وه‌رگێڕانی ماناكانی قورئانی پیرۆز - وەرگێڕاوی سواحیلی - علی محسن البرواني * - پێڕستی وه‌رگێڕاوه‌كان

XML CSV Excel API
Please review the Terms and Policies

وه‌رگێڕانی ماناكان سوره‌تی: سورەتی النبأ   ئایه‌تی:

Surat An-Naba

عَمَّ يَتَسَآءَلُونَ
WANAULIZANA nini?
Wanaulizana nini hao makafiri?
تەفسیرە عەرەبیەکان:
عَنِ ٱلنَّبَإِ ٱلۡعَظِيمِ
Ile khabari kuu!
Wanaulizana khabari kubwa, khabari ya kufufuliwa,
تەفسیرە عەرەبیەکان:
ٱلَّذِي هُمۡ فِيهِ مُخۡتَلِفُونَ
Ambayo kwayo wanakhitalifiana.
Ambayo wao wamezama ndani yake kukhitalifiana baina ya wenye kuikataa na wenye kuitilia shaka.
تەفسیرە عەرەبیەکان:
كَلَّا سَيَعۡلَمُونَ
La! Karibu watakuja jua.
Kuwazuia kuulizana huko wanaambiwa kuwa watakuja ujua ukweli wa mambo hapo watapo ona kufufuliwa kumetokea khasa.
تەفسیرە عەرەبیەکان:
ثُمَّ كَلَّا سَيَعۡلَمُونَ
Tena la! Karibu watakuja jua.
Tena kuwazuia, watakuja jua itapo wateremkia adhabu.
تەفسیرە عەرەبیەکان:
أَلَمۡ نَجۡعَلِ ٱلۡأَرۡضَ مِهَٰدٗا
kaKwani hatukuifanya ardhi ma tandiko?
Kwani wao hawaoni Ishara za uweza wetu kwamba Sisi tumeifanya ardhi imetandikwa upatikane utulivu juu yake na iwezekane kutembea juu yake?
تەفسیرە عەرەبیەکان:
وَٱلۡجِبَالَ أَوۡتَادٗا
kama Na milima vigingi?
Na tukaifanya milima ni vigingi vya ardhi vya kuituliza? Sehemu ya gamba gumu lilio juu ya ardhi linfikilia kiasi ya kilomita 60 unene wake, na inazidi mikunjo, mifimbi, inapanda juu kuwa milima, na huteremka chini kuwa ni vina vya bahari; na hiyo hulingana kwa sababu ya uzito unao patikana kutokana na milima. Na kulingana huko hakuharibiki ila kwa kubugunyika, kwani gamba kavu la ardhi linazuiliwa na milima, kama vigingi vinavyo zuilia khema. (Rejea Maoni ya Wataalamu juu ya Aya 7 ya Surat Qaf).
تەفسیرە عەرەبیەکان:
وَخَلَقۡنَٰكُمۡ أَزۡوَٰجٗا
Na tukakuumbeni kwa jozi?
Na tukakuumbeni kwa jozi, wanaume na wanawake?
تەفسیرە عەرەبیەکان:
وَجَعَلۡنَا نَوۡمَكُمۡ سُبَاتٗا
Na tukakufanya kulala kwenu ni mapumziko?
Na tukafanya kulala kwenu ni mapumziko ya machofu ya kazi? Kulala usingizi ni kusita nishat'i ya sehemu ya ubongo yenye kutambua na kuwa macho. Yaani gamba la ubongo, au kupunguka nishat'i yake kwa wingi, ukilinganisha na daraja za nishat'i ya sehemu za viungo vilio baki. Na kwa hivyo kunapunguka nguvu na joto la mwili, tena mwili hapo wakati wa usingizi hupata kutua na kupumzika baada ya kuhangaika viungo au akili au vyote viwili. Basi kazi za kimwili zote hupunguka isipo kuwa kazi za kusaga chakula, na kupitisha mkojo katika mafigo, na kutoka majasho katika ngozi, kwani yakisita hayo hupatikana madhara juu ya maisha ya mtu. Ama kuvuta pumzi huko nako hupunguka, na huwa ni kwa ndani zaidi, na huwa kwa kifua zaidi kuliko kwa tumbo. Na mpigo wa mishipa hupungua kasi kwa kunavyo tokana na moyo, na hudhoofika mkazano wa musulo (muscular tension), na kwa hivyo huwa taabu kupata harakati za kinyume. Na yote haya ni ili binaadamu apate kupumzika wakati wa kulala.
