Enyi mlio amini! Msitangulie mbele ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua.
Enyi mlio amini! Msitangulie na kulikata jambo lolote la kidini na la kidunia bila ya kukuamrisheni Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na jiwekeeni kinga ya nafsi zenu isikupateni adhabu ya Mwenyezi Mungu kwa kufuata sharia yake. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia baraabara yote mnayo yasema, ni Mwenye kuyajua vilivyo mambo yote.
Enyi mlio amini! Msinyanyue sauti zenu kuliko sauti ya Nabii, wala msiseme naye kwa kelele kama mnavyo semezana nyinyi kwa nyinyi, visije vitendo vyenu vikaharibika, na hali hamtambui.
Enyi mlio amini! Msinyanyue sauti zenu juu ya sauti ya Nabii anapo sema na nyinyi mnasema. Wala msipambanishe sauti zenu na sauti yake, kama mnapo semezana nyinyi kwa nyinyi, kwa kuchelea visiharibike vitendo vyenu bila ya nyinyi wenyewe kutambua.
Kwa hakika wanao teremsha sauti zao mbele ya Mtume wa Mwenyezi Mungu, hao ndio Mwenyezi Mungu amezisafisha nyoyo zao kwa uchamngu. Hao watakuwa na maghfira na ujira mkubwa.
Hakika wanao teremsha sauti zao katika baraza ya Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa kumtukuza yeye, hao peke yao ndio Mwenyezi Mungu amezisafisha nyoyo zao kwa uchamngu. Kwa wengineo si hivyo. Nao watapata msamaha mkubwa kufutiwa madhambi yao, na thawabu zilizo fika ukomo wa kufika kwake.
Na lau wao wangeli ngojea mpaka uwatokee ingeli kuwa kheri kwao. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye maghfira, Mwenye kurehemu.
Na lau kuwa hao wangeli ngojea, kwa kukufanyia adabu, mpaka ukatoka, bila ya shaka ingeli kuwa ni bora zaidi katika Dini yao. Na Mwenyezi Mungu ni Mkubwa wa kusamehe, Mwenye rehema kunjufu.
Enyi mlio amini! Akikujieni mpotovu na khabari yoyote, ichunguzeni, msije mkawasibu watu kwa kuto jua, na mkawa tena wenye kujuta kwa mliyo yatenda.
Enyi mlio amini! Akikujieni mtu ambaye yuko nje ya sharia ya Mwenyezi Mungu akakupeni khabari yoyote, basi chungueni mjue ukweli wake, kwa kuchelea msije mkawaletea watu madhara, kwa kutojua hali yao. Hapo tena baada ya kwisha dhihiri kuwa hawana makosa mkaingia katika majuto ya daima, mkatamani yasingeli kuwa.
Na jueni kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu yuko nanyi. Lau angeli kut'iini katika mambo mengi, bila ya shaka mngeli taabika. Lakini Mwenyezi Mungu amekupendezeeni Imani, na akaipamba katika nyoyo zenu, na amekufanyeni muuchukie ukafiri, na upotovu, na uasi. Hao ndio walio ongoka!
Na jueni, enyi Waumini, kwamba Mtume yuko nanyi. Basi mkadirieni kama anavyo stahiki kadiri yake, na msadikini. Lau yeye angeli wafuata walio wachache wa Imani kati yenu katika mambo mengi, basi hapana shaka mngeli ingia katika mashaka na hilaki. Lakini Mwenyezi Mungu amewapendezesha Imani wale walio kamilika katika nyinyi, na akaipamba katika nyoyo zenu. Basi jilindeni na kujipamba na yasiyo takikana. Na amekufanyeni mchukie kukufuru neema za Mwenyezi Mungu, na kutokana na sharia zake, na kwenda kinyume na amri zake. Hao tu, peke yao, ndio wanao ijua njia ya uwongofu na wameishikilia.
Kwa fadhila za Mwenyezi Mungu na neema zake. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye hikima.
Na hiyo ni fadhila tukufu na neema kubwa ya Mwenyezi Mungu juu yao. Na Mwenyezi Mungu amekizunguka kila kitu kwa ujuzi wake, ni Mwenye hikima ya kupita mpaka katika kuendesha kila jambo.
Na ikiwa makundi mawili katika Waumini yanapigana, basi yapatanisheni. Na likiwa moja la hao linamdhulumu mwenzie, basi lipigeni linalo dhulumu mpaka lirejee kwenye amri ya Mwenyezi Mungu. Na likirudi basi yapatanisheni kwa uadilifu. Na hukumuni kwa haki. Hakika Mwenyezi Mungu anawapenda wanao hukumu kwa haki.
