Check out the new design

Përkthimi i kuptimeve të Kuranit Fisnik - Përkthimi suahilisht - Ali Muhsin el-Beruani * - Përmbajtja e përkthimeve

XML CSV Excel API
Please review the Terms and Policies

Përkthimi i kuptimeve Surja: El Fexhr   Ajeti:

Al-Fajr

وَٱلۡفَجۡرِ
Naapa kwa alfajiri! [1]
[1] Naapa kwa mwangaza wa asubuhi unapo ufukuza usiku.
Tefsiret në gjuhën arabe:
وَلَيَالٍ عَشۡرٖ
Na kwa masiku kumi! [2]
[2] Na kwa masiku kumi yaliyo tukuzwa na Mwenyezi Mungu. (Na hayo ni masiku kumi ya mwanzo wa Mwezi wa Alhaj, Mfungo Tatu).
Tefsiret në gjuhën arabe:
وَٱلشَّفۡعِ وَٱلۡوَتۡرِ
Na kwa viwili viwili na kimoja kimoja! [3]
[3] Na shafi' yaani hisabu inayo gawika kwa mbili, kama 4, 6, 8 n.k. na witri, yaani isiyo gawika kwa mbili, kama 1, 3, 5 n.k. katika kila kitu.
Tefsiret në gjuhën arabe:
وَٱلَّيۡلِ إِذَا يَسۡرِ
Na kwa usiku unapo pita! [4]
[4] Na kwa usiku unapo pita kwa kwenda ulimwengu kwa namna ya ajabu.
Tefsiret në gjuhën arabe:
هَلۡ فِي ذَٰلِكَ قَسَمٞ لِّذِي حِجۡرٍ
Je! Hapana katika haya kiapo kwa mwenye akili? [5]
[5] Je! Katika vitu vilivyo tajwa vinavyo onekana kwa akili hapana kiapo cha kukinaisha?
Tefsiret në gjuhën arabe:
أَلَمۡ تَرَ كَيۡفَ فَعَلَ رَبُّكَ بِعَادٍ
Kwani hukuona jinsi Mola wako Mlezi alivyo wafanya kina A'di? [6]
[6] Kwani hujui jinsi Mola wako Mlezi alivyo wateremshia adhabu yake kaumu ya Hud, ?
Tefsiret në gjuhën arabe:
إِرَمَ ذَاتِ ٱلۡعِمَادِ
Wa Iram, wenye majumba marefu? [7]
[7] Watu wa Iram wenye majengo marefu?
Tefsiret në gjuhën arabe:
ٱلَّتِي لَمۡ يُخۡلَقۡ مِثۡلُهَا فِي ٱلۡبِلَٰدِ
Ambao haukuumbwa mfano wake katika nchi? [8]
[8] Ambayo haikupata kujengwa mfano wake kwa umadhubuti na ujenzi katika nchi.
Tefsiret në gjuhën arabe:
وَثَمُودَ ٱلَّذِينَ جَابُواْ ٱلصَّخۡرَ بِٱلۡوَادِ
Na Thamudi walio chonga majabali huko bondeni? [9]
[9] Kwani hukujua jinsi Mola wako Mlezi alivyo teremsha adhabu yake kwa Thamudi, kaumu ya Saleh, walio chonga majabali kujengea nyumba zao huko bondeni?
Tefsiret në gjuhën arabe:
وَفِرۡعَوۡنَ ذِي ٱلۡأَوۡتَادِ
Na Firauni mwenye vigingi? [10]
[10] Au kwani hukujua vipi Mola wako Mlezi alivyo wateremshia adhabu yake Firauni mwenye majeshi yaliyo upa nguvu ufalme wake kama vigingi vinavyo simamisha makhema?
Tefsiret në gjuhën arabe:
ٱلَّذِينَ طَغَوۡاْ فِي ٱلۡبِلَٰدِ
Ambao walifanya jeuri katika nchi? [11]
[11] Ambao walipita mipaka katika nchi?
Tefsiret në gjuhën arabe:
فَأَكۡثَرُواْ فِيهَا ٱلۡفَسَادَ
Wakakithirisha humo ufisadi? [12]
[12] Na wakazidisha kufanya uharibifu kwa ukafiri na udhalimu?
Tefsiret në gjuhën arabe:
فَصَبَّ عَلَيۡهِمۡ رَبُّكَ سَوۡطَ عَذَابٍ
