Check out the new design

Tradução dos significados do Nobre Qur’an. - Tradução Suaíli - Centro de tradução Rawad * - Índice de tradução


Tradução dos significados Surah: Saba   Versículo:

Saba

ٱلۡحَمۡدُ لِلَّهِ ٱلَّذِي لَهُۥ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِ وَلَهُ ٱلۡحَمۡدُ فِي ٱلۡأٓخِرَةِۚ وَهُوَ ٱلۡحَكِيمُ ٱلۡخَبِيرُ
Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, ambaye ni vyake vyote vilivyo mbinguni na katika ardhi. Na sifa ni zake Yeye katika Akhera. Naye ni Mwenye hekima, Mwenye habari.
Os Tafssir em língua árabe:
يَعۡلَمُ مَا يَلِجُ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَمَا يَخۡرُجُ مِنۡهَا وَمَا يَنزِلُ مِنَ ٱلسَّمَآءِ وَمَا يَعۡرُجُ فِيهَاۚ وَهُوَ ٱلرَّحِيمُ ٱلۡغَفُورُ
Anajua yanayoingia katika ardhi na yanayotoka humo, na yanayoteremka kutoka mbinguni, na yanayopanda huko. Na Yeye ni Mwenye kurehemu, Mwenye kusamehe.
Os Tafssir em língua árabe:
وَقَالَ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ لَا تَأۡتِينَا ٱلسَّاعَةُۖ قُلۡ بَلَىٰ وَرَبِّي لَتَأۡتِيَنَّكُمۡ عَٰلِمِ ٱلۡغَيۡبِۖ لَا يَعۡزُبُ عَنۡهُ مِثۡقَالُ ذَرَّةٖ فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَلَا فِي ٱلۡأَرۡضِ وَلَآ أَصۡغَرُ مِن ذَٰلِكَ وَلَآ أَكۡبَرُ إِلَّا فِي كِتَٰبٖ مُّبِينٖ
Na walisema wale waliokufuru: "Haitatufikia Saa ya Kiyama." Sema: Kwani hapana shaka itakufikieni, ninaapa kwa haki ya Mola wangu Mlezi, Mwenye kujua ya ghaibu! Hapana kinachofichikana kwake hata chenye uzito wa chembe tu, si katika mbingu wala katika ardhi, wala kilicho kidogo kuliko hivyo, wala kikubwa zaidi, isipokuwa vyote hivyo vimo katika Kitabu chake chenye kubainisha.
Os Tafssir em língua árabe:
لِّيَجۡزِيَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّٰلِحَٰتِۚ أُوْلَٰٓئِكَ لَهُم مَّغۡفِرَةٞ وَرِزۡقٞ كَرِيمٞ
Ili awalipe wale walioamini na wakatenda mema. Hao watapata msamaha na riziki ya ukarimu.
Os Tafssir em língua árabe:
وَٱلَّذِينَ سَعَوۡ فِيٓ ءَايَٰتِنَا مُعَٰجِزِينَ أُوْلَٰٓئِكَ لَهُمۡ عَذَابٞ مِّن رِّجۡزٍ أَلِيمٞ
Na wale waliojitahidi kuzipinga Ishara zetu wakaona watashinda, hao watapata adhabu mbaya yenye uchungu.
Os Tafssir em língua árabe:
وَيَرَى ٱلَّذِينَ أُوتُواْ ٱلۡعِلۡمَ ٱلَّذِيٓ أُنزِلَ إِلَيۡكَ مِن رَّبِّكَ هُوَ ٱلۡحَقَّ وَيَهۡدِيٓ إِلَىٰ صِرَٰطِ ٱلۡعَزِيزِ ٱلۡحَمِيدِ
Na wale waliopewa elimu wanaona ya kuwa yale uliyoteremshiwa kutoka kwa Mola wako Mlezi ndiyo haki, nayo huongoa kwendea njia ya Mwenye nguvu, Mwenye kusifiwa.
Os Tafssir em língua árabe:
وَقَالَ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ هَلۡ نَدُلُّكُمۡ عَلَىٰ رَجُلٖ يُنَبِّئُكُمۡ إِذَا مُزِّقۡتُمۡ كُلَّ مُمَزَّقٍ إِنَّكُمۡ لَفِي خَلۡقٖ جَدِيدٍ
Na wale waliokufuru walisema: Je, tuwajulisheni mtu anayewaambieni kwamba mtakapochambuliwa mapande mapande mtakuwa katika umbo jipya?
Os Tafssir em língua árabe:
أَفۡتَرَىٰ عَلَى ٱللَّهِ كَذِبًا أَم بِهِۦ جِنَّةُۢۗ بَلِ ٱلَّذِينَ لَا يُؤۡمِنُونَ بِٱلۡأٓخِرَةِ فِي ٱلۡعَذَابِ وَٱلضَّلَٰلِ ٱلۡبَعِيدِ
Ama amemzulia Mwenyezi Mungu uongo, au ana wazimu. Bali wale wasioamini Akhera wamo adhabuni na upotofu wa mbali kabisa.
Os Tafssir em língua árabe:
أَفَلَمۡ يَرَوۡاْ إِلَىٰ مَا بَيۡنَ أَيۡدِيهِمۡ وَمَا خَلۡفَهُم مِّنَ ٱلسَّمَآءِ وَٱلۡأَرۡضِۚ إِن نَّشَأۡ نَخۡسِفۡ بِهِمُ ٱلۡأَرۡضَ أَوۡ نُسۡقِطۡ عَلَيۡهِمۡ كِسَفٗا مِّنَ ٱلسَّمَآءِۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَةٗ لِّكُلِّ عَبۡدٖ مُّنِيبٖ
Kwani hawaoni yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao, ya mbingu na ardhi? Tungelipenda, tungeliwadidimiza ndani ya ardhi, au tungeliwateremshia juu yao vipande vya mbingu. Hakika katika haya zipo Ishara kwa kila mja aliyetubia.
Os Tafssir em língua árabe:
۞ وَلَقَدۡ ءَاتَيۡنَا دَاوُۥدَ مِنَّا فَضۡلٗاۖ يَٰجِبَالُ أَوِّبِي مَعَهُۥ وَٱلطَّيۡرَۖ وَأَلَنَّا لَهُ ٱلۡحَدِيدَ
Na tulimpa Daudi fadhila kutoka kwetu, tukasema: "Enyi milima, karirini kumtakasa Mwenyezi Mungu pamoja naye! Na ndege pia." Na tukamlainishia chuma.
Os Tafssir em língua árabe:
أَنِ ٱعۡمَلۡ سَٰبِغَٰتٖ وَقَدِّرۡ فِي ٱلسَّرۡدِۖ وَٱعۡمَلُواْ صَٰلِحًاۖ إِنِّي بِمَا تَعۡمَلُونَ بَصِيرٞ
Tukamwambia: "Tengeneza nguo za chuma pana, na kadiria sawa katika kuunganisha. Na tendeni mema. Hakika Mimi nayaona vyema mnayoyatenda."
Os Tafssir em língua árabe:
وَلِسُلَيۡمَٰنَ ٱلرِّيحَ غُدُوُّهَا شَهۡرٞ وَرَوَاحُهَا شَهۡرٞۖ وَأَسَلۡنَا لَهُۥ عَيۡنَ ٱلۡقِطۡرِۖ وَمِنَ ٱلۡجِنِّ مَن يَعۡمَلُ بَيۡنَ يَدَيۡهِ بِإِذۡنِ رَبِّهِۦۖ وَمَن يَزِغۡ مِنۡهُمۡ عَنۡ أَمۡرِنَا نُذِقۡهُ مِنۡ عَذَابِ ٱلسَّعِيرِ
Naye Suleiman tuliufanya upepo umtumikie. Safari yake ya asubuhi ni mwendo wa mwezi mmoja, na safari yake ya jioni ni mwendo wa mwezi mmoja. Na tukamyeyushia chemichemi ya shaba. Na katika majini, walikuwako waliokuwa wakifanya kazi mbele yake kwa idhini ya Mola wake Mlezi. Na kila anayejitenga na amri yetu katika wao, tunamuonjesha adhabu ya Moto unaowaka.
