للإطلاع على الموقع بحلته الجديدة

ترجمة معاني القرآن الكريم - الترجمة السواحلية - علي محسن البرواني * - فهرس التراجم

XML CSV Excel API
تنزيل الملفات يتضمن الموافقة على هذه الشروط والسياسات

ترجمة معاني سورة: الشعراء   آية:
قَالَ فَعَلۡتُهَآ إِذٗا وَأَنَا۠ مِنَ ٱلضَّآلِّينَ
(Musa) akasema: Nilitenda hayo hapo nilipo kuwa miongoni mwa wale walio potea.
Musa akasema: Niliyafanya uliyo yataja kwa kutojua yanayo faa kutambulikana kwa akili nayo ni jambo la kuuwa. Basi hapana masimbulizi juu yangu.
التفاسير العربية:
فَفَرَرۡتُ مِنكُمۡ لَمَّا خِفۡتُكُمۡ فَوَهَبَ لِي رَبِّي حُكۡمٗا وَجَعَلَنِي مِنَ ٱلۡمُرۡسَلِينَ
Basi nilikukimbieni nilipo kuogopeni, tena Mola wangu Mlezi, akanitunukia hukumu, na akanijaali niwe miongoni mwa Mitume.
Nikakukimbieni nilipo khofu kuwa mtakuja niuwa kwa jinaya hii ambayo sikuukusudia. Mola wangu Mlezi akanitunukia fahamu na ilimu, kwa fadhila zake na neema zake, na akanifanya mmoja katika Mitume.
التفاسير العربية:
وَتِلۡكَ نِعۡمَةٞ تَمُنُّهَا عَلَيَّ أَنۡ عَبَّدتَّ بَنِيٓ إِسۡرَٰٓءِيلَ
Na hiyo ndiyo neema ya kunisumbulia, na wewe umewatia utumwani Wana wa Israili?
Musa akaashiria sifa katika sifa ovu kabisa za Firauni, nayo ni kuwa kawafanya watumwa Wana wa Israili, na akiwauwa watoto wao wanaume. Na akakataa kukuita kule kulelewa kwake katika jumba la Firauni kuwa ni neema, kwani yaliyo sabibisha hayo ni yale aliyo kwisha yataja, ndio yeye alitupwa mtoni aokoke asiuliwe. Akaishia kwenye jumba la Firauni. Na lau kuwa si hivyo basi angeli lelewa na wazazi wake.
التفاسير العربية:
قَالَ فِرۡعَوۡنُ وَمَا رَبُّ ٱلۡعَٰلَمِينَ
Firauni akasema: Na nani huyo Mola Mlezi wa walimwengu wote?
Firauni akasema: Na nini hizo sifa za Mola Mlezi wa walimwengu wote ambaye unakithiri kumtaja, na wewe unadai kuwa ni Mtume wake, na hali sisi hatujui lolote khabari zake?
التفاسير العربية:
قَالَ رَبُّ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَمَا بَيۡنَهُمَآۖ إِن كُنتُم مُّوقِنِينَ
Akasema: Ndiye Mola Mlezi wa mbingu na ardhi, na viliomo baina yao, ikiwa nyinyi ni wenye yakini.
Musa akasema: Yeye huyo ndiye Mwenye kuzimiliki mbingu na ardhi na kila kilio baina yao. Ikiwa nyinyi mna yakini ya ukweli wa jawabu hii basi mtanafiika, na mtaongoka, na mtajua kuwa ufalme wa Firauni wa kujidai haufui dafu mbele ya Ufalme wake Mwenyezi Mungu. Kwani ufalme wa Firauni haupindukii hata eneo moja katika hii dunia.
التفاسير العربية:
قَالَ لِمَنۡ حَوۡلَهُۥٓ أَلَا تَسۡتَمِعُونَ
(Firauni) akawaambia walio mzunguka: Hamsikilizi?
