للإطلاع على الموقع بحلته الجديدة

ترجمة معاني القرآن الكريم - الترجمة السواحلية - علي محسن البرواني * - فهرس التراجم

XML CSV Excel API
تنزيل الملفات يتضمن الموافقة على هذه الشروط والسياسات

ترجمة معاني سورة: محمد   آية:
وَلَوۡ نَشَآءُ لَأَرَيۡنَٰكَهُمۡ فَلَعَرَفۡتَهُم بِسِيمَٰهُمۡۚ وَلَتَعۡرِفَنَّهُمۡ فِي لَحۡنِ ٱلۡقَوۡلِۚ وَٱللَّهُ يَعۡلَمُ أَعۡمَٰلَكُمۡ
Na tungeli penda tungeli kuonyesha hao na ungeli watambua kwa alama zao; lakini bila ya shaka utawajua kwa namna ya msemo wao. Na Mwenyezi Mungu anavijua vitendo vyenu. [30]
[30] Tungeli penda bila ya shaka tungeli kuonyesha hao wanaafiki, nawe ungeli wajua kwa alama zao, na ungeli wajua kwa namna yao wanavyo sema. Na Mwenyezi Mungu anajua ukweli wa vitendo vyenu vyote.
التفاسير العربية:
وَلَنَبۡلُوَنَّكُمۡ حَتَّىٰ نَعۡلَمَ ٱلۡمُجَٰهِدِينَ مِنكُمۡ وَٱلصَّٰبِرِينَ وَنَبۡلُوَاْ أَخۡبَارَكُمۡ
Na bila ya shaka tutakujaribuni mpaka tuwadhihirishe wapignao Jihadi katika nyinyi na wanao subiri. Nasi tutazifanyia mtihani khabari zenu. [31]
[31] Na ninaapa: Bila ya shaka tutakujaribuni kama kukufanyieni mtihani, mpaka tuwajue Mujaahidina, wanao pigana kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, katika nyinyi, na wenye kuvumilia wakati wa shida na dhiki, na tuzijue khabari zenu za ut'iifu na maasi katika Jihadi na penginepo.
التفاسير العربية:
إِنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ وَصَدُّواْ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ وَشَآقُّواْ ٱلرَّسُولَ مِنۢ بَعۡدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُمُ ٱلۡهُدَىٰ لَن يَضُرُّواْ ٱللَّهَ شَيۡـٔٗا وَسَيُحۡبِطُ أَعۡمَٰلَهُمۡ
Kwa hakika walio kufuru na wakazuilia njia ya Mwenyezi Mungu na wakapinzana na Mtume baada ya kwisha wabainikia uwongofu, hao hawatamdhuru Mwenyezi Mungu kwa lolote. Naye ataviangusha vitendo vyao. [32]
[32] Hakika walio kufuru na wakazuia njia ya Mwenyezi Mungu, na wakenda kinyume na Mtume kwa inda na ukaidi, baada ya kwisha wadhihirikia uwongofu, hao hawatamdhuru Mwenyezi Mungu kwa lolote. Na Yeye atayabat'ilisha yote waliyo yatenda.
التفاسير العربية:
۞ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ أَطِيعُواْ ٱللَّهَ وَأَطِيعُواْ ٱلرَّسُولَ وَلَا تُبۡطِلُوٓاْ أَعۡمَٰلَكُمۡ
Enyi mlio amini! Mt'iini Mwenyezi Mungu, na mt'iini Mtume, wala msiviharibu vitendo vyenu. [33]
[33] Enyi mlio amini! Mt'iini Mwenyezi Mungu katika aliyo kuamrisheni, na mt'iini Mtume kwa hayo anayo kuitieni, wala msivipoteze vitendo vyenu.
التفاسير العربية:
إِنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ وَصَدُّواْ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِ ثُمَّ مَاتُواْ وَهُمۡ كُفَّارٞ فَلَن يَغۡفِرَ ٱللَّهُ لَهُمۡ
Hakika walio kufuru na wakazuilia njia ya Mwenyezi Mungu, kisha wakafa na hali ni makafiri, Mwenyezi Mungu hatawasamehe makosa yao. [34]
