Na inapo kufikieni taabu katika bahari, hao mnao waomba wanapotea, isipo kuwa Yeye tu. Na anapo kuvueni mkafika nchi kavu, mnageuka. Ama mwanaadamu ni mwingi wa kukanusha.
Mkisibiwa na madhara na mkakabiliwa na khatari katika bahari, hukukimbieni wote hao muwaombao kwa haja zenu isipo kuwa Mwenyezi Mungu peke yake. Kwani nyinyi hapo hamumkumbuki mwenginewe. Lakini akