Enyi mlio amini! Mnapo simama kwa ajili ya Swala basi osheni nyuso zenu, na mikono yenu mpaka vifundoni, na mpake vichwa vyenu, na osheni miguu yenu mpaka vifundoni. Na mkiwa na janaba basi ogeni. Na mkiwa wagonjwa au mmo safarini, au mmoja wenu ametoka chooni au mmewagusa wanawake, na hamkupata maji, basi tayamamuni vumbi lilio safi, na mpake nyuso zenu na mikono yenu. Hapendi Mwenyezi Mungu kukutieni katika taabu; bali anataka kukutakaseni na kutimiza neema yake juu yenu ili mpate kushukuru.
Enyi Waumini! Mkitaka kuswali nanyi hamna udhu, tawadhini kwa kukosha nyuso zenu, na mikono yenu mpaka vifundoni, na mpake maji kichwa kizima au baadhi yake. Na mkoshe miguu yenu mpaka vifundoni. Mnapo taka kuswali nanyi mna janaba kwa kuingiliana na wake zenu, basi kogeni mwili mzima. Ikiwa mna maradhi ambayo hayakufaliini kutumia maji, au mpo safarini na ipo taabu ya maji, au mmetoka chooni kukidhi haja, au mmeingiliana (kwa lugha ya Qur'ani "kugusana") na wanawake na msipate maji, basi inakupaseni kutayamamu, yaani kujipaka vumbi lilio safi. Na hayo ni kwa kupangusa kwa hilo vumbi nyuso zenu na mikono yenu. Na Mwenyezi Mungu hataki kukudhikini katika hayo anayo kuamrisheni, bali anakupeni sharia za kukusafisheni ndani na nje, ili atimize neema zake juu yenu kwa uwongofu, na kubainisha na kusahilisha, mpate kumshukuru kwa uwongofu wake na kutimilia neema yake kwa kudumisha ut'iifu kwake. T'ahara (Usafi) wa Kiislamu una maana mbili: Moja ni kumwelekea Mwenyezi Mungu Mtukufu moyoni kwa kujiweka tayari kwa hayo, na kufunga azimio kusimama mbele yake na hali ni mwenye nafsi iliyo t'aahiri, na moyo ulio safi kabisa kwake Yeye tu. Pili ni unadhifu wa dhaahiri kwa udhu. Na katika hayo ni kuvikosha viungo vyote vinavyo weza kuchafuka. Na udhu ni jambo la kufanywa mara kwa mara, na huweza kufika hata kutwa mara tano. Pia kuna kukoga unapo ingiliana na mke, na wakati wa damu ya mwezi na uzazi. Udhu na kukoga ni kuondoa takataka zenye vijidudu vya maradhi, na pia huleta uchangamfu kwa kusisimua damu ya kwenye ngozi, na kupoza mishipa. Na kwa hivyo Mtume s.a.w. aliusia: "Ukihamaki tawadha".
Na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu iliyo juu yenu, na ahadi yake aliyo fungamana nanyi mlipo sema: Tumesikia na tumet'ii. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi sana wa yaliyomo vifuani.
Kumbukeni, enyi Waumini, neema za Mwenyezi Mungu alizo kuneemesheni kwa kukuongoeni kwenye Uislamu. Jitahidini kutimiza ahadi yake aliyo itaka kwenu wakati mlipo muunga mkono Mtume wake, Muhammad, kuwa mtamsikia na mtamt'ii. Na mcheni Mwenyezi Mungu kwa kuzihifadhi ahadi hizi. Yeye, Subhanahu, ni Mjuzi sana wa yote yaliyo fichikana nyoyoni mwenu, naye atakulipeni kwayo.
Enyi mlio amini! Kuweni wasimamizi madhubuti kwa ajili ya Mwenyezi Mungu mkitoa ushahidi kwa haki. Wala kuchukiana na watu kusikupelekeeni kutofanya uadilifu. Fanyeni uadilifu. Hivyo ndio kuwa karibu mno na uchamngu. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu anazo khabari za mnayo yatenda.
Enyi Waumini! Jitahidini kutimiza haki za Mwenyezi Mungu, na shuhudieni kwa haki baina ya watu. Chuki zenu kubwa kwa watu fulani zisikupelekeeni mkaacha kuwafanyia uadilifu. Bali jilazimisheni uadilifu, kwani hiyo ndiyo njia ya kupelekea kumcha Mwenyezi Mungu, na kuepukana na ghadhabu yake. Na mcheni Mwenyezi Mungu katika mambo yenu yote; kwani Yeye, Sub hanahu, anayajua vilivyo yote mnayo yafanya, naye atakulipeni kwayo. Uislamu unalingania uadilifu moja kwa moja, sawa kwa rafiki na adui.Haifai chuki ikakupelekea kudhulumu. Na hayo unapo amiliana na watu, na kuamiliana baina ya dola ya Kiislamu na dola nyenginezo. Na kumfanyia uadilifu adui kunaambiwa na Qur'ani kuwa ni karibu zaidi na uchamngu na usafi wa kidini. Lau kuwa wasia huu ungeli tumiwa katika sharia za baina ya madola basi pasingeli kuwapo vita. Kama kila dini ina kitambulisho chake na alama, basi kitambulisho cha Uislamu ni Dini ya Mungu Mmoja na Uadilifu.
Contents of the translations can be downloaded and re-published, with the following terms and conditions:
1. No modification, addition, or deletion of the content.
2. Clearly referring to the publisher and the source (QuranEnc.com).
3. Mentioning the version number when re-publishing the translation.
4. Keeping the transcript information inside the document.
5. Notifying the source (QuranEnc.com) of any note on the translation.
6. Updating the translation according to the latest version issued from the source (QuranEnc.com).
7. Inappropriate advertisements must not be included when displaying translations of the meanings of the Noble Quran.
Излов натижалари:
API specs
Endpoints:
Sura translation
GET / https://quranenc.com/api/v1/translation/sura/{translation_key}/{sura_number} description: get the specified translation (by its translation_key) for the speicified sura (by its number)
Parameters: translation_key: (the key of the currently selected translation) sura_number: [1-114] (Sura number in the mosshaf which should be between 1 and 114)
Returns:
json object containing array of objects, each object contains the "sura", "aya", "translation" and "footnotes".
GET / https://quranenc.com/api/v1/translation/aya/{translation_key}/{sura_number}/{aya_number} description: get the specified translation (by its translation_key) for the speicified aya (by its number sura_number and aya_number)
Parameters: translation_key: (the key of the currently selected translation) sura_number: [1-114] (Sura number in the mosshaf which should be between 1 and 114) aya_number: [1-...] (Aya number in the sura)
Returns:
json object containing the "sura", "aya", "translation" and "footnotes".