تەفسیرە عەرەبیەکان:
وَجَعَلۡنَا ٱلَّيۡلَ لِبَاسٗا
Na tukaufanya usiku ni nguo?
Na tumeufanya usiku ni sitara kwenu kwa kiza kinacho kufunikeni.
تەفسیرە عەرەبیەکان:
وَجَعَلۡنَا ٱلنَّهَارَ مَعَاشٗا
Na tukaufanya mchana ni wa kuchumia maisha?
Na tumeufanya mchana ni wakati wa kuhangaika kwenu kutafuta cha kukusaidieni katika maisha yenu.
تەفسیرە عەرەبیەکان:
وَبَنَيۡنَا فَوۡقَكُمۡ سَبۡعٗا شِدَادٗا
Na tukajenga juu yenu saba zenye nguvu?
Na tumesimamisha juu yenu mbingu saba zenye nguvu madhubuti.
تەفسیرە عەرەبیەکان:
وَجَعَلۡنَا سِرَاجٗا وَهَّاجٗا
Na tukaifanya taa yenye mwanga na joto;
Na Sisi tumeliumba jua lenye mwangaza na linalo waka. Makusudio ya Assiraj Alwahhaaj, Taa yenye mwanga na joto, ni Jua. Na hayo kama ilivyo thibiti katika sayansi kuwa daraja ya joto la uso wake inafika daraja 6000. Ama kati yake daraja yake inazidi daraja 30 milioni kwa sababu ya mdidimizo mkubwa unao patikana juu ya madda ziliomo ndani yake. Na jua linatoa nishat'i hizi zifuatazo: 9 katika 100 ya miale ya Ultraviolet rays, 46 katika 100 ya miale ya mwangaza, 45 katika 100 miale ya joto, au Infra red rays. Na kwa hivyo hii Aya tukufu imeliita kuwa ni Taa yenye mwangaza na joto.
تەفسیرە عەرەبیەکان:
وَأَنزَلۡنَا مِنَ ٱلۡمُعۡصِرَٰتِ مَآءٗ ثَجَّاجٗا
Na tukateremsha maji yanayo anguka kwa kasi kutoka mawinguni,
Na tumeteremsha kutokana na mawingu yaliyo karibia kunyesha maji yenye kumiminika kwa nguvu. Mvua ndio kitu pekee kinacho toka asli yake maji matamu katika ardhi. Na asli ya mvua ni kukusanyika vijisehemu vya maji yanayo panda kutoka baharini, na maziwa na mito, yakakusanyika kama mawingu na yakageuka chembe za mvua au vipande vya barafu, na khatimaye yakaanguka kwa sura ya mvua au theluji.
تەفسیرە عەرەبیەکان:
لِّنُخۡرِجَ بِهِۦ حَبّٗا وَنَبَاتٗا
Ili tutoe kwayo nafaka na mimea.
Ili tutoe kwa maji haya nafaka na mimea kuwa ni chakula kwa ajili ya watu na wanyama.
تەفسیرە عەرەبیەکان:
وَجَنَّٰتٍ أَلۡفَافًا
Na mabustani yenye miti iliyo kamatana.
Na mabustani yenye miti iliyo fungamana na matawi yake yameingiliana.
تەفسیرە عەرەبیەکان:
إِنَّ يَوۡمَ ٱلۡفَصۡلِ كَانَ مِيقَٰتٗا
Hakika siku ya uamuzi imewekewa wakati wake,
Hakika siku ya uamuzi baina ya viumbe imewekewa miadi ilio kwisha kadiriwa kwa ajili ya kufufuliwa.
تەفسیرە عەرەبیەکان:
يَوۡمَ يُنفَخُ فِي ٱلصُّورِ فَتَأۡتُونَ أَفۡوَاجٗا
