Check out the new design

د قرآن کریم د معناګانو ژباړه - سواحلي ژباړه - د رواد الترجمې مرکز * - د ژباړو فهرست (لړلیک)


د معناګانو ژباړه سورت: انفال   آیت:
۞ وَٱعۡلَمُوٓاْ أَنَّمَا غَنِمۡتُم مِّن شَيۡءٖ فَأَنَّ لِلَّهِ خُمُسَهُۥ وَلِلرَّسُولِ وَلِذِي ٱلۡقُرۡبَىٰ وَٱلۡيَتَٰمَىٰ وَٱلۡمَسَٰكِينِ وَٱبۡنِ ٱلسَّبِيلِ إِن كُنتُمۡ ءَامَنتُم بِٱللَّهِ وَمَآ أَنزَلۡنَا عَلَىٰ عَبۡدِنَا يَوۡمَ ٱلۡفُرۡقَانِ يَوۡمَ ٱلۡتَقَى ٱلۡجَمۡعَانِۗ وَٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٌ
Na jueni ya kwamba ngawira yoyote mnayoipata, basi humusi yake ni ya Mwenyezi Mungu na ni ya Mtume, na ni ya jamaa, na mayatima, na masikini, na wasafiri, ikiwa nyinyi mlimwamini Mwenyezi Mungu na yale tuliyoyateremsha kwa mja wetu siku ya kipambanuo, siku yalipokutana makundi yale mawili. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu.
عربي تفسیرونه:
إِذۡ أَنتُم بِٱلۡعُدۡوَةِ ٱلدُّنۡيَا وَهُم بِٱلۡعُدۡوَةِ ٱلۡقُصۡوَىٰ وَٱلرَّكۡبُ أَسۡفَلَ مِنكُمۡۚ وَلَوۡ تَوَاعَدتُّمۡ لَٱخۡتَلَفۡتُمۡ فِي ٱلۡمِيعَٰدِ وَلَٰكِن لِّيَقۡضِيَ ٱللَّهُ أَمۡرٗا كَانَ مَفۡعُولٗا لِّيَهۡلِكَ مَنۡ هَلَكَ عَنۢ بَيِّنَةٖ وَيَحۡيَىٰ مَنۡ حَيَّ عَنۢ بَيِّنَةٖۗ وَإِنَّ ٱللَّهَ لَسَمِيعٌ عَلِيمٌ
Kumbukeni pale mlipokuwa nyinyi kwenye ng'ambo ya karibu ya bonde, na wao wakawa kwenye ng'ambo ya mbali, na msafara ulipokuwa chini yenu. Na ingelikuwa mliagana, basi mngelihitalifiana katika miadi. Lakini (mkakutana) ili Mwenyezi Mungu atimize jambo liliokuwa lazima litendwe. Ili aangamie wa kuangamia kwa ushahidi ulio wazi, na asalimike wa kusalimika kwa ushahidi ulio wazi. Na hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia vyema, Mwenye kujua yote.
عربي تفسیرونه:
إِذۡ يُرِيكَهُمُ ٱللَّهُ فِي مَنَامِكَ قَلِيلٗاۖ وَلَوۡ أَرَىٰكَهُمۡ كَثِيرٗا لَّفَشِلۡتُمۡ وَلَتَنَٰزَعۡتُمۡ فِي ٱلۡأَمۡرِ وَلَٰكِنَّ ٱللَّهَ سَلَّمَۚ إِنَّهُۥ عَلِيمُۢ بِذَاتِ ٱلصُّدُورِ
Kumbuka Mwenyezi Mungu alipokuonyesha wao katika usingizi wako kwamba wao ni wachache, na lau angelikuonyesha kuwa ni wengi, basi mngeliingiwa na woga, na mngelizozana katika jambo hilo. Lakini Mwenyezi Mungu akawapa salama. Hakika Yeye ni Mwenye kuyajua vyema yaliyo vifuani.
عربي تفسیرونه:
وَإِذۡ يُرِيكُمُوهُمۡ إِذِ ٱلۡتَقَيۡتُمۡ فِيٓ أَعۡيُنِكُمۡ قَلِيلٗا وَيُقَلِّلُكُمۡ فِيٓ أَعۡيُنِهِمۡ لِيَقۡضِيَ ٱللَّهُ أَمۡرٗا كَانَ مَفۡعُولٗاۗ وَإِلَى ٱللَّهِ تُرۡجَعُ ٱلۡأُمُورُ
Na alipowaonyesha mlipokutana, katika macho yenu kuwa wao ni wachache, na akawafanya nyinyi ni wachache katika macho yao, ili Mwenyezi Mungu atimize jambo lililokuwa lifanywe. Na kwa Mwenyezi Mungu yatarejeshwa mambo yote.
عربي تفسیرونه:
يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ إِذَا لَقِيتُمۡ فِئَةٗ فَٱثۡبُتُواْ وَٱذۡكُرُواْ ٱللَّهَ كَثِيرٗا لَّعَلَّكُمۡ تُفۡلِحُونَ
Enyi mlioamini! Mkikutana na kikundi, basi kueni imara, na mkumbukeni Mwenyezi Mungu sana ili mfaulu.
عربي تفسیرونه:
 
د معناګانو ژباړه سورت: انفال
د سورتونو فهرست (لړلیک) د مخ نمبر
 
د قرآن کریم د معناګانو ژباړه - سواحلي ژباړه - د رواد الترجمې مرکز - د ژباړو فهرست (لړلیک)

دا ژباړه د مرکز رواد الترجمة ټیم لخوا د ربوہ د تبلیغ ټولنې او د اسلامي منځپانګې د خدماتو ټولنې په همکارۍ شوې.

بندول