పవిత్ర ఖురాన్ యొక్క భావార్థాల అనువాదం - స్వాహిలి అనువాదం * - అనువాదాల విషయసూచిక

XML CSV Excel API
Please review the Terms and Policies

భావార్ధాల అనువాదం వచనం: (12) సూరహ్: సూరహ్ ఫాతిర్
وَمَا يَسۡتَوِي ٱلۡبَحۡرَانِ هَٰذَا عَذۡبٞ فُرَاتٞ سَآئِغٞ شَرَابُهُۥ وَهَٰذَا مِلۡحٌ أُجَاجٞۖ وَمِن كُلّٖ تَأۡكُلُونَ لَحۡمٗا طَرِيّٗا وَتَسۡتَخۡرِجُونَ حِلۡيَةٗ تَلۡبَسُونَهَاۖ وَتَرَى ٱلۡفُلۡكَ فِيهِ مَوَاخِرَ لِتَبۡتَغُواْ مِن فَضۡلِهِۦ وَلَعَلَّكُمۡ تَشۡكُرُونَ
Na bahari mbili haziwi sawa; haya ni matamu yenye ladha, mazuri kunywa. Na haya ni ya chumvi, machungu. Na kutokana na bahari zote mnakula nyama mpya (isiyo chacha). Na mnatoa mapambo mnayo yavaa. Na unaona ndani yake marikebu zinakata maji ili mtafute fadhila zake, na ili mpate kushukuru.
Na haziwi sawa bahari mbili katika ujuzi wetu na makadirio yetu, ijapo kuwa zinashirikiana katika baadhi ya manufaa yao. Haya maji matamu yanakata kiu kwa uzuri wake, na utamu wake, na wepesi wake kuyanywa. Na haya mengine ni maji ya chumvi, uchumvi wake mkali. Na kutokana na namna zote mbili mnakula nyama mpya (fresh, haikuchacha) nayo ni samaki mnao wavua. Na mnatoa kutoka maji ya chumvi mapambo mnayo yavaa, kama lulu na marijani. Na wewe, mwenye kutazama, unaona vipi vyombo vya baharini vinavyo kwenda, vikipasua maji kwa mwendo wake, ili mkatafute baadhi ya fadhila za Mwenyezi Mungu kwa kufanya biashara, na ili asaa mpate kumshukuru Mola wenu Mlezi kwa neema hizi. Na katika Ishara za Mwenyezi Mungu ambazo anawaitia watu wazizingatie na ambazo amewaneemesha fadhila zake ni mwendo wa marikebu na kukata kwake maji baharini kwa mujibu wa kawaida zake alizo ziwekea katika tabia za maumbile, nazo ni hizo sharia za vitu kuelea, (The law of boayancy). Ni maarufu kuwa baadhi ya mapambo yanapatikana kutoka maji ya chumvi, na baadhi ya watu labda wanaona haiwi maji matamu kutoa mapambo vile vile. Lakini ilimu na mambo yalivyo yamethibitisha kinyume cha hivyo. Ama lulu kama zinavyo patikana katika maji ya chumvi, basi vile vile zinapatikana kwenye namna fulani nyengine za chaza wa mitoni. Hupatikana lulu katika maji matamu katika Uingereza, Scotland, Wales. Czechoslovakia na Japan.. n.k. mbali na lulu za baharini maarufu. Na pia vinaingia katika vinavyo patikana katika maji matamu maadini thamini ngumu kama almasi, zinazo patikana katika udongo unao tupwa na mito. Hupatikana pia Yaakuti, katika mito ya Mojok karibu na Andalas katika Burma ya juu. Ama katika Siam (Thailand) na Sri Lanka hupatikana Yaakuti katika mito. Na katika mawe ambayo yashabihiana na ya ghali na hutumiwa kwa pambo ni Topaz. Na hupatikana pia kwenye mito mwahali mwingi katika Brazil na Urusi (Ural na Siberia) Fluro-sylicate of aluminium. Aghlabu hiyo huwa ya manjano au rangi ya kahawia. Circom ni jiwe thamini linavutia. Sifa zake zinakaribia za Almasi. Namna zake nyingi hupatikana kwenye mito. (Kadhaalika dhahabu, ambayo inaitwa Alluvial gold yaani dhahabu ya mtoni, hupatikana nchi nyingi, mojawapo ni Zaire.)
అరబీ భాషలోని ఖుర్ఆన్ వ్యాఖ్యానాలు:
 
భావార్ధాల అనువాదం వచనం: (12) సూరహ్: సూరహ్ ఫాతిర్
సూరాల విషయసూచిక పేజీ నెంబరు
 
పవిత్ర ఖురాన్ యొక్క భావార్థాల అనువాదం - స్వాహిలి అనువాదం - అనువాదాల విషయసూచిక

స్వాహిలి భాషలో అల్ ఖుర్ఆన్ అల్ కరీమ్ భావానువాదం - అనువాదం ముహ్సిన్ అల్ బరూనీ

మూసివేయటం