Na pale Ibrahim alipo mwambia baba yake, Azar: Unayafanya masanamu kuwa ni miungu? Hakika mimi nakuona wewe na watu wako mmo katika opotofu ulio wazi.
Na ewe Nabii! Kumbuka yaliyo kuwa pale Ibrahim alipo mwambia baba yake, Azar, naye ameudhika naye kwa kuwaabudu asiye kuwa Mwenyezi Mungu: Haikufalii wewe kuyafanya masanamu kuwa ni miungu. Hakika mimi nakuona wewe na kaumu yako walio nawe katika ibada hii, ni dhaahiri kuwa mko mbali na Njia ya Haki.
Na kadhaalika tulimwonyesha Ibrahim ufalme wa mbingu na ardhi, na ili awe miongoni mwa wenye yakini.
Kama alivyo ona Ibrahim - kwa tawfiqi yetu - upotovu wa watu wake katika kuyafanya masanamu ndio miungu, kadhaalika tumemwonyesha ufalme wetu mkubwa wa mbinguni na duniani na viliomo humo, ili aweze kusimamisha hoja kwa watu wake, na ili azidi kuamini.
Alipo uona mwezi unachomoza alisema: Huyu ndiye Mola Mlezi wangu. Ulipotua akasema: Kama Mola Mlezi wangu hakuniongoa, nitakuwa katika kaumu walio potea.
Alipo uona mwezi umechomoza baada ya hayo, akasema akijiambia mwenyewe: Huyu ndiye Mola wangu Mlezi. Ulipo ondoka mwezi, na kukadhihiri kuvunjika ungu wake, akasema ili kuzielekeza nafsi zao ziombe hidaya: Ninaapa, kama Mola Mlezi wangu hakunihidi kwenye Haki, basi hapana shaka nitakuwa katika watu wanao babaika, (wasio jua mojapo la kulishika).
Na alipo liona jua linachomoza akasema: Huyu ndiye Mola Mlezi wangu. Huyu mkubwa kuliko wote. Lilipo tua, alisema: Enyi watu wangu! Mimi simo katika hayo mnayo fanyia ushirikina.
Tena baada ya hayo, akaliona jua linachomoza. Akasema: Huyu ndiye Mola Mlezi wangu, kwani huyu ni mkubwa kuliko nyota zinavyo onekana. Lilipo kuchwa, likapotea, akasema: Enyi watu wangu! Mimi simo katika kumshirikisha kwenu Mwenyezi Mungu na masanamu kwa kuyaabudu.
Hakika mimi nimeuelekeza uso wangu sawa sawa kwa aliye ziumba mbingu na ardhi, wala mimi si miongoni mwa washirikina.
Alipo kwisha ona udhaifu wa viumbe alimuelekea aliye viumba, akisema: Mimi nimeyaelekeza makusudio yangu kwa kumuabudu Mwenyezi Mungu pekee, ambaye ndiye aliye ziumba mbingu na ardhi. Nimejitenga na kila njia isipo kuwa Njia yake Yeye tu. Wala mimi, baada ya nilivyo kwisha ona dalili za Tawhidi (Umoja wa Allah), si katika wanao ridhia kuwa miongoni mwa washirikina kama wao.
Na watu wake wakamhoji. Akasema: Je, mnanihoji juu ya Mwenyezi Mungu, na hali Yeye ameniongoa? Wala siogopi hao mnao washirikisha naye, ila Mola wangu Mlezi akipenda kitu. Mola wangu Mlezi amekusanya ilimu ya kila kitu. Basi je, hamkumbuki?
Na juu ya hivyo, watu wake walijadiliana naye katika Umoja wa Mwenyezi Mungu, na wakamtisha kuwa atapata ghadhabu ya miungu yao. Basi yeye akawaambia: Haikufaliini nyinyi kuzozana nami katika Umoja wa Mwenyezi Mungu, naye amekwisha nihidi kufikia Haki. Wala siogopi ghadhabu ya miungu yenu mnayo ifanya ni washirika wa Mwenyezi Mungu. Lakini Mola wangu Mlezi akipenda madhara yatatokea, kwa kuwa Yeye pekee ndiye Muweza. Naye Mola wangu Mlezi amekusanya ilimu ya vitu vyote, na hao miungu yenu haina chochote inacho jua! Je, mmeghafilika na yote hayo, na hamtambui kuwa mjinga aliye emewa hastahiki kuabudiwa?
Na vipi nivikhofu hivyo mnavyo vishirikisha, hali nyinyi hamkhofu kuwa nyinyi mmemshirikisha Mwenyezi Mungu na kitu ambacho hakukiteremshia uthibitisho. Basi kundi gani katika mawili haya lina haki zaidi kupata amani, kama nyinyi mnajua?
Na katika ajabu ni kuwa mimi niiogope hiyo miungu yenu ya uwongo, na nyinyi hamna khofu kuwa pamoja na Mwenyezi Mungu iliyo simama ushahidi wa Umoja wake, nyinyi mna shiriki kuabudu vitu ambavyo havina ushahidi kuwa vinastahiki kuabudiwa. Basi katika hali hii kikundi gani baina ya sisi chenye haki ya utulivu na amani, ikiwa kweli nyinyi mnaijua Haki na mnaitambua?
Contents of the translations can be downloaded and re-published, with the following terms and conditions:
1. No modification, addition, or deletion of the content.
2. Clearly referring to the publisher and the source (QuranEnc.com).
3. Mentioning the version number when re-publishing the translation.
4. Keeping the transcript information inside the document.
5. Notifying the source (QuranEnc.com) of any note on the translation.
6. Updating the translation according to the latest version issued from the source (QuranEnc.com).
7. Inappropriate advertisements must not be included when displaying translations of the meanings of the Noble Quran.
د لټون پایلې:
API specs
Endpoints:
Sura translation
GET / https://quranenc.com/api/v1/translation/sura/{translation_key}/{sura_number} description: get the specified translation (by its translation_key) for the speicified sura (by its number)
Parameters: translation_key: (the key of the currently selected translation) sura_number: [1-114] (Sura number in the mosshaf which should be between 1 and 114)
Returns:
json object containing array of objects, each object contains the "sura", "aya", "translation" and "footnotes".
GET / https://quranenc.com/api/v1/translation/aya/{translation_key}/{sura_number}/{aya_number} description: get the specified translation (by its translation_key) for the speicified aya (by its number sura_number and aya_number)
Parameters: translation_key: (the key of the currently selected translation) sura_number: [1-114] (Sura number in the mosshaf which should be between 1 and 114) aya_number: [1-...] (Aya number in the sura)
Returns:
json object containing the "sura", "aya", "translation" and "footnotes".