Check out the new design

قرآن کریم کے معانی کا ترجمہ - سواحلی ترجمہ - مرکز رواد الترجمہ * - ترجمے کی لسٹ


معانی کا ترجمہ سورت: انعام   آیت:
وَقَالُواْ هَٰذِهِۦٓ أَنۡعَٰمٞ وَحَرۡثٌ حِجۡرٞ لَّا يَطۡعَمُهَآ إِلَّا مَن نَّشَآءُ بِزَعۡمِهِمۡ وَأَنۡعَٰمٌ حُرِّمَتۡ ظُهُورُهَا وَأَنۡعَٰمٞ لَّا يَذۡكُرُونَ ٱسۡمَ ٱللَّهِ عَلَيۡهَا ٱفۡتِرَآءً عَلَيۡهِۚ سَيَجۡزِيهِم بِمَا كَانُواْ يَفۡتَرُونَ
Nao walisema: "Mifugo hawa na mimea ni miiko. Hawavili isipokuwa tumtakaye" - kwa madai yao tu. Na mifugo wengine imeharimishwa migongo. Na mifugo wengine hawalitaji jina la Mwenyezi Mungu juu yao, kwa kumzulia uongo tu. Atawalipa kwa hayo ya uongo waliyokuwa wakiyazua.
عربی تفاسیر:
وَقَالُواْ مَا فِي بُطُونِ هَٰذِهِ ٱلۡأَنۡعَٰمِ خَالِصَةٞ لِّذُكُورِنَا وَمُحَرَّمٌ عَلَىٰٓ أَزۡوَٰجِنَاۖ وَإِن يَكُن مَّيۡتَةٗ فَهُمۡ فِيهِ شُرَكَآءُۚ سَيَجۡزِيهِمۡ وَصۡفَهُمۡۚ إِنَّهُۥ حَكِيمٌ عَلِيمٞ
Na walisema: Vile vilivyo katika matumbo ya mifugo hawa ni ya wanaume wetu tu, na vimeharimishwa kwa wake zetu. Lakini wakiwa nyamafu, basi wanashirikiana ndani yake. Atawalipa maelezo yao hayo. Hakika Yeye ni Mwenye hekima kubwa, Mwenye kujua vyema.
عربی تفاسیر:
قَدۡ خَسِرَ ٱلَّذِينَ قَتَلُوٓاْ أَوۡلَٰدَهُمۡ سَفَهَۢا بِغَيۡرِ عِلۡمٖ وَحَرَّمُواْ مَا رَزَقَهُمُ ٱللَّهُ ٱفۡتِرَآءً عَلَى ٱللَّهِۚ قَدۡ ضَلُّواْ وَمَا كَانُواْ مُهۡتَدِينَ
Hakika walipata hasara wale waliowaua watoto wao kwa upumbavu bila ya elimu, na wakaharimisha vile alivyowaruzuku Mwenyezi Mungu kwa kumzulia Mwenyezi Mungu uongo. Hakika walipotea, wala hawakuwa wenye kuongoka.
عربی تفاسیر:
۞ وَهُوَ ٱلَّذِيٓ أَنشَأَ جَنَّٰتٖ مَّعۡرُوشَٰتٖ وَغَيۡرَ مَعۡرُوشَٰتٖ وَٱلنَّخۡلَ وَٱلزَّرۡعَ مُخۡتَلِفًا أُكُلُهُۥ وَٱلزَّيۡتُونَ وَٱلرُّمَّانَ مُتَشَٰبِهٗا وَغَيۡرَ مُتَشَٰبِهٖۚ كُلُواْ مِن ثَمَرِهِۦٓ إِذَآ أَثۡمَرَ وَءَاتُواْ حَقَّهُۥ يَوۡمَ حَصَادِهِۦۖ وَلَا تُسۡرِفُوٓاْۚ إِنَّهُۥ لَا يُحِبُّ ٱلۡمُسۡرِفِينَ
Na Yeye ndiye aliyeziumba mabustani yenye kutambaa kwenye fito, na yasiyotambaa kwenye fito, na mitende, na mimea yenye vyakula mbali mbali, na mizaituni na mikomanga inayofanana na isiyofanana. Kuleni katika matunda yake inapozaa, na toeni haki yake siku ya kuvunwa kwake. Wala msitumie kwa kupitiliza. Hakika Yeye hawapendi watumiao kwa kupitiliza.
عربی تفاسیر:
وَمِنَ ٱلۡأَنۡعَٰمِ حَمُولَةٗ وَفَرۡشٗاۚ كُلُواْ مِمَّا رَزَقَكُمُ ٱللَّهُ وَلَا تَتَّبِعُواْ خُطُوَٰتِ ٱلشَّيۡطَٰنِۚ إِنَّهُۥ لَكُمۡ عَدُوّٞ مُّبِينٞ
Na katika mifugo kuna wale wabebao mizigo na kutoa matandiko. Kuleni katika vile alivyowaruzuku Mwenyezi Mungu, wala msifuate nyayo za Shetani. Hakika yeye kwenu ni adui wa wazi.
عربی تفاسیر:
 
معانی کا ترجمہ سورت: انعام
سورتوں کی لسٹ صفحہ نمبر
 
قرآن کریم کے معانی کا ترجمہ - سواحلی ترجمہ - مرکز رواد الترجمہ - ترجمے کی لسٹ

مرکز رواد الترجمہ گروپ نے جمعیۃ الدعوۃ‘ ربوہ اور جمعیۃ خدمۃ المحتوى الاسلامی باللغات کے تعاون سے ترجمہ کیا۔

بند کریں