للإطلاع على الموقع بحلته الجديدة

ترجمة معاني القرآن الكريم - الترجمة السواحلية - علي محسن البرواني * - فهرس التراجم

XML CSV Excel API
تنزيل الملفات يتضمن الموافقة على هذه الشروط والسياسات

ترجمة معاني سورة: الشعراء   آية:
إِنۡ هَٰذَآ إِلَّا خُلُقُ ٱلۡأَوَّلِينَ
Haya si chochote ila ni mtindo wa watu wa tokea zamani.
Haya uliyo tuletea si lolote ila ni uwongo na upotovu wa watu wa zamani. Wao wamezoea kuzua kama hivyo. Kwa hivyo sisi hatutaacha tuliyo kuwa nayo.
التفاسير العربية:
وَمَا نَحۡنُ بِمُعَذَّبِينَ
Wala sisi hatutaadhibiwa.
Wala sisi hatutaadhibiwa kwa vitendo tuvitendavyo.
التفاسير العربية:
فَكَذَّبُوهُ فَأَهۡلَكۡنَٰهُمۡۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَةٗۖ وَمَا كَانَ أَكۡثَرُهُم مُّؤۡمِنِينَ
Wakamkanusha; nasi tukawaangamiza. Hakika bila ya shaka katika haya ipo Ishara. Lakini hawakuwa wengi wao wenye kuamini.
Basi wakaendelea kushikilia kumkanusha. Mwenyezi Mungu akawafanyia haraka kuwateketeza. Hakika katika hayo aliyo wateremshia Mwenyezi Mungu kina A'di kwa kuwa ni malipo kwa ukanushi wao, ni hoja inayo juulisha ukamilifu wa uwezo wa Mwenyezi Mungu. Na si wengi katika wanao somewa khabari za A'adi walio Waumini.
التفاسير العربية:
وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلرَّحِيمُ
Na hakika Mola wako Mlezi ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu.
Na Mola wako Mlezi ndiye Mtenda nguvu wa kuwashinda hao majabari, Mwenye kuwarehemu Waumini.
التفاسير العربية:
كَذَّبَتۡ ثَمُودُ ٱلۡمُرۡسَلِينَ
Kina Thamud waliwakanusha Mitume.
Kabila ya Thamud ilimkanusha Swaleh katika Ujumbe wake na wito wake, na kwa hivyo ikawa wamewakanusha Mitume wote, kwa kuwa asli ya Ujumbe ni moja, na lengo ni moja.
التفاسير العربية:
إِذۡ قَالَ لَهُمۡ أَخُوهُمۡ صَٰلِحٌ أَلَا تَتَّقُونَ
Alipo waambia ndugu yao Swaleh: Je! Hamumchimngu?
Ewe Mtume! Watajie watu wako, wakati ule kina Thamud walipo ambiwa na ndugu yao kwa uzao na uwananchi, si kwa dini, Swaleh: Hamumwogopi Mwenyezi Mungu, mkamuaabudu Yeye tu?
التفاسير العربية:
إِنِّي لَكُمۡ رَسُولٌ أَمِينٞ
Hakika mimi kwenu ni Mtume muaminifu.
Hakika mimi nimetumwa na Mwenyezi Mungu kwenu kwa mambo yenye kheri yenu na mafanikio yenu. Na mimi ni mwenye kuuhifadhi Ujumbe huu kama nilivyo upokea kwa Mwenyezi Mungu.
التفاسير العربية:
فَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَأَطِيعُونِ
Basi mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini.
Kwa hivyo tahadharini na adhabu ya Mwenyezi Mungu, na nifuateni kwa haya ninayo kuitieni kwayo kutokana na amri zake.
التفاسير العربية:
وَمَآ أَسۡـَٔلُكُمۡ عَلَيۡهِ مِنۡ أَجۡرٍۖ إِنۡ أَجۡرِيَ إِلَّا عَلَىٰ رَبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ
Wala sikutakini ujira juu yake. Ujira wangu hauko ila kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote.
Wala sitaki kwenu ujira wowote kwa hii nasaha yangu na uwongozi wangu. Ujira wangu uko kwa Mwenye kumiliki walimwengu wote.
التفاسير العربية:
أَتُتۡرَكُونَ فِي مَا هَٰهُنَآ ءَامِنِينَ
Je! Mtaachwa salama usalimina katika haya yaliyopo hapa?
Lilio wazuia ni kule kuamini kwao kwamba ati wataselelea katika zile starehe, watasalimika na adhabu, na kutoweka, na mauti,
التفاسير العربية:
فِي جَنَّٰتٖ وَعُيُونٖ
Katika mabustani, na chemchem?
Katika mabustani ya matunda, na chemchem zenye kutoa maji matamu,
التفاسير العربية:
وَزُرُوعٖ وَنَخۡلٖ طَلۡعُهَا هَضِيمٞ
Na konde na mitende yenye makole yaliyo wiva.
Na konde zilizo wiva, na mitende ambayo mazao yake yamedhihiri mapevu na laini.
التفاسير العربية:
