Check out the new design

Kilniojo Korano reikšmių vertimas - Suahilių k. vertimas - Ruad vertimo centras * - Vertimų turinys


Reikšmių vertimas Sūra: Al-An’am   Aja (Korano eilutė):
فَقُطِعَ دَابِرُ ٱلۡقَوۡمِ ٱلَّذِينَ ظَلَمُواْۚ وَٱلۡحَمۡدُ لِلَّهِ رَبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ
Ikakatwa mizizi ya kaumu waliodhulumu, na kuhimidiwa ni kwa Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote.
Tafsyrai arabų kalba:
قُلۡ أَرَءَيۡتُمۡ إِنۡ أَخَذَ ٱللَّهُ سَمۡعَكُمۡ وَأَبۡصَٰرَكُمۡ وَخَتَمَ عَلَىٰ قُلُوبِكُم مَّنۡ إِلَٰهٌ غَيۡرُ ٱللَّهِ يَأۡتِيكُم بِهِۗ ٱنظُرۡ كَيۡفَ نُصَرِّفُ ٱلۡأٓيَٰتِ ثُمَّ هُمۡ يَصۡدِفُونَ
Sema: Mwaonaje Mwenyezi Mungu akinyakua kusikia kwenu, na kuona kwenu, na akaziziba nyoyo zenu, ni mungu gani asiyekuwa Mwenyezi Mungu atakayewaletea hayo tena? Angalia vipi tunavyozieleza Ishara, kisha wao wanapuuza.
Tafsyrai arabų kalba:
قُلۡ أَرَءَيۡتَكُمۡ إِنۡ أَتَىٰكُمۡ عَذَابُ ٱللَّهِ بَغۡتَةً أَوۡ جَهۡرَةً هَلۡ يُهۡلَكُ إِلَّا ٱلۡقَوۡمُ ٱلظَّٰلِمُونَ
Sema: Mwaonaje, ikiwafikia adhabu ya Mwenyezi Mungu kwa ghafla, au kwa dhahiri, je wataangamizwa isipokuwa kaumu waliodhulumu?
Tafsyrai arabų kalba:
وَمَا نُرۡسِلُ ٱلۡمُرۡسَلِينَ إِلَّا مُبَشِّرِينَ وَمُنذِرِينَۖ فَمَنۡ ءَامَنَ وَأَصۡلَحَ فَلَا خَوۡفٌ عَلَيۡهِمۡ وَلَا هُمۡ يَحۡزَنُونَ
Na hatuwatumi Mitume isipokuwa huwa ni wabashiri na waonyaji. Basi mwenye kuamini na akatengenea, haitakuwa hofu yoyote juu yao, wala hawatahuzunika.
Tafsyrai arabų kalba:
وَٱلَّذِينَ كَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَا يَمَسُّهُمُ ٱلۡعَذَابُ بِمَا كَانُواْ يَفۡسُقُونَ
Na wale waliozikadhibisha Ishara zetu itawagusa adhabu kwa vile walivyokuwa wakivuka mipaka.
Tafsyrai arabų kalba:
قُل لَّآ أَقُولُ لَكُمۡ عِندِي خَزَآئِنُ ٱللَّهِ وَلَآ أَعۡلَمُ ٱلۡغَيۡبَ وَلَآ أَقُولُ لَكُمۡ إِنِّي مَلَكٌۖ إِنۡ أَتَّبِعُ إِلَّا مَا يُوحَىٰٓ إِلَيَّۚ قُلۡ هَلۡ يَسۡتَوِي ٱلۡأَعۡمَىٰ وَٱلۡبَصِيرُۚ أَفَلَا تَتَفَكَّرُونَ
Sema: Mimi siwaambii kuwa ninazo hazina za Mwenyezi Mungu. Wala sijui mambo yaliyofichikana. Wala siwaambii kuwa mimi ni Malaika. Mimi sifuati isipokuwa yanayofunuliwa kwangu. Sema: Je, wanakuwa sawa, kipofu na mwenye kuona. Basi hamfikiri?
Tafsyrai arabų kalba:
وَأَنذِرۡ بِهِ ٱلَّذِينَ يَخَافُونَ أَن يُحۡشَرُوٓاْ إِلَىٰ رَبِّهِمۡ لَيۡسَ لَهُم مِّن دُونِهِۦ وَلِيّٞ وَلَا شَفِيعٞ لَّعَلَّهُمۡ يَتَّقُونَ
Na waonye kwayo wale wanaohofu kuwa watakusanywa kwa Mola wao Mlezi, hali ya kuwa hawana kando naye mlinzi wala mwombezi, ili wamche Mwenyezi Mungu.
Tafsyrai arabų kalba:
وَلَا تَطۡرُدِ ٱلَّذِينَ يَدۡعُونَ رَبَّهُم بِٱلۡغَدَوٰةِ وَٱلۡعَشِيِّ يُرِيدُونَ وَجۡهَهُۥۖ مَا عَلَيۡكَ مِنۡ حِسَابِهِم مِّن شَيۡءٖ وَمَا مِنۡ حِسَابِكَ عَلَيۡهِم مِّن شَيۡءٖ فَتَطۡرُدَهُمۡ فَتَكُونَ مِنَ ٱلظَّٰلِمِينَ
Wala usiwafukuze wale wanaomwomba Mola Mlezi wao asubuhi na jioni kwa kutaka radhi yake. Si juu yako hisabu yao hata kidogo, wala hisabu yako si juu yao hata kidogo, hata uwafukuze na uwe miongoni mwa wenye kudhulumu.
Tafsyrai arabų kalba:
 
Reikšmių vertimas Sūra: Al-An’am
Sūrų turinys Puslapio numeris
 
Kilniojo Korano reikšmių vertimas - Suahilių k. vertimas - Ruad vertimo centras - Vertimų turinys

Vertė Ruad vertimo centro komanda bendradarbiaujant su Religinės sklaidos ir orientavimo asociacija Rabwah bei Islamo turinio kalbos asociacija.

Uždaryti