Siku litapo pulizwa barugumu, nanyi mtakuja kwa makundi,
Siku litakapo pulizwa barugumu na kufufuliwa watu, mtakuja kwenye mkutano makundi kwa makundi.
تەفسیرە عەرەبیەکان:
وَفُتِحَتِ ٱلسَّمَآءُ فَكَانَتۡ أَبۡوَٰبٗا
Na mbingu zitafunguliwa, ziwe milango.
Na mbingu zitapasuliwa kila upande hata zitakuwa ni milango milango.
تەفسیرە عەرەبیەکان:
وَسُيِّرَتِ ٱلۡجِبَالُ فَكَانَتۡ سَرَابًا
Na milima itaondolewa na itakuwa kama sarabi.
Na milima itaondolewa baada ya kung'olewa mwahala mwake, na kuvurugwa, ikawa unaiona kama sura ya milima na hali hiyo ni kifusi tu kilicho rindikwa, kama uonavyo mangati, sarabi, unaona kama sura ya maji nayo si maji.
تەفسیرە عەرەبیەکان:
إِنَّ جَهَنَّمَ كَانَتۡ مِرۡصَادٗا
Hakika Jahannamu inangojea!
Hakika Jahannamu imekuwa kama ni kitu kinacho ngojea, walinzi wake wanawangojea watu watakao kuja kuingia.
تەفسیرە عەرەبیەکان:
لِّلطَّٰغِينَ مَـَٔابٗا
Kwa walio asi ndio makaazi yao,
Yawe ni marejeo na mafikio kwa wenye kupindukia mipaka ya Mwenyezi Mungu.
تەفسیرە عەرەبیەکان:
لَّٰبِثِينَ فِيهَآ أَحۡقَابٗا
Wakae humo karne baada ya karne,
Watakaa humo dahari baada ya dahari.
تەفسیرە عەرەبیەکان:
لَّا يَذُوقُونَ فِيهَا بَرۡدٗا وَلَا شَرَابًا
Hawataonja humo chochote kibaridi wala kinywaji,
Hawataonja humo hata chembe ya upepo wa kuburudisha joto lake, wala kinywaji cha kupoza kiu chao.
تەفسیرە عەرەبیەکان:
إِلَّا حَمِيمٗا وَغَسَّاقٗا
Ila maji yamoto sana na usaha,
Lakini watakunywa maji yalio pita ukomo kwa umoto wake, na usaha unao miminika kutokana na ngozi za watu wa Motoni.
تەفسیرە عەرەبیەکان:
جَزَآءٗ وِفَاقًا
Ndio jaza muwafaka.
Malipo ya kuwafikiana na vitendo vyao viovu.
تەفسیرە عەرەبیەکان:
إِنَّهُمۡ كَانُواْ لَا يَرۡجُونَ حِسَابٗا
Hakika hao hawakuwa wakitaraji kuwa kuna hisabu.
Kwani hao hawakutaraji kuwa itakuwapo kuhisabiwa, hata watende ya kuwaokoa humo.
تەفسیرە عەرەبیەکان:
وَكَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَا كِذَّابٗا
Na wakikanusha Aya zetu kwa nguvu.
Wakazikadhibisha Ishara za Mwenyezi Mungu zenye kuthibitisha kufufuliwa kwa mkadhibisho mkali.
تەفسیرە عەرەبیەکان:
وَكُلَّ شَيۡءٍ أَحۡصَيۡنَٰهُ كِتَٰبٗا
Na kila kitu Sisi tumekidhibiti kwa kukiandika.
Na kila kitu tumekidhibiti kwa kukiandika.
تەفسیرە عەرەبیەکان:
فَذُوقُواْ فَلَن نَّزِيدَكُمۡ إِلَّا عَذَابًا
Basi onjeni! Nasi hatutakuzidishieni ila adhabu!
Basi onjeni, wala hampati kwetu ila kuzidishiwa adhabu tu.
تەفسیرە عەرەبیەکان:
إِنَّ لِلۡمُتَّقِينَ مَفَازًا
Hakika wachamngu wanastahiki kufuzu,
Hakika wenye kumcha Mola wao Mlezi watapata kuokoka na adhabu, na wataipata Pepo,
تەفسیرە عەرەبیەکان:
حَدَآئِقَ وَأَعۡنَٰبٗا
Mabustani na mizabibu,