Na ikiwa makundi mawili ya Waumini yanapigana, basi enyi Waumini, yapatanisheni. Ikiwa moja ndilo linalishambulia la pili, na likakataa kupatanishwa, basi lipigeni hilo linalo shambulia, mpaka lirejee kwenye hukumu ya Mwenyezi Mungu. Likirejea basi wapatanisheni kwa insafu. Na fanyeni uadilifu baina ya watu wote katika kila jambo. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wenye kufanya uadilifu.
Hakika Waumini ni ndugu, basi patanisheni baina ya ndugu zenu, na mcheni Mwenyezi Mungu ili mrehemewe.
Hakika wote wenye kumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake ni ndugu, Imani imezifanya nyoyo zao pamoja. Basi patanisheni baina ya ndugu zenu kwa kufuata udugu wa Imani. Na jiwekeeni nafsi zenu kinga cha kukinga adhabu ya Mwenyezi Mungu, kwa kufuata amri yake, na kuepuka anayo yakataza, na huku mkitaraji Mwenyezi Mungu akurehemuni kwa uchamngu wenu.
Enyi mlio amini! Wanaume wasiwadharau wanaume wenzao, wala wanawake wasiwadharau wanawake wenzao. Huenda hao wakawa bora kuliko wao. Wala msivunjiane hishima, wala msiitane kwa majina ya kejeli. Ni uovu kutumia jina baya baada ya kwisha amini. Na wasio tubu, hao ndio wenye kudhulumu.
Enyi mlio amini! Wanaume katika nyinyi wasiwadharau wanaume wenginewe, huenda hao mbele ya Mwenyezi Mungu wakawa bora kuliko wao. Wala wanawake Waumini wasiwadharau wanawake wenzao, huenda pengine wakawa hao ni bora kwa Mwenyezi Mungu kuliko wao. Wala msifanye kuaibishana nyinyi kwa nyinyi, wala mtu asimwite mwenzie kwa jina la kumuudhi. Ni uovu mno kwa Waumini kutajwa kwa upotovu baada ya kwisha sifika kwa Imani. Na wasio rudi wakaacha waliyo katazwa, basi hao peke yao ndio walio jidhulumu nafsi zao na wakawadhulumu wengineo.
Enyi mlio amini! Jiepusheni na dhana nyingi, kwani baadhi ya dhana ni dhambi. Wala msipelelezane, wala msisengenyane nyinyi kwa nyinyi. Je! Yupo katika nyinyi anaye penda kuila nyama ya nduguye aliye kufa? Mnalichukia hilo! Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kupokea toba, Mwenye kurehemu.
Enyi mlio amini, jitengeni mbali na wingi wa kudhania dhana mbovu kwa watu wa kheri. Kwani hakika baadhi ya dhana ni dhambi zinazo stahiki adhabu. Wala msiwe mkitafuta aibu za Waislamu. Wala msisengenyane, yaani kumsema mtu nyuma yake kwa jambo linalo muudhi. Hebu yupo yeyote kati yenu anaye penda kula nyama ya nduguye aliye kufa? Bila ya shaka hayo yanakuchukizeni! Basi ichukieni pia tabia ya kusengenyana na kusemana, kwani haya nayo ni mfano wa hayo. Na zikingeni nafsi zenu na adhabu ya Mwenyezi Mungu kwa kufuata amri zake, na kuyaepuka ayakatazayo. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mkubwa wa kukubali toba ya wenye kutubia, Mwenye rehema kunjufu kwa walimwengu wote.
Enyi watu! Hakika Sisi tumekuumbeni kutokana na mwanamume na mwanamke. Na tumekujaalieni kuwa ni mataifa na makabila ili mjuane. Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni huyo aliye mchamngu zaidi katika nyinyi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye khabari.
Enyi watu! Hakika Sisi tumekuumbeni nyinyi sawa sawa kutokana na asli moja, ya Adamu na Hawa. Na tukakufanyeni mkawa wengi kwa mataifa makubwa na makabila mengi, ili kutimie kujuana na kuawiniana baina yenu, sio kubaguana. Na hakika mwenye cheo cha juu miongoni mwenu kwa Mwenyezi Mungu duniani na Akhera ni yule anaye mcha Yeye zaidi. Hakika Mwenyezi Mungu amevizunguka vitu vyote kwa kuvijua, ni Mwenye khabari za dogo na kubwa la kila jambo.
