ترجمة معاني القرآن الكريم - الترجمة السواحلية - علي محسن البرواني * - فهرس التراجم

XML CSV Excel API
تنزيل الملفات يتضمن الموافقة على هذه الشروط والسياسات

ترجمة معاني آية: (31) سورة: يونس
قُلۡ مَن يَرۡزُقُكُم مِّنَ ٱلسَّمَآءِ وَٱلۡأَرۡضِ أَمَّن يَمۡلِكُ ٱلسَّمۡعَ وَٱلۡأَبۡصَٰرَ وَمَن يُخۡرِجُ ٱلۡحَيَّ مِنَ ٱلۡمَيِّتِ وَيُخۡرِجُ ٱلۡمَيِّتَ مِنَ ٱلۡحَيِّ وَمَن يُدَبِّرُ ٱلۡأَمۡرَۚ فَسَيَقُولُونَ ٱللَّهُۚ فَقُلۡ أَفَلَا تَتَّقُونَ
Sema: Ni nani anaye kuruzukuni kutoka mbinguni na kwenye ardhi? Au ni nani anaye miliki kusikia na kuona? Na nani amtoaye hai kutoka maiti, na akamtoa maiti kutoka aliye hai? Na nani anaye yadabiri mambo yote? Watasema:Allah, Mwenyezi Mungu. Basi sema: Je! Hamchi?
Ewe Mtume! Lingania kwenye Tawhidi safi, na useme: Nani anaye kuleteeni riziki kutoka mbinguni inapo teremka mvua, na katika ardhi inapo mea mimea na kuzaa? Na nani aliye kupeni kusikia na kuona? Na nani anaye toa vilio hai kutokana na vilio maiti, kama mimea, nayo ni hai kutokana na ardhi maiti? Nani anaye mtoa maiti kutokana na hai, kama mtu anavyo kufa? Na nani anaye panga na kuendesha mambo yote ya ulimwengu kwa kudra yake na hikima yake? Wataungama: Hapana pa kukimbilia! Kwa hakika ni Mwenyezi Mungu peke yake ndiye mtenda yote. Ewe Mtume! Waambie watapo ungama: Si waajibu mkubwa kuit'ii Haki, na kumkhofu Mwenyezi Mungu, Mmiliki Ufalme wote?
التفاسير العربية:
 
ترجمة معاني آية: (31) سورة: يونس
فهرس السور رقم الصفحة
 
ترجمة معاني القرآن الكريم - الترجمة السواحلية - علي محسن البرواني - فهرس التراجم

ترجمة معاني القرآن الكريم إلى اللغة السواحلية، ترجمها علي محسن البرواني.

إغلاق