Os Tafssir em língua árabe:
يَعۡمَلُونَ لَهُۥ مَا يَشَآءُ مِن مَّحَٰرِيبَ وَتَمَٰثِيلَ وَجِفَانٖ كَٱلۡجَوَابِ وَقُدُورٖ رَّاسِيَٰتٍۚ ٱعۡمَلُوٓاْ ءَالَ دَاوُۥدَ شُكۡرٗاۚ وَقَلِيلٞ مِّنۡ عِبَادِيَ ٱلشَّكُورُ
Walikuwa wakimfanyia alipendalo, kama mihrabu, na vitu vifananavyo vingine, na madeste makubwa kama mahodhi, na masufuria makubwa yaliyo madhubuti. Enyi watu wa Daudi, fanyeni kazi kwa kushukuru. Na ni wachache katika waja wangu wanaoshukuru.
Os Tafssir em língua árabe:
فَلَمَّا قَضَيۡنَا عَلَيۡهِ ٱلۡمَوۡتَ مَا دَلَّهُمۡ عَلَىٰ مَوۡتِهِۦٓ إِلَّا دَآبَّةُ ٱلۡأَرۡضِ تَأۡكُلُ مِنسَأَتَهُۥۖ فَلَمَّا خَرَّ تَبَيَّنَتِ ٱلۡجِنُّ أَن لَّوۡ كَانُواْ يَعۡلَمُونَ ٱلۡغَيۡبَ مَا لَبِثُواْ فِي ٱلۡعَذَابِ ٱلۡمُهِينِ
Na tulipomhukumia kufa, hapana aliyewajulisha kufa kwake ila mnyama wa ardhi aliyekula fimbo yake. Na alipoanguka, majini wakatambua lau kuwa wangelijua ya ghaibu wasingelikaa katika adhabu hiyo ya kufedhehesha.
Os Tafssir em língua árabe:
لَقَدۡ كَانَ لِسَبَإٖ فِي مَسۡكَنِهِمۡ ءَايَةٞۖ جَنَّتَانِ عَن يَمِينٖ وَشِمَالٖۖ كُلُواْ مِن رِّزۡقِ رَبِّكُمۡ وَٱشۡكُرُواْ لَهُۥۚ بَلۡدَةٞ طَيِّبَةٞ وَرَبٌّ غَفُورٞ
Hakika ilikuwepo Ishara kwa (watu wa nchi ya) Sabaa katika maskani yao - bustani mbili, kulia na kushoto. Kuleni katika riziki ya Mwenyezi Mungu, na mumshukuru. Mji mzuri na Mola Mlezi aliye Msamehevu.
Os Tafssir em língua árabe:
فَأَعۡرَضُواْ فَأَرۡسَلۡنَا عَلَيۡهِمۡ سَيۡلَ ٱلۡعَرِمِ وَبَدَّلۡنَٰهُم بِجَنَّتَيۡهِمۡ جَنَّتَيۡنِ ذَوَاتَيۡ أُكُلٍ خَمۡطٖ وَأَثۡلٖ وَشَيۡءٖ مِّن سِدۡرٖ قَلِيلٖ
Lakini wakayapa mgongo. Kwa hivyo, tukawatumia mafuriko makubwa, na tukawabadilishia badala ya bustani zao hizo kwa bustani nyingine zenye matunda makali, machungu, na mivinje, na kidogo katika miti ya kunazi.
Os Tafssir em língua árabe:
ذَٰلِكَ جَزَيۡنَٰهُم بِمَا كَفَرُواْۖ وَهَلۡ نُجَٰزِيٓ إِلَّا ٱلۡكَفُورَ
Hayo tuliwalipa kwa sababu ya walivyokufuru. Nasi kwani tunamuadhibu isipokuwa anayekufuru?
Os Tafssir em língua árabe:
وَجَعَلۡنَا بَيۡنَهُمۡ وَبَيۡنَ ٱلۡقُرَى ٱلَّتِي بَٰرَكۡنَا فِيهَا قُرٗى ظَٰهِرَةٗ وَقَدَّرۡنَا فِيهَا ٱلسَّيۡرَۖ سِيرُواْ فِيهَا لَيَالِيَ وَأَيَّامًا ءَامِنِينَ
Na baina yao na miji mingine tuliyoibariki tuliweka miji iliyo dhahiri, na tukaweka humo vituo vya safari. Tukawaambia, "Nendeni humo usiku na mchana kwa amani."
Os Tafssir em língua árabe:
فَقَالُواْ رَبَّنَا بَٰعِدۡ بَيۡنَ أَسۡفَارِنَا وَظَلَمُوٓاْ أَنفُسَهُمۡ فَجَعَلۡنَٰهُمۡ أَحَادِيثَ وَمَزَّقۡنَٰهُمۡ كُلَّ مُمَزَّقٍۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَٰتٖ لِّكُلِّ صَبَّارٖ شَكُورٖ
Lakini wakasema, "Mola wetu Mlezi! Weka mwendo mrefu baina ya safari zetu." Na wakazidhulumu nafsi zao. Basi tukawafanya ni masimulizi tu, na tukawatawanya tawanya. Hakika katika hayo bila ya shaka zimo Ishara kwa kila mwenye kusubiri sana na akashukuru mno.
Os Tafssir em língua árabe:
وَلَقَدۡ صَدَّقَ عَلَيۡهِمۡ إِبۡلِيسُ ظَنَّهُۥ فَٱتَّبَعُوهُ إِلَّا فَرِيقٗا مِّنَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ
Na bila ya shaka Iblisi aliihakikisha ile dhana yake juu yao. Nao walimfuata, isipokuwa kundi katika Waumini.
Os Tafssir em língua árabe:
وَمَا كَانَ لَهُۥ عَلَيۡهِم مِّن سُلۡطَٰنٍ إِلَّا لِنَعۡلَمَ مَن يُؤۡمِنُ بِٱلۡأٓخِرَةِ مِمَّنۡ هُوَ مِنۡهَا فِي شَكّٖۗ وَرَبُّكَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٍ حَفِيظٞ
Na yeye hakuwa na mamlaka yoyote juu yao, isipokuwa kwa sababu ya kuwajaribu ili tumjue ni nani mwenye kuamini Akhera, na ni nani anayeitilia shaka. Na Mola wako Mlezi ni Mwenye kuhifadhi kila kitu.
Os Tafssir em língua árabe:
قُلِ ٱدۡعُواْ ٱلَّذِينَ زَعَمۡتُم مِّن دُونِ ٱللَّهِ لَا يَمۡلِكُونَ مِثۡقَالَ ذَرَّةٖ فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَلَا فِي ٱلۡأَرۡضِ وَمَا لَهُمۡ فِيهِمَا مِن شِرۡكٖ وَمَا لَهُۥ مِنۡهُم مِّن ظَهِيرٖ
Sema, "Waiteni wale mnaowadaia kuwa ni badala ya Mwenyezi Mungu. Hawamiliki hata uzito wa chembe katika mbingu wala ardhi. Wala hawana ushirika wowote humo. Wala Yeye hana msaidizi miongoni mwao."
Os Tafssir em língua árabe:
وَلَا تَنفَعُ ٱلشَّفَٰعَةُ عِندَهُۥٓ إِلَّا لِمَنۡ أَذِنَ لَهُۥۚ حَتَّىٰٓ إِذَا فُزِّعَ عَن قُلُوبِهِمۡ قَالُواْ مَاذَا قَالَ رَبُّكُمۡۖ قَالُواْ ٱلۡحَقَّۖ وَهُوَ ٱلۡعَلِيُّ ٱلۡكَبِيرُ
Wala uombezi mbele yake hautafaa kitu, isipokuwa kwa aliyempa idhini. Hata itakapoondolewa hofu kwenye nyoyo zao, watasema: "Mola wenu Mlezi amesema nini?" Watasema: "Yaliyo kweli! Na Yeye ndiye Aliye juu, Mkubwa."
Os Tafssir em língua árabe:
۞ قُلۡ مَن يَرۡزُقُكُم مِّنَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۖ قُلِ ٱللَّهُۖ وَإِنَّآ أَوۡ إِيَّاكُمۡ لَعَلَىٰ هُدًى أَوۡ فِي ضَلَٰلٖ مُّبِينٖ
Sema: Ni nani anayewaruzuku kutoka mbinguni na kwenye ardhi? Sema: Mwenyezi Mungu! Na hakika sisi au nyinyi bila ya shaka tuko kwenye uongofu au upotofu ulio wazi.
Os Tafssir em língua árabe:
قُل لَّا تُسۡـَٔلُونَ عَمَّآ أَجۡرَمۡنَا وَلَا نُسۡـَٔلُ عَمَّا تَعۡمَلُونَ
Sema: Nyinyi hamtaulizwa kwa makosa tuliyoyafanya, wala sisi hatutaulizwa kwa mnayoyatenda nyinyi.
Os Tafssir em língua árabe:
قُلۡ يَجۡمَعُ بَيۡنَنَا رَبُّنَا ثُمَّ يَفۡتَحُ بَيۡنَنَا بِٱلۡحَقِّ وَهُوَ ٱلۡفَتَّاحُ ٱلۡعَلِيمُ
Sema: Mola wetu Mlezi atatukusanya, kisha atatuhukumu kwa haki; na Yeye ndiye Hakimu, Mwenye kujua vyema.
Os Tafssir em língua árabe:
قُلۡ أَرُونِيَ ٱلَّذِينَ أَلۡحَقۡتُم بِهِۦ شُرَكَآءَۖ كَلَّاۚ بَلۡ هُوَ ٱللَّهُ ٱلۡعَزِيزُ ٱلۡحَكِيمُ
Sema: Nionyesheni mliowaunganisha naye kuwa washirika. Hasha! Bali Yeye ndiye Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Mwenye hekima.
Os Tafssir em língua árabe:
وَمَآ أَرۡسَلۡنَٰكَ إِلَّا كَآفَّةٗ لِّلنَّاسِ بَشِيرٗا وَنَذِيرٗا وَلَٰكِنَّ أَكۡثَرَ ٱلنَّاسِ لَا يَعۡلَمُونَ
Na hatukukutuma ila kwa watu wote, uwe mbashiri na mwonyaji. Lakini watu wengi hawajui.
Os Tafssir em língua árabe:
وَيَقُولُونَ مَتَىٰ هَٰذَا ٱلۡوَعۡدُ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ
Na wanasema: "Ahadi hii itakuwa lini, ikiwa nyinyi mnasema kweli?"
Os Tafssir em língua árabe:
قُل لَّكُم مِّيعَادُ يَوۡمٖ لَّا تَسۡتَـٔۡخِرُونَ عَنۡهُ سَاعَةٗ وَلَا تَسۡتَقۡدِمُونَ
Sema: "Nyinyi mnayo miadi ya Siku ambayo hamtaakhirika nayo kwa saa moja, wala hamtaitangulia."
Os Tafssir em língua árabe:
وَقَالَ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ لَن نُّؤۡمِنَ بِهَٰذَا ٱلۡقُرۡءَانِ وَلَا بِٱلَّذِي بَيۡنَ يَدَيۡهِۗ وَلَوۡ تَرَىٰٓ إِذِ ٱلظَّٰلِمُونَ مَوۡقُوفُونَ عِندَ رَبِّهِمۡ يَرۡجِعُ بَعۡضُهُمۡ إِلَىٰ بَعۡضٍ ٱلۡقَوۡلَ يَقُولُ ٱلَّذِينَ ٱسۡتُضۡعِفُواْ لِلَّذِينَ ٱسۡتَكۡبَرُواْ لَوۡلَآ أَنتُمۡ لَكُنَّا مُؤۡمِنِينَ
Na walisema wale waliokufuru, "Hatutaiamini Qur-ani hii, wala yale yaliyokuwa kabla yake." Na ungeliwaona madhalimu watakaposimamishwa mbele ya Mola wao Mlezi, wakirudishiana maneno wao kwa wao! Wanyonge wakiwaambia wale waliotakabari, "Lau kuwa si nyinyi, bila ya shaka tungelikuwa Waumini sisi."
Os Tafssir em língua árabe:
قَالَ ٱلَّذِينَ ٱسۡتَكۡبَرُواْ لِلَّذِينَ ٱسۡتُضۡعِفُوٓاْ أَنَحۡنُ صَدَدۡنَٰكُمۡ عَنِ ٱلۡهُدَىٰ بَعۡدَ إِذۡ جَآءَكُمۖ بَلۡ كُنتُم مُّجۡرِمِينَ
Na wale waliotakabari watawaambia wanyonge, "Kwani sisi ndio tuliwazuia na uongofu baada ya huo kukujieni? Bali nyinyi wenyewe ni wahalifu."
Os Tafssir em língua árabe:
وَقَالَ ٱلَّذِينَ ٱسۡتُضۡعِفُواْ لِلَّذِينَ ٱسۡتَكۡبَرُواْ بَلۡ مَكۡرُ ٱلَّيۡلِ وَٱلنَّهَارِ إِذۡ تَأۡمُرُونَنَآ أَن نَّكۡفُرَ بِٱللَّهِ وَنَجۡعَلَ لَهُۥٓ أَندَادٗاۚ وَأَسَرُّواْ ٱلنَّدَامَةَ لَمَّا رَأَوُاْ ٱلۡعَذَابَۚ وَجَعَلۡنَا ٱلۡأَغۡلَٰلَ فِيٓ أَعۡنَاقِ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْۖ هَلۡ يُجۡزَوۡنَ إِلَّا مَا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ
Na wanyonge wakawaambia wale waliotakabari, "Bali ni vitimbi vyenu vya usiku na mchana, mlipokuwa mkituamrisha tumkufuru Mwenyezi Mungu, na tumfanyie washirika." Nao wataficha majuto watakapoiona adhabu. Na tutaweka makongwa shingoni mwa wale waliokufuru. Kwani wanalipwa isipokuwa kwa yale waliyokuwa wakiyatenda?
Os Tafssir em língua árabe:
وَمَآ أَرۡسَلۡنَا فِي قَرۡيَةٖ مِّن نَّذِيرٍ إِلَّا قَالَ مُتۡرَفُوهَآ إِنَّا بِمَآ أُرۡسِلۡتُم بِهِۦ كَٰفِرُونَ
Na hatukumtuma mwonyaji yeyote kwenye mji, isipokuwa walisema wale waliojidekeza kwa starehe zao, wa mji huo, "Hakika sisi tunayakataa hayo mliyotumwa nayo."
Os Tafssir em língua árabe:
وَقَالُواْ نَحۡنُ أَكۡثَرُ أَمۡوَٰلٗا وَأَوۡلَٰدٗا وَمَا نَحۡنُ بِمُعَذَّبِينَ
Na wakasema, "Sisi tuna mali nyingi zaidi na watoto, wala sisi hatutaadhibiwa."
Os Tafssir em língua árabe:
قُلۡ إِنَّ رَبِّي يَبۡسُطُ ٱلرِّزۡقَ لِمَن يَشَآءُ وَيَقۡدِرُ وَلَٰكِنَّ أَكۡثَرَ ٱلنَّاسِ لَا يَعۡلَمُونَ
Sema, "Hakika Mola wangu Mlezi humkunjulia riziki amtakaye na humdhikisha amtakaye. Lakini watu wengi hawajui."
Os Tafssir em língua árabe:
وَمَآ أَمۡوَٰلُكُمۡ وَلَآ أَوۡلَٰدُكُم بِٱلَّتِي تُقَرِّبُكُمۡ عِندَنَا زُلۡفَىٰٓ إِلَّا مَنۡ ءَامَنَ وَعَمِلَ صَٰلِحٗا فَأُوْلَٰٓئِكَ لَهُمۡ جَزَآءُ ٱلضِّعۡفِ بِمَا عَمِلُواْ وَهُمۡ فِي ٱلۡغُرُفَٰتِ ءَامِنُونَ
Na si mali zenu wala watoto wenu watakaowasongesha karibu na sisi, muwe karibu sana, isipokuwa yule aliyeamini na akatenda mema. Hao basi watapata malipo maradufu kwa yale waliyoyafanya. Nao watakuwa salama katika maghorofa.
Os Tafssir em língua árabe:
وَٱلَّذِينَ يَسۡعَوۡنَ فِيٓ ءَايَٰتِنَا مُعَٰجِزِينَ أُوْلَٰٓئِكَ فِي ٱلۡعَذَابِ مُحۡضَرُونَ
Na wale wanaojitahidi kuzipinga Ishara zetu, wakaona watashinda, hao watahudhurishwa kwenye adhabu.
Os Tafssir em língua árabe:
قُلۡ إِنَّ رَبِّي يَبۡسُطُ ٱلرِّزۡقَ لِمَن يَشَآءُ مِنۡ عِبَادِهِۦ وَيَقۡدِرُ لَهُۥۚ وَمَآ أَنفَقۡتُم مِّن شَيۡءٖ فَهُوَ يُخۡلِفُهُۥۖ وَهُوَ خَيۡرُ ٱلرَّٰزِقِينَ
Sema: "Kwa hakika Mola wangu Mlezi humkunjulia riziki amtakaye na humdhikisha amtakaye katika waja wake. Na chochote mtakachokitoa, Yeye atakilipa. Naye ni Mbora wa wanaoruzuku."