Na mabustani yenye matunda, na mizabibu mizuri,
تەفسیرە عەرەبیەکان:
وَكَوَاعِبَ أَتۡرَابٗا
Na wake walio lingana nao,
Na wanawari walio watipwatipwa wa hirimu yao,
تەفسیرە عەرەبیەکان:
وَكَأۡسٗا دِهَاقٗا
Na bilauri zilizo jaa,
Na bilauri safi zilizo jaa pomoni,
تەفسیرە عەرەبیەکان:
لَّا يَسۡمَعُونَ فِيهَا لَغۡوٗا وَلَا كِذَّٰبٗا
Hawatasikia humo upuuzi wala uwongo,
Hawasikii huko Peponi upuuzi wala uwongo.
تەفسیرە عەرەبیەکان:
جَزَآءٗ مِّن رَّبِّكَ عَطَآءً حِسَابٗا
Malipo kutoka kwa Mola wako Mlezi, kipawa cha kutosha.
Ni malipo kutokana na Mola wako Mlezi, kwa fadhila yake na ihsani ya kutosha.
تەفسیرە عەرەبیەکان:
رَّبِّ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَمَا بَيۡنَهُمَا ٱلرَّحۡمَٰنِۖ لَا يَمۡلِكُونَ مِنۡهُ خِطَابٗا
Mola Mlezi wa mbingu na ardhi na vilio baina yao, Arrahman, Mwingi wa rehema; hawamiliki usemi mbele yake!
Mola Mlezi wa mbinguni na duniani na vilio baina yao, ambaye rehema yake imeenea juu ya kila kitu. Hapana yeyote mwenye madaraka ya kusema mbele yake.
تەفسیرە عەرەبیەکان:
يَوۡمَ يَقُومُ ٱلرُّوحُ وَٱلۡمَلَٰٓئِكَةُ صَفّٗاۖ لَّا يَتَكَلَّمُونَ إِلَّا مَنۡ أَذِنَ لَهُ ٱلرَّحۡمَٰنُ وَقَالَ صَوَابٗا
Siku atakapo simama Roho na Malaika kwa safu. Hawatasema ila Mwingi wa rehema aliye mruhusu, na atasema yaliyo sawa tu.
Siku atakapo simama Jibrili na Malaika walio teuliwa nao wamenyenyekea, hasemi mmoja wao ila akipewa idhini na Arrahman, Mwingi wa rehema, kuwa aseme, naye atasema lilio sawa tu.
تەفسیرە عەرەبیەکان:
ذَٰلِكَ ٱلۡيَوۡمُ ٱلۡحَقُّۖ فَمَن شَآءَ ٱتَّخَذَ إِلَىٰ رَبِّهِۦ مَـَٔابًا
Hiyo ndiyo Siku ya haki. Basi anaye taka na ashike njia arejee kwa Mola wake Mlezi
Hiyo ndiyo siku isiyo na shaka. Basi atakaye na ashike njia ya kwenda kwa Mola wake Mlezi arejee kwa Imani, na a'mali njema.
تەفسیرە عەرەبیەکان:
إِنَّآ أَنذَرۡنَٰكُمۡ عَذَابٗا قَرِيبٗا يَوۡمَ يَنظُرُ ٱلۡمَرۡءُ مَا قَدَّمَتۡ يَدَاهُ وَيَقُولُ ٱلۡكَافِرُ يَٰلَيۡتَنِي كُنتُ تُرَٰبَۢا
Hakika tumekuhadharisheni adhabu iliyo karibu kufika; Siku ambayo mtu atakapo ona yaliyo tangulizwa na mikono yake; na kafiri atasema: Laiti ningeli kuwa udongo!
Hakika Sisi tumekuhadharisheni na adhabu itakayo tokea karibu, siku atakapo angalia mtu vitendo vyake vilivyo tangulizwa na mikono yake, na atakapo sema kafiri kwa kutamani kuokoka: Laiti ningeli bakia udongo baada ya kufa, nisifufuliwe wala nisihisabiwe!
تەفسیرە عەرەبیەکان:
 
وه‌رگێڕانی ماناكان سوره‌تی: سورەتی النبأ
پێڕستی سوره‌ته‌كان ژمارەی پەڕە
 
وه‌رگێڕانی ماناكانی قورئانی پیرۆز - وەرگێڕاوی سواحیلی - علی محسن البرواني - پێڕستی وه‌رگێڕاوه‌كان

وەرگێڕاوی ماناکانی قورئانی پیرۆز بۆ زمانی سواحیلی، وەرگێڕان: علی محسن البرواني.

داخستن