Na walio amini, na wakatenda mema, na wakaamini aliyo teremshiwa Muhammad - nayo ni Haki iliyo toka kwa Mola wao Mlezi - atawafutia makosa yao na ataitengeneza hali yao.
Na walio amini, na wakatenda mema, na wakasadiki yaliyo teremshwa kwa Muhammad, nayo ni Haki iliyo toka kwa Mola wao Mlezi, atawafutia makosa yao, na atawatengenezea hali yao ya Dini na dunia.
Hayo ni kwa sababu walio kufuru wamefuata upotovu, na walio amini wamefuata Haki iliyo toka kwa Mola wao Mlezi. Hivyo ndivyo Mwenyezi Mungu anavyo wapigia watu mifano yao.
Hayo ni kwa sababu walio kufuru wamefuata njia ya upotovu, na kwamba walio amini wamefuata njia ya Haki iliyo toka kwa Mola wao Mlezi. Kwa mfano kama huu wa kubainisha kwa uwazi ndio Mwenyezi Mungu anawaeleza watu hali zao ili wapate kuzingatia.
Basi mnapo wakuta walio kufuru wapigeni shingoni mwao, mpaka mkiwadhoofisha wafungeni pingu. Tena waachilieni kwa hisani au wajikomboe, mpaka vita vipoe. Ndio hivyo. Na lau angeli taka Mwenyezi Mungu angeli washinda mwenyewe, lakini haya ni kwa sababu akutieni mitihani nyinyi kwa nyinyi. Na walio uliwa katika njia ya Mwenyezi Mungu hatazipoteza a'mali zao.
Mtapo kutana na walio kufuru katika vita basi wapigeni kwenye shingo zao, mpaka mtakapo wadhoofisha kwa wingi wa kuwauwa, basi tena wafungeni mateka. Tena ama waachilieni wende zao kwa wema na ihsani, baada ya kwisha vita, kwa kuwaachia bila ya fidia, au kwa fidia ya kutoa mali au kubadilishana kwa mateka wa Kiislamu. Inakuwa mmewaachilia kwa badali. Huu ndio uwe mwendo wenu na makafiri mpaka vita vimalizike kabisa. Mwenyezi Mungu anawahukumieni hivyo. Na lau angeli taka bila ya shaka angeli washinda bila ya vita, lakini haya ni ili awajaribu Waumini kwa makafiri kama mtihani ndio ameamrisha Jihadi. Na walio uwawa katika njia ya Mwenyezi Mungu kabisa hatoacha vitendo vyao vipotee. Atawahidi, na azitengeneze nyoyo zao, na awatie katika Pepo aliyo kwisha wajuulisha. Katika Aya hii tukufu zimetajwa "shingo" khasa, kwa sababu kuzipiga hizo ndio njia inayo faa mno kummaliza upesi mwenye kupigwa bila ya kumuadhibu na kumtesa. Kwani imethibiti kwa ilimu kuwa shingo ndiyo kiungo baina ya kichwa na kiwiliwili kizima. Basi ukikatika mshipa wa uti wa mgongo wenye kupeleka hisiya zote, basi viungo vyote muhimu vinapooza. Na ikikatika mishipa ya damu, damu inasita kufika kwenye ubongo. Na zikikatika njia za kupitisha hewa, basi pumzi husita. Na katika hali hizi zote uhai unakatika mara moja.
Na walio uwawa katika njia ya Mwenyezi Mungu kabisa hatoacha vitendo vyao vipotee. Atawahidi, na azitengeneze nyoyo zao, na awatie katika Pepo aliyo kwisha wajuulisha.
Hayo ni kwa sababu waliyachukia aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, basi akaviangusha vitendo vyao.
Mambo yao ni hivyo kwa sababu wao wanakereka na aliyo teremsha Mwenyezi Mungu, yaani Qur'ani na amri zake. Basi Mwenyezi Mungu amevibat'ilisha vitendo vyao.
Kwani hawakutembea katika ardhi wakaona ulikuwaje mwisho wa walio kuwa kabla yao? Mwenyezi Mungu aliwaangamiza, na kwa makafiri hawa itakuwa mfano wa hayo.
Wameshindwa kutafuta ya kuwazindua, hata hawakutembea katika ardhi wakaangalia hali gani ulikuwa mwisho wa walio wakadhibisha Mitume kabla yao? Mwenyezi Mungu aliwateremshia hilaki katika kila kilicho khusiana nao, nafsi zao, mali yao, na watoto wao. Na wenye kumkataa Mwenyezi Mungu na Mitume wake ndio hupata mwisho mfano wa huo.
Hayo ni kwa sababu Mwenyezi Mungu ni Mlinzi wa walio amini. Na makafiri hawana mlinzi.
