للإطلاع على الموقع بحلته الجديدة

ترجمة معاني القرآن الكريم - الترجمة السواحيلية - جمعية خدمة المحتوى * - فهرس التراجم


ترجمة معاني سورة: طه   آية:

سورة طه - Taha

طه
'TAHA!
التفاسير العربية:
مَآ أَنزَلۡنَا عَلَيۡكَ ٱلۡقُرۡءَانَ لِتَشۡقَىٰٓ
Hatukukuteremshia Qur-ani ili upate mashaka.
التفاسير العربية:
إِلَّا تَذۡكِرَةٗ لِّمَن يَخۡشَىٰ
Bali ni ukumbusho kwa mwenye kunyenyekea.
التفاسير العربية:
تَنزِيلٗا مِّمَّنۡ خَلَقَ ٱلۡأَرۡضَ وَٱلسَّمَٰوَٰتِ ٱلۡعُلَى
Ni uteremsho kutoka kwa aliyeumba ardhi na mbingu zilizo juu.
التفاسير العربية:
ٱلرَّحۡمَٰنُ عَلَى ٱلۡعَرۡشِ ٱسۡتَوَىٰ
Arrahmani (Mwingi wa rehema), aliyeinuka juu ya Kiti cha Enzi.
التفاسير العربية:
لَهُۥ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِ وَمَا بَيۡنَهُمَا وَمَا تَحۡتَ ٱلثَّرَىٰ
Ni vyake vyote vilivyo katika mbingu na vilivyo katika ardhi, na vilivyo baina yake, na vilivyo chini ya ardhi.
التفاسير العربية:
وَإِن تَجۡهَرۡ بِٱلۡقَوۡلِ فَإِنَّهُۥ يَعۡلَمُ ٱلسِّرَّ وَأَخۡفَى
Na ukinyanyua sauti kwa kusema, basi hakika Yeye anajua siri na chini zaidi kuliko siri.
التفاسير العربية:
ٱللَّهُ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَۖ لَهُ ٱلۡأَسۡمَآءُ ٱلۡحُسۡنَىٰ
Mwenyezi Mungu! Hapana mungu yeyote isipokuwa Yeye. Yeye ana majina mazuri zaidi.
التفاسير العربية:
وَهَلۡ أَتَىٰكَ حَدِيثُ مُوسَىٰٓ
Na je, imekufikia hadithi ya Musa?
التفاسير العربية:
إِذۡ رَءَا نَارٗا فَقَالَ لِأَهۡلِهِ ٱمۡكُثُوٓاْ إِنِّيٓ ءَانَسۡتُ نَارٗا لَّعَلِّيٓ ءَاتِيكُم مِّنۡهَا بِقَبَسٍ أَوۡ أَجِدُ عَلَى ٱلنَّارِ هُدٗى
Alipouona moto, kwa hivyo akawaambia ahali zake: Ngojeni! Hakika mimi nimeuona moto, huenda nikawaletea kijinga kutoka humo, au nikapata wongofu kwenye moto huo.
التفاسير العربية:
فَلَمَّآ أَتَىٰهَا نُودِيَ يَٰمُوسَىٰٓ
Basi alipoufikia, akaitwa: Ewe Musa!
التفاسير العربية:
إِنِّيٓ أَنَا۠ رَبُّكَ فَٱخۡلَعۡ نَعۡلَيۡكَ إِنَّكَ بِٱلۡوَادِ ٱلۡمُقَدَّسِ طُوٗى
Hakika Mimi ndiye Mola wako Mlezi! Basi vua viatu vyako. Kwani upo katika bonde takatifu la 'Tuwa.
التفاسير العربية:
وَأَنَا ٱخۡتَرۡتُكَ فَٱسۡتَمِعۡ لِمَا يُوحَىٰٓ
Nami nimekuteua wewe; basi sikiliza yanayofunuliwa.
التفاسير العربية:
إِنَّنِيٓ أَنَا ٱللَّهُ لَآ إِلَٰهَ إِلَّآ أَنَا۠ فَٱعۡبُدۡنِي وَأَقِمِ ٱلصَّلَوٰةَ لِذِكۡرِيٓ
Hakika Mimi ndiye Mwenyezi Mungu. Hapana mungu isipokuwa Mimi tu. Basi niabudu Mimi, na usimamishe Swala kwa ajili ya kunikumbuka Mimi.
التفاسير العربية:
إِنَّ ٱلسَّاعَةَ ءَاتِيَةٌ أَكَادُ أُخۡفِيهَا لِتُجۡزَىٰ كُلُّ نَفۡسِۭ بِمَا تَسۡعَىٰ
Hakika Saa itakuja bila ya shaka. Nimekaribia mno kuificha, ili kila nafsi ilipwe kwa iliyoyafanya.
التفاسير العربية:
فَلَا يَصُدَّنَّكَ عَنۡهَا مَن لَّا يُؤۡمِنُ بِهَا وَٱتَّبَعَ هَوَىٰهُ فَتَرۡدَىٰ
Kwa hivyo, kamwe asikuzuilie nayo yule ambaye haiamini na akafuata matamanio yake ukaja kuangamia.
التفاسير العربية:
وَمَا تِلۡكَ بِيَمِينِكَ يَٰمُوسَىٰ
Na nini hicho kilichomo mkononi mwako wa kulia, ewe Musa?
التفاسير العربية:
قَالَ هِيَ عَصَايَ أَتَوَكَّؤُاْ عَلَيۡهَا وَأَهُشُّ بِهَا عَلَىٰ غَنَمِي وَلِيَ فِيهَا مَـَٔارِبُ أُخۡرَىٰ
Akasema: Hii ni fimbo yangu; ninaiegemea na ninawaangushia majani kwayo kondoo na mbuzi wangu. Tena inanifaa kwa matumizi mengine.
التفاسير العربية:
قَالَ أَلۡقِهَا يَٰمُوسَىٰ
Akasema: Itupe, ewe Musa!
التفاسير العربية:
فَأَلۡقَىٰهَا فَإِذَا هِيَ حَيَّةٞ تَسۡعَىٰ
Akaitupa. Mara ikawa nyoka anayekwenda mbio.
التفاسير العربية:
قَالَ خُذۡهَا وَلَا تَخَفۡۖ سَنُعِيدُهَا سِيرَتَهَا ٱلۡأُولَىٰ
Akasema: Ikamate, wala usiogope! Tutairudisha hali yake ya kwanza.
التفاسير العربية:
وَٱضۡمُمۡ يَدَكَ إِلَىٰ جَنَاحِكَ تَخۡرُجۡ بَيۡضَآءَ مِنۡ غَيۡرِ سُوٓءٍ ءَايَةً أُخۡرَىٰ
Na uambatishe mkono wako kwenye ubavu, utatoka mweupe pasipo na madhara yoyote. Hiyo ni ishara nyingine.
