Check out the new design

د قرآن کریم د معناګانو ژباړه - سواحلي ژباړه - علی محسن البرواني * - د ژباړو فهرست (لړلیک)

XML CSV Excel API
Please review the Terms and Policies

د معناګانو ژباړه سورت: صافات   آیت:

As-Saffat

وَٱلصَّٰٓفَّٰتِ صَفّٗا
Naapa kwa wanao jipanga kwa safu.
Naapa kwa mataifa katika viumbe vyangu, walio jipanga wenyewe kwa safu zilio sawa katika msimamo wa ibada na ut'iifu.
عربي تفسیرونه:
فَٱلزَّٰجِرَٰتِ زَجۡرٗا
Na kwa wenye kukataza mabaya.
Na kwa wanao zuia wanao pindukia mipaka kwa mzuio mkali, nidhamu ibakie, na ulimwengu uhifadhiwe.
عربي تفسیرونه:
فَٱلتَّٰلِيَٰتِ ذِكۡرًا
Na kwa wenye kusoma Ukumbusho.
Na kwa wenye kusoma Aya, na wanamdhukuru Mwenyezi Mungu kwa dhikri ya Tasbihi, Kumtakasa, na Kumhimidi, kumsifu.
عربي تفسیرونه:
إِنَّ إِلَٰهَكُمۡ لَوَٰحِدٞ
Hakika Mungu wenu bila ya shaka ni Mmoja.
Hakika Mungu wenu anaye faa kuabudiwa bila ya shaka ni Mmoja tu. Hana mshirika wake, kwa dhati, wala kitendo, wala sifa.
عربي تفسیرونه:
رَّبُّ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَمَا بَيۡنَهُمَا وَرَبُّ ٱلۡمَشَٰرِقِ
Mola Mlezi wa mbingu na ardhi, na yaliyomo kati yao, na ni Mola Mlezi wa mashariki zote.
Yeye - peke yake - ndiye Muumba mbingu na ardhi na viliomo baina yao, na ndiye Mwenye kupanga mambo, na ndiye Mwenye kutawala mashariki za kila chenye mashariki. Mwenyezi Mungu ndiye Muumba mbingu saba na viliomo baina yao, navyo ni hivyo vyombo vya mbinguni na nyota zake. Naye ndiye Mwenye kusimamisha, Mwenye kulinda vile vile juu ya mwahali zinapo chomozea jua na nyota zote. Na Yeye ndiye anaye vionyesha hivyo kila siku katika pahala huko upeo wa macho, kila siku pahala mbali na vilipo dhihiri siku iliyo tangulia. Na hayo ni kwa mwendo wa mpango wa jua maalumu kwa inavyo zunguka dunia juu ya msumari-kati wake kutoka magharibi kwendea mashariki kila siku na wakati huo huo inavyo lizunguka jua katika njia yake katika falaki. Na jua na nyota huonekana na wakaazi wa ardhi kila siku kama zinachomoza mwahala mbali mbali. Na kila ardhi ikigeuza mahala pake katika safari yake katika mbingu linaonekana jua linachomoza pahala pengine. Ukiliangalia jua kwa utulivu kuanzia mwishoni wa mwezi wa Machi, yaani linapo kuwa jua lipo kati ya mstari wa Ikweta mwanzo wa musimu wa Rabii, yaani Spring, kwa nusu ya kaskazini ya dunia, utaliona linachomoza pahala katika mashariki juu ya upeo wa macho. Kwa mwenye kupeleleza kila siku ikipita ataona kuchomoza kwake kunajongelea kaskazini. Na mwishoni mwa mwezi wa Juni utaona linachomozea mwisho wa kukaribia kaskazini. Kisha baada ya hapo utaliona jua linarejea linafuata kugeuka kule kule mpaka mwisho wa Septemba (wakati wa kuwa sawa wakati wa Khariif yaani Autumn) utaliona jua linachomoza pale pale lilipo chomoza mwanzo wa Machi. Kisha litaendelea kuelekea