د قرآن کریم د معناوو ژباړه - سواحلي ژباړه - عبد الله محمد او ناصر خمیس

44 : 43

وَإِنَّهُۥ لَذِكۡرٞ لَّكَ وَلِقَوۡمِكَۖ وَسَوۡفَ تُسۡـَٔلُونَ

Na hii Qur’ani ni utukufu na ukumbusho kwako na kwa watu wako miongoni mwa washirikina wa kikureishi (na wengineo), kwa kuwa imeteremshwa kwa lugha yao, kwa kuwa wao wanaifahamu zaidi kuliko watu wengine, na kwa hivyo inatakiwa wawe ni watu wenye kusimama nayo zaidi, na ni wenye kufanya matendo yanayoambatana nayo zaidi. Na mtaulizwa, wewe na walio pamoja na wewe, kuhusu vile mlivyoshukuru kuletewa hiyo Qur’ani na mlivyoifanyia kazi. info
التفاسير: |
next

Az-Zukhruf

prev
:
0:00 0:00