التفاسير العربية:
لِنُرِيَكَ مِنۡ ءَايَٰتِنَا ٱلۡكُبۡرَى
Ili tukuonyeshe katika ishara zetu kubwa.
التفاسير العربية:
ٱذۡهَبۡ إِلَىٰ فِرۡعَوۡنَ إِنَّهُۥ طَغَىٰ
Nenda kwa Firauni. Hakika yeye amepindukia mipaka.
التفاسير العربية:
قَالَ رَبِّ ٱشۡرَحۡ لِي صَدۡرِي
(Musa) akasema: Ewe Mola wangu Mlezi! Nikunjulie kifua changu.
التفاسير العربية:
وَيَسِّرۡ لِيٓ أَمۡرِي
Na nirahisishie kazi yangu hii.
التفاسير العربية:
وَٱحۡلُلۡ عُقۡدَةٗ مِّن لِّسَانِي
Na lifungue fundo lililo katika ulimi wangu.
التفاسير العربية:
يَفۡقَهُواْ قَوۡلِي
Wapate kufahamu maneno yangu.
التفاسير العربية:
وَٱجۡعَل لِّي وَزِيرٗا مِّنۡ أَهۡلِي
Na nipe msaidizi katika ahali zangu.
التفاسير العربية:
هَٰرُونَ أَخِي
Harun, kaka yangu.
التفاسير العربية:
ٱشۡدُدۡ بِهِۦٓ أَزۡرِي
Kwake yeye niongeze nguvu zangu.
التفاسير العربية:
وَأَشۡرِكۡهُ فِيٓ أَمۡرِي
Na mshirikishe katika jambo langu hili.
التفاسير العربية:
كَيۡ نُسَبِّحَكَ كَثِيرٗا
Ili tukutakase kwa wingi.
التفاسير العربية:
وَنَذۡكُرَكَ كَثِيرًا
Na tukutaje kwa wingi.
التفاسير العربية:
إِنَّكَ كُنتَ بِنَا بَصِيرٗا
Hakika Wewe unatuona vyema.
التفاسير العربية:
قَالَ قَدۡ أُوتِيتَ سُؤۡلَكَ يَٰمُوسَىٰ
Akasema: Hakika Umepewa maombi yako, ewe Musa!
التفاسير العربية:
وَلَقَدۡ مَنَنَّا عَلَيۡكَ مَرَّةً أُخۡرَىٰٓ
Na hakika tulikwisha kufanyia hisani mara nyingine.
التفاسير العربية:
إِذۡ أَوۡحَيۡنَآ إِلَىٰٓ أُمِّكَ مَا يُوحَىٰٓ
Pale tulipomfunulia mama yako yaliyofunuliwa,
التفاسير العربية:
أَنِ ٱقۡذِفِيهِ فِي ٱلتَّابُوتِ فَٱقۡذِفِيهِ فِي ٱلۡيَمِّ فَلۡيُلۡقِهِ ٱلۡيَمُّ بِٱلسَّاحِلِ يَأۡخُذۡهُ عَدُوّٞ لِّي وَعَدُوّٞ لَّهُۥۚ وَأَلۡقَيۡتُ عَلَيۡكَ مَحَبَّةٗ مِّنِّي وَلِتُصۡنَعَ عَلَىٰ عَيۡنِيٓ
Ya kuwa mtie katika kisanduku, na kisha kitie mtoni, na mto utamfikisha ufukweni. Atamchukua adui yangu naye ni adui yake. Na nimekutilia mapenzi yanayotokana kwangu, na ili ulelewe machoni mwangu.
التفاسير العربية:
إِذۡ تَمۡشِيٓ أُخۡتُكَ فَتَقُولُ هَلۡ أَدُلُّكُمۡ عَلَىٰ مَن يَكۡفُلُهُۥۖ فَرَجَعۡنَٰكَ إِلَىٰٓ أُمِّكَ كَيۡ تَقَرَّ عَيۡنُهَا وَلَا تَحۡزَنَۚ وَقَتَلۡتَ نَفۡسٗا فَنَجَّيۡنَٰكَ مِنَ ٱلۡغَمِّ وَفَتَنَّٰكَ فُتُونٗاۚ فَلَبِثۡتَ سِنِينَ فِيٓ أَهۡلِ مَدۡيَنَ ثُمَّ جِئۡتَ عَلَىٰ قَدَرٖ يَٰمُوسَىٰ
Dada yako alipokwenda na akasema: Je! Niwajulishe mtu wa kuweza kumlea? Basi tukakurejesha kwa mama yako ili macho yake yaburudike, wala asihuzunike. Na ulimuua mtu, nasi tukakuokoa katika dhiki, na tukakujaribu kwa majaribio mengi. Ukakaa miaka kwa watu wa Madyana. Kisha ukaja kama ilivyokadiriwa, ewe Musa!
التفاسير العربية:
وَٱصۡطَنَعۡتُكَ لِنَفۡسِي
Na nimekuteua kwa ajili ya nafsi yangu.
التفاسير العربية:
ٱذۡهَبۡ أَنتَ وَأَخُوكَ بِـَٔايَٰتِي وَلَا تَنِيَا فِي ذِكۡرِي
Nenda, wewe na ndugu yako, pamoja na ishara zangu, wala msichoke kunikumbuka.
التفاسير العربية:
ٱذۡهَبَآ إِلَىٰ فِرۡعَوۡنَ إِنَّهُۥ طَغَىٰ
Nendeni kwa Firauni. Hakika yeye amepindukia mipaka.
التفاسير العربية:
فَقُولَا لَهُۥ قَوۡلٗا لَّيِّنٗا لَّعَلَّهُۥ يَتَذَكَّرُ أَوۡ يَخۡشَىٰ
Mwambieni maneno laini, huenda akazingatia au akaogopa.
التفاسير العربية:
قَالَا رَبَّنَآ إِنَّنَا نَخَافُ أَن يَفۡرُطَ عَلَيۡنَآ أَوۡ أَن يَطۡغَىٰ
Wakasema: Ewe Mola wetu Mlezi! Hakika sisi tunaogopa asije akapindukia mipaka juu yetu au kufanya jeuri.
التفاسير العربية:
قَالَ لَا تَخَافَآۖ إِنَّنِي مَعَكُمَآ أَسۡمَعُ وَأَرَىٰ
Akasema: Msiogope! Hakika Mimi ni pamoja nanyi. Nasikia na ninaona.
