسِيتُمۡ لِقَآءَ يَوۡمِكُمۡ هَٰذَا وَمَأۡوَىٰكُمُ ٱلنَّارُ وَمَا لَكُم مِّن نَّٰصِرِينَ

Na itasemwa: 'Leo tunawasahau kama nyinyi mlivyosahau mkutano wa siku yenu hii; na mahali penu ni Motoni, wala hamna wowote wa kuwanusuru.' info
التفاسير: |

external-link copy
35 : 45

ذَٰلِكُم بِأَنَّكُمُ ٱتَّخَذۡتُمۡ ءَايَٰتِ ٱللَّهِ هُزُوٗا وَغَرَّتۡكُمُ ٱلۡحَيَوٰةُ ٱلدُّنۡيَاۚ فَٱلۡيَوۡمَ لَا يُخۡرَجُونَ مِنۡهَا وَلَا هُمۡ يُسۡتَعۡتَبُونَ

Hayo ni kwa sababu nyinyi mlizifanyia mzaha Aya za Mwenyezi Mungu, na maisha ya dunia yakawadanganya. Basi leo hawatatolewa humo wala hao hawatakubaliwa udhuru wao. info
التفاسير: |

external-link copy
36 : 45

فَلِلَّهِ ٱلۡحَمۡدُ رَبِّ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَرَبِّ ٱلۡأَرۡضِ رَبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ

Basi sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa mbingu na Mola Mlezi wa ardhi, na Mola Mlezi wa walimwengu wote. info
التفاسير: |

external-link copy
37 : 45

وَلَهُ ٱلۡكِبۡرِيَآءُ فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۖ وَهُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡحَكِيمُ

Na ukubwa ni wake Yeye tu, mbinguni na katika ardhi, naye ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima. info
التفاسير: |

Al-Jathiyah