[34] Hakika walio kufuru na wakazuia watu wasiingie katika Uislamu, kisha wakafa nao ni makafiri, basi Mwenyezi Mungu hatawasamehe.
التفاسير العربية:
فَلَا تَهِنُواْ وَتَدۡعُوٓاْ إِلَى ٱلسَّلۡمِ وَأَنتُمُ ٱلۡأَعۡلَوۡنَ وَٱللَّهُ مَعَكُمۡ وَلَن يَتِرَكُمۡ أَعۡمَٰلَكُمۡ
Basi msiregee na kutaka suluhu, maana nyinyi ndio mtakao shinda. Na Mwenyezi Mungu yu pamoja nanyi, wala hatakunyimeni malipo ya vitendo vyenu. [35]
[35] Basi msijifanye wanyonge mbele ya maadui zenu mnapo kutana nao. Wala msiwatake suluhu kwa kuwaogopa, na hali nyinyi ndio mko juu, na ni wenye kushinda kwa nguvu za Imani. Na Mwenyezi Mungu yu pamoja nanyi kwa nusra yake; na wala hatakupunguzieni malipo ya vitendo vyenu.
التفاسير العربية:
إِنَّمَا ٱلۡحَيَوٰةُ ٱلدُّنۡيَا لَعِبٞ وَلَهۡوٞۚ وَإِن تُؤۡمِنُواْ وَتَتَّقُواْ يُؤۡتِكُمۡ أُجُورَكُمۡ وَلَا يَسۡـَٔلۡكُمۡ أَمۡوَٰلَكُمۡ
Hakika uhai wa duniani ni mchezo na pumbao. Na mkiamini na mkamchamngu Mwenyezi Mungu atakupeni ujira wenu, wala hakutakeni mali yenu. [36]
[36] Hakika uhai wa dunia ni upotovu na udanganyifu. Na nyinyi mkiamini na mkaacha maasi, na mkafanya kheri, Mwenyezi Mungu atakupeni thawabu ya hayo, wala hakutakini mali yenu. Akikutakeni na akakushikilieni basi nyinyi mtafanya uchoyo, na chuki zenu zitaonekana kwa mnavyo yapenda mali.
التفاسير العربية:
إِن يَسۡـَٔلۡكُمُوهَا فَيُحۡفِكُمۡ تَبۡخَلُواْ وَيُخۡرِجۡ أَضۡغَٰنَكُمۡ
Na akikutakeni hayo na kukushikilieni mtafanya ubakhili, na atatoa undani wa chuki zenu. [37]
[37] Akikutakeni na akakushikilieni basi nyinyi mtafanya uchoyo, na chuki zenu zitaonekana kwa mnavyo yapenda mali.
التفاسير العربية:
هَٰٓأَنتُمۡ هَٰٓؤُلَآءِ تُدۡعَوۡنَ لِتُنفِقُواْ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ فَمِنكُم مَّن يَبۡخَلُۖ وَمَن يَبۡخَلۡ فَإِنَّمَا يَبۡخَلُ عَن نَّفۡسِهِۦۚ وَٱللَّهُ ٱلۡغَنِيُّ وَأَنتُمُ ٱلۡفُقَرَآءُۚ وَإِن تَتَوَلَّوۡاْ يَسۡتَبۡدِلۡ قَوۡمًا غَيۡرَكُمۡ ثُمَّ لَا يَكُونُوٓاْ أَمۡثَٰلَكُم
Angalieni! Nyinyi mnaitwa mtumie katika njia ya Mwenyezi Mungu, na wapo katika nyinyi wanao fanya ubakhili. Na anaye fanya ubakhili basi anajifanyia ubakhili mwenyewe. Na Mwenyezi Mungu si mhitaji, na nyinyi ndio wahitaji. Na mkigeuka atawaleta watu wengine badala yenu, nao hawatakuwa kama nyinyi. [38]
[38] Hivi mnaitwa mtumie katika njia ya Mwenyezi Mungu aliyo iamrisha. Kati yenu wapo wanao fanya ubakhili kutoa. Na mwenye kufanya ubakhili hamdhuru mtu ila nafsi yake. Na Mwenyezi Mungu peke yake ndiye tajiri, hana haja ya mtu, na nyinyi ndio mafakiri wenye kumhitajia Yeye. Na mkiacha kumt'ii Mwenyezi Mungu basi atakubadilisheni pahala penu awalete watu wengine, tena hao hawatakuwa mfano wenu wa kuacha kumt'ii.
التفاسير العربية:
 
ترجمة معاني سورة: محمد
فهرس السور رقم الصفحة
 
ترجمة معاني القرآن الكريم - الترجمة السواحلية - علي محسن البرواني - فهرس التراجم

ترجمها علي محسن البرواني.

إغلاق