التفاسير العربية:
فَأۡتِيَاهُ فَقُولَآ إِنَّا رَسُولَا رَبِّكَ فَأَرۡسِلۡ مَعَنَا بَنِيٓ إِسۡرَٰٓءِيلَ وَلَا تُعَذِّبۡهُمۡۖ قَدۡ جِئۡنَٰكَ بِـَٔايَةٖ مِّن رَّبِّكَۖ وَٱلسَّلَٰمُ عَلَىٰ مَنِ ٱتَّبَعَ ٱلۡهُدَىٰٓ
Basi mwendeeni, na mwambieni: Hakika sisi ni Mitume wa Mola wako Mlezi! Basi waache Wana wa Israili watoke nasi, wala usiwaadhibu. Sisi tumekuletea ishara itokayo kwa Mola wako Mlezi. Na amani iwe juu ya atakayefuata uwongofu.
التفاسير العربية:
إِنَّا قَدۡ أُوحِيَ إِلَيۡنَآ أَنَّ ٱلۡعَذَابَ عَلَىٰ مَن كَذَّبَ وَتَوَلَّىٰ
Hakika tumefunuliwa sisi kwamba hapana shaka adhabu itamsibu anayekadhibisha na akapuuza
التفاسير العربية:
قَالَ فَمَن رَّبُّكُمَا يَٰمُوسَىٰ
(Firauni) akasema: Basi Mola wenu Mlezi ni nani, ewe Musa?
التفاسير العربية:
قَالَ رَبُّنَا ٱلَّذِيٓ أَعۡطَىٰ كُلَّ شَيۡءٍ خَلۡقَهُۥ ثُمَّ هَدَىٰ
Akasema: Mola wetu Mlezi ni yule aliyekipa kila kitu umbo lake, kisha akakiongoa.
التفاسير العربية:
قَالَ فَمَا بَالُ ٱلۡقُرُونِ ٱلۡأُولَىٰ
Akasema: Nini hali ya karne za kwanza?
التفاسير العربية:
قَالَ عِلۡمُهَا عِندَ رَبِّي فِي كِتَٰبٖۖ لَّا يَضِلُّ رَبِّي وَلَا يَنسَى
Akasema: Elimu yake iko kwa Mola wangu Mlezi katika Kitabu. Mola wangu Mlezi hapotei wala hasahau.
التفاسير العربية:
ٱلَّذِي جَعَلَ لَكُمُ ٱلۡأَرۡضَ مَهۡدٗا وَسَلَكَ لَكُمۡ فِيهَا سُبُلٗا وَأَنزَلَ مِنَ ٱلسَّمَآءِ مَآءٗ فَأَخۡرَجۡنَا بِهِۦٓ أَزۡوَٰجٗا مِّن نَّبَاتٖ شَتَّىٰ
Ambaye amewafanyia ardhi kuwa tandiko, na akawapitishia humo njia, na akawateremshia kutoka mbinguni maji. Na kwa hayo tukatoa namna mbalimbali za mimea.
التفاسير العربية:
كُلُواْ وَٱرۡعَوۡاْ أَنۡعَٰمَكُمۡۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَٰتٖ لِّأُوْلِي ٱلنُّهَىٰ
Kuleni, na mchunge wanyama wenu. Hakika katika hayo zipo ishara kwa wenye akili.
التفاسير العربية:
۞ مِنۡهَا خَلَقۡنَٰكُمۡ وَفِيهَا نُعِيدُكُمۡ وَمِنۡهَا نُخۡرِجُكُمۡ تَارَةً أُخۡرَىٰ
Tumewaumba kutokana nayo (ardhi), na humo tutawarudisha, na tutawatoa kutoka humo mara nyengine.
التفاسير العربية:
وَلَقَدۡ أَرَيۡنَٰهُ ءَايَٰتِنَا كُلَّهَا فَكَذَّبَ وَأَبَىٰ
Na hakika tulimwonyesha ishara zetu zote. Lakini alikadhibisha na akakataa.
التفاسير العربية:
قَالَ أَجِئۡتَنَا لِتُخۡرِجَنَا مِنۡ أَرۡضِنَا بِسِحۡرِكَ يَٰمُوسَىٰ
Akasema: Ewe Musa! Hivyo umetujia kututoa katika nchi yetu kwa uchawi wako?
التفاسير العربية:
فَلَنَأۡتِيَنَّكَ بِسِحۡرٖ مِّثۡلِهِۦ فَٱجۡعَلۡ بَيۡنَنَا وَبَيۡنَكَ مَوۡعِدٗا لَّا نُخۡلِفُهُۥ نَحۡنُ وَلَآ أَنتَ مَكَانٗا سُوٗى
Basi sisi hakika tutakuletea uchawi kama huo. Basi weka miadi baina yetu na wewe, ambayo tusiivunje sisi wala wewe, mahali patakapokuwa sawa.
التفاسير العربية:
قَالَ مَوۡعِدُكُمۡ يَوۡمُ ٱلزِّينَةِ وَأَن يُحۡشَرَ ٱلنَّاسُ ضُحٗى
Akasema: Miadi yenu ni siku ya Sikukuu ya mapambo; na watu wakusanywe kabla ya adhuhuri.
التفاسير العربية:
فَتَوَلَّىٰ فِرۡعَوۡنُ فَجَمَعَ كَيۡدَهُۥ ثُمَّ أَتَىٰ
Basi Firauni akageuka akarudi, na akatengeneza hila yake, kisha akaja.
التفاسير العربية:
قَالَ لَهُم مُّوسَىٰ وَيۡلَكُمۡ لَا تَفۡتَرُواْ عَلَى ٱللَّهِ كَذِبٗا فَيُسۡحِتَكُم بِعَذَابٖۖ وَقَدۡ خَابَ مَنِ ٱفۡتَرَىٰ
Musa akawaambia: Ole wenu! Msimzulie Mwenyezi Mungu uongo, akaja kuwafutilia mbali kwa adhabu. Na hakika mwenye kuzua lazima ashindwe!
التفاسير العربية:
فَتَنَٰزَعُوٓاْ أَمۡرَهُم بَيۡنَهُمۡ وَأَسَرُّواْ ٱلنَّجۡوَىٰ
Basi wakazozana wenyewe kwa wenyewe kuhusiana na jambo lao hilo, na wakanong'ona kwa siri.
التفاسير العربية:
قَالُوٓاْ إِنۡ هَٰذَٰنِ لَسَٰحِرَٰنِ يُرِيدَانِ أَن يُخۡرِجَاكُم مِّنۡ أَرۡضِكُم بِسِحۡرِهِمَا وَيَذۡهَبَا بِطَرِيقَتِكُمُ ٱلۡمُثۡلَىٰ
Wakasema: Hakika hawa wawili ni wachawi, wanataka kuwatoa katika nchi yenu kwa uchawi wao, na waondoe mila zenu zilizo bora kabisa.