Firauni kuonyesha mastaajabu kwa wale walio mzunguka kwa kuwa Musa katika jawabu yake alipo mtaja Mola wake Mlezi na akadhukuru Ufalme wake hakuugusia hata kidogo ufalme wa Firauni, alisema: Mwayasikiaje maneno ya Musa?
التفاسير العربية:
قَالَ رَبُّكُمۡ وَرَبُّ ءَابَآئِكُمُ ٱلۡأَوَّلِينَ
(Musa) akasema: Ndiye Mola wenu Mlezi, na Mola Mlezi wa baba zenu wa kwanza.
Musa akiendelea na usemi wake bila ya kujali hasira za Firauni na uchafu wa maneno yake, akasema: Ndiye huyo Mola Mlezi wa walimwengu wote, aliye kuumbeni nyinyi na baba zenu walio tangulia. Na miongoni mwa hao walikuwako walio dai ungu kama unavyo dai wewe. Na wao wameteketea. Na wewe utateketea, na hayo unayo yadai yatapotelea mbali. Kwani Mungu wa kweli hafi.
التفاسير العربية:
قَالَ إِنَّ رَسُولَكُمُ ٱلَّذِيٓ أُرۡسِلَ إِلَيۡكُمۡ لَمَجۡنُونٞ
(Firauni) akasema: Hakika huyu Mtume wenu aliye tumwa kwenu ni mwendawazimu.
Firauni akwaambia watu wake yale yanayo mtibuwa roho na kumghadhibisha, akautaja Utume wa Musa ni kwao wao, wala si kwake yeye, na akambandikiza wazimu, kwa kuwa ati akiulizwa kitu hujibu kingine, na anamsifu Mola Mlezi kwa sifa za kiajabu ajabu. Na kwa hivyo Firauni anawahimiza wamkadhibishe.
التفاسير العربية:
قَالَ رَبُّ ٱلۡمَشۡرِقِ وَٱلۡمَغۡرِبِ وَمَا بَيۡنَهُمَآۖ إِن كُنتُمۡ تَعۡقِلُونَ
. (Musa) akasema: Ndiye Mola Mlezi wa Mashariki na Magharibi na viliomo baina yao, ikiwa nyinyi mnatia akilini.
Musa akasema: Ikiwa nyinyi mna akili, basi uaminini Ujumbe wangu. Kwani kuchomoza jua na kuchwa kwake kwa mpango madhubuti ni dalili wazi ya Mwenye kuumba. Kwa hivyo basi ni nyinyi ndio mnastahiki kuambiwa wendawazimu.
التفاسير العربية:
قَالَ لَئِنِ ٱتَّخَذۡتَ إِلَٰهًا غَيۡرِي لَأَجۡعَلَنَّكَ مِنَ ٱلۡمَسۡجُونِينَ
(Firauni) akasema: Ukimfuata mungu mwengine asiye kuwa mimi, basi bila ya shaka nitakufunga gerezani.
Firauni akamwambia Musa: Ukimfuata mungu yeyote badala yangu mimi, utakuwa mmoja katika wanao ijua hali yao mbaya katika magereza yangu. Na yeye Firauni kaangukia kitisho hichi baada ya kushindwa kuondoa athari za kazi za Muumbaji.
التفاسير العربية:
قَالَ أَوَلَوۡ جِئۡتُكَ بِشَيۡءٖ مُّبِينٖ
Akasema: Je! Ijapo kuwa nitakuletea kitu cha kubainisha wazi?
Musa akasema kwa upole kwa kutumai asaa akaamini: Utanitia gerezani hata nikikuletea ushahidi mkubwa wa ukweli wa haya niyasemayo?
التفاسير العربية:
قَالَ فَأۡتِ بِهِۦٓ إِن كُنتَ مِنَ ٱلصَّٰدِقِينَ
Akasema: Kilete basi, kama wewe ni katika wasemao kweli.
Firauni akasema: Ulete ushahidi utao onyesha Unabii wako kama wewe kweli unasema kweli katika wito wako. Kasema hayo kwa tamaa ya kuwa huenda akapata kipengee cha udhaifu katika hoja zake.
