Check out the new design

Kilniojo Korano reikšmių vertimas - Suahilių k. vertimas - Ruad vertimo centras * - Vertimų turinys


Reikšmių vertimas Sūra: An-Nachl   Aja (Korano eilutė):
وَقَالَ ٱلَّذِينَ أَشۡرَكُواْ لَوۡ شَآءَ ٱللَّهُ مَا عَبَدۡنَا مِن دُونِهِۦ مِن شَيۡءٖ نَّحۡنُ وَلَآ ءَابَآؤُنَا وَلَا حَرَّمۡنَا مِن دُونِهِۦ مِن شَيۡءٖۚ كَذَٰلِكَ فَعَلَ ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِمۡۚ فَهَلۡ عَلَى ٱلرُّسُلِ إِلَّا ٱلۡبَلَٰغُ ٱلۡمُبِينُ
Na washirikina walisema: Mwenyezi Mungu angelitaka, tusingeliabudu chochote badala yake, sisi wala baba zetu, wala tusingeliharimisha chochote bila ya Yeye. Kama hivyo, walifanya wale waliokuwa kabla yao. Basi lipo lolote juu ya Mitume isipokuwa kufikisha tu kwa wazi?
Tafsyrai arabų kalba:
وَلَقَدۡ بَعَثۡنَا فِي كُلِّ أُمَّةٖ رَّسُولًا أَنِ ٱعۡبُدُواْ ٱللَّهَ وَٱجۡتَنِبُواْ ٱلطَّٰغُوتَۖ فَمِنۡهُم مَّنۡ هَدَى ٱللَّهُ وَمِنۡهُم مَّنۡ حَقَّتۡ عَلَيۡهِ ٱلضَّلَٰلَةُۚ فَسِيرُواْ فِي ٱلۡأَرۡضِ فَٱنظُرُواْ كَيۡفَ كَانَ عَٰقِبَةُ ٱلۡمُكَذِّبِينَ
Na hakika kwa kila umma tuliutumia Mtume kwamba: Muabuduni Mwenyezi Mungu, na muepukeni Shetani. Basi kati yao wapo aliowaongoa Mwenyezi Mungu. Na kati yao wapo ambao uliwathibitikia upotovu. Basi tembeeni katika ardhi, muangalie ulikuwaje mwisho wa wale wanaokadhibisha.
Tafsyrai arabų kalba:
إِن تَحۡرِصۡ عَلَىٰ هُدَىٰهُمۡ فَإِنَّ ٱللَّهَ لَا يَهۡدِي مَن يُضِلُّۖ وَمَا لَهُم مِّن نَّٰصِرِينَ
Hata ukiwa na pupa juu ya kuongoka kwao, basi hakika Mwenyezi Mungu hamwongoi yule anayeshikilia kupotea. Wala hawatapata yeyote wa kuwanusuru.
Tafsyrai arabų kalba:
وَأَقۡسَمُواْ بِٱللَّهِ جَهۡدَ أَيۡمَٰنِهِمۡ لَا يَبۡعَثُ ٱللَّهُ مَن يَمُوتُۚ بَلَىٰ وَعۡدًا عَلَيۡهِ حَقّٗا وَلَٰكِنَّ أَكۡثَرَ ٱلنَّاسِ لَا يَعۡلَمُونَ
Na waliapa kwa Mwenyezi Mungu ukomo wa viapo vyao kwamba Mwenyezi Mungu hatamfufua aliyekufa. Kwani! Ni ahadi iliyo juu yake kikweli; lakini wengi wa watu hawajui.
Tafsyrai arabų kalba:
لِيُبَيِّنَ لَهُمُ ٱلَّذِي يَخۡتَلِفُونَ فِيهِ وَلِيَعۡلَمَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓاْ أَنَّهُمۡ كَانُواْ كَٰذِبِينَ
Ili awabainishie yale waliyohitalifiana ndani yake, na ili wajue wale waliokufuru kwamba wao walikuwa waongo.
Tafsyrai arabų kalba:
إِنَّمَا قَوۡلُنَا لِشَيۡءٍ إِذَآ أَرَدۡنَٰهُ أَن نَّقُولَ لَهُۥ كُن فَيَكُونُ
Hakika, kauli yetu kwa kitu tunapokitaka kiwe, ni kukiambia tu: Kuwa! Basi kinakuwa.
Tafsyrai arabų kalba:
وَٱلَّذِينَ هَاجَرُواْ فِي ٱللَّهِ مِنۢ بَعۡدِ مَا ظُلِمُواْ لَنُبَوِّئَنَّهُمۡ فِي ٱلدُّنۡيَا حَسَنَةٗۖ وَلَأَجۡرُ ٱلۡأٓخِرَةِ أَكۡبَرُۚ لَوۡ كَانُواْ يَعۡلَمُونَ
Na wale waliohama kwa ajili ya Mwenyezi Mungu baada ya kudhulumiwa, bila ya shaka tutawaweka katika maskani mazuri katika dunia; na katika ujira wa Akhera ni mkubwa zaidi; lau wangekuwa wanajua!
Tafsyrai arabų kalba:
ٱلَّذِينَ صَبَرُواْ وَعَلَىٰ رَبِّهِمۡ يَتَوَكَّلُونَ
Wale waliosubiri na wakamtegemea Mola wao Mlezi.
Tafsyrai arabų kalba:
 
Reikšmių vertimas Sūra: An-Nachl
Sūrų turinys Puslapio numeris
 
Kilniojo Korano reikšmių vertimas - Suahilių k. vertimas - Ruad vertimo centras - Vertimų turinys

Vertė Ruad vertimo centro komanda bendradarbiaujant su Religinės sklaidos ir orientavimo asociacija Rabwah bei Islamo turinio kalbos asociacija.

Uždaryti