Check out the new design

Ibisobanuro bya qoran ntagatifu - Ibisobanuro bya Qur'an mu rurimi rw'igiswahili - Ikigo Rowad cy'ubusobanuzi. * - Ishakiro ry'ibisobanuro


Ibisobanuro by'amagambo Isura: Al A’araf   Umurongo:
قَالَ ٱدۡخُلُواْ فِيٓ أُمَمٖ قَدۡ خَلَتۡ مِن قَبۡلِكُم مِّنَ ٱلۡجِنِّ وَٱلۡإِنسِ فِي ٱلنَّارِۖ كُلَّمَا دَخَلَتۡ أُمَّةٞ لَّعَنَتۡ أُخۡتَهَاۖ حَتَّىٰٓ إِذَا ٱدَّارَكُواْ فِيهَا جَمِيعٗا قَالَتۡ أُخۡرَىٰهُمۡ لِأُولَىٰهُمۡ رَبَّنَا هَٰٓؤُلَآءِ أَضَلُّونَا فَـَٔاتِهِمۡ عَذَابٗا ضِعۡفٗا مِّنَ ٱلنَّارِۖ قَالَ لِكُلّٖ ضِعۡفٞ وَلَٰكِن لَّا تَعۡلَمُونَ
Mwenyezi Mungu atasema: Ingieni (Motoni) pamoja na umma zilizopita kabla yenu miongoni mwa majini na watu. Kila utakapoingia umma, utalaani dada yake. Mpaka watakapokusanyika wote humo, wa mwisho wao atasema juu ya wa mwanzo wao: Mola wetu Mlezi! Hawa ndio waliotupoteza. Basi wape adhabu ya Motoni marudufu. Atasema: Kila mmoja ana marudufu, lakini nyinyi hamjui tu.
Ibisobanuro by'icyarabu:
وَقَالَتۡ أُولَىٰهُمۡ لِأُخۡرَىٰهُمۡ فَمَا كَانَ لَكُمۡ عَلَيۡنَا مِن فَضۡلٖ فَذُوقُواْ ٱلۡعَذَابَ بِمَا كُنتُمۡ تَكۡسِبُونَ
Na wa mwanzo wao atamwambia wa mwisho wao: Basi nyinyi pia hamkuwa na ubora wowote kuliko sisi. Basi onjeni adhabu kwa sababu ya yale mliyokuwa mkiyachuma.
Ibisobanuro by'icyarabu:
إِنَّ ٱلَّذِينَ كَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَا وَٱسۡتَكۡبَرُواْ عَنۡهَا لَا تُفَتَّحُ لَهُمۡ أَبۡوَٰبُ ٱلسَّمَآءِ وَلَا يَدۡخُلُونَ ٱلۡجَنَّةَ حَتَّىٰ يَلِجَ ٱلۡجَمَلُ فِي سَمِّ ٱلۡخِيَاطِۚ وَكَذَٰلِكَ نَجۡزِي ٱلۡمُجۡرِمِينَ
Hakika wale waliozikadhibisha Ishara zetu na wakazifanyia kiburi, hawatafunguliwa milango ya mbingu, wala hawataingia Bustanini mle mpaka aingie ngamia katika tundu ya sindano. Na hivyo ndivyo tunavyowalipa wahalifu.
Ibisobanuro by'icyarabu:
لَهُم مِّن جَهَنَّمَ مِهَادٞ وَمِن فَوۡقِهِمۡ غَوَاشٖۚ وَكَذَٰلِكَ نَجۡزِي ٱلظَّٰلِمِينَ
Wana kitanda chao katika Jahannamu, na juu yao nguo za moto za kujifunika. Na hivyo ndivyo tunavyowalipa madhalimu.
Ibisobanuro by'icyarabu:
وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّٰلِحَٰتِ لَا نُكَلِّفُ نَفۡسًا إِلَّا وُسۡعَهَآ أُوْلَٰٓئِكَ أَصۡحَٰبُ ٱلۡجَنَّةِۖ هُمۡ فِيهَا خَٰلِدُونَ
Na wale walioamini na wakatenda mema, hatuitwiki nafsi yoyote isipokuwa kwa kiasi cha uwezo wake. Hao ndio wenza wa Bustani ile. Wao watadumu humo.
Ibisobanuro by'icyarabu:
وَنَزَعۡنَا مَا فِي صُدُورِهِم مِّنۡ غِلّٖ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهِمُ ٱلۡأَنۡهَٰرُۖ وَقَالُواْ ٱلۡحَمۡدُ لِلَّهِ ٱلَّذِي هَدَىٰنَا لِهَٰذَا وَمَا كُنَّا لِنَهۡتَدِيَ لَوۡلَآ أَنۡ هَدَىٰنَا ٱللَّهُۖ لَقَدۡ جَآءَتۡ رُسُلُ رَبِّنَا بِٱلۡحَقِّۖ وَنُودُوٓاْ أَن تِلۡكُمُ ٱلۡجَنَّةُ أُورِثۡتُمُوهَا بِمَا كُنتُمۡ تَعۡمَلُونَ
Na tutaondoa kilicho katika vifua vyao ya chuki, na chini yao itapita mito. Na watasema: Alhamdulillah (kuhimidiwa ni kwa Mwenyezi Mungu), ambaye alituongoa kuyafikia haya. Wala hatukuwa wenye kuongoka wenyewe lau kuwa Mwenyezi Mungu hakutuongoa. Hakika Mitume wa Mola wetu Mlezi walikuja na haki. Na watanadiwa kwamba: Hiyo ndiyo Bustani mliyorithishwa kwa sababu ya yale mliyokuwa mkiyafanya.
Ibisobanuro by'icyarabu:
 
Ibisobanuro by'amagambo Isura: Al A’araf
Urutonde rw'amasura numero y'urupapuro
 
Ibisobanuro bya qoran ntagatifu - Ibisobanuro bya Qur'an mu rurimi rw'igiswahili - Ikigo Rowad cy'ubusobanuzi. - Ishakiro ry'ibisobanuro

Yasobanuwe n'itsinda ry'ikigo Rowad cy'ubusobanuzi ku bufatanye n'ishyirahamwe ryo kwamamaza idini rya Rabwa n'ishyirahamwe ryo gutanga serivisi z'ibikubiyemo idini mu ndimi zitandukanye.

Gufunga