وَتَنۡحِتُونَ مِنَ ٱلۡجِبَالِ بُيُوتٗا فَٰرِهِينَ
Na mnachonga milimani majumba kwa ustadi.
Na mnachonga milimani majumba kwa ufundi na ustadi katika hayo mnayo yaunda.
التفاسير العربية:
فَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَأَطِيعُونِ
Basi mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini mimi.
Basi iogopeni adhabu ya Mwenyezi Mungu, kwa kuto mshukuru kwenu kwa neema zake; na pokeeni nasiha yangu na muitende.
التفاسير العربية:
وَلَا تُطِيعُوٓاْ أَمۡرَ ٱلۡمُسۡرِفِينَ
Wala msit'ii amri za walio pindukia mipaka,.
Wala msiit'ii amri ya walio pindukia mipaka kwa ushirikina na kufuata pumbao na matamanio.
التفاسير العربية:
ٱلَّذِينَ يُفۡسِدُونَ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَلَا يُصۡلِحُونَ
Ambao wanafanya ufisadi katika nchi, wala hawatengenezi.
Ambao wanapitisha maisha yao katika ardhi kwa uharibifu, wala hawafanyi ya maslaha ya kutengeneza nchi.
التفاسير العربية:
قَالُوٓاْ إِنَّمَآ أَنتَ مِنَ ٱلۡمُسَحَّرِينَ
Wakasema: Hakika wewe ni miongoni mwa walio rogwa.
Wakasema: Wewe si chochote isipo kuwa miongoni mwa walio rogwa kikweli mpaka zikapotea akili zao. Na katika jawabu hii mna ukali na usafihi.
التفاسير العربية:
مَآ أَنتَ إِلَّا بَشَرٞ مِّثۡلُنَا فَأۡتِ بِـَٔايَةٍ إِن كُنتَ مِنَ ٱلصَّٰدِقِينَ
Wewe si chochote ila ni mtu kama sisi. Basi lete Ishara ukiwa wewe ni miongoni mwa wasemao kweli.
Wewe si chochote ila ni mmoja unaye fanana na sisi kwa ubinaadamu, basi yawaje uwe bora kuliko sisi kwa Unabii na Utume? Na ukiwa wewe ni mkweli katika madai yako basi lete muujiza wa kuonyesha uthibitisho wa Utume wako.
التفاسير العربية:
قَالَ هَٰذِهِۦ نَاقَةٞ لَّهَا شِرۡبٞ وَلَكُمۡ شِرۡبُ يَوۡمٖ مَّعۡلُومٖ
Akasema: Huyu ngamia jike; awe na zamu yake ya kunywa, na nyinyi muwe na zamu yenu ya kunywa katika siku maalumu.
Saleh akawaambia - alipo pewa na Mwenyezi Mungu ngamia jike kuwa ni muujiza wake: Huyu hapa ngamia jike wa Mwenyezi Mungu, amekutoleeni kuwa ni Ishara. Yeye ana sehemu yake ya maji katika siku moja; siku hiyo msinywe nyinyi. Na nyinyi mna sehemu yenu siku nyengine. Kunyweni siku hiyo.
التفاسير العربية:
وَلَا تَمَسُّوهَا بِسُوٓءٖ فَيَأۡخُذَكُمۡ عَذَابُ يَوۡمٍ عَظِيمٖ
Wala ms!imguse kwa uwovu, isije ikakushikeni adhabu ya Siku Kubwa.
Wala msimletee madhara yoyote huyu ngamia, msije mkahiliki kwa adhabu kubwa.
التفاسير العربية:
فَعَقَرُوهَا فَأَصۡبَحُواْ نَٰدِمِينَ
Lakini wakamuuwa, na wakawa wenye kujuta.
Wakamchinja ngamia, kinyume na walivyo wafikiana na Swaleh. Kwa hivyo wakastahiki kuwashukia adhabu, wakawa ni wenye kujuta kwa kitendo chao hicho.
التفاسير العربية:
فَأَخَذَهُمُ ٱلۡعَذَابُۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَةٗۖ وَمَا كَانَ أَكۡثَرُهُم مُّؤۡمِنِينَ
Basi ikawapata adhabu. Hakika katika hayo ipo Ishara. Lakini hawakuwa wengi wao wenye kuamini.
Basi ikawateketeza adhabu aliyo waahidi Swaleh, wala majuto hayakuwakinga na adhabu ya ukosefu wao. Hakika katika kusimulia kisa chao pana dalili ya kuonyesha uwezo wa Mwenyezi Mungu kuwateketeza makafiri na kuwaokoa Waumini. Na si wengi katika watu wako wenye kuamini.
التفاسير العربية:
وَإِنَّ رَبَّكَ لَهُوَ ٱلۡعَزِيزُ ٱلرَّحِيمُ
Na hakika Mola wako Mlezi ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu.
Na hakika bila ya shaka aliye kuumba ndiye Yeye Muweza wa kuwateketeza wapinzani, na Mfadhili wa kuwaokoa wachamngu.
التفاسير العربية:
 
ترجمة معاني سورة: الشعراء
فهرس السور رقم الصفحة
 
ترجمة معاني القرآن الكريم - الترجمة السواحلية - علي محسن البرواني - فهرس التراجم

ترجمها علي محسن البرواني.

إغلاق