التفاسير العربية:
فَأَجۡمِعُواْ كَيۡدَكُمۡ ثُمَّ ٱئۡتُواْ صَفّٗاۚ وَقَدۡ أَفۡلَحَ ٱلۡيَوۡمَ مَنِ ٱسۡتَعۡلَىٰ
Kwa hivyo kusanyeni hila zenu zote, kisha mfike kwa kujipanga safu, na kwa yakini atafuzu kweli kweli leo atakayeshinda.
التفاسير العربية:
قَالُواْ يَٰمُوسَىٰٓ إِمَّآ أَن تُلۡقِيَ وَإِمَّآ أَن نَّكُونَ أَوَّلَ مَنۡ أَلۡقَىٰ
Wakasema: Ewe Musa! Ima utupe wewe, au tuwe sisi ndio wa kwanza wa kutupa?
التفاسير العربية:
قَالَ بَلۡ أَلۡقُواْۖ فَإِذَا حِبَالُهُمۡ وَعِصِيُّهُمۡ يُخَيَّلُ إِلَيۡهِ مِن سِحۡرِهِمۡ أَنَّهَا تَسۡعَىٰ
Akasema: Bali tupeni nyinyi! Tahamaki! Kamba zao na fimbo zao zikaonekana mbele yake, kwa uchawi wao, kuwa zinakwenda mbio.
التفاسير العربية:
فَأَوۡجَسَ فِي نَفۡسِهِۦ خِيفَةٗ مُّوسَىٰ
Basi Musa akaingia hofu katika nafsi yake.
التفاسير العربية:
قُلۡنَا لَا تَخَفۡ إِنَّكَ أَنتَ ٱلۡأَعۡلَىٰ
Tukasema: Usihofu! Hakika wewe ndiye utakayeshinda.
التفاسير العربية:
وَأَلۡقِ مَا فِي يَمِينِكَ تَلۡقَفۡ مَا صَنَعُوٓاْۖ إِنَّمَا صَنَعُواْ كَيۡدُ سَٰحِرٖۖ وَلَا يُفۡلِحُ ٱلسَّاحِرُ حَيۡثُ أَتَىٰ
Na kitupe kilicho katika mkono wako wa kulia; kitavimeza walivyoviunda. Hakika walivyounda ni hila za mchawi tu, na mchawi hafanikiwi popote afikapo.
التفاسير العربية:
فَأُلۡقِيَ ٱلسَّحَرَةُ سُجَّدٗا قَالُوٓاْ ءَامَنَّا بِرَبِّ هَٰرُونَ وَمُوسَىٰ
Basi wachawi hao wakaangushwa chini wakasujudu. Wakasema: Tumemuamini Mola Mlezi wa Harun na Musa!
التفاسير العربية:
قَالَ ءَامَنتُمۡ لَهُۥ قَبۡلَ أَنۡ ءَاذَنَ لَكُمۡۖ إِنَّهُۥ لَكَبِيرُكُمُ ٱلَّذِي عَلَّمَكُمُ ٱلسِّحۡرَۖ فَلَأُقَطِّعَنَّ أَيۡدِيَكُمۡ وَأَرۡجُلَكُم مِّنۡ خِلَٰفٖ وَلَأُصَلِّبَنَّكُمۡ فِي جُذُوعِ ٱلنَّخۡلِ وَلَتَعۡلَمُنَّ أَيُّنَآ أَشَدُّ عَذَابٗا وَأَبۡقَىٰ
(Firauni) akasema: Oh! Mmemuamini kabla ya mimi kuwapa ruhusa? Hakika yeye ndiye mkubwa wenu aliyewafundisha uchawi huu. Basi kwa yakini nitawakata mikono yenu na miguu yenu kwa kutofautisha. Na lazima nitawatundika misalabani katika vigogo vya mitende, na hapo kwa yakini mtajua ni nani katika sisi aliye mkali zaidi wa kuadhibu na kuiendeleza zaidi adhabu yake.
التفاسير العربية:
قَالُواْ لَن نُّؤۡثِرَكَ عَلَىٰ مَا جَآءَنَا مِنَ ٱلۡبَيِّنَٰتِ وَٱلَّذِي فَطَرَنَاۖ فَٱقۡضِ مَآ أَنتَ قَاضٍۖ إِنَّمَا تَقۡضِي هَٰذِهِ ٱلۡحَيَوٰةَ ٱلدُّنۡيَآ
kasema: Hatutakupendelea wewe kuliko ishara waziwazi zilizotujia, na kuliko yule aliyetuumba. Basi hukumu utavyohukumu; kwani wewe hakika unahukumu tu haya ya maisha ya duniani.
التفاسير العربية:
إِنَّآ ءَامَنَّا بِرَبِّنَا لِيَغۡفِرَ لَنَا خَطَٰيَٰنَا وَمَآ أَكۡرَهۡتَنَا عَلَيۡهِ مِنَ ٱلسِّحۡرِۗ وَٱللَّهُ خَيۡرٞ وَأَبۡقَىٰٓ
Hakika sisi tumemuamini Mola wetu Mlezi ili atusamehe makosa yetu na uchawi uliotulazimisha kuufanya. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mbora na Mwenye kudumu zaidi.
التفاسير العربية:
إِنَّهُۥ مَن يَأۡتِ رَبَّهُۥ مُجۡرِمٗا فَإِنَّ لَهُۥ جَهَنَّمَ لَا يَمُوتُ فِيهَا وَلَا يَحۡيَىٰ
Hakika atakayemjia Mola wake Mlezi naye ni mhalifu, basi kwa yakini, yake huyo ni Jahannamu. Hafi humo wala haishi.
التفاسير العربية:
وَمَن يَأۡتِهِۦ مُؤۡمِنٗا قَدۡ عَمِلَ ٱلصَّٰلِحَٰتِ فَأُوْلَٰٓئِكَ لَهُمُ ٱلدَّرَجَٰتُ ٱلۡعُلَىٰ
Na anayemjia Yeye naye ni Muumini na akatenda mema, basi hao watakuwa na daraja za juu.
التفاسير العربية:
جَنَّٰتُ عَدۡنٖ تَجۡرِي مِن تَحۡتِهَا ٱلۡأَنۡهَٰرُ خَٰلِدِينَ فِيهَاۚ وَذَٰلِكَ جَزَآءُ مَن تَزَكَّىٰ
Bustani za milele zipitazo mito kati yake, wadumu humo. Na hayo ni malipo ya mwenye kujitakasa.
التفاسير العربية:
وَلَقَدۡ أَوۡحَيۡنَآ إِلَىٰ مُوسَىٰٓ أَنۡ أَسۡرِ بِعِبَادِي فَٱضۡرِبۡ لَهُمۡ طَرِيقٗا فِي ٱلۡبَحۡرِ يَبَسٗا لَّا تَخَٰفُ دَرَكٗا وَلَا تَخۡشَىٰ
Na tulimfunulia Musa: Toka usiku na waja wangu, na uwapigie njia kavu baharini. Usihofu kukamatwa, wala usiogope.
