Check out the new design

Ibisobanuro bya qoran ntagatifu - Ibisobanuro bya Qur'an mu rurimi rw'igiswahili - Abdallah Mohamed na Nassor Khamis * - Ishakiro ry'ibisobanuro


Ibisobanuro by'amagambo Isura: Al A’araf   Umurongo:
قَالَا رَبَّنَا ظَلَمۡنَآ أَنفُسَنَا وَإِن لَّمۡ تَغۡفِرۡ لَنَا وَتَرۡحَمۡنَا لَنَكُونَنَّ مِنَ ٱلۡخَٰسِرِينَ
Ādam na Ḥawwā’ walisema, «Ewe Mola wetu, tumejidhulumu nafsi zetu kwa kula kutoka kwenye mti ule. Na iwapo hutatusamehe na kuturehemu, tutakuwa ni miongoni mwa waliopoteza bahati zao katiku ulimengu wao na Akhera yao.» Maneno haya ndiyo yale aliyoyapokea Ādam kutoka kwa Mola wake akayatumia katika kumuomba, ndipo Mola wake Akaikubali toba yake.
Ibisobanuro by'icyarabu:
قَالَ ٱهۡبِطُواْ بَعۡضُكُمۡ لِبَعۡضٍ عَدُوّٞۖ وَلَكُمۡ فِي ٱلۡأَرۡضِ مُسۡتَقَرّٞ وَمَتَٰعٌ إِلَىٰ حِينٖ
Akasema, Aliyetukuka, kumwambia Ādam, Ḥawwā’ na Iblisi, «Shukeni kutoka mbinguni muende ardhini, baadhi yenu mkiwa ni maadui ya wengine. Huko mtakuwa na mahala pa nyinyi kutulia na pa kujiliwaza mpaka muda wenu ukome.»
Ibisobanuro by'icyarabu:
قَالَ فِيهَا تَحۡيَوۡنَ وَفِيهَا تَمُوتُونَ وَمِنۡهَا تُخۡرَجُونَ
Mwenyezi Mngu, Aliyetukuka, Akasema kumwambia Ādam, Ḥawwā’ na kizazi chao, «Huko ardhini mtaishi, yaani mtapitisha siku za uhai wenu duniani, na huko kitakuwa kifo chenu, na kutoka huko Mola wenu atawatoa na awakusanye mkiwa hai Siku ya Ufufuzi.»
Ibisobanuro by'icyarabu:
يَٰبَنِيٓ ءَادَمَ قَدۡ أَنزَلۡنَا عَلَيۡكُمۡ لِبَاسٗا يُوَٰرِي سَوۡءَٰتِكُمۡ وَرِيشٗاۖ وَلِبَاسُ ٱلتَّقۡوَىٰ ذَٰلِكَ خَيۡرٞۚ ذَٰلِكَ مِنۡ ءَايَٰتِ ٱللَّهِ لَعَلَّهُمۡ يَذَّكَّرُونَ
Enyi wanadamu, tumewaekea vazi lenyi kusitiri tupu zenu, nalo ni vazi la lazima, na vazi la pambo na kujirembesha, nalo ni vazi la kujikamilisha na kujifurahisha. Na vazi la uchaji Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, kwa kutekeleza maamrisho na kujiepusha na makatazo, ndilo vazi bora kwa aliyeamini. Hayo Ndiyo ambayo Mwenyezi Mungu Amewaneemesha nayo miongoni mwa alama za uola wa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, upweke Wake, wema Wake na rehema Zake kwa waja Wake, ili mpate kuzikumbuka neema hizi na mumshukuru Mwenyezi Mungu juu yake.
Ibisobanuro by'icyarabu:
يَٰبَنِيٓ ءَادَمَ لَا يَفۡتِنَنَّكُمُ ٱلشَّيۡطَٰنُ كَمَآ أَخۡرَجَ أَبَوَيۡكُم مِّنَ ٱلۡجَنَّةِ يَنزِعُ عَنۡهُمَا لِبَاسَهُمَا لِيُرِيَهُمَا سَوۡءَٰتِهِمَآۚ إِنَّهُۥ يَرَىٰكُمۡ هُوَ وَقَبِيلُهُۥ مِنۡ حَيۡثُ لَا تَرَوۡنَهُمۡۗ إِنَّا جَعَلۡنَا ٱلشَّيَٰطِينَ أَوۡلِيَآءَ لِلَّذِينَ لَا يُؤۡمِنُونَ
