Check out the new design

Tradução dos significados do Nobre Qur’an. - Tradução Suaíli - Abdullah Muhammad e Nasser Khamis * - Índice de tradução


Tradução dos significados Surah: Al-Araaf   Versículo:
قُل لَّآ أَمۡلِكُ لِنَفۡسِي نَفۡعٗا وَلَا ضَرًّا إِلَّا مَا شَآءَ ٱللَّهُۚ وَلَوۡ كُنتُ أَعۡلَمُ ٱلۡغَيۡبَ لَٱسۡتَكۡثَرۡتُ مِنَ ٱلۡخَيۡرِ وَمَا مَسَّنِيَ ٱلسُّوٓءُۚ إِنۡ أَنَا۠ إِلَّا نَذِيرٞ وَبَشِيرٞ لِّقَوۡمٖ يُؤۡمِنُونَ
Sema, ewe Mtume, «Siwezi kuiletea mema nafsi yangu wala kuiepushia shari yenye kuifikia, isipokuwa iwapo Mwenyezi Mungu Alitaka. Na lau mimi ningalikuwa najua yaliyofichika ningalifanya njia ambazo najua kwamba zitaniongezea maslahi na manufaa na ningalijikinga na shari yenye kuwa kabla haijatukia. Mimi si yoyote isipokuwa ni mjumbe wa Mwenyezi Mungu, Amenituma kwenu, naogopesha mateso Yake na natoa bishara njema ya thawabu Zake kuwalipa watu wanaoamini kuwa mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na wakafuata sheria Yake kivitendo.
Os Tafssir em língua árabe:
۞ هُوَ ٱلَّذِي خَلَقَكُم مِّن نَّفۡسٖ وَٰحِدَةٖ وَجَعَلَ مِنۡهَا زَوۡجَهَا لِيَسۡكُنَ إِلَيۡهَاۖ فَلَمَّا تَغَشَّىٰهَا حَمَلَتۡ حَمۡلًا خَفِيفٗا فَمَرَّتۡ بِهِۦۖ فَلَمَّآ أَثۡقَلَت دَّعَوَا ٱللَّهَ رَبَّهُمَا لَئِنۡ ءَاتَيۡتَنَا صَٰلِحٗا لَّنَكُونَنَّ مِنَ ٱلشَّٰكِرِينَ
Yeye Ndiye ambaye Aliyewaumba nyinyi, enyi watu, kutokana na nafsi moja, nayo ni Ādam, amani imshukiye. Na akaumba kutokana na nafsi hiyo ya pili yake, nayo ni Ḥawwā’, ili aliwazike naye na ajitulize. Alipomuundama - makusudio ni jinsi ya mke na mume miongoni mwa kizazi cha Ādam - alibeba maji mapesi, akainuka nayo na akakaa nayo mpaka mimba ikatimia. Kilipokaribia kipindi cha kuzaa kwake na akawa mzito, walimuomba, mume na mke, Mola wao, «Tunaapa lau utatupatia mwanadamu aliye sawa, aliye mwema, hakika tutakuwa ni wenye kukushukuru kwa kutupa mtoto mwema.»
Os Tafssir em língua árabe:
فَلَمَّآ ءَاتَىٰهُمَا صَٰلِحٗا جَعَلَا لَهُۥ شُرَكَآءَ فِيمَآ ءَاتَىٰهُمَاۚ فَتَعَٰلَى ٱللَّهُ عَمَّا يُشۡرِكُونَ
Mwenyezi Mungu Alipowaruzuku, yule mume na mke, mtoto mwema walimfanyia Mwenyezi Mungu washirika katika mtoto yule ambaye Mwenyezi Mungu Alipwekeka katika kumuumba wakamfanya ni mja wa asiyekuwa Mwenyezi Mungu; Ametukukuka Mwenyezi Mungu na Ameepukana na kila mshirika.
Os Tafssir em língua árabe:
أَيُشۡرِكُونَ مَا لَا يَخۡلُقُ شَيۡـٔٗا وَهُمۡ يُخۡلَقُونَ
Je, washirikina hawa wawashirikisha viumbe vya Mwenyezi Mungu katika ibada ya Mwenyezi Mungu, hali washirikishwa hao hawawezi kuumba chochote, bali wao wameumbwa?
Os Tafssir em língua árabe:
وَلَا يَسۡتَطِيعُونَ لَهُمۡ نَصۡرٗا وَلَآ أَنفُسَهُمۡ يَنصُرُونَ