Malipo hayo ndio ushindi wa Waumini na kushindwa nguvu makafiri, ni kwa sababu hakika Mwenyezi Mungu ni rafiki mlinzi wa walio amini na ndiye Mwenye kuwanusuru; na makafiri hawana rafiki mlinzi wa kuwanusuru wala kuwakinga na kuangamia.
Hakika Mwenyezi Mungu atawaingiza walio amini na wakatenda mema katika Bustani zipitiwazo na mito kati yake. Na walio kufuru hujifurahisha na hula kama walavyo wanyama, na Moto ndio makaazi yao.
Hakika Mwenyezi Mungu atawatia wenye kuamini na wakatenda mema katika Pepo tukufu zenye kupitiwa ndani yake mito. Na makafiri wanastarehe duniani kidogo, na wanakula kama walavyo wanyama, wamepigwa na mghafala wala hawajifikirii mwisho wao. Hawanalo lao ila matamanio yao. Na kesho Akhera nyumba yao ni Motoni.
Na miji mingapi iliyo kuwa na nguvu zaidi kuliko mji wako huu ulio kutoa; nao tuliwateketeza na wala hawakuwa wa kuwanusuru.
Na wengi katika watu wa miji walio tangulia walio kuwa na nguvu zaidi kushinda watu wa mji wako wa Makka ambao watu wake wamekufukuza, ewe Muhammad, tuliwaangamiza kwa namna mbali mbali za adhabu. Na hakutokea yeyote wa kuwanusuru nasi.
Je! Mwenye kuwa na bayana kutoka kwa Mola wake Mlezi ni kama aliye pambiwa uovu wa vitendo vyake, na wakafuata pumbao lao?
Je! Wanaweza kuwa sawa makundi mawili haya katika malipo? Mwenye kuwa na ujuzi wazi kumjua Muumba wake na Mlezi wake, naye akawa anamt'ii, atakuwa sawa na mwenye kuwa na vitendo vyake viovu naye akaviona ni vizuri, na akafuata hayo ayatendayo na akaeneza pumbao lake la upotovu.
Mfano wa Pepo walio ahidiwa wachamngu ina mito ya maji yasiyo vunda, na mito ya maziwa isiyo haribika ladha yake, na mito ya mvinyo yenye ladha kwa wanywao, na mito ya asali iliyo safishwa. Na wao humo watakuwa na kila namna ya matunda, na maghfira kutoka kwa Mola wao Mlezi. Basi hao ni kama watakao dumu Motoni na wakinyweshwa maji yanayo chemka ya kuwakata matumbo yao?
Sifa ya Pepo walio ahidiwa wachamngu ni kama hivi: ndani yake imo mito ya maji yasiyo chafuka, na mito ya maziwa yasiyo haribika utamu wake, na mito ya mvinyo yenye ladha kwa wanywao, na mito ya asali iliyo safishwa na takataka zote. Na humo watakuwa na kila namna ya matunda, na msamaha mkubwa kutokana na Mola wao Mlezi. Je! Sifa za Pepo ya hawa ni kama sifa itayo kuwa ni malipo ya mwenye kudumu milele Motoni, na akanyweshwa maji yaliyo tokota ya kukata matumbo? Aya hii tukufu inataka tuzingatie kuwa maji yaliyo vunda, yaliyo tuama, yenye kutaghayari, ni maji yenye madhara. Na Aya hii tukufu imesema hayo kabla ya kuvumbuliwa darubini za kutazamia vijidudu (Microscope) kwa makarne ya miaka, ndipo ilipo juulikana kuwa maji yaliyo tuama yaliyo taghayari yanakuwamo ndani yake mamilioni ya vijidudu vyenye madhara ya kuwasibu watu na wanyama kwa namna mbali mbali ya magonjwa.
Na wapo miongoni mwao wanao kusikiliza, mpaka wakiondoka kwako huwauliza walio pewa ilimu: Amesema nini sasa hivi? Hao ndio ambao Mwenyezi Mungu amepiga muhuri juu ya nyoyo zao, na wakafuata pumbao lao.
Na miongoni mwa makafiri kipo kikundi cha watu wanao kusikiliza wewe, Muhammad. Hawakuamini wewe, wala hawanafiiki na maneno yako. Mpaka wakisha ondoka kwenye baraza yako husema kwa kejeli kuwaambia walio pewa ujuzi: Kasema nini huyu Muhammad sasa hivi? Watu hao ndio Mwenyezi Mungu amepiga muhuri wa ukafiri juu ya nyoyo zao. Ndio wameiacha kheri wakifuata matamanio yao.
Kwani wanangojea jengine isipo kuwa iwafikie Saa (ya Kiyama) kwa ghafla? Na hakika alama zake zimekwisha kuja. Na itapo wajia kutawafaa wapi kukumbuka hapo?