Enyi wanadamu! Asiwadanganye Shetani akawapambia maasia, kama alivyowapambia wazazi wenu, Ādam na Ḥawwā’, akawatoa Peponi kwa sababu hiyo, akawavua vazi lao ambalo Mwenyezi Mungu Aliwasitiri nalo ili tupu zao zifunuke. Shetani na kizazi chake na viumbe wa jinsi yake wanawaona nyinyi, na nyinyi hamuwaoni, basi jichungeni nao. Hakika sisi tumewafanya Mashetani ni wategemewa wa makafiri ambao hawampwekeshi Mwenyezi Mungu wala hawawaamini Mitume Wake wala hawautumii muongozo Wake.
Ibisobanuro by'icyarabu:
وَإِذَا فَعَلُواْ فَٰحِشَةٗ قَالُواْ وَجَدۡنَا عَلَيۡهَآ ءَابَآءَنَا وَٱللَّهُ أَمَرَنَا بِهَاۗ قُلۡ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يَأۡمُرُ بِٱلۡفَحۡشَآءِۖ أَتَقُولُونَ عَلَى ٱللَّهِ مَا لَا تَعۡلَمُونَ
Na makafiri wanapofanya tendo ovu, wanajitetea kwa kusema kwamba hilo ni miongoni mwa yale waliyoyapokea kutoka kwa baba zao na kwamba hilo ni katika yale Aliyoyaamrisha Mwenyzi Mungu. Waambie, ewe Mtume, «Mwenyezi Mungu Hawaamrishi waja Wake vitendo vichafu na viovu. Je, mnasema, kumsingizia Mwenyezi Mungu msiyoyajua, urongo na uzushi?»
Ibisobanuro by'icyarabu:
قُلۡ أَمَرَ رَبِّي بِٱلۡقِسۡطِۖ وَأَقِيمُواْ وُجُوهَكُمۡ عِندَ كُلِّ مَسۡجِدٖ وَٱدۡعُوهُ مُخۡلِصِينَ لَهُ ٱلدِّينَۚ كَمَا بَدَأَكُمۡ تَعُودُونَ
Sema, ewe Mtume, kuwaambia washirikina hawa, «Mola wangu Ameniamrisha usawa, na Amewaamrisha nyinyi mumtakasie ibada katika kila sehemu za ibada, hasa katika misikiti, na mumuombe Yeye hali ya kumtakasia utiifu na ibada, na muamini kufufuliwa baada ya kufa. Na kama Alivyowaleta kutoka kuwa hamkuwako,Yeye ni Muweza kuwarudishia uhai mara nyingine.»
Ibisobanuro by'icyarabu:
فَرِيقًا هَدَىٰ وَفَرِيقًا حَقَّ عَلَيۡهِمُ ٱلضَّلَٰلَةُۚ إِنَّهُمُ ٱتَّخَذُواْ ٱلشَّيَٰطِينَ أَوۡلِيَآءَ مِن دُونِ ٱللَّهِ وَيَحۡسَبُونَ أَنَّهُم مُّهۡتَدُونَ
Mwenyezi Mungu Amewafanya waja wake makundi mawili: kundi moja Amelielekeza kwenye uongofu, kwenye njia iliyolingana; na kundi lingine limelazimika kupotea njia iliyolingana, kwani wao wamewafanya Mashetani ni wategemewa wao badala ya Mwenyezi Mungu, waliwasikiliza Mashetani kwa ujinga wao na kudhania kwao kuwa wao wamefuata njia ya uongofu.
Ibisobanuro by'icyarabu:
 
Ibisobanuro by'amagambo Isura: Al A’araf
Urutonde rw'amasura numero y'urupapuro
 
Ibisobanuro bya qoran ntagatifu - Ibisobanuro bya Qur'an mu rurimi rw'igiswahili - Abdallah Mohamed na Nassor Khamis - Ishakiro ry'ibisobanuro

Byasobanuwe na Dr. Abdalla Mohamed Abubakar na Sheikh Nassor Khamis.

Gufunga