Wala hawawezi kuwanusuru wenye kuwaabudu au kuzilinda nafsi zao na ubaya. Iwapo wao hawaumbi kitu, bali wao wameumbwa na hawawezi kuwalinda wanaowaabudu, wasipatikane na mambo wanayoyachukia, wala kuzilinda nafsi zao. Basi vipi wanafanywa ni waungu? Huu haukuwa isipokuwa ni upeo wa udhalimu na upeo wa uchache wa akili.
Os Tafssir em língua árabe:
وَإِن تَدۡعُوهُمۡ إِلَى ٱلۡهُدَىٰ لَا يَتَّبِعُوكُمۡۚ سَوَآءٌ عَلَيۡكُمۡ أَدَعَوۡتُمُوهُمۡ أَمۡ أَنتُمۡ صَٰمِتُونَ
Na mnapowalingania, enyi washirikina, masanamu hawa ambao mliwaabudu badala ya Mwenyezi Mungu kwenye uongofu, hawasikii ulinganizi wenu wala hawawafuati nyinyi; inalingana sawa kuwalingania au kuwanyamazia. Kwani wao hawasikii wala hawaoni wala hawaongozi wala hawaongozwi.
Os Tafssir em língua árabe:
إِنَّ ٱلَّذِينَ تَدۡعُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ عِبَادٌ أَمۡثَالُكُمۡۖ فَٱدۡعُوهُمۡ فَلۡيَسۡتَجِيبُواْ لَكُمۡ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ
Kwa hakika wale ambao mnawaabudu badala ya Mwenyezi Mungu, enyi washirikina, wamemilikiwa na Mola wao, kama mlivyomilikiwa nyinyi na Mola wenu. Basi iwapo nyinyi, kama mnavyodai, ni wakweli kwamba wao wanastahiki wafayiwe chochote kile cha ibada, waiteni wawaitikie. Iwapo watawaitikia na watawapatia matakwa yenu, mtakuwa ni wakweli, na isipokuwa hivyo, itakuwa wazi kwamba nyinyi ni warongo mnamzulia Mwenyezi Mungu uzushi mkubwa kabisa.
Os Tafssir em língua árabe:
أَلَهُمۡ أَرۡجُلٞ يَمۡشُونَ بِهَآۖ أَمۡ لَهُمۡ أَيۡدٖ يَبۡطِشُونَ بِهَآۖ أَمۡ لَهُمۡ أَعۡيُنٞ يُبۡصِرُونَ بِهَآۖ أَمۡ لَهُمۡ ءَاذَانٞ يَسۡمَعُونَ بِهَاۗ قُلِ ٱدۡعُواْ شُرَكَآءَكُمۡ ثُمَّ كِيدُونِ فَلَا تُنظِرُونِ
Je, waungu hawa na masanamu wana miguu ya kutembelea na nyinyi katika haja zenu? Au wao wana mikono ya kuwatetea na kuwanusuru juu ya anayewatakia shari na maovu? Au wao wana macho ya kutazamia, wakapata kuwajulisha yale waliyoyashuhudia na wakayaona miongoni mwa yale yaliyofichika kwenu mkawa hamuyaoni? Au wao wana masikio ya kusikia kwayo, wapate kuwapa habari ya yale msiyoyasikia? Iwapo waungu wenu ambao mnawaabudu hawana vyombo hivi, kuna maana gani kuwaabudu, ilhali wao hawana vitu hivi ambavyo kwavyo kunapelekea kujipatia manufaa au kujiepushia madhara? Waambie, ewe Mtume, kuwaambia hawa washirikina wenye kuwaabudu masanamu, «Waiteni waungu wenu ambao mliwafanya ni washirika wa Mwenyezi Mungu katika ibada, kisha kusanyikeni kunifanyia ubaya na maudhi, msinipe muhula na lifanyieni haraka hilo, kwani mimi siwajali waungu wenu kwa kuwa nategemea hifadhi ya Mwenyezi Mungu Peke Yake.
Os Tafssir em língua árabe:
 
Tradução dos significados Surah: Al-Araaf
Índice de capítulos Número de página
 
Tradução dos significados do Nobre Qur’an. - Tradução Suaíli - Abdullah Muhammad e Nasser Khamis - Índice de tradução

Traduzido pelo Dr. Abdalla Mohamed Abubakar e Sheikh Nassor Khamis.

Fechar