Check out the new design

Ibisobanuro bya qoran ntagatifu - Ibisobanuro bya Qur'an mu rurimi rw'igiswahili - Ikigo Rowad cy'ubusobanuzi. * - Ishakiro ry'ibisobanuro


Ibisobanuro by'amagambo Isura: Al Isr’au   Umurongo:
۞ قُلۡ كُونُواْ حِجَارَةً أَوۡ حَدِيدًا
Sema: Kuweni hata mawe na chuma.
Ibisobanuro by'icyarabu:
أَوۡ خَلۡقٗا مِّمَّا يَكۡبُرُ فِي صُدُورِكُمۡۚ فَسَيَقُولُونَ مَن يُعِيدُنَاۖ قُلِ ٱلَّذِي فَطَرَكُمۡ أَوَّلَ مَرَّةٖۚ فَسَيُنۡغِضُونَ إِلَيۡكَ رُءُوسَهُمۡ وَيَقُولُونَ مَتَىٰ هُوَۖ قُلۡ عَسَىٰٓ أَن يَكُونَ قَرِيبٗا
Au umbo lolote mnaloliona kubwa katika vifua vyenu. Watasema: Nani atakayeturudisha tena? Sema: Yule yule aliyewaumba mara ya kwanza! Watakutikisia vichwa vyao, na watasema: Ni lini hayo? Sema: Labda huenda itakuwa hivi karibuni!
Ibisobanuro by'icyarabu:
يَوۡمَ يَدۡعُوكُمۡ فَتَسۡتَجِيبُونَ بِحَمۡدِهِۦ وَتَظُنُّونَ إِن لَّبِثۡتُمۡ إِلَّا قَلِيلٗا
Siku atakapowaita, nanyi mtamuitikia kwa kumsifu, na mtaadhani kuwa hamkukaa isipokuwa muda mdogo tu.
Ibisobanuro by'icyarabu:
وَقُل لِّعِبَادِي يَقُولُواْ ٱلَّتِي هِيَ أَحۡسَنُۚ إِنَّ ٱلشَّيۡطَٰنَ يَنزَغُ بَيۡنَهُمۡۚ إِنَّ ٱلشَّيۡطَٰنَ كَانَ لِلۡإِنسَٰنِ عَدُوّٗا مُّبِينٗا
Waambie waja wangu waseme maneno mazuri, kwa maana hakika Shetani huchochea ugomvi baina yao. Hakika Shetani ni adui aliye dhahiri kwa mwanadamu.
Ibisobanuro by'icyarabu:
رَّبُّكُمۡ أَعۡلَمُ بِكُمۡۖ إِن يَشَأۡ يَرۡحَمۡكُمۡ أَوۡ إِن يَشَأۡ يُعَذِّبۡكُمۡۚ وَمَآ أَرۡسَلۡنَٰكَ عَلَيۡهِمۡ وَكِيلٗا
Mola wenu Mlezi anawajua vilivyo. Akitaka, atawarehemu, na akitaka, atawaadhibu. Na hatukukutuma ili uwe msimamizi wao.
Ibisobanuro by'icyarabu:
وَرَبُّكَ أَعۡلَمُ بِمَن فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۗ وَلَقَدۡ فَضَّلۡنَا بَعۡضَ ٱلنَّبِيِّـۧنَ عَلَىٰ بَعۡضٖۖ وَءَاتَيۡنَا دَاوُۥدَ زَبُورٗا
Na Mola wako Mlezi anawajua vilivyo waliomo mbinguni na katika ardhi. Na hakika tumewafadhilisha baadhi ya Manabii kuliko wengine, na Daudi tulimpa Zaburi.
Ibisobanuro by'icyarabu:
قُلِ ٱدۡعُواْ ٱلَّذِينَ زَعَمۡتُم مِّن دُونِهِۦ فَلَا يَمۡلِكُونَ كَشۡفَ ٱلضُّرِّ عَنكُمۡ وَلَا تَحۡوِيلًا
Sema: Waombeni hao mnaowadai badala yake Yeye. Hawawezi kuwaondolea madhara, wala kuyaweka pengine.
Ibisobanuro by'icyarabu:
أُوْلَٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ يَدۡعُونَ يَبۡتَغُونَ إِلَىٰ رَبِّهِمُ ٱلۡوَسِيلَةَ أَيُّهُمۡ أَقۡرَبُ وَيَرۡجُونَ رَحۡمَتَهُۥ وَيَخَافُونَ عَذَابَهُۥٓۚ إِنَّ عَذَابَ رَبِّكَ كَانَ مَحۡذُورٗا
Hao ambao wao wanaowaomba, wao wenyewe wanatafuta njia ya kwendea kwa Mola wao Mlezi hata miongoni mwao walio karibu mno, na wanataraji rehema zake, na wanaihofu adhabu yake. Hakika adhabu ya Mola wako Mlezi yafaa kutahadhariwa.
Ibisobanuro by'icyarabu:
وَإِن مِّن قَرۡيَةٍ إِلَّا نَحۡنُ مُهۡلِكُوهَا قَبۡلَ يَوۡمِ ٱلۡقِيَٰمَةِ أَوۡ مُعَذِّبُوهَا عَذَابٗا شَدِيدٗاۚ كَانَ ذَٰلِكَ فِي ٱلۡكِتَٰبِ مَسۡطُورٗا
Na hapana mji wowote ila Sisi tutauteketeza kabla ya Siku ya Kiyama, au tutaupa adhabu kali. Haya yamekwisha andikwa katika Kitabu.
Ibisobanuro by'icyarabu:
 
Ibisobanuro by'amagambo Isura: Al Isr’au
Urutonde rw'amasura numero y'urupapuro
 
Ibisobanuro bya qoran ntagatifu - Ibisobanuro bya Qur'an mu rurimi rw'igiswahili - Ikigo Rowad cy'ubusobanuzi. - Ishakiro ry'ibisobanuro

Yasobanuwe n'itsinda ry'ikigo Rowad cy'ubusobanuzi ku bufatanye n'ishyirahamwe ryo kwamamaza idini rya Rabwa n'ishyirahamwe ryo gutanga serivisi z'ibikubiyemo idini mu ndimi zitandukanye.

Gufunga