Check out the new design

د قرآن کریم د معناګانو ژباړه - سواحلي ژباړه - عبد الله محمد او ناصر خمیس * - د ژباړو فهرست (لړلیک)


د معناګانو ژباړه سورت: طه   آیت:
فَتَعَٰلَى ٱللَّهُ ٱلۡمَلِكُ ٱلۡحَقُّۗ وَلَا تَعۡجَلۡ بِٱلۡقُرۡءَانِ مِن قَبۡلِ أَن يُقۡضَىٰٓ إِلَيۡكَ وَحۡيُهُۥۖ وَقُل رَّبِّ زِدۡنِي عِلۡمٗا
Ameepukana Mwenyezi Mungu, kutakata ni Kwake, na Amekuwa juu na ametakasika na kila upungufu, Aliye Mfalme Ambaye mamlaka Yake yamemtendesha nguvu kila mfalme na mjeuri, Mwenye kuendesha kila kitu, Ambaye Yeye Ndiye ukweli, na agizo Lake ni kweli, na onyo Lake ni kweli, na kila kitu kinachotoka Kwake ni kweli. Na usifanye haraka, ewe Mtume, ya kushindana na Jibrili katika kuipokea Qur’ani kabla hajaimaliza, na useme, «Mola wangu! Niongezee elimu juu ya ile uliyonifundisha.»
عربي تفسیرونه:
وَلَقَدۡ عَهِدۡنَآ إِلَىٰٓ ءَادَمَ مِن قَبۡلُ فَنَسِيَ وَلَمۡ نَجِدۡ لَهُۥ عَزۡمٗا
Na kwa hakika tulimuusia Ādam kabla hajakula kutoka kwenye ule mti, asile kutoka kwenye mti huo na tukamwambia kwamba Iblisi ni adui yako na mke wako, basi wasiwatoe nyinyi wawili kutoka Peponi, mkajasumbuka wewe na mke wako duniani. Basi Shetani akamshawishi, naye akamtii na akausahau wasia. Na hatukumpata na nia ya nguvu yenye kumfanya aitunze ile amri aliyopewa.
عربي تفسیرونه:
وَإِذۡ قُلۡنَا لِلۡمَلَٰٓئِكَةِ ٱسۡجُدُواْ لِأٓدَمَ فَسَجَدُوٓاْ إِلَّآ إِبۡلِيسَ أَبَىٰ
Na kumbuka, ewe Mtume, pindi tuliposema kuwaambia Malaika, «Msujudieni Ādam sijida ya maamkizi na kutoa heshima, nao wakatii na wakasujudu, lakini Iblisi alikataa kusujudu.
عربي تفسیرونه:
فَقُلۡنَا يَٰٓـَٔادَمُ إِنَّ هَٰذَا عَدُوّٞ لَّكَ وَلِزَوۡجِكَ فَلَا يُخۡرِجَنَّكُمَا مِنَ ٱلۡجَنَّةِ فَتَشۡقَىٰٓ
Tukasema, «Ewe Ādam! Kwa hakika, huyu Iblisi ni adui yako na mke wako, basi jihadharini naye na msimtii kwa kuniasi mimi, asije akawatoa Peponi ukasumbuka ukitolewa humo.
عربي تفسیرونه:
إِنَّ لَكَ أَلَّا تَجُوعَ فِيهَا وَلَا تَعۡرَىٰ
Hakika yako wewe, ewe Ādam, una neema ya kula kwenye Pepo hii na hutashikwa na njaa, na pia kuvaa na hutakaa tupu.
عربي تفسیرونه:
وَأَنَّكَ لَا تَظۡمَؤُاْ فِيهَا وَلَا تَضۡحَىٰ
na una neema ya kutoshikwa na kiu katika hii Pepo na kutopatwa na joto la jua.
عربي تفسیرونه:
فَوَسۡوَسَ إِلَيۡهِ ٱلشَّيۡطَٰنُ قَالَ يَٰٓـَٔادَمُ هَلۡ أَدُلُّكَ عَلَىٰ شَجَرَةِ ٱلۡخُلۡدِ وَمُلۡكٖ لَّا يَبۡلَىٰ