Wanao kanusha hawawaidhiki na hali za walio tangulia. Basi je! Wanangojea Saa (ya Kiyama) iwajie kwa ghafla? Kwa hakika alama zake zimekwisha dhihiri, na wao hawajazingatia kuwa inakuja. Basi watakumbuka wapi itapo wajia mara moja kwa ghafla?
Basi jua ya kwamba hapana mungu ila Mwenyezi Mungu, na omba maghufira kwa dhambi zako na za Waumini wanaume na Waumini wanawake. Na Mwenyezi Mungu anajua mahali penu pa kwenda na kurudi, na mahali penu pa kukaa.
Basi thibiti juu ya ujuzi ya kwamba hakika hapana wa kuabudiwa kwa Haki ila Mwenyezi Mungu tu. Na muombe maghfira Mwenyezi Mungu kwa dhambi yako na madhambi ya Waumini wanaume na Waumini wanawake. Na Mwenyezi Mungu anajua kila lenu, la kupita na la kukaa.
Na Waumini wanasema: Kwa nini haiteremshwi Sura? Na inapo teremshwa Sura madhubuti na ikatajwa ndani yake khabari ya vita, utawaona wenye maradhi katika nyoyo zao wanakutazama mtazamo wa anaye zimia kwa mauti. Basi ni bora kwao
Walio amini wanasema: Haiteremki Sura ya kututaka tupigane? Na ikiteremka Sura ambayo haifasiriki vyenginevyo ila ni kulazimisha tu, na ikataja ndani yake kuamrishwa vita, utawaona ambao katika nyoyo zao mna unaafiki wanakuangalia kwa muangalio wa mwenye kuzimia kwa mauti, jinsi ya kuviogopa na kuvichukia vita. Linalo wastahikia kulifanya ni kumt'ii Mwenyezi Mungu na kusema neno linalo kubaliana na sharia.
Ut'iifu na kauli njema. Na jambo likisha azimiwa, basi wakiwa ni wakweli kwa Mwenyezi Mungu, bila ya shaka itakuwa ni kheri kwao.
Na mambo yakawa ni kweli, na ikawalazimu kupigana, basi lau kuwa ni kweli wana Imani ya Mwenyezi Mungu na ut'iifu ingeli kuwa bora kwao kuliko huo unaafiki. Basi ndio mnavyo tarajiwa, enyi wanaafiki, kuwa mkipata madaraka ndio mfisidi katika nchi na mkate makhusiano yenu na jamaa zenu?
Hao ndio Mwenyezi Mungu alio walaani, na akawatia uziwi, na akawapofoa macho yao.
Hao ndio alio watenga mbali kabisa Mwenyezi Mungu na rehema yake, na akawatia uziwi wasiisikie Haki, na akawatia upofu wa macho wasiione Njia ya Uwongofu.
Kwa hakika wanao rudi nyuma baada ya kwisha wabainikia uwongofu, Shetani huyo amewashawishi na amewaghuri.
Hakika wale walio ritadi, wakarejea nyuma kwenye ukafiri na upotofu walio kuwa nao baada ya kuwadhihirikia njia ya uwongofu, Shetani ndiye aliye wapambia, na akawakunjulia matamanio ya uwongo.
Hayo ni kwa sababu waliwaambia walio chukia aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu: Tutakut'iini katika baadhi ya mambo. Na Mwenyezi Mungu anajua siri zao.
Kurejea huko ukafirini ni kwa kuwa waliwaambia wenye kuchukia aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu: Tutakut'iini katika baadhi ya mambo. Na Mwenyezi Mungu anazijua siri za hawa wanaafiki.
Basi itakuwaje Malaika watakapo wafisha wakawa wanawapiga nyuso zao na migongo yao!
Hiyo ndiyo hali katika maisha ya duniani, basi watakuwa katika hali gani Malaika watapo wafisha huku wakiwapiga nyuso zao na migongo yao kwa kuwadhalilisha?
Hayo ni kwa sababu wao waliyafuata yaliyo mchukiza Mwenyezi Mungu na wakachukia yanayo mridhisha, basi akaviangusha vitendo vyao.
Kufishwa namna hiyo ya kutisha katika hali hiyo ni kwa kuwa hakika wao waliufuata upotovu ulio mkasirisha Mwenyezi Mungu, na wakaichukia Haki inayo mpendeza Mwenyezi Mungu. Basi akayabat'ilisha waliyo yatenda.
Na tungeli penda tungeli kuonyesha hao na ungeli watambua kwa alama zao; lakini bila ya shaka utawajua kwa namna ya msemo wao. Na Mwenyezi Mungu anavijua vitendo vyenu.
Tungeli penda bila ya shaka tungeli kuonyesha hao wanaafiki, nawe ungeli wajua kwa alama zao, na ungeli wajua kwa namna yao wanavyo sema. Na Mwenyezi Mungu anajua ukweli wa vitendo vyenu vyote.
