13 : 60

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا تَتَوَلَّوۡاْ قَوۡمًا غَضِبَ ٱللَّهُ عَلَيۡهِمۡ قَدۡ يَئِسُواْ مِنَ ٱلۡأٓخِرَةِ كَمَا يَئِسَ ٱلۡكُفَّارُ مِنۡ أَصۡحَٰبِ ٱلۡقُبُورِ

Enyi mliomuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake! Msiwafanye wale ambao Allah Mtukufu Amewakasirikia kwa ukafiri wao kuwa ni marafiki na vipenzi, kwani hao washakata tamaa kupata thawabu za Allah Mtukufu kesho Akhera, kama makafiri walio makaburini walivyokata tamaa ya kupata rehema za Allah Mtukufu huko Akhera, watakaposhuhudia ukweli wa mambo na wakajua ujuzi wa yakini kuwa hawatakuwa na fungu lolote huko, au kama walivyokata tamaa makafiri kufufuliwa wafu wao- walio makaburini- kwa kuitakidi kwao kuwa hakuna kufufuliwa. info
التفاسير: |
prev

Al-Mumtahanah

next
:
0:00 0:00