Os Tafssir em língua árabe:
وَيَوۡمَ يَحۡشُرُهُمۡ جَمِيعٗا ثُمَّ يَقُولُ لِلۡمَلَٰٓئِكَةِ أَهَٰٓؤُلَآءِ إِيَّاكُمۡ كَانُواْ يَعۡبُدُونَ
Na siku atakayowakusanya wote, kisha atawaambia Malaika, "Je, hawa walikuwa wakikuabuduni?"
Os Tafssir em língua árabe:
قَالُواْ سُبۡحَٰنَكَ أَنتَ وَلِيُّنَا مِن دُونِهِمۖ بَلۡ كَانُواْ يَعۡبُدُونَ ٱلۡجِنَّۖ أَكۡثَرُهُم بِهِم مُّؤۡمِنُونَ
Waseme, "Subhanak (umetakasika). Wewe ndiye kipenzi chetu, si hao. Bali wao walikuwa wakiwaabudu majini; wengi wao wakiwaamini hao."
Os Tafssir em língua árabe:
فَٱلۡيَوۡمَ لَا يَمۡلِكُ بَعۡضُكُمۡ لِبَعۡضٖ نَّفۡعٗا وَلَا ضَرّٗا وَنَقُولُ لِلَّذِينَ ظَلَمُواْ ذُوقُواْ عَذَابَ ٱلنَّارِ ٱلَّتِي كُنتُم بِهَا تُكَذِّبُونَ
Basi hii leo hataweza yeyote kumletea nafuu wala madhara mwenziwe. Na tutawaambia wale waliodhulumu, "Onjeni adhabu ya Moto mliokuwa mkiukadhibisha."
Os Tafssir em língua árabe:
وَإِذَا تُتۡلَىٰ عَلَيۡهِمۡ ءَايَٰتُنَا بَيِّنَٰتٖ قَالُواْ مَا هَٰذَآ إِلَّا رَجُلٞ يُرِيدُ أَن يَصُدَّكُمۡ عَمَّا كَانَ يَعۡبُدُ ءَابَآؤُكُمۡ وَقَالُواْ مَا هَٰذَآ إِلَّآ إِفۡكٞ مُّفۡتَرٗىۚ وَقَالَ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ لِلۡحَقِّ لَمَّا جَآءَهُمۡ إِنۡ هَٰذَآ إِلَّا سِحۡرٞ مُّبِينٞ
Na wanaposomewa Aya zetu zilizo wazi, wanasema: "Huyu si chochote isipokuwa ni mtu anayetaka kuwazuia na yale waliyokuwa wakiabudu baba zenu." Na wakasema: "Haya si chochote isipokuwa ni uongo uliozuliwa." Na wale waliokufuru waliiambia haki ilipowajia: "Haya si chochote isipokuwa ni uchawi ulio dhahiri."
Os Tafssir em língua árabe:
وَمَآ ءَاتَيۡنَٰهُم مِّن كُتُبٖ يَدۡرُسُونَهَاۖ وَمَآ أَرۡسَلۡنَآ إِلَيۡهِمۡ قَبۡلَكَ مِن نَّذِيرٖ
Wala hatukuwapa Vitabu wavisome, wala hatukuwatumia mwonyaji kabla yako wewe.
Os Tafssir em língua árabe:
وَكَذَّبَ ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِمۡ وَمَا بَلَغُواْ مِعۡشَارَ مَآ ءَاتَيۡنَٰهُمۡ فَكَذَّبُواْ رُسُلِيۖ فَكَيۡفَ كَانَ نَكِيرِ
Na walikadhibisha wale waliokuwa kabla yao. Na hawakufikia hata sehemu moja katika kumi ya tulivyowapa hao. Nao waliwakadhibisha Mitume wangu. Basi kuangamiza kwangu kulikuwa namna gani!
Os Tafssir em língua árabe:
۞ قُلۡ إِنَّمَآ أَعِظُكُم بِوَٰحِدَةٍۖ أَن تَقُومُواْ لِلَّهِ مَثۡنَىٰ وَفُرَٰدَىٰ ثُمَّ تَتَفَكَّرُواْۚ مَا بِصَاحِبِكُم مِّن جِنَّةٍۚ إِنۡ هُوَ إِلَّا نَذِيرٞ لَّكُم بَيۡنَ يَدَيۡ عَذَابٖ شَدِيدٖ
Sema: "Mimi ninawanasihi kwa jambo moja tu - ya kwamba msimame kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, wawili wawili na mmoja mmoja; kisha mfikiri. Mwenzenu huyu hana wazimu. Yeye si chochote isipokuwa ni mwonyaji kwenu kabla ya kufika adhabu kali."
Os Tafssir em língua árabe:
قُلۡ مَا سَأَلۡتُكُم مِّنۡ أَجۡرٖ فَهُوَ لَكُمۡۖ إِنۡ أَجۡرِيَ إِلَّا عَلَى ٱللَّهِۖ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ شَهِيدٞ
Sema: "Ujira niliowaomba ni wenu nyinyi. Sina ujira isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu. Na Yeye ni Shahidi juu ya kila kitu."
Os Tafssir em língua árabe:
قُلۡ إِنَّ رَبِّي يَقۡذِفُ بِٱلۡحَقِّ عَلَّٰمُ ٱلۡغُيُوبِ
Sema: "Hakika Mola wangu Mlezi anaondoa upotovu kwa haki. Yeye ndiye Mwenye kujua vyema ya ghaibu."
Os Tafssir em língua árabe:
قُلۡ جَآءَ ٱلۡحَقُّ وَمَا يُبۡدِئُ ٱلۡبَٰطِلُ وَمَا يُعِيدُ
Sema: "Kweli imefika, na batili haijitokezi, wala hairudi."
Os Tafssir em língua árabe:
قُلۡ إِن ضَلَلۡتُ فَإِنَّمَآ أَضِلُّ عَلَىٰ نَفۡسِيۖ وَإِنِ ٱهۡتَدَيۡتُ فَبِمَا يُوحِيٓ إِلَيَّ رَبِّيٓۚ إِنَّهُۥ سَمِيعٞ قَرِيبٞ
Sema: "Ikiwa mimi nimepotea, basi nimepotea kwa kudhuru nafsi yangu mwenyewe. Na ikiwa nimeongoka, basi ni kwa sababu ya kunifunulia Mola wangu Mlezi. Hakika Yeye ni Mwenye kusikia, aliye karibu."
Os Tafssir em língua árabe:
وَلَوۡ تَرَىٰٓ إِذۡ فَزِعُواْ فَلَا فَوۡتَ وَأُخِذُواْ مِن مَّكَانٖ قَرِيبٖ
Na lau ungeliona watakapobabaika, basi hapana pa kukimbilia! Na watakamatwa mahala pa karibu.
Os Tafssir em língua árabe:
وَقَالُوٓاْ ءَامَنَّا بِهِۦ وَأَنَّىٰ لَهُمُ ٱلتَّنَاوُشُ مِن مَّكَانِۭ بَعِيدٖ
Na watasema: "Tunaiamini!" Lakini wataipata wapi kutoka huko mahala mbali?
Os Tafssir em língua árabe:
وَقَدۡ كَفَرُواْ بِهِۦ مِن قَبۡلُۖ وَيَقۡذِفُونَ بِٱلۡغَيۡبِ مِن مَّكَانِۭ بَعِيدٖ
Na hapo kabla yake waliikataa, na wakiyatupilia mbali maneno ya ghaibu kutoka mahali mbali.
Os Tafssir em língua árabe:
وَحِيلَ بَيۡنَهُمۡ وَبَيۡنَ مَا يَشۡتَهُونَ كَمَا فُعِلَ بِأَشۡيَاعِهِم مِّن قَبۡلُۚ إِنَّهُمۡ كَانُواْ فِي شَكّٖ مُّرِيبِۭ
Na watatiliwa kizuizi baina yao na hayo wanayoyatamani, kama walivyofanyiwa wenzao zamani. Hakika hao walikuwa na shaka ya kutia wasiwasi.
Os Tafssir em língua árabe:
 
Tradução dos significados Surah: Saba
Índice de capítulos Número de página
 
Tradução dos significados do Nobre Qur’an. - Tradução Suaíli - Centro de tradução Rawad - Índice de tradução

Tradução realizada pela equipe do Centro de Tradução Rowwad em cooperação com a Associação de Chamada em Al-Rabwah e a Associação para o Serviço do Conteúdo Islâmico em Idiomas.

Fechar