التفاسير العربية:
فَأَلۡقَىٰ عَصَاهُ فَإِذَا هِيَ ثُعۡبَانٞ مُّبِينٞ
Basi akaitupa fimbo yake, mara ikawa nyoka wa kuonekana dhaahiri.
Musa akaitupa fimbo yake mbele yao. Ikageuka nyoka kweli kweli, si kitu cha uwongo cha uchawi kinacho fanana na nyoka.
التفاسير العربية:
وَنَزَعَ يَدَهُۥ فَإِذَا هِيَ بَيۡضَآءُ لِلنَّٰظِرِينَ
Na akautoa mkono wake, na mara ukawa mweupe kwa watazamao.
Musa akautoa mkono wake kutoka mfukoni mwake. Hiyo ni Ishara ya pili. Nao ukawa mweupe, bila ya maradhi, hata wakashangaa watazamaji kwa kumetuka kwake.
التفاسير العربية:
قَالَ لِلۡمَلَإِ حَوۡلَهُۥٓ إِنَّ هَٰذَا لَسَٰحِرٌ عَلِيمٞ
(Firauni) akawaambia waheshimiwa walio mzunguka: Hakika huyu ni mchawi mtaalamu.
Firauni akawaambia watu wake: Hakika Musa ni mchawi bingwa katika uchawi wake. Kasema hayo kwa kuchelea watu wake wasiifuate Haki waliyo iona kwa Musa.
التفاسير العربية:
يُرِيدُ أَن يُخۡرِجَكُم مِّنۡ أَرۡضِكُم بِسِحۡرِهِۦ فَمَاذَا تَأۡمُرُونَ
Anataka kukutoeni katika nchi yenu kwa uchawi wake. Basi mna shauri gani?
Tena Firauni akasema: Mchawi huyu anataka kunifanyia kahari apate kukutoeni katika hii nchi yenu. Na haya ni uchochezi dhidi ya Musa, kwani katika la dhiki mno katika hayo yaliyo dhiki ni mtu kuiacha nchi yake, na khasa ikiwa kwa kahari. Naye akataka mawazo ya wale walio kuwa wanamuabudu. Kasahau ungu wake kwa nguvu za Ishara za Musa.
التفاسير العربية:
قَالُوٓاْ أَرۡجِهۡ وَأَخَاهُ وَٱبۡعَثۡ فِي ٱلۡمَدَآئِنِ حَٰشِرِينَ
Wakasema: Mpe muda yeye na nduguye na uwatume mijini wapigao mbiu ya mgambo.
Watu wake wakamwambia: Akhirisha kukata shauri yao hawa, na uwatume askari wende wawakusanye wachawi katika raia zako. Kwani uchawi hupingwa kwa uchawi.
التفاسير العربية:
يَأۡتُوكَ بِكُلِّ سَحَّارٍ عَلِيمٖ
Wakuletee kila mchawi bingwa mtaalamu.
Watakuletea wengi, na wote wamebobea kwa uchawi, na wamemshinda Musa kwa ufundi na ustadi. Wamekusudia kwa haya kumpunguzia dukuduku lake Firauni.
التفاسير العربية:
فَجُمِعَ ٱلسَّحَرَةُ لِمِيقَٰتِ يَوۡمٖ مَّعۡلُومٖ
Basi wakakusanywa wachawi wakati na siku maalumu.
Wakakusanywa wachawi kutoka kila upande wa nchi. Wakawekewa wakati wa mchana siku ya Sikukuu kukutana na Musa.
التفاسير العربية:
وَقِيلَ لِلنَّاسِ هَلۡ أَنتُم مُّجۡتَمِعُونَ
Na watu wakaambiwa: Je! Mtakusanyika?
Na watu wakahimizana kuhudhuria siku hiyo waone ramsa wakiambizana: Mtakusanyika? Yaani ndio: Mkusanyike!
التفاسير العربية:
 
ترجمة معاني سورة: الشعراء
فهرس السور رقم الصفحة
 
ترجمة معاني القرآن الكريم - الترجمة السواحلية - علي محسن البرواني - فهرس التراجم

ترجمها علي محسن البرواني.

إغلاق