Check out the new design

Kur'an-ı Kerim meal tercümesi - Savahili Dili Tercüme - Rowad Tercüme Merkezi * - Mealler fihristi


Anlam tercümesi Sure: Sûratu'l-En'âm   Ayet:
وَقَالُواْ هَٰذِهِۦٓ أَنۡعَٰمٞ وَحَرۡثٌ حِجۡرٞ لَّا يَطۡعَمُهَآ إِلَّا مَن نَّشَآءُ بِزَعۡمِهِمۡ وَأَنۡعَٰمٌ حُرِّمَتۡ ظُهُورُهَا وَأَنۡعَٰمٞ لَّا يَذۡكُرُونَ ٱسۡمَ ٱللَّهِ عَلَيۡهَا ٱفۡتِرَآءً عَلَيۡهِۚ سَيَجۡزِيهِم بِمَا كَانُواْ يَفۡتَرُونَ
Nao walisema: "Mifugo hawa na mimea ni miiko. Hawavili isipokuwa tumtakaye" - kwa madai yao tu. Na mifugo wengine imeharamishwa migongo. Na mifugo wengine hawalitaji jina la Mwenyezi Mungu juu yao, kwa kumzulia uongo tu. Atawalipa kwa hayo ya uongo waliyokuwa wakiyazua.
Arapça tefsirler:
وَقَالُواْ مَا فِي بُطُونِ هَٰذِهِ ٱلۡأَنۡعَٰمِ خَالِصَةٞ لِّذُكُورِنَا وَمُحَرَّمٌ عَلَىٰٓ أَزۡوَٰجِنَاۖ وَإِن يَكُن مَّيۡتَةٗ فَهُمۡ فِيهِ شُرَكَآءُۚ سَيَجۡزِيهِمۡ وَصۡفَهُمۡۚ إِنَّهُۥ حَكِيمٌ عَلِيمٞ
Na walisema: Vile vilivyo katika matumbo ya mifugo hawa ni vya wanaume wetu tu, na vimeharamishwa kwa wake zetu. Lakini wakiwa nyamafu, basi wanashirikiana ndani yake. Atawalipa maelezo yao hayo. Hakika Yeye ni Mwenye hekima, Mwenye kujua vyema.
Arapça tefsirler:
قَدۡ خَسِرَ ٱلَّذِينَ قَتَلُوٓاْ أَوۡلَٰدَهُمۡ سَفَهَۢا بِغَيۡرِ عِلۡمٖ وَحَرَّمُواْ مَا رَزَقَهُمُ ٱللَّهُ ٱفۡتِرَآءً عَلَى ٱللَّهِۚ قَدۡ ضَلُّواْ وَمَا كَانُواْ مُهۡتَدِينَ
Hakika walipata hasara wale waliowaua watoto wao kwa upumbavu bila ya elimu, na wakaharamisha vile alivyowaruzuku Mwenyezi Mungu kwa kumzulia Mwenyezi Mungu uongo. Hakika walipotea, wala hawakuwa wenye kuongoka.
Arapça tefsirler:
۞ وَهُوَ ٱلَّذِيٓ أَنشَأَ جَنَّٰتٖ مَّعۡرُوشَٰتٖ وَغَيۡرَ مَعۡرُوشَٰتٖ وَٱلنَّخۡلَ وَٱلزَّرۡعَ مُخۡتَلِفًا أُكُلُهُۥ وَٱلزَّيۡتُونَ وَٱلرُّمَّانَ مُتَشَٰبِهٗا وَغَيۡرَ مُتَشَٰبِهٖۚ كُلُواْ مِن ثَمَرِهِۦٓ إِذَآ أَثۡمَرَ وَءَاتُواْ حَقَّهُۥ يَوۡمَ حَصَادِهِۦۖ وَلَا تُسۡرِفُوٓاْۚ إِنَّهُۥ لَا يُحِبُّ ٱلۡمُسۡرِفِينَ
Na Yeye ndiye aliyeyaanzisha mabustani yenye kutambaa kwenye fito, na yasiyotambaa kwenye fito, na mitende, na mimea yenye vyakula mbali mbali, na mizaituni na mikomanga inayofanana na isiyofanana. Kuleni katika matunda yake inapozaa, na toeni haki yake siku ya kuvunwa kwake. Wala msitumie kwa kupitiliza. Hakika Yeye hawapendi watumiao kwa kupitiliza.
Arapça tefsirler:
وَمِنَ ٱلۡأَنۡعَٰمِ حَمُولَةٗ وَفَرۡشٗاۚ كُلُواْ مِمَّا رَزَقَكُمُ ٱللَّهُ وَلَا تَتَّبِعُواْ خُطُوَٰتِ ٱلشَّيۡطَٰنِۚ إِنَّهُۥ لَكُمۡ عَدُوّٞ مُّبِينٞ
Na katika mifugo kuna wale wabebao mizigo na kutoa matandiko. Kuleni katika vile alivyowaruzuku Mwenyezi Mungu, wala msifuate nyayo za Shetani. Hakika yeye kwenu ni adui wa wazi.
Arapça tefsirler:
 
Anlam tercümesi Sure: Sûratu'l-En'âm
Surelerin fihristi Sayfa numarası
 
Kur'an-ı Kerim meal tercümesi - Savahili Dili Tercüme - Rowad Tercüme Merkezi - Mealler fihristi

Rowad Tercüme Merkezi Ekibi tarafından Rabvede'ki Tebliğ, İrşat ve Toplum Bilinçlendirme Derneği ve Dünya dillerinde İslami içerik ve hizmet cemiyeti işbirliğiyle tercüme edilmiştir.

Kapat