Check out the new design

قرآن کریم کے معانی کا ترجمہ - سواحلی ترجمہ - عبد اللہ محمد اور ناصر خمیس * - ترجمے کی لسٹ


معانی کا ترجمہ سورت: لیل   آیت:

Al-Lail

وَٱلَّيۡلِ إِذَا يَغۡشَىٰ
Mwenyezi Mungu Anaapa kwa usiku unapoifinika ardhi na vilivyoko juu yake kwa giza lake.
عربی تفاسیر:
وَٱلنَّهَارِ إِذَا تَجَلَّىٰ
Na kwa mchana unapofunuka mwangaza wake kutoka kwenye giza la usiku.
عربی تفاسیر:
وَمَا خَلَقَ ٱلذَّكَرَ وَٱلۡأُنثَىٰٓ
Na kwa kuumba mbea mbili: ya kiume na ya kike,
عربی تفاسیر:
إِنَّ سَعۡيَكُمۡ لَشَتَّىٰ
Kuwa vitendo vyenu vinatofautiana: kuna wenye kufanyia dunia na wenye kufanyia Akhera.
عربی تفاسیر:
فَأَمَّا مَنۡ أَعۡطَىٰ وَٱتَّقَىٰ
Ama mwenye kutoa kwenye mali yake, akamcha Mwenyezi Mungu katika huko kutoa,
عربی تفاسیر:
وَصَدَّقَ بِٱلۡحُسۡنَىٰ
akaamini «Lā Ilāha Illā Allāh» na yanayotakiwa na Imani hiyo na akaamini malipo yanayofungamana nayo,
عربی تفاسیر:
فَسَنُيَسِّرُهُۥ لِلۡيُسۡرَىٰ
Tutamuongoza na kumuafikia njia za kheri na wema na kumsahilishia mambo yake.
عربی تفاسیر:
وَأَمَّا مَنۢ بَخِلَ وَٱسۡتَغۡنَىٰ
Na ama mwenye kuyafanyia ubakhili mali yake, asiwe na haja ya malipo ya Mola wake,
عربی تفاسیر:
وَكَذَّبَ بِٱلۡحُسۡنَىٰ
akakanusha neno la «Lā Ilāha Illā Allāh» na yanayotakiwa na neno hilo na akakanusha malipo yanayofungamana nalo,
عربی تفاسیر:
 
معانی کا ترجمہ سورت: لیل
سورتوں کی لسٹ صفحہ نمبر
 
قرآن کریم کے معانی کا ترجمہ - سواحلی ترجمہ - عبد اللہ محمد اور ناصر خمیس - ترجمے کی لسٹ

ڈاکٹر عبد اللہ محمد ابو بکر اور شیخ ناصر خمیس نے ترجمہ کیا ہے۔

بند کریں