Check out the new design

Kur'an-ı Kerim meal tercümesi - Savahili Dili Tercüme - Rowad Tercüme Merkezi * - Mealler fihristi


Anlam tercümesi Sure: Sûretu'l-Hakkâh   Ayet:
وَجَآءَ فِرۡعَوۡنُ وَمَن قَبۡلَهُۥ وَٱلۡمُؤۡتَفِكَٰتُ بِٱلۡخَاطِئَةِ
Na Firauni na waliomtangulia, na miji iliyopinduliwa chini juu, walileta khatia.
Arapça tefsirler:
فَعَصَوۡاْ رَسُولَ رَبِّهِمۡ فَأَخَذَهُمۡ أَخۡذَةٗ رَّابِيَةً
akamuasi Mtume wa Mola wao Mlezi, ndipo Yeye Mola akawakamata kwa mkamato uliozidi nguvu.
Arapça tefsirler:
إِنَّا لَمَّا طَغَا ٱلۡمَآءُ حَمَلۡنَٰكُمۡ فِي ٱلۡجَارِيَةِ
Maji yalipofurika Sisi tulikupandisheni katika safina.
Arapça tefsirler:
لِنَجۡعَلَهَا لَكُمۡ تَذۡكِرَةٗ وَتَعِيَهَآ أُذُنٞ وَٰعِيَةٞ
Ili tuyafanye hayo kuwa ni waadhi kwenu na kila sikio linalosikia liyahifadhi.
Arapça tefsirler:
فَإِذَا نُفِخَ فِي ٱلصُّورِ نَفۡخَةٞ وَٰحِدَةٞ
Na litapopulizwa barugumu mpulizo mmoja tu.
Arapça tefsirler:
وَحُمِلَتِ ٱلۡأَرۡضُ وَٱلۡجِبَالُ فَدُكَّتَا دَكَّةٗ وَٰحِدَةٗ
Na ardhi na milima ikaondolewa, na ikavunjwa kwa mvunjo mmoja.
Arapça tefsirler:
فَيَوۡمَئِذٖ وَقَعَتِ ٱلۡوَاقِعَةُ
Siku hiyo ndio Tukio litatukia.
Arapça tefsirler:
وَٱنشَقَّتِ ٱلسَّمَآءُ فَهِيَ يَوۡمَئِذٖ وَاهِيَةٞ
Na mbingu zitapasuka, kwani siku hiyo zitakuwa dhaifu kabisa.
Arapça tefsirler:
وَٱلۡمَلَكُ عَلَىٰٓ أَرۡجَآئِهَاۚ وَيَحۡمِلُ عَرۡشَ رَبِّكَ فَوۡقَهُمۡ يَوۡمَئِذٖ ثَمَٰنِيَةٞ
Na Malaika watakuwa pembezoni mwa mbingu; na wanane juu ya hawa watakuwa wamebeba Kiti cha Enzi cha Mola wako Mlezi.
Arapça tefsirler:
يَوۡمَئِذٖ تُعۡرَضُونَ لَا تَخۡفَىٰ مِنكُمۡ خَافِيَةٞ
Siku hiyo mtahudhurishwa - haitafichika siri yoyote yenu.
Arapça tefsirler:
فَأَمَّا مَنۡ أُوتِيَ كِتَٰبَهُۥ بِيَمِينِهِۦ فَيَقُولُ هَآؤُمُ ٱقۡرَءُواْ كِتَٰبِيَهۡ
Basi ama atakayepewa kitabu chake kwa mkono wake wa kulia, atasema: Haya someni kitabu changu!
Arapça tefsirler:
إِنِّي ظَنَنتُ أَنِّي مُلَٰقٍ حِسَابِيَهۡ
Hakika nilijua ya kuwa nitapokea hisabu yangu.
Arapça tefsirler:
فَهُوَ فِي عِيشَةٖ رَّاضِيَةٖ
Basi yeye atakuwa katika maisha ya kupendeza.
Arapça tefsirler:
فِي جَنَّةٍ عَالِيَةٖ
Katika Bustani ya juu.
Arapça tefsirler:
قُطُوفُهَا دَانِيَةٞ
Matunda yake ya karibu.
Arapça tefsirler:
كُلُواْ وَٱشۡرَبُواْ هَنِيٓـَٔۢا بِمَآ أَسۡلَفۡتُمۡ فِي ٱلۡأَيَّامِ ٱلۡخَالِيَةِ
Waambiwe: Kuleni na mnywe kwa furaha kwa sababu ya mlivyotanguliza katika siku zilizopita.
Arapça tefsirler:
وَأَمَّا مَنۡ أُوتِيَ كِتَٰبَهُۥ بِشِمَالِهِۦ فَيَقُولُ يَٰلَيۡتَنِي لَمۡ أُوتَ كِتَٰبِيَهۡ
Na ama atakayepewa kitabu chake katika mkono wake wa kushoto, basi yeye atasema: Laiti nisingelipewa kitabu changu!
Arapça tefsirler:
وَلَمۡ أَدۡرِ مَا حِسَابِيَهۡ
Wala nisingelijua nini hisabu yangu.
Arapça tefsirler:
يَٰلَيۡتَهَا كَانَتِ ٱلۡقَاضِيَةَ
Laiti mauti ndiyo yangelikuwa ya kunimaliza kabisa.
Arapça tefsirler:
مَآ أَغۡنَىٰ عَنِّي مَالِيَهۡۜ
Mali yangu hayakunifaa kitu.
Arapça tefsirler:
هَلَكَ عَنِّي سُلۡطَٰنِيَهۡ
Madaraka yangu yamenipotea.
Arapça tefsirler:
خُذُوهُ فَغُلُّوهُ
(Pasemwe): Mshikeni! Mtieni pingu!
Arapça tefsirler:
ثُمَّ ٱلۡجَحِيمَ صَلُّوهُ
Kisha mtupeni Motoni!
Arapça tefsirler:
ثُمَّ فِي سِلۡسِلَةٖ ذَرۡعُهَا سَبۡعُونَ ذِرَاعٗا فَٱسۡلُكُوهُ
Tena mtatizeni katika mnyororo wenye urefu wa dhiraa sabini!
Arapça tefsirler:
إِنَّهُۥ كَانَ لَا يُؤۡمِنُ بِٱللَّهِ ٱلۡعَظِيمِ
Kwani huyo hakika alikuwa hamuamini Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Arapça tefsirler:
وَلَا يَحُضُّ عَلَىٰ طَعَامِ ٱلۡمِسۡكِينِ
Wala hahimizi kulisha masikini.
Arapça tefsirler:
فَلَيۡسَ لَهُ ٱلۡيَوۡمَ هَٰهُنَا حَمِيمٞ
Basi leo hapa hana jamaa wa kumwonea uchungu.
Arapça tefsirler:
 
Anlam tercümesi Sure: Sûretu'l-Hakkâh
Surelerin fihristi Sayfa numarası
 
Kur'an-ı Kerim meal tercümesi - Savahili Dili Tercüme - Rowad Tercüme Merkezi - Mealler fihristi

Rowad Tercüme Merkezi Ekibi tarafından Rabvede'ki Tebliğ, İrşat ve Toplum Bilinçlendirme Derneği ve Dünya dillerinde İslami içerik ve hizmet cemiyeti işbirliğiyle tercüme edilmiştir.

Kapat