التفاسير العربية:
فَأَتۡبَعَهُمۡ فِرۡعَوۡنُ بِجُنُودِهِۦ فَغَشِيَهُم مِّنَ ٱلۡيَمِّ مَا غَشِيَهُمۡ
Firauni akawafuata pamoja na majeshi yake. Basi kiliwafudikiza humo baharini kilichowafudikiza.
التفاسير العربية:
وَأَضَلَّ فِرۡعَوۡنُ قَوۡمَهُۥ وَمَا هَدَىٰ
Na Firauni aliwapoteza watu wake wala hakuwaongoa.
التفاسير العربية:
يَٰبَنِيٓ إِسۡرَٰٓءِيلَ قَدۡ أَنجَيۡنَٰكُم مِّنۡ عَدُوِّكُمۡ وَوَٰعَدۡنَٰكُمۡ جَانِبَ ٱلطُّورِ ٱلۡأَيۡمَنَ وَنَزَّلۡنَا عَلَيۡكُمُ ٱلۡمَنَّ وَٱلسَّلۡوَىٰ
Enyi Wana wa Israili! Hakika tuliwaokoa na adui yenu, na tukawaahidi upande wa kulia wa mlima. Na tuliwateremshia Manna na Salwa.
التفاسير العربية:
كُلُواْ مِن طَيِّبَٰتِ مَا رَزَقۡنَٰكُمۡ وَلَا تَطۡغَوۡاْ فِيهِ فَيَحِلَّ عَلَيۡكُمۡ غَضَبِيۖ وَمَن يَحۡلِلۡ عَلَيۡهِ غَضَبِي فَقَدۡ هَوَىٰ
Kuleni katika vitu vizuri hivyo tulivyowaruzuku, wala msiruke mipaka katika hayo, isije ikawashika ghadhabu yangu. Na yule inayemshukia ghadhabu yangu basi huyo ameangamia.
التفاسير العربية:
وَإِنِّي لَغَفَّارٞ لِّمَن تَابَ وَءَامَنَ وَعَمِلَ صَٰلِحٗا ثُمَّ ٱهۡتَدَىٰ
Na hakika Mimi ni Mwingi wa Kusamehe kwa anayetubia, na akaamini, na akatenda mema, kisha akaongoka.
التفاسير العربية:
۞ وَمَآ أَعۡجَلَكَ عَن قَوۡمِكَ يَٰمُوسَىٰ
a nini kilichokutia haraka ukawaacha watu wako, ewe Musa?
التفاسير العربية:
قَالَ هُمۡ أُوْلَآءِ عَلَىٰٓ أَثَرِي وَعَجِلۡتُ إِلَيۡكَ رَبِّ لِتَرۡضَىٰ
Akasema: Hao wapo nyuma yangu wananifuatia. Na nimefanya haraka kukujia, Mola wangu Mlezi, ili uridhike.
التفاسير العربية:
قَالَ فَإِنَّا قَدۡ فَتَنَّا قَوۡمَكَ مِنۢ بَعۡدِكَ وَأَضَلَّهُمُ ٱلسَّامِرِيُّ
(Mwenyezi Mungu) akasema: Sisi tumewatia mtihani watu wako baada yako, na Msamaria amewapoteza.
التفاسير العربية:
فَرَجَعَ مُوسَىٰٓ إِلَىٰ قَوۡمِهِۦ غَضۡبَٰنَ أَسِفٗاۚ قَالَ يَٰقَوۡمِ أَلَمۡ يَعِدۡكُمۡ رَبُّكُمۡ وَعۡدًا حَسَنًاۚ أَفَطَالَ عَلَيۡكُمُ ٱلۡعَهۡدُ أَمۡ أَرَدتُّمۡ أَن يَحِلَّ عَلَيۡكُمۡ غَضَبٞ مِّن رَّبِّكُمۡ فَأَخۡلَفۡتُم مَّوۡعِدِي
Musa akarudi kwa watu wake kwa ghadhabu na kusikitika. Akasema: Enyi watu wangu! Kwani Mola wenu Mlezi hakuwaahidi ahadi nzuri? Je, umekuwa muda mrefu kwenu au mmetaka ghadhabu ya Mola wenu Mlezi iwashukie, ndiyo maana mkavunja miadi yangu?
التفاسير العربية:
قَالُواْ مَآ أَخۡلَفۡنَا مَوۡعِدَكَ بِمَلۡكِنَا وَلَٰكِنَّا حُمِّلۡنَآ أَوۡزَارٗا مِّن زِينَةِ ٱلۡقَوۡمِ فَقَذَفۡنَٰهَا فَكَذَٰلِكَ أَلۡقَى ٱلسَّامِرِيُّ
Wakasema: Sisi hatukuvunja miadi yako kwa hiari yetu, lakini tulibebeshwa mizigo ya mapambo ya watu, basi tukaitupa. Na hivyo ndivyo alivyotupa yule Msamaria.
التفاسير العربية:
فَأَخۡرَجَ لَهُمۡ عِجۡلٗا جَسَدٗا لَّهُۥ خُوَارٞ فَقَالُواْ هَٰذَآ إِلَٰهُكُمۡ وَإِلَٰهُ مُوسَىٰ فَنَسِيَ
Na akawaundia ndama, kiwiliwili chenye sauti. Na wakasema: Huyu ndiye mungu wenu, na mungu wa Musa, lakini alisahau.
التفاسير العربية:
أَفَلَا يَرَوۡنَ أَلَّا يَرۡجِعُ إِلَيۡهِمۡ قَوۡلٗا وَلَا يَمۡلِكُ لَهُمۡ ضَرّٗا وَلَا نَفۡعٗا
Je, hawakuona kuwa hakuwarudishia neno, wala kuwamilikia kudhuru wala kufaa?
التفاسير العربية:
وَلَقَدۡ قَالَ لَهُمۡ هَٰرُونُ مِن قَبۡلُ يَٰقَوۡمِ إِنَّمَا فُتِنتُم بِهِۦۖ وَإِنَّ رَبَّكُمُ ٱلرَّحۡمَٰنُ فَٱتَّبِعُونِي وَأَطِيعُوٓاْ أَمۡرِي
Na hakika Harun alikwisha waambia kabla yake: Enyi watu wangu! Hakika nyinyi mmetiwa mtihanini tu kwa kitu hiki. Na kwa yakini Mola wenu Mlezi ni Arrahmani (Mwingi wa Rehema). Basi nifuateni mimi, na tiini amri yangu!
التفاسير العربية:
قَالُواْ لَن نَّبۡرَحَ عَلَيۡهِ عَٰكِفِينَ حَتَّىٰ يَرۡجِعَ إِلَيۡنَا مُوسَىٰ
Wakasema: Hatutaacha kumwabudu mpaka Musa atakaporejea kwetu.
