Na kwa nini msile katika walio somewa jina la Mwenyezi Mungu, naye amekwisha kubainishieni alivyo kuharimishieni, isipo kuwa vile mnavyo lazimishwa? Na hakika wengi wanapoteza kwa matamanio yao bila ya kuwa na ilimu. Hakika Mola wako Mlezi ndiye Mjuzi kushinda wote kuwajua wanao pindukia mipaka.
Na hakika hapana sababu yoyote au dalili ya kukuzuieni kula nyama aliye tajiwa jina la Mwenyezi Mungu Mtukufu juu yake wakati wa kuchinja miongoni mwa nyama hoa. (yaani nyama wa kufuga.) Na Mwenyezi Mungu Aliye takasika na Aliye tukuka amekwisha kubainishieni vilio harimishwa, katika hali isiyo kuwa ya dharura, kama mzoga na damu (na nguruwe). Watu wengi wanaacha Haki, si kwa lolote, ila kufuata pumbao la nafsi zao tu, bila ya kuwa wamepewa ilimu, au hoja iliyo thibiti kwao. Kama hao Waarabu walio jiharimishia wenyewe baadhi ya wanyama wa kufuga. Wala nyinyi hamna makosa kwa kula kilicho zaliwa, bali wao ndio wamepita mipaka kwa kuharimisha kilicho halali. Na Mwenyezi Mungu peke yake ndiye Mjuzi wa hao walio pindukia mipaka kwa ujuzi usio na mfano wake kwa hakika.
Na acheni dhambi zilizo dhaahiri na zilizo fichikana. Hakika wanao chuma dhambi watalipwa kwa waliyo kuwa wakiyachuma.
Sio uchamngu kuharimisha alicho halalisha Mwenyezi Mungu. Hakika uchamngu ni kuacha madhambi ya nje na ndani. Basi wacheni madhambi katika vitendo vyenu, vinavyo onekana na vilivyo fichika. Na bila ya shaka wanao chuma madhambi watalipwa kwa kadri ya madhambi wayatendayo.
Wala msile katika wale wasio somewa jina la Mwenyezi Mungu. Kwani huo ni upotofu. Na kwa yakini mashet'ani wanawafunza marafiki zao kubishana nanyi. Na mkiwafuata basi hapana shaka nyinyi mtakuwa washirikina.
Ilivyo kuwa hao wanyama ni halali kwenu kwa kuwachinja, basi msile yule ambaye hakutajiwa jina la Mwenyezi Mungu Mtukufu wakati wa kumchinja, ikiwa limeachwa kutajwa makusudi, au limetajwa jina jingine lisilo kuwa la Mwenyezi Mungu Mtukufu. Kwani hivyo ni upotovu, na kutokana na hukumu ya Mwenyezi Mungu! Na hakika majeuri, Iblisi na wasaidizi wake, huwatia tia katika vifua vya wale walio kwisha watawala, ili wajadiliane nanyi kwa upotovu, na wakupelekeeni kuharimisha alivyo halalisha Mwenyezi Mungu. Nanyi mkiwafuata mtakuwa mfano wao katika kumshirikisha Mwenyezi Mungu.
Je, aliye kuwa maiti kisha tukamhuisha, na tukamjaalia nuru inakwenda naye mbele za watu, mfano wake ni kama aliyoko gizani akawa hata hawezi kutoka humo? Kama hivyo makafiri wamepambiwa waliyo kuwa wakiyafanya.
Na nyinyi kwa Imani yenu si mfano wa washirikina hata kidogo. Basi haiwezi kuwa hali ya aliye kama maiti katika kupotea kwake, na Mwenyezi Mungu akampa nuru ya kuhidika, ambayo ni kama uhai, na akampa nuru ya Imani na hoja zilizo wazi, na kwa mwangaza wa nuru hiyo akaongoka na akawa anatembea nayo, haiwezi kuwa hali hiyo mfano wa hali ya ambaye kwamba anaishi katika giza lilio gubika. Na kama Mwenyezi Mungu alivyo ipamba Imani katika nyoyo za watu wa Imani, vile vile Shetani ameipamba shirki katika nafsi za madhaalimu wapinzani.
Kadhaalika katika kila mji tumewajaalia wakubwa wa wakosefu wao wafanye vitimbi ndani yake. Na wala hawafanyii vitimbi isipo kuwa nafsi zao, nao hawatambui.
Ewe Nabii! Usistaajabu ukiwaona wakuu wa wakosefu katika Makka wanapanga njama za shari za kila namna! Kwani huo ndio mtindo wao katika kila mji mkubwa. Wakuu wa wakosefu wake huwa kazi yao kuzua vitimbi vya shari. Na malipo ya uovu wake utakuja waangukia wenyewe, lakini wao hawatambui wala hawahisi.
Na inapo wajia Ishara, wao husema: Hatutoamini mpaka tupewe mfano wa walio pewa Mitume wa Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu ndiye Mjuzi kuliko wote kujua wapi anaweka ujumbe wake. Itawafikia hao walio kosa udhalili na adhabu kali kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa sababu ya vitimbi walivyo kuwa wakivifanya.
Hakika hawa wakuu wa wakosefu huwahusudu watu walio pewa na Mwenyezi Mungu ilimu, na Unabii, na uwongofu. Basi ikiwajia hoja ya kukata hawaikubali, lakini husema: Hatuikubali Haki mpaka tuteremshiwe wahyi kama wanavyo teremshiwa Mitume. Na hali ni Mwenyezi Mungu peke yake ndiye Mwenye ujuzi ambao haulingani na ujuzi wa mtu yoyote, kujua nani anaye stahiki kupata Utume wake. Ni Yeye ndiye anaye teuwa nani katika viumbe vyake ampe Utume wake. Hawa wenye inda, ikiwa wanataka ukubwa kwa inadi ya namna hii, basi watakuja pata unyonge na udhalili hapa duniani kwa sababu hiyo, na kesho Akhera watakuja pata adhabu kali kwa sababu ya huko kupanga kwao uwovu.
Contents of the translations can be downloaded and re-published, with the following terms and conditions:
1. No modification, addition, or deletion of the content.
2. Clearly referring to the publisher and the source (QuranEnc.com).
3. Mentioning the version number when re-publishing the translation.
4. Keeping the transcript information inside the document.
5. Notifying the source (QuranEnc.com) of any note on the translation.
6. Updating the translation according to the latest version issued from the source (QuranEnc.com).
7. Inappropriate advertisements must not be included when displaying translations of the meanings of the Noble Quran.
தேடல் முடிவுகள்:
API specs
Endpoints:
Sura translation
GET / https://quranenc.com/api/v1/translation/sura/{translation_key}/{sura_number} description: get the specified translation (by its translation_key) for the speicified sura (by its number)
Parameters: translation_key: (the key of the currently selected translation) sura_number: [1-114] (Sura number in the mosshaf which should be between 1 and 114)
Returns:
json object containing array of objects, each object contains the "sura", "aya", "translation" and "footnotes".
GET / https://quranenc.com/api/v1/translation/aya/{translation_key}/{sura_number}/{aya_number} description: get the specified translation (by its translation_key) for the speicified aya (by its number sura_number and aya_number)
Parameters: translation_key: (the key of the currently selected translation) sura_number: [1-114] (Sura number in the mosshaf which should be between 1 and 114) aya_number: [1-...] (Aya number in the sura)
Returns:
json object containing the "sura", "aya", "translation" and "footnotes".