kusini kuchomoza kwake mpaka mwisho wa Desemba linakuwa linachomoza karibu kabisa na kusini. Baada ya hapo huanza tena kurejea kuelekea kaskazini mpaka limalize safari yake ya kufika kati sawa katika Rabii ya pili. Na safari hii yote inachukua siku 365 na robo siku. Na inaonekana kuwa nyota nazo zinachomoza mwahala mbali mbali katika upeo wa macho inapo kuwa dunia imo katika safari yake ya mbinguni, na khasa nyota za buruji (au vituo) 12 vinavyo pitiwa na jua katika mwendo wake wa mwaka.
عربي تفسیرونه:
إِنَّا زَيَّنَّا ٱلسَّمَآءَ ٱلدُّنۡيَا بِزِينَةٍ ٱلۡكَوَاكِبِ
Hakika Sisi tumeipamba mbingu ya karibu kwa pambo la nyota.
Sisi tumeipamba hii mbingu ya karibu na watu wa duniani kwa mapambo, nayo ni hizo nyota zinazong'ara, zenye ukubwa mbali mbali, na mwahala pao mbali mbali kwenye anga la ulimwengu kama ionekanavyo kwa macho.
عربي تفسیرونه:
وَحِفۡظٗا مِّن كُلِّ شَيۡطَٰنٖ مَّارِدٖ
Na kulinda na kila shet'ani a'si.
Na tukaihifadhi hiyo mbingu na kila shetani jabari aliye a'si.
عربي تفسیرونه:
لَّا يَسَّمَّعُونَ إِلَى ٱلۡمَلَإِ ٱلۡأَعۡلَىٰ وَيُقۡذَفُونَ مِن كُلِّ جَانِبٖ
Wasiweze kuwasikiliza viumbe watukufu. Na wanafukuzwa huko kila upande.
Hao majabari wa kishetani hawawezi kusikiliza yanayo pita katika ulimwengu wa Malaika. Na wao hupopolewa kwa kila kinacho faa cha kuwazuia.
عربي تفسیرونه:
دُحُورٗاۖ وَلَهُمۡ عَذَابٞ وَاصِبٌ
Wakifurushwa. Na wanayo adhabu ya kudumu.
Hufukuzwa hao kwa nguvu wasifikilie kuweza kusikiliza khabari za mbinguni. Na Akhera watapata adhabu kali ya kudumu.
عربي تفسیرونه:
إِلَّا مَنۡ خَطِفَ ٱلۡخَطۡفَةَ فَأَتۡبَعَهُۥ شِهَابٞ ثَاقِبٞ
Isipo kuwa anaye nyakua kitu kidogo, na mara humfwatia kimondo kinacho ng'ara.
Isipo kuwa anaye lipata neno moja hivi katika khabari za mbinguni kwa kuibia. Na huyo naye tunamwandama kwa mwenge wa moto unao murika anga kwa mwangaza wake, ukamuunguzilia mbali.
عربي تفسیرونه:
فَٱسۡتَفۡتِهِمۡ أَهُمۡ أَشَدُّ خَلۡقًا أَم مَّنۡ خَلَقۡنَآۚ إِنَّا خَلَقۡنَٰهُم مِّن طِينٖ لَّازِبِۭ
Hebu waulize: Je! Wao ni wenye umbo gumu zaidi au hao wengine tulio waumba. Hakika Sisi tuliwaumba wao kwa udongo unao nata.
Ewe Nabii! Hebu waulize hao wanao kanya kufufuliwa wanao ona hayawi hayo: Je! Kwani kuwaumba wao hawa ni kugumu zaidi au kuziumba mbingu, na ardhi, na nyota, na vyenginevyo, tulivyo viumba Sisi?
عربي تفسیرونه:
بَلۡ عَجِبۡتَ وَيَسۡخَرُونَ
Bali unastaajabu, na wao wanafanya maskhara.
Hakika Sisi tumewaumba wao kutokana na udongo unao gandana. Basi kwa nini wanaona ajabu kurejezwa tena wao?
عربي تفسیرونه:
وَإِذَا ذُكِّرُواْ لَا يَذۡكُرُونَ
Na wanapo kumbushwa hawakumbuki.
Na wanapo kabiliwa kwa dalili za uweza wa Mwenyezi Mungu kufufua, hata hawazishughulikii wakanufaika kwa hizo dalili.
عربي تفسیرونه:
وَإِذَا رَأَوۡاْ ءَايَةٗ يَسۡتَسۡخِرُونَ
Na wanapo ona Ishara, wanafanya maskhara.