التفاسير العربية:
قَالَ يَٰهَٰرُونُ مَا مَنَعَكَ إِذۡ رَأَيۡتَهُمۡ ضَلُّوٓاْ
(Musa) akasema: Ewe Harun! Ni nini kilichokuzuia, ulipowaona wamepotea?
التفاسير العربية:
أَلَّا تَتَّبِعَنِۖ أَفَعَصَيۡتَ أَمۡرِي
Basi usinifuate. Je, umeasi amri yangu?
التفاسير العربية:
قَالَ يَبۡنَؤُمَّ لَا تَأۡخُذۡ بِلِحۡيَتِي وَلَا بِرَأۡسِيٓۖ إِنِّي خَشِيتُ أَن تَقُولَ فَرَّقۡتَ بَيۡنَ بَنِيٓ إِسۡرَٰٓءِيلَ وَلَمۡ تَرۡقُبۡ قَوۡلِي
Akasema: Ewe mwana wa mama yangu! Usinishike ndevu zangu, wala kichwa changu. Kwa hakika naliogopa usije sema: Umewafarikisha Wana wa Israil, na hukungojea kauli yangu.
التفاسير العربية:
قَالَ فَمَا خَطۡبُكَ يَٰسَٰمِرِيُّ
(Musa) akasema: Ewe Msamaria! Unataka nini ?
التفاسير العربية:
قَالَ بَصُرۡتُ بِمَا لَمۡ يَبۡصُرُواْ بِهِۦ فَقَبَضۡتُ قَبۡضَةٗ مِّنۡ أَثَرِ ٱلرَّسُولِ فَنَبَذۡتُهَا وَكَذَٰلِكَ سَوَّلَتۡ لِي نَفۡسِي
Akasema: Niliona wasiyoyaona wao, nikachukua mkono katika athari za unyayo wa Mtume. Kisha nikalitupa. Na hivi ndivyo ilivyonielekeza nafsi yangu.
التفاسير العربية:
قَالَ فَٱذۡهَبۡ فَإِنَّ لَكَ فِي ٱلۡحَيَوٰةِ أَن تَقُولَ لَا مِسَاسَۖ وَإِنَّ لَكَ مَوۡعِدٗا لَّن تُخۡلَفَهُۥۖ وَٱنظُرۡ إِلَىٰٓ إِلَٰهِكَ ٱلَّذِي ظَلۡتَ عَلَيۡهِ عَاكِفٗاۖ لَّنُحَرِّقَنَّهُۥ ثُمَّ لَنَنسِفَنَّهُۥ فِي ٱلۡيَمِّ نَسۡفًا
(Musa) akasema: Basi ondoka! Na kwa yakini utakuwa katika maisha ukisema: Usiniguse. Na hakika una ahadi kwako isiyovunjwa. Na mtazame huyo mungu wako uliyeendelea kumuabudu. Sisi kwa hakika tutamchoma moto, kisha tutamtawanya baharini atawanyike.
التفاسير العربية:
إِنَّمَآ إِلَٰهُكُمُ ٱللَّهُ ٱلَّذِي لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَۚ وَسِعَ كُلَّ شَيۡءٍ عِلۡمٗا
Hakika mungu wenu ni Allah (Mwenyezi Mungu) tu. Hapana mungu isipokuwa Yeye. Ujuzi wake umeenea kila kitu.
التفاسير العربية:
كَذَٰلِكَ نَقُصُّ عَلَيۡكَ مِنۡ أَنۢبَآءِ مَا قَدۡ سَبَقَۚ وَقَدۡ ءَاتَيۡنَٰكَ مِن لَّدُنَّا ذِكۡرٗا
Namna hivi tunakuhadithia katika khabari za yaliyotangulia. Na hakika tumekuletea kutoka kwetu mawaidha ya kukumbukwa.
التفاسير العربية:
مَّنۡ أَعۡرَضَ عَنۡهُ فَإِنَّهُۥ يَحۡمِلُ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ وِزۡرًا
Atakayeyapa mgongo, basi kwa yakini Siku ya Kiyama atabeba mzigo.
التفاسير العربية:
خَٰلِدِينَ فِيهِۖ وَسَآءَ لَهُمۡ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ حِمۡلٗا
Wadumu humo. Na ni mzigo muovu kwao kuubeba Siku ya Kiyama!
التفاسير العربية:
يَوۡمَ يُنفَخُ فِي ٱلصُّورِۚ وَنَحۡشُرُ ٱلۡمُجۡرِمِينَ يَوۡمَئِذٖ زُرۡقٗا
Siku litakapopulizwa barugumu, na tukawakusanya wahalifu Siku hiyo, hali macho yao ni ya buluu.
التفاسير العربية:
يَتَخَٰفَتُونَ بَيۡنَهُمۡ إِن لَّبِثۡتُمۡ إِلَّا عَشۡرٗا
Watanong'onezana wao kwa wao: Hamkukaa ila siku kumi tu.
التفاسير العربية:
نَّحۡنُ أَعۡلَمُ بِمَا يَقُولُونَ إِذۡ يَقُولُ أَمۡثَلُهُمۡ طَرِيقَةً إِن لَّبِثۡتُمۡ إِلَّا يَوۡمٗا
Sisi tunajua zaidi watakayoyasema, atakaposema mbora wao katika mwendo: Nyinyi hamkukaa ila siku moja tu.
التفاسير العربية:
وَيَسۡـَٔلُونَكَ عَنِ ٱلۡجِبَالِ فَقُلۡ يَنسِفُهَا رَبِّي نَسۡفٗا
Na wanakuuliza habari za milima. Waambie: Mola wangu Mlezi ataivurugavuruga.
التفاسير العربية:
فَيَذَرُهَا قَاعٗا صَفۡصَفٗا
Na ataiacha tambarare, uwanda.
التفاسير العربية:
لَّا تَرَىٰ فِيهَا عِوَجٗا وَلَآ أَمۡتٗا
Hutaona humo mdidimio wowote wala muinuko.
التفاسير العربية:
يَوۡمَئِذٖ يَتَّبِعُونَ ٱلدَّاعِيَ لَا عِوَجَ لَهُۥۖ وَخَشَعَتِ ٱلۡأَصۡوَاتُ لِلرَّحۡمَٰنِ فَلَا تَسۡمَعُ إِلَّا هَمۡسٗا
Siku hiyo watamfuata muitaji huyo bila ya yeyote kumkengeuka.. Na sauti zote zitamnyenyekea Arrahmani (Mwingi wa Rehema). Basi hutasikia ila mnong'ono tu.