Na bila ya shaka tutakujaribuni mpaka tuwadhihirishe wapignao Jihadi katika nyinyi na wanao subiri. Nasi tutazifanyia mtihani khabari zenu.
Na ninaapa: Bila ya shaka tutakujaribuni kama kukufanyieni mtihani, mpaka tuwajue Mujaahidina, wanao pigana kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, katika nyinyi, na wenye kuvumilia wakati wa shida na dhiki, na tuzijue khabari zenu za ut'iifu na maasi katika Jihadi na penginepo.
Kwa hakika walio kufuru na wakazuilia njia ya Mwenyezi Mungu na wakapinzana na Mtume baada ya kwisha wabainikia uwongofu, hao hawatamdhuru Mwenyezi Mungu kwa lolote. Naye ataviangusha vitendo vyao.
Hakika walio kufuru na wakazuia njia ya Mwenyezi Mungu, na wakenda kinyume na Mtume kwa inda na ukaidi, baada ya kwisha wadhihirikia uwongofu, hao hawatamdhuru Mwenyezi Mungu kwa lolote. Na Yeye atayabat'ilisha yote waliyo yatenda.
Basi msiregee na kutaka suluhu, maana nyinyi ndio mtakao shinda. Na Mwenyezi Mungu yu pamoja nanyi, wala hatakunyimeni malipo ya vitendo vyenu.
Basi msijifanye wanyonge mbele ya maadui zenu mnapo kutana nao. Wala msiwatake suluhu kwa kuwaogopa, na hali nyinyi ndio mko juu, na ni wenye kushinda kwa nguvu za Imani. Na Mwenyezi Mungu yu pamoja nanyi kwa nusra yake; na wala hatakupunguzieni malipo ya vitendo vyenu.
Hakika uhai wa duniani ni mchezo na pumbao. Na mkiamini na mkamchamngu Mwenyezi Mungu atakupeni ujira wenu, wala hakutakeni mali yenu.
Hakika uhai wa dunia ni upotovu na udanganyifu. Na nyinyi mkiamini na mkaacha maasi, na mkafanya kheri, Mwenyezi Mungu atakupeni thawabu ya hayo, wala hakutakini mali yenu. Akikutakeni na akakushikilieni basi nyinyi mtafanya uchoyo, na chuki zenu zitaonekana kwa mnavyo yapenda mali.
Angalieni! Nyinyi mnaitwa mtumie katika njia ya Mwenyezi Mungu, na wapo katika nyinyi wanao fanya ubakhili. Na anaye fanya ubakhili basi anajifanyia ubakhili mwenyewe. Na Mwenyezi Mungu si mhitaji, na nyinyi ndio wahitaji. Na mkigeuka atawaleta watu wengine badala yenu, nao hawatakuwa kama nyinyi.
Hivi mnaitwa mtumie katika njia ya Mwenyezi Mungu aliyo iamrisha. Kati yenu wapo wanao fanya ubakhili kutoa. Na mwenye kufanya ubakhili hamdhuru mtu ila nafsi yake. Na Mwenyezi Mungu peke yake ndiye tajiri, hana haja ya mtu, na nyinyi ndio mafakiri wenye kumhitajia Yeye. Na mkiacha kumt'ii Mwenyezi Mungu basi atakubadilisheni pahala penu awalete watu wengine, tena hao hawatakuwa mfano wenu wa kuacha kumt'ii.
Contents of the translations can be downloaded and re-published, with the following terms and conditions:
1. No modification, addition, or deletion of the content.
2. Clearly referring to the publisher and the source (QuranEnc.com).
3. Mentioning the version number when re-publishing the translation.
4. Keeping the transcript information inside the document.
5. Notifying the source (QuranEnc.com) of any note on the translation.
6. Updating the translation according to the latest version issued from the source (QuranEnc.com).
7. Inappropriate advertisements must not be included when displaying translations of the meanings of the Noble Quran.
Zoekresultaten:
API specs
Endpoints:
Sura translation
GET / https://quranenc.com/api/v1/translation/sura/{translation_key}/{sura_number} description: get the specified translation (by its translation_key) for the speicified sura (by its number)
Parameters: translation_key: (the key of the currently selected translation) sura_number: [1-114] (Sura number in the mosshaf which should be between 1 and 114)
Returns:
json object containing array of objects, each object contains the "sura", "aya", "translation" and "footnotes".
GET / https://quranenc.com/api/v1/translation/aya/{translation_key}/{sura_number}/{aya_number} description: get the specified translation (by its translation_key) for the speicified aya (by its number sura_number and aya_number)
Parameters: translation_key: (the key of the currently selected translation) sura_number: [1-114] (Sura number in the mosshaf which should be between 1 and 114) aya_number: [1-...] (Aya number in the sura)
Returns:
json object containing the "sura", "aya", "translation" and "footnotes".