Na wanapo ona ushahidi wa kuonyesha uweza wa Mwenyezi Mungu huitana wapate kupita mipaka katika kumkejeli.
عربي تفسیرونه:
وَقَالُوٓاْ إِنۡ هَٰذَآ إِلَّا سِحۡرٞ مُّبِينٌ
Na husema: Haya si chochote ila ni uchawi tu ulio dhaahiri.
Na makafiri husema juu ya Ishara zinazo onyesha uweza wa Mwenyezi Mungu: Haya tunayo yaona si chochote ila ni uchawi tu.
عربي تفسیرونه:
أَءِذَا مِتۡنَا وَكُنَّا تُرَابٗا وَعِظَٰمًا أَءِنَّا لَمَبۡعُوثُونَ
Ati tukisha kufa na tukawa udongo na mifupa ndio kweli tutafufuliwa?
Hivyo sisi tukisha kufa tukawa udongo na mafupa tutatolewa tena makaburini kwetu tuwe wahai?
عربي تفسیرونه:
أَوَءَابَآؤُنَا ٱلۡأَوَّلُونَ
Hata baba zetu wa zamani?
Sisi tuwe wahai, na pia watafufuliwa baba zetu wa zamani walio kufa kabla yetu, na wakapotea, na wakateketea?
عربي تفسیرونه:
قُلۡ نَعَمۡ وَأَنتُمۡ دَٰخِرُونَ
Sema: Naam! Hali nanyi ni madhalili.
Ewe Nabii! Waambie: Ndio mtafufuliwa nyote, nanyi ni madhalili na wanyonge.
عربي تفسیرونه:
فَإِنَّمَا هِيَ زَجۡرَةٞ وَٰحِدَةٞ فَإِذَا هُمۡ يَنظُرُونَ
Huko utapigwa ukelele mmoja tu! Na hapo ndio wataona!
Kwani hakika kufufuliwa ni Ukelele mmoja tu, mara wote watakuwa wahai wakiyaona waliyo ahidiwa.
عربي تفسیرونه:
وَقَالُواْ يَٰوَيۡلَنَا هَٰذَا يَوۡمُ ٱلدِّينِ
Watasema: Ole wetu! Hii ndiyo Siku ya Malipo.
Na washirikina watasema: Ee msiba wetu huu! Hii ndiyo Siku ya Hisabu na Malipo kwa a'mali zilio tendwa!
عربي تفسیرونه:
هَٰذَا يَوۡمُ ٱلۡفَصۡلِ ٱلَّذِي كُنتُم بِهِۦ تُكَذِّبُونَ
Hii ndiyo Siku ya Hukumu mliyo kuwa mkiikadhibisha.
Watajibiwa: Hii ndiyo Siku ya Hukumu na kufarikisha vitendo, mliyo kuwa mkiikadhibisha.
عربي تفسیرونه:
۞ ٱحۡشُرُواْ ٱلَّذِينَ ظَلَمُواْ وَأَزۡوَٰجَهُمۡ وَمَا كَانُواْ يَعۡبُدُونَ
Wakusanyeni walio dhulumu, na wake zao, na hao walio kuwa wakiwaabudu.
Enyi Malaika wangu! Wakusanyeni walio jidhulumu nafsi zao kwa kufuru, pamoja na wake zao wa kikafiri, na miungu yao waliyo kuwa wakiiabudu badala ya Mwenyezi Mungu, yakiwa masanamu au watu, na waonyesheni njia ya kwendea Motoni waingie humo.
عربي تفسیرونه:
مِن دُونِ ٱللَّهِ فَٱهۡدُوهُمۡ إِلَىٰ صِرَٰطِ ٱلۡجَحِيمِ
Badala ya Mwenyezi Mungu. Waongozeni njia ya Jahannamu!
Enyi Malaika wangu! Wakusanyeni walio jidhulumu nafsi zao kwa kufuru, pamoja na wake zao wa kikafiri, na miungu yao waliyo kuwa wakiiabudu badala ya Mwenyezi Mungu, yakiwa masanamu au watu, na waonyesheni njia ya kwendea Motoni waingie humo.
عربي تفسیرونه:
وَقِفُوهُمۡۖ إِنَّهُم مَّسۡـُٔولُونَ
Na wasimamisheni. Hakika hao watasailiwa:
Na wazuieni hapo hapo; kwani wao hakika watahojiwa juu ya imani zao na vitendo vyao.
عربي تفسیرونه:
 
د معناګانو ژباړه سورت: صافات
د سورتونو فهرست (لړلیک) د مخ نمبر
 
د قرآن کریم د معناګانو ژباړه - سواحلي ژباړه - علی محسن البرواني - د ژباړو فهرست (لړلیک)

علی محسن البرواني ژباړلې ده.

بندول