Basi Mola wako Mlezi aliwapiga mjeledi wa adhabu. [13]
[13] Basi Mola wako Mlezi aliwateremshia adhabu kali ya kuwaunguza.
Tefsiret në gjuhën arabe:
إِنَّ رَبَّكَ لَبِٱلۡمِرۡصَادِ
Hakika Mola wako Mlezi yupo kwenye mavizio anawavizia. [14]
[14] Hakika Mola wako Mlezi anaviangalia vitendo vya watu, na anawahisabia, na atakuja kuwalipa kwavyo.
Tefsiret në gjuhën arabe:
فَأَمَّا ٱلۡإِنسَٰنُ إِذَا مَا ٱبۡتَلَىٰهُ رَبُّهُۥ فَأَكۡرَمَهُۥ وَنَعَّمَهُۥ فَيَقُولُ رَبِّيٓ أَكۡرَمَنِ
Ama mtu anapo jaribiwa na Mola wake Mlezi, akamkirimu na akamneemesha, husema: Mola wangu Mlezi amenikirimu! [15]
[15] Ama mtu akijaribiwa na Mola wake Mlezi na akamkirimu, na akamneemesha kwa mali na cheo na nguvu, basi husema kwa kughurika na hayo: Mola wangu Mlezi amenitukuza kwa kuwa ninastahiki haya!
Tefsiret në gjuhën arabe:
وَأَمَّآ إِذَا مَا ٱبۡتَلَىٰهُ فَقَدَرَ عَلَيۡهِ رِزۡقَهُۥ فَيَقُولُ رَبِّيٓ أَهَٰنَنِ
Na ama anapo mjaribu akampunguzia riziki yake, husema: Mola wangu Mlezi amenitia unyonge! [16]
[16] Na pindi Mola wake Mlezi akimjaribu mtu kwa kumdhikisha riziki, basi hughafilika na hikima ya hayo na husema: Mola wangu Mlezi kanidhalilisha!
Tefsiret në gjuhën arabe:
كَلَّاۖ بَل لَّا تُكۡرِمُونَ ٱلۡيَتِيمَ
Sivyo hivyo! Bali nyinyi hamuwakirimu mayatima, [17]
[17] Wacheni mtindo huo! Mambo siyo hayo kama msemavyo; bali nyinyi hamumkirimu yatima;
Tefsiret në gjuhën arabe:
وَلَا تَحَٰٓضُّونَ عَلَىٰ طَعَامِ ٱلۡمِسۡكِينِ
Wala hamhimizani kulisha masikini; [18]
[18] Wala hamhimizani kuwalisha masikini;
Tefsiret në gjuhën arabe:
وَتَأۡكُلُونَ ٱلتُّرَاثَ أَكۡلٗا لَّمّٗا
Na mnakula urithi kwa ulaji wa pupa, [19]
[19] Na mnakula mali ya urithi kwa pupa, hamchagui linalo faa na lisilo faa.
Tefsiret në gjuhën arabe:
وَتُحِبُّونَ ٱلۡمَالَ حُبّٗا جَمّٗا
Na mnapenda mali pendo la kupita kiasi. [20]
[20] Na mnayapenda mali mno, yanayo kupelekeeni kupapatika katika kuyakusanya na ubakhili wa kuyatumia.
Tefsiret në gjuhën arabe:
كَلَّآۖ إِذَا دُكَّتِ ٱلۡأَرۡضُ دَكّٗا دَكّٗا
Sivyo hivyo! Itakapo vunjwa ardhi vipande vipande, [21]
[21] Wacheni vitendo hivyo! Kwani inakungojeeni siku itapo lazwa ardhi iwe sawa sawa,
Tefsiret në gjuhën arabe:
وَجَآءَ رَبُّكَ وَٱلۡمَلَكُ صَفّٗا صَفّٗا
Na akaja Mola wako Mlezi na Malaika safu safu, [22]
[22] Na aje Mola wako Mlezi kama anavyo stahiki kuja kwake Subhanahu na Malaika waje kwa safu safu;
Tefsiret në gjuhën arabe:
 
Përkthimi i kuptimeve Surja: El Fexhr
Përmbajtja e sureve Numri i faqes
 
Përkthimi i kuptimeve të Kuranit Fisnik - Përkthimi suahilisht - Ali Muhsin el-Beruani - Përmbajtja e përkthimeve

E përktheu Ali Muhsin el-Beruani.

Mbyll