Check out the new design

Ibisobanuro bya qoran ntagatifu - Ibisobanuro bya Qur'an mu rurimi rw'igiswahili - Ikigo Rowad cy'ubusobanuzi. * - Ishakiro ry'ibisobanuro


Ibisobanuro by'amagambo Isura: Annisau   Umurongo:
۞ وَٱلۡمُحۡصَنَٰتُ مِنَ ٱلنِّسَآءِ إِلَّا مَا مَلَكَتۡ أَيۡمَٰنُكُمۡۖ كِتَٰبَ ٱللَّهِ عَلَيۡكُمۡۚ وَأُحِلَّ لَكُم مَّا وَرَآءَ ذَٰلِكُمۡ أَن تَبۡتَغُواْ بِأَمۡوَٰلِكُم مُّحۡصِنِينَ غَيۡرَ مُسَٰفِحِينَۚ فَمَا ٱسۡتَمۡتَعۡتُم بِهِۦ مِنۡهُنَّ فَـَٔاتُوهُنَّ أُجُورَهُنَّ فَرِيضَةٗۚ وَلَا جُنَاحَ عَلَيۡكُمۡ فِيمَا تَرَٰضَيۡتُم بِهِۦ مِنۢ بَعۡدِ ٱلۡفَرِيضَةِۚ إِنَّ ٱللَّهَ كَانَ عَلِيمًا حَكِيمٗا
Na wanawake wenye waume, isipokuwa waliomilikiwa na mikono yenu ya kulia. Ndiyo Sheria ya Mwenyezi Mungu juu yenu. Na mmehalilishiwa wasiokuwa hao, mtafute kwa mali zenu kwa kuoa pasi na kuzini. Kama mnavyostarehe nao, basi wapeni mahari yao kwa kuwa ni wajibu. Wala hakuna ubaya juu yenu kwa mtakachokubaliana baada ya kutimiza wajibu. Hakika, Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye hekima.
Ibisobanuro by'icyarabu:
وَمَن لَّمۡ يَسۡتَطِعۡ مِنكُمۡ طَوۡلًا أَن يَنكِحَ ٱلۡمُحۡصَنَٰتِ ٱلۡمُؤۡمِنَٰتِ فَمِن مَّا مَلَكَتۡ أَيۡمَٰنُكُم مِّن فَتَيَٰتِكُمُ ٱلۡمُؤۡمِنَٰتِۚ وَٱللَّهُ أَعۡلَمُ بِإِيمَٰنِكُمۚ بَعۡضُكُم مِّنۢ بَعۡضٖۚ فَٱنكِحُوهُنَّ بِإِذۡنِ أَهۡلِهِنَّ وَءَاتُوهُنَّ أُجُورَهُنَّ بِٱلۡمَعۡرُوفِ مُحۡصَنَٰتٍ غَيۡرَ مُسَٰفِحَٰتٖ وَلَا مُتَّخِذَٰتِ أَخۡدَانٖۚ فَإِذَآ أُحۡصِنَّ فَإِنۡ أَتَيۡنَ بِفَٰحِشَةٖ فَعَلَيۡهِنَّ نِصۡفُ مَا عَلَى ٱلۡمُحۡصَنَٰتِ مِنَ ٱلۡعَذَابِۚ ذَٰلِكَ لِمَنۡ خَشِيَ ٱلۡعَنَتَ مِنكُمۡۚ وَأَن تَصۡبِرُواْ خَيۡرٞ لَّكُمۡۗ وَٱللَّهُ غَفُورٞ رَّحِيمٞ
Na asiyeweza kati yenu kupata mali ya kuolea wanawake wa kiungwana Waumini, basi na aoe katika vijakazi Waumini iliyowamiliki mikono yenu ya kulia. Na Mwenyezi Mungu anajua vyema imani yenu. Nyinyi mmetokana wenyewe kwa wenyewe. Basi waoeni kwa idhini ya watu wao, na wapeni mahari yao kulingana na ada, wawe wanawake wema, si makahaba wala si mahawara. Na wanapoolewa kisha wakafanya uchafu basi adhabu yao itakuwa ni nusu ya adhabu waliyowekewa waungwana. Hayo ni kwa yule miongoni mwenu anayeogopa kuingia katika zinaa. Na mkisubiri ndio bora kwenu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kufuta dhambi, Mwenye kurehemu.
Ibisobanuro by'icyarabu:
يُرِيدُ ٱللَّهُ لِيُبَيِّنَ لَكُمۡ وَيَهۡدِيَكُمۡ سُنَنَ ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِكُمۡ وَيَتُوبَ عَلَيۡكُمۡۗ وَٱللَّهُ عَلِيمٌ حَكِيمٞ
Mwenyezi Mungu anataka kwamba awabainishie, na awaongoze nyendo za wale waliokuwa kabla yenu, na akubali toba zenu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye hekima.
Ibisobanuro by'icyarabu:
 
Ibisobanuro by'amagambo Isura: Annisau
Urutonde rw'amasura numero y'urupapuro
 
Ibisobanuro bya qoran ntagatifu - Ibisobanuro bya Qur'an mu rurimi rw'igiswahili - Ikigo Rowad cy'ubusobanuzi. - Ishakiro ry'ibisobanuro

Yasobanuwe n'itsinda ry'ikigo Rowad cy'ubusobanuzi ku bufatanye n'ishyirahamwe ryo kwamamaza idini rya Rabwa n'ishyirahamwe ryo gutanga serivisi z'ibikubiyemo idini mu ndimi zitandukanye.

Gufunga