Hapo Shetani akamshawishi Ādam na akamwambia, «Je, nikushauri kwa kukuonesha mti ambao lau utakula kutoka mti huo utakaa milele na hutakufa na utakuwa na ufalme usiokoma na usiokatika?
عربي تفسیرونه:
فَأَكَلَا مِنۡهَا فَبَدَتۡ لَهُمَا سَوۡءَٰتُهُمَا وَطَفِقَا يَخۡصِفَانِ عَلَيۡهِمَا مِن وَرَقِ ٱلۡجَنَّةِۚ وَعَصَىٰٓ ءَادَمُ رَبَّهُۥ فَغَوَىٰ
Basi Ādam na Ḥawwā’ wakala kutoka kwenye mti ambao Mwenyezi Mungu Aliwakataza nao, na papo hapo tupu zao zikafunuka, na kabla ya hapo zilikuwa zimesitiriwa na macho yao hayazioni. Hapo wakawa wanakata majani ya miti ya Peponi na kujiambisa nayo ili kufinika tupu zao zilizowafunuka. Na Ādam alienda kinyume na amri ya Mola wake na akapotea kwa kula kutoka kwenye mti ambao Mwenyezi Mungu Alimkataza asiukaribie.
عربي تفسیرونه:
ثُمَّ ٱجۡتَبَٰهُ رَبُّهُۥ فَتَابَ عَلَيۡهِ وَهَدَىٰ
Kisha Mwenyezi Mungu Akamteua Ādam, Akamkaribisha, Akaikubali toba yake na Akamuongoza njia njema ya kuifuata.
عربي تفسیرونه:
قَالَ ٱهۡبِطَا مِنۡهَا جَمِيعَۢاۖ بَعۡضُكُمۡ لِبَعۡضٍ عَدُوّٞۖ فَإِمَّا يَأۡتِيَنَّكُم مِّنِّي هُدٗى فَمَنِ ٱتَّبَعَ هُدَايَ فَلَا يَضِلُّ وَلَا يَشۡقَىٰ
Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Akamwambia Ādam na Ḥawwā’ «Shukeni kutoka kwenye Pepo muende ardhini nyote pamoja na Iblisi, kwani nyinyi na yeye ni maadui. Mtakapojiwa na uongofu na maelezo kutoka kwangu, basi mwenye kufuata uongofu wangu na maelezo yangu na akayatumia yote mawili, yeye atakuwa amefuata usawa duniani na ataongoka, na hatasumbuka huko Akhera kwa kuteswa na Mwenyezi Mungu.
عربي تفسیرونه:
وَمَنۡ أَعۡرَضَ عَن ذِكۡرِي فَإِنَّ لَهُۥ مَعِيشَةٗ ضَنكٗا وَنَحۡشُرُهُۥ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ أَعۡمَىٰ
Na mwenye kuupa mgongo utajo wangu ambao ninamkumbusha nao, atakuwa na maisha ya dhiki na usumbufu katika uhai wa kilimwengu, hata kama inaonekana kuwa yeye ni miongoni mwa watu wa utajiri na nafasi, na kaburi yake itambana na aadhibiwe humo, na tutamfufua Siku ya Kiyama akiwa kipofu wa kutoona na wa hoja.
عربي تفسیرونه:
قَالَ رَبِّ لِمَ حَشَرۡتَنِيٓ أَعۡمَىٰ وَقَدۡ كُنتُ بَصِيرٗا
Atasema huyo mwenye kuupa mgongo utajo wa Mwenyezi Mungu , «Mola wangu! Kwa nini umenifufua nikiwa kipofu na hali nilikuwa nikiona duniani?»
عربي تفسیرونه:
 
د معناګانو ژباړه سورت: طه
د سورتونو فهرست (لړلیک) د مخ نمبر
 
د قرآن کریم د معناګانو ژباړه - سواحلي ژباړه - عبد الله محمد او ناصر خمیس - د ژباړو فهرست (لړلیک)

ژباړوونکي: ډاکټر عبدالله محمد ابوبکر او شیخ ناصر خمیس.

بندول