Inafaa nisiseme juu ya Mwenyezi Mungu ila lilio la Haki. Nami hakika nimekujieni na dalili waziwazi kutokana na Mola Mlezi wenu. Basi waache Wana wa Israili wende nami.
Na mimi pupa yangu ni kumsemea kweli Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na nimekujieni na Ishara yenye shani kubwa, yenye hoja iliyo dhaahiri katika kubainisha Haki niliyo kuja nayo. Basi waachilie waje nami Wana wa Israili, na uwatoe kwenye utumwa wa kahari yako, wende nami kwenye nchi nyengine isiyo kuwa yako, na huko wapate kumuabudu Mola Mlezi wao na wako.
Akasema Firauni: Ikiwa umekuja na Ishara, basi ilete ukiwa ni katika wasemao kweli.
Firauni akamwambia Musa: Ikiwa umekuja na Ishara (muujiza) kutokana na huyo aliye kutuma, basi nionyeshe kama wewe ni katika watu wakweli wanalo lishika neno la haki.
Basi akaitupa fimbo yake, na mara ikawa nyoka dhaahiri.
Kiasi ya Musa kuitupa fimbo aliyo kuwa nayo mkononi mwake wa kulia mbele ya Firauni, mara hiyo fimbo ikawa nyoka khasa dhaahiri, anakwenda mbio huku na huku, kwa nguvu zinazo onyesha kuwa ana uhai timamu.
Wakasema waheshimiwa wa kaumu ya Firauni: Hakika huyo ni mchawi mjuzi.
Musa alipo ionyesha Ishara ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, zilitibuka roho za wapambe wa Firauni na waheshimiwa wa kaumu yake, wakasema katika kujipendekeza kwa Firauni na kumtetea: Hakika huyu ni bingwa katika ilimu ya uchawi, wala hii si Ishara itokayo kwa Mwenyezi Mungu!!
Anataka kukutoeni katika nchi yenu. Basi mnatoa shauri gani?.
Na yeye ameelekeza lengo lake akupokonyeni ufalme wenu, na akutoeni katika nchi yenu kwa uchawi wake na yatayo tokea hapo kwa kuwavutia watu wamili na wamfuate. Basi tazameni, mnaamrisha njia gani ya kutokana naye huyu?
Wakasema: Mwache kidogo yeye na nduguye, na watume mijini wakusanyao,.
Wakasema: Akhirisha kukata shauri juu yake na nduguye huyu anaye msaidia katika wito wake, na watume watu katika askari wako wende katika miji ya ufalme wako wawakusanye walio mafundi katika ilimu ya uchawi.
Wakaja wachawi kwa Firauni, wakasema: Hakika tutapata ujira ikiwa tutashinda.
Basi wakaja kwa Firauni wachawi walio kusanywa na askari wake. Nao wakasema: Hapana shaka nasi tutapata malipo makubwa yanayo lingana na hili linalo takikana kwetu, ikiwa sisi tutamshinda Musa.
Akasema: Naam! Nanyi bila ya shaka mtakuwa katika wa karibu nami.
Haraka haraka Firauni akawajibu kwa walitakalo: Naam! Hapana shaka mtapata malipo makubwa. Na hapana shaka juu ya hayo nyinyi mtakuwa watu wenye cheo kwangu.
Wakasema: Ewe Musa! Je, utatupa wewe, au tutakuwa sisi tutao tupa?
Kisha wachawi wakamgeukia Musa, baada ya Firauni kuwaahidi alivyo waahidi, na wao wakaonyesha wana imani na nafsi zao na kujitayarisha kwao kwa uchawi wao katika uwanja wa mapambano. Wakamwabia: Ama utupe ulicho nacho kwanza, au sisi tuwe wenye kutupa tulicho nacho.
Akasema: Tupeni! Basi walipo tupa waliyazuga macho ya watu na wakawatia khofu, na wakaleta uchawi mkubwa.
Musa akwajibu jawabu ya mwenye imani ya kushinda, akionyesha kutowabali: Tupeni nyinyi kwanza hicho mnacho tupa. Walipo tupa kila mmoja wao, navyo ni kamba na fimbo, macho ya watu yalizugwa, na ikawapitikia kuwa walicho kifanya kile ni hakika kweli. Na hali haikuwa ila ni kiini macho tu. Mambo yale yaliwatisha watu, na nyoyo zao zikaingia khofu na kitisho. Kwani wachawi wale waliwaletea watu uchawi unao onekana ni mkubwa, na athari yake katika macho yao ni kubwa!
Nasi tukamfunulia Musa kumwambia: Tupa fimbo yako. Mara ikavimeza vyote vile walivyo vibuni.
Mwenyezi Mungu akaitoa amri yake kumpelekea Musa: Tupa fimbo yako. Sasa umekwisha fika wakati wake. Akaitupa kama alivyo amrishwa. Mara hiyo fimbo ikaingia kuvimeza vile vizushi vyao walivyo zua na kubuni!
Kwa hivyo walishindwa hapo, na wakageuka kuwa wadogo.
Firauni na waheshimiwa wake wakashindwa katika ule mkutano mkubwa, na wakawa madhalili mbele ya watu wote kwa masaibu yaliyo wapata, nayo ni kuvunjika moyo na kukata tamaa.
Haya ni mambo yaliyo wafika Firauni na waheshimiwa wake. Ama wale wachawi Haki iliangaza kwao, na wakaanguka kwa kumsujudia Mwenyezi Mungu nao wanainyenyekea Haki.
Contents of the translations can be downloaded and re-published, with the following terms and conditions:
1. No modification, addition, or deletion of the content.
2. Clearly referring to the publisher and the source (QuranEnc.com).
3. Mentioning the version number when re-publishing the translation.
4. Keeping the transcript information inside the document.
5. Notifying the source (QuranEnc.com) of any note on the translation.
6. Updating the translation according to the latest version issued from the source (QuranEnc.com).
7. Inappropriate advertisements must not be included when displaying translations of the meanings of the Noble Quran.
Rezultatet e kërkimit:
API specs
Endpoints:
Sura translation
GET / https://quranenc.com/api/v1/translation/sura/{translation_key}/{sura_number} description: get the specified translation (by its translation_key) for the speicified sura (by its number)
Parameters: translation_key: (the key of the currently selected translation) sura_number: [1-114] (Sura number in the mosshaf which should be between 1 and 114)
Returns:
json object containing array of objects, each object contains the "sura", "aya", "translation" and "footnotes".
GET / https://quranenc.com/api/v1/translation/aya/{translation_key}/{sura_number}/{aya_number} description: get the specified translation (by its translation_key) for the speicified aya (by its number sura_number and aya_number)
Parameters: translation_key: (the key of the currently selected translation) sura_number: [1-114] (Sura number in the mosshaf which should be between 1 and 114) aya_number: [1-...] (Aya number in the sura)
Returns:
json object containing the "sura", "aya", "translation" and "footnotes".