Check out the new design

Vertaling van de betekenissen Edele Qur'an - Swahili vertaling - Centrum van Pionierende Vertalers * - Index van vertaling


Vertaling van de betekenissen Surah: el-Araf   Vers:
وَلَوۡ أَنَّ أَهۡلَ ٱلۡقُرَىٰٓ ءَامَنُواْ وَٱتَّقَوۡاْ لَفَتَحۡنَا عَلَيۡهِم بَرَكَٰتٖ مِّنَ ٱلسَّمَآءِ وَٱلۡأَرۡضِ وَلَٰكِن كَذَّبُواْ فَأَخَذۡنَٰهُم بِمَا كَانُواْ يَكۡسِبُونَ
Na lau kuwa watu wa miji wangeliamini na wakamcha Mungu, basi hakika tungeliwafungulia baraka za kutoka mbinguni na ardhi. Lakini walikadhibisha, basi tukawachukua kwa sababu ya yale waliyokuwa wakiyachuma.
Arabische uitleg van de Qur'an:
أَفَأَمِنَ أَهۡلُ ٱلۡقُرَىٰٓ أَن يَأۡتِيَهُم بَأۡسُنَا بَيَٰتٗا وَهُمۡ نَآئِمُونَ
Je, wakazi wa vijijini wana amani ya kuwa iwajie adhabu yetu usiku hali ya kuwa wamelala?
Arabische uitleg van de Qur'an:
أَوَأَمِنَ أَهۡلُ ٱلۡقُرَىٰٓ أَن يَأۡتِيَهُم بَأۡسُنَا ضُحٗى وَهُمۡ يَلۡعَبُونَ
Au wakazi wa vijijini wana amani ya kuwa iwajie adhabu yetu mchana hali ya kuwa wanacheza?
Arabische uitleg van de Qur'an:
أَفَأَمِنُواْ مَكۡرَ ٱللَّهِۚ فَلَا يَأۡمَنُ مَكۡرَ ٱللَّهِ إِلَّا ٱلۡقَوۡمُ ٱلۡخَٰسِرُونَ
Je, wana amani dhidi ya mipango ya Mwenyezi Mungu? Kwani hawawi na amani dhidi ya mipango ya Mwenyezi Mungu isipokuwa kaumu waliohasiri.
Arabische uitleg van de Qur'an:
أَوَلَمۡ يَهۡدِ لِلَّذِينَ يَرِثُونَ ٱلۡأَرۡضَ مِنۢ بَعۡدِ أَهۡلِهَآ أَن لَّوۡ نَشَآءُ أَصَبۡنَٰهُم بِذُنُوبِهِمۡۚ وَنَطۡبَعُ عَلَىٰ قُلُوبِهِمۡ فَهُمۡ لَا يَسۡمَعُونَ
Kwani haijawabainikia wale wanaoirithi ardhi baada ya wale wenyewe kwamba tukitaka tunawasibu kwa madhambi yao, na tukaziba nyoyo zao, kwa hivyo hawatasikia?
Arabische uitleg van de Qur'an:
تِلۡكَ ٱلۡقُرَىٰ نَقُصُّ عَلَيۡكَ مِنۡ أَنۢبَآئِهَاۚ وَلَقَدۡ جَآءَتۡهُمۡ رُسُلُهُم بِٱلۡبَيِّنَٰتِ فَمَا كَانُواْ لِيُؤۡمِنُواْ بِمَا كَذَّبُواْ مِن قَبۡلُۚ كَذَٰلِكَ يَطۡبَعُ ٱللَّهُ عَلَىٰ قُلُوبِ ٱلۡكَٰفِرِينَ
Vijiji hivyo, tunakusimulia katika habari zake. Na hakika waliwajia Mitume wao na hoja zilizo waziwazi. Lakini hawakuwa wenye kuamini yale waliyoyakadhibisha zamani. Namna hivi ndivyo Mwenyezi Mungu anavyoziba kwenye nyoyo za makafiri.
Arabische uitleg van de Qur'an:
وَمَا وَجَدۡنَا لِأَكۡثَرِهِم مِّنۡ عَهۡدٖۖ وَإِن وَجَدۡنَآ أَكۡثَرَهُمۡ لَفَٰسِقِينَ
Wala hatukuwapata wengi wao wakiwa ni wenye ahadi yoyote, bali kwa hakika tuliwapata wengi wao ni wavukao mno mipaka.
Arabische uitleg van de Qur'an:
ثُمَّ بَعَثۡنَا مِنۢ بَعۡدِهِم مُّوسَىٰ بِـَٔايَٰتِنَآ إِلَىٰ فِرۡعَوۡنَ وَمَلَإِيْهِۦ فَظَلَمُواْ بِهَاۖ فَٱنظُرۡ كَيۡفَ كَانَ عَٰقِبَةُ ٱلۡمُفۡسِدِينَ
Kisha tukamtuma baada yao Musa na Ishara zetu kwa Firauni na waheshimiwa wake. Nao wakazifanyia dhuluma. Basi tazama namna ulivyokuwa mwisho wa waharibifu.
Arabische uitleg van de Qur'an:
وَقَالَ مُوسَىٰ يَٰفِرۡعَوۡنُ إِنِّي رَسُولٞ مِّن رَّبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ
Na Musa akasema, "Ewe Firauni! Hakika mimi ni Mtume kutoka kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote "
Arabische uitleg van de Qur'an:
 
Vertaling van de betekenissen Surah: el-Araf
Surah's Index Pagina nummer
 
Vertaling van de betekenissen Edele Qur'an - Swahili vertaling - Centrum van Pionierende Vertalers - Index van vertaling

Vertaald door het vertaalteam van het Centrum van Pionierende Vertalers in samenwerking met de Vereniging voor Da'wa in Al-Rabwa en de Vereniging voor de Dienstverlening van Islamitische Inhoud in Talen.

Sluit