Mabedui wamesema: Tumeamini. Sema: Hamjaamini, lakini semeni: Tumesilimu. Kwani Imani haijaingia katika nyoyo zenu. Na mkimt'ii Mwenyezi Mungu na Mtume wake, hatakupunguzieni chochote katika vitendo vyenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.
Wakaazi wa majangwani wamesema kwa ndimi zao: Tumeamini. Ewe Muhammad! Waambie: Bado hamjaamini; kwa sababu nyoyo zenu bado hazijasadiki hayo mnayo yatamka. Lakini nyinyi semeni: Tumefuata dhaahiri ya Ujumbe wako. Bado Imani haijaingia katika nyoyo zenu. Na mkimt'ii Mwenyezi Mungu na Mtume wake kwa kweli, hato kunyimeni hata chembe katika malipo ya vitendo vyenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mkubwa wa kuwasamehe waja wake, ni Mwenye rehema kunjufu kwa kila kitu.
Hakika Waumini ni wale walio muamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake tena wasitie shaka kabisa, na wakapigana Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu kwa mali yao na nafsi zao. Hao ndio wakweli.
Hakika Waumini wa kweli ni wale ambao wanamuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, kisha hapana shaka yoyote inayo ingia katika nyoyo zao kwa hayo wanayo yaamini; tena wakapigana Jihadi kwa kutoa mali yao na roho zao katika njia ya ut'iifu wa Mwenyezi Mungu. Hao peke yao ndio walio wakweli katika Imani yao.
Sema: Ati ndio mnamfundisha Mwenyezi Mungu Dini yenu, na hali Mwenyezi Mungu anayajua ya katika mbingu na ardhi, na Mwenyezi Mungu anajua kila kitu?
Ewe Muhammad! Waambie kwa kuwakanusha ile kauli yao kuwa wameamini: Ndio hivyo ati mnampa khabari Mwenyezi Mungu kuwa nyoyo zenu zimesadiki? Na Mwenyezi Mungu peke yake anajua kila kiliomo katika mbingu na katika ardhi. Na Mwenyezi Mungu amevizunguka vitu vyote kwa ujuzi wake.
Wanakusimbulia kuwa wamesilimu! Sema: Msinisimbulie kwa kusilimu kwenu. Bali Mwenyezi Mungu ndiye aliye kufanyieni hisani kwa kukuongoeni kwenye Imani, ikiwa nyinyi ni wakweli.
Wanaona kuwa kusilimu kwao ni kukuunga mkono wewe, Muhammad, na hivyo inastahiki wewe uwashukuru. Sema: Msinisimbulie kusilimu kwenu; kwani kheri yake mnaipata nyinyi. Bali ni Mwenyezi Mungu peke yake ndiye aliye kufanyieni ihsani kwa kukuongoeni kwenye Imani, ikiwa nyinyi ni wakweli katika hayo madai yenu.
Contents of the translations can be downloaded and re-published, with the following terms and conditions:
1. No modification, addition, or deletion of the content.
2. Clearly referring to the publisher and the source (QuranEnc.com).
3. Mentioning the version number when re-publishing the translation.
4. Keeping the transcript information inside the document.
5. Notifying the source (QuranEnc.com) of any note on the translation.
6. Updating the translation according to the latest version issued from the source (QuranEnc.com).
7. Inappropriate advertisements must not be included when displaying translations of the meanings of the Noble Quran.
అన్వేషణ ఫలితాలు:
API specs
Endpoints:
Sura translation
GET / https://quranenc.com/api/v1/translation/sura/{translation_key}/{sura_number} description: get the specified translation (by its translation_key) for the speicified sura (by its number)
Parameters: translation_key: (the key of the currently selected translation) sura_number: [1-114] (Sura number in the mosshaf which should be between 1 and 114)
Returns:
json object containing array of objects, each object contains the "sura", "aya", "translation" and "footnotes".
GET / https://quranenc.com/api/v1/translation/aya/{translation_key}/{sura_number}/{aya_number} description: get the specified translation (by its translation_key) for the speicified aya (by its number sura_number and aya_number)
Parameters: translation_key: (the key of the currently selected translation) sura_number: [1-114] (Sura number in the mosshaf which should be between 1 and 114) aya_number: [1-...] (Aya number in the sura)
Returns:
json object containing the "sura", "aya", "translation" and "footnotes".