التفاسير العربية:
يَوۡمَئِذٖ لَّا تَنفَعُ ٱلشَّفَٰعَةُ إِلَّا مَنۡ أَذِنَ لَهُ ٱلرَّحۡمَٰنُ وَرَضِيَ لَهُۥ قَوۡلٗا
Siku hiyo uombezi haufai kitu, ila kwa aliyemruhusu Arrahmani (Mwingi wa Rehema) na akaridhia na maneno yake.
التفاسير العربية:
يَعۡلَمُ مَا بَيۡنَ أَيۡدِيهِمۡ وَمَا خَلۡفَهُمۡ وَلَا يُحِيطُونَ بِهِۦ عِلۡمٗا
Yeye anajua yaliyo mbele yao, na yaliyo nyuma yao. Wala wao hawawezi kumjua Yeye vilivyo.
التفاسير العربية:
۞ وَعَنَتِ ٱلۡوُجُوهُ لِلۡحَيِّ ٱلۡقَيُّومِۖ وَقَدۡ خَابَ مَنۡ حَمَلَ ظُلۡمٗا
Na zitadhalilika nyuso mbele ya Aliye Hai Milele, Mwangalizi Mkuu. Na atakuwa ameharibikiwa mwenye kubeba dhuluma.
التفاسير العربية:
وَمَن يَعۡمَلۡ مِنَ ٱلصَّٰلِحَٰتِ وَهُوَ مُؤۡمِنٞ فَلَا يَخَافُ ظُلۡمٗا وَلَا هَضۡمٗا
Na anayetenda katika mema, naye ni Muumini, basi hatahofu kudhulumiwa wala kupunjwa.
التفاسير العربية:
وَكَذَٰلِكَ أَنزَلۡنَٰهُ قُرۡءَانًا عَرَبِيّٗا وَصَرَّفۡنَا فِيهِ مِنَ ٱلۡوَعِيدِ لَعَلَّهُمۡ يَتَّقُونَ أَوۡ يُحۡدِثُ لَهُمۡ ذِكۡرٗا
Na namna hivi tumeiteremsha Qur-ani kwa Kiarabu, na tumekariri humo vitisho ili wapate kuogopa na kujilinda na iwaletee makumbusho.Na namna hivi tumeiteremsha Qur-ani kwa Kiarabu, na tumetoa humo tishio ili wapate kumcha Mungu au iwafikie ukumbusho.
التفاسير العربية:
فَتَعَٰلَى ٱللَّهُ ٱلۡمَلِكُ ٱلۡحَقُّۗ وَلَا تَعۡجَلۡ بِٱلۡقُرۡءَانِ مِن قَبۡلِ أَن يُقۡضَىٰٓ إِلَيۡكَ وَحۡيُهُۥۖ وَقُل رَّبِّ زِدۡنِي عِلۡمٗا
Ametukuka Mwenyezi Mungu, Mmiliki wa Haki. Wala usiifanyie haraka hii Qur-ani, kabla haujamalizika ufunuo wake. Na sema: Mola wangu Mlezi! Nizidishie elimu.
التفاسير العربية:
وَلَقَدۡ عَهِدۡنَآ إِلَىٰٓ ءَادَمَ مِن قَبۡلُ فَنَسِيَ وَلَمۡ نَجِدۡ لَهُۥ عَزۡمٗا
Na hapo zamani tuliagana na Adam, lakini alisahau, wala hatukupata kwake azma kubwa.
التفاسير العربية:
وَإِذۡ قُلۡنَا لِلۡمَلَٰٓئِكَةِ ٱسۡجُدُواْ لِأٓدَمَ فَسَجَدُوٓاْ إِلَّآ إِبۡلِيسَ أَبَىٰ
التفاسير العربية:
فَقُلۡنَا يَٰٓـَٔادَمُ إِنَّ هَٰذَا عَدُوّٞ لَّكَ وَلِزَوۡجِكَ فَلَا يُخۡرِجَنَّكُمَا مِنَ ٱلۡجَنَّةِ فَتَشۡقَىٰٓ
Tukasema: Ewe Adam! Hakika huyu ni adui yako na wa mkeo. Basi asiwatoeni katika Bustani hii, mkaingia mashakani.
التفاسير العربية:
إِنَّ لَكَ أَلَّا تَجُوعَ فِيهَا وَلَا تَعۡرَىٰ
Hakika humo hutakuwa na njaa wala hutakuwa uchi.
التفاسير العربية:
وَأَنَّكَ لَا تَظۡمَؤُاْ فِيهَا وَلَا تَضۡحَىٰ
Na hakika hutapata kiu humo wala hutapata joto.
التفاسير العربية:
فَوَسۡوَسَ إِلَيۡهِ ٱلشَّيۡطَٰنُ قَالَ يَٰٓـَٔادَمُ هَلۡ أَدُلُّكَ عَلَىٰ شَجَرَةِ ٱلۡخُلۡدِ وَمُلۡكٖ لَّا يَبۡلَىٰ
Lakini Shetani alimtia wasiwasi, akamwambia: Ewe Adam! Nikujuulishe mti wa kuishi maisha ya milele na ufalme usiokoma?
التفاسير العربية:
فَأَكَلَا مِنۡهَا فَبَدَتۡ لَهُمَا سَوۡءَٰتُهُمَا وَطَفِقَا يَخۡصِفَانِ عَلَيۡهِمَا مِن وَرَقِ ٱلۡجَنَّةِۚ وَعَصَىٰٓ ءَادَمُ رَبَّهُۥ فَغَوَىٰ
Basi wakaula wote wawili, na uchi wao ukawadhihirikia na wakaanza kujibandika majani ya Bustani. Na Adam akamuasi Mola wake Mlezi, na akapotea njia.
التفاسير العربية:
ثُمَّ ٱجۡتَبَٰهُ رَبُّهُۥ فَتَابَ عَلَيۡهِ وَهَدَىٰ
Kisha Mola wake Mlezi akamteua, na akamkubalia toba yake, na akamwongoa.
التفاسير العربية:
قَالَ ٱهۡبِطَا مِنۡهَا جَمِيعَۢاۖ بَعۡضُكُمۡ لِبَعۡضٍ عَدُوّٞۖ فَإِمَّا يَأۡتِيَنَّكُم مِّنِّي هُدٗى فَمَنِ ٱتَّبَعَ هُدَايَ فَلَا يَضِلُّ وَلَا يَشۡقَىٰ
Akasema: Ondokeni humu nyote, hali ya kuwa ni maadui nyinyi kwa nyinyi. Na ukiwafikia uwongofu kutoka kwangu basi atakayeufuata uwongofu wangu, hatapotea wala hatataabika.
التفاسير العربية:
وَمَنۡ أَعۡرَضَ عَن ذِكۡرِي فَإِنَّ لَهُۥ مَعِيشَةٗ ضَنكٗا وَنَحۡشُرُهُۥ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ أَعۡمَىٰ
Na atakayeupa ukumbusho wangu mgongo, basi kwa yakini atapata maisha yenye dhiki, na Siku ya Kiyama tutamfufua hali ya kuwa kipofu.
التفاسير العربية:
قَالَ رَبِّ لِمَ حَشَرۡتَنِيٓ أَعۡمَىٰ وَقَدۡ كُنتُ بَصِيرٗا
Aseme: Ewe Mola wangu Mlezi! Mbona umenifufua kipofu, nami nilikuwa nikiona?
التفاسير العربية:
قَالَ كَذَٰلِكَ أَتَتۡكَ ءَايَٰتُنَا فَنَسِيتَهَاۖ وَكَذَٰلِكَ ٱلۡيَوۡمَ تُنسَىٰ
(Mwenyezi Mungu) atasema: Ndivyo vivyo hivyo. Zilikufikia ishara zetu, nawe ukazisahau; na vivyo hivyo leo utasahauliwa.
التفاسير العربية:
وَكَذَٰلِكَ نَجۡزِي مَنۡ أَسۡرَفَ وَلَمۡ يُؤۡمِنۢ بِـَٔايَٰتِ رَبِّهِۦۚ وَلَعَذَابُ ٱلۡأٓخِرَةِ أَشَدُّ وَأَبۡقَىٰٓ
Na hivyo ndivyo tutakavyomlipa kila apitaye kiasi, na asiziamini ishara za Mola wake Mlezi. Na hakika adhabu ya Akhera ni kali zaidi, na inadumu zaidi.
التفاسير العربية:
أَفَلَمۡ يَهۡدِ لَهُمۡ كَمۡ أَهۡلَكۡنَا قَبۡلَهُم مِّنَ ٱلۡقُرُونِ يَمۡشُونَ فِي مَسَٰكِنِهِمۡۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَٰتٖ لِّأُوْلِي ٱلنُّهَىٰ
Je, haikuwabainikia ni ngapi katika vizazi tuliviangamiza kabla yao, nao wanatembea katika maskani zao? Hakika katika hayo zimo ishara kwa wenye akili.
التفاسير العربية:
وَلَوۡلَا كَلِمَةٞ سَبَقَتۡ مِن رَّبِّكَ لَكَانَ لِزَامٗا وَأَجَلٞ مُّسَمّٗى
Na lau kuwa si neno lililokwishatangulia kutoka kwa Mola wako Mlezi na muda uliowekwa, bila ya shaka ingefika adhabu (hapa hapa).
التفاسير العربية:
فَٱصۡبِرۡ عَلَىٰ مَا يَقُولُونَ وَسَبِّحۡ بِحَمۡدِ رَبِّكَ قَبۡلَ طُلُوعِ ٱلشَّمۡسِ وَقَبۡلَ غُرُوبِهَاۖ وَمِنۡ ءَانَآيِٕ ٱلَّيۡلِ فَسَبِّحۡ وَأَطۡرَافَ ٱلنَّهَارِ لَعَلَّكَ تَرۡضَىٰ
Basi yavumilie haya wayasemayo. Na umtakase Mola wako Mlezi kwa kumsifu kabla ya kuchomoza jua, na kabla ya kuzama kwake, na nyakati za usiku pia umtakase, na nyakati za mwisho za mchana ili upate ya kukuridhisha.
التفاسير العربية:
وَلَا تَمُدَّنَّ عَيۡنَيۡكَ إِلَىٰ مَا مَتَّعۡنَا بِهِۦٓ أَزۡوَٰجٗا مِّنۡهُمۡ زَهۡرَةَ ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَا لِنَفۡتِنَهُمۡ فِيهِۚ وَرِزۡقُ رَبِّكَ خَيۡرٞ وَأَبۡقَىٰ
Wala kamwe usivikodolee macho tulivyowastarehesha kwavyo baadhi ya watu miongoni mwao, kwa ajili ya mapambo ya duniani, ili tuwajaribu katika hivyo. Na riziki ya Mola wako Mlezi ni bora na yenye kudumu zaidi.
التفاسير العربية:
وَأۡمُرۡ أَهۡلَكَ بِٱلصَّلَوٰةِ وَٱصۡطَبِرۡ عَلَيۡهَاۖ لَا نَسۡـَٔلُكَ رِزۡقٗاۖ نَّحۡنُ نَرۡزُقُكَۗ وَٱلۡعَٰقِبَةُ لِلتَّقۡوَىٰ
Na waamrishe ahali zako kuswali, na usubiri juu yake. Sisi hatukuombi wewe riziki, bali Sisi ndio tunakuruzuku. Na mwisho mwema ni kwa uchamungu.
التفاسير العربية:
وَقَالُواْ لَوۡلَا يَأۡتِينَا بِـَٔايَةٖ مِّن رَّبِّهِۦٓۚ أَوَلَمۡ تَأۡتِهِم بَيِّنَةُ مَا فِي ٱلصُّحُفِ ٱلۡأُولَىٰ
Na walisema: Kwa nini hakutuletea muujiza kutoka kwa Mola wake Mlezi? Je, haukuwajia ushahidi wazi wa yaliyomo katika Vitabu vya mwanzo?
التفاسير العربية:
وَلَوۡ أَنَّآ أَهۡلَكۡنَٰهُم بِعَذَابٖ مِّن قَبۡلِهِۦ لَقَالُواْ رَبَّنَا لَوۡلَآ أَرۡسَلۡتَ إِلَيۡنَا رَسُولٗا فَنَتَّبِعَ ءَايَٰتِكَ مِن قَبۡلِ أَن نَّذِلَّ وَنَخۡزَىٰ
Na lau kuwa tuliwaangamiza kwa adhabu kabla yake, wangelisema: Ewe Mola wetu Mlezi! Kwa nini hukutuletea Mtume tukazifuata ishara zako kabla ya kudhalilika na kuhizika.
التفاسير العربية:
قُلۡ كُلّٞ مُّتَرَبِّصٞ فَتَرَبَّصُواْۖ فَسَتَعۡلَمُونَ مَنۡ أَصۡحَٰبُ ٱلصِّرَٰطِ ٱلسَّوِيِّ وَمَنِ ٱهۡتَدَىٰ
Sema: Kila mmoja anangoja. Basi ngojeni! Hivi karibuni mtajua ni akina nani ndio wenye njia sawa na ni nani aliyeongoka.
التفاسير العربية:
 
ترجمة معاني سورة: طه
فهرس السور رقم الصفحة
 
ترجمة معاني القرآن الكريم - الترجمة السواحيلية - جمعية خدمة المحتوى - فهرس التراجم

صادرة عن جمعية خدمة المحتوى الإسلامي باللغات.

إغلاق