Check out the new design

د قرآن کریم د معناګانو ژباړه - سواحلي ژباړه - عبد الله محمد او ناصر خمیس * - د ژباړو فهرست (لړلیک)


د معناګانو ژباړه سورت: هود   آیت:
فَلَا تَكُ فِي مِرۡيَةٖ مِّمَّا يَعۡبُدُ هَٰٓؤُلَآءِۚ مَا يَعۡبُدُونَ إِلَّا كَمَا يَعۡبُدُ ءَابَآؤُهُم مِّن قَبۡلُۚ وَإِنَّا لَمُوَفُّوهُمۡ نَصِيبَهُمۡ غَيۡرَ مَنقُوصٖ
Basi usiwe, ewe Mtume, katika shaka kuhusu ubatilifu wa vitu wanavyoviabudu washirikina hawa miongoni mwa watu wako. Wao hawaabudu, miongoni mwa masanamu, isipokuwa kama vile baba zao walikuwa wakiabudu huko nyuma. Na sisi ni wenye kuwatekelezea kile tulichowaahidi kikiwa kikamilifu kisichopunguzwa. Huu ni muelekezo kwa ummah wote, ingawa tamko lake limeelekezwa kwa Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani ziwashukie.
عربي تفسیرونه:
وَلَقَدۡ ءَاتَيۡنَا مُوسَى ٱلۡكِتَٰبَ فَٱخۡتُلِفَ فِيهِۚ وَلَوۡلَا كَلِمَةٞ سَبَقَتۡ مِن رَّبِّكَ لَقُضِيَ بَيۡنَهُمۡۚ وَإِنَّهُمۡ لَفِي شَكّٖ مِّنۡهُ مُرِيبٖ
Na hakika tulimpa Mūsā Kitabu , nacho ni Taurati, wakatafautiana watu wake juu yake: baadhi yao walikiamini na wengine walikikanusha, kama walivyofanya watu wako kuhusu Qur'ani. Na lao si neno lililotangulia kutoka kwa Mola wako la kutowaharakishia adhabu viumbe Wake, ingaliwashukia wao duniani kwao hukumu ya Mwenyezi Mungu ya kuwaangamiza wenye kukanusha na kuwaokoa Waumini. Na makafiri wa watu wako, miongoni mwa mayahudi na washirikina, ewe Mtume, wako kwenye shaka inayowatia wasiwasi juu hii Qur'ani.
عربي تفسیرونه:
وَإِنَّ كُلّٗا لَّمَّا لَيُوَفِّيَنَّهُمۡ رَبُّكَ أَعۡمَٰلَهُمۡۚ إِنَّهُۥ بِمَا يَعۡمَلُونَ خَبِيرٞ
Na hakika watu wote hao wanaotafautiana tuliokutajia habari zao , ewe Mtume, Mwenyezi Mungu Atawatekelezea malipo ya matendo yao Siku ya Kiyama, yakiwa mema watalipwa wema na yakiwa maovu watalipwa uovu. Hakika Mola wako , kwa wanayoyafanya hawa washirikina, ni Mtambuzi, hakuna kitendo chao chochote kinachofichamana Kwake. Katika hii pana kitisho na onyo kwao.
عربي تفسیرونه:
فَٱسۡتَقِمۡ كَمَآ أُمِرۡتَ وَمَن تَابَ مَعَكَ وَلَا تَطۡغَوۡاْۚ إِنَّهُۥ بِمَا تَعۡمَلُونَ بَصِيرٞ
Basi kumana msimamo, ewe Nabii, kama Alivyokuamurisha Mola wako, wewe na waliotubia pamoja nawe, wala msikipite kile Alichowaekea mpaka Mwenyezi Mungu. Hakika Mola wenu, kwa matendo yote mnayoyafanya, ni Muoni, hakuna kitu kinachofichika Kwake, na Atawalipa nyinyi kwa hayo.
عربي تفسیرونه:
وَلَا تَرۡكَنُوٓاْ إِلَى ٱلَّذِينَ ظَلَمُواْ فَتَمَسَّكُمُ ٱلنَّارُ وَمَا لَكُم مِّن دُونِ ٱللَّهِ مِنۡ أَوۡلِيَآءَ ثُمَّ لَا تُنصَرُونَ
Wala msilemee upande wa hawa makafiri walio madhalimu, msije mkapatwa na Moto. Na hamna nyinyi msaidizi mwenye kuwanusuru na kusimamia mambo yenu isipokuwa Mwenyezi Mungu.
عربي تفسیرونه:
وَأَقِمِ ٱلصَّلَوٰةَ طَرَفَيِ ٱلنَّهَارِ وَزُلَفٗا مِّنَ ٱلَّيۡلِۚ إِنَّ ٱلۡحَسَنَٰتِ يُذۡهِبۡنَ ٱلسَّيِّـَٔاتِۚ ذَٰلِكَ ذِكۡرَىٰ لِلذَّٰكِرِينَ
Na tekeleza Swala, ewe Nabii, kwa njia ya ukamilifu katika ncha mbili za mchana: asubuhi na jioni, na katika nyakati za usiku. Kwani kufanya mema kunafuta dhambi zilizopita na kuondoa athari zake. Kuamrisha kusimamisha Swala na kueleza kwamba mema huondoa mabaya ni mawaidha kwa anayewaidhika nayo na akakumbuka.
عربي تفسیرونه:
وَٱصۡبِرۡ فَإِنَّ ٱللَّهَ لَا يُضِيعُ أَجۡرَ ٱلۡمُحۡسِنِينَ
Na usubiri, ew Nabii, juu ya hiyo Swala na juu ya makero unayoyakuta kutoka kwa washirina wa watu wako, kwani Mwenyezi Mungu Hapotezi malipo ya walio wema katika matendo yao.
عربي تفسیرونه:
فَلَوۡلَا كَانَ مِنَ ٱلۡقُرُونِ مِن قَبۡلِكُمۡ أُوْلُواْ بَقِيَّةٖ يَنۡهَوۡنَ عَنِ ٱلۡفَسَادِ فِي ٱلۡأَرۡضِ إِلَّا قَلِيلٗا مِّمَّنۡ أَنجَيۡنَا مِنۡهُمۡۗ وَٱتَّبَعَ ٱلَّذِينَ ظَلَمُواْ مَآ أُتۡرِفُواْ فِيهِ وَكَانُواْ مُجۡرِمِينَ
Si ilikuwa wapatikane, miongoni mwa vizazi viliyopita kabla yenu, wasalia wa watu wazuri walio wema wanaowakataza makafiri waache ukafiri wao na kufanya uharibifu katika ardhi. Hawakupatikana katika hao isipokuwa wachache miongoni mwa walioamini na Mwenyezi Mungu akawaokoa na adhabu Yake Alipowapatiliza madhalimu. Na waliozidhulumu nafsi zao, miongoni mwa watu wa kila ummah uliopita, walifuata ladha za duniani na anasa zake walizostareheshwa, na wakawa wahalifu, wenye kudhulumu kwa kufuata kwao starehe walizokuwa nazo, ndipo adhabu ikathibiti juu yao. Katika hii aya pana mazingatio na mawaidha kwa wanaofanya maasia miongoni mwa Waislamu, kwa kuwa hawaepukani na udhalimu wa nafsi zao.
عربي تفسیرونه:
وَمَا كَانَ رَبُّكَ لِيُهۡلِكَ ٱلۡقُرَىٰ بِظُلۡمٖ وَأَهۡلُهَا مُصۡلِحُونَ
Na hakuwa Mola wako, ewe Mtume, ni Mwenye kuuangamiza mji wowote miongoni mwa miji na hali watu wake ni wenye kufanya mambo mazuri katika ardhi, wenye kujiepusha na uharibifu na udhalimu; Yeye huwaangamiza wao kwa sababu ya udhalimu wao na uharibifu wao.
عربي تفسیرونه:
 
د معناګانو ژباړه سورت: هود
د سورتونو فهرست (لړلیک) د مخ نمبر
 
د قرآن کریم د معناګانو ژباړه - سواحلي ژباړه - عبد الله محمد او ناصر خمیس - د ژباړو فهرست (لړلیک)

ژباړوونکي: ډاکټر عبدالله محمد ابوبکر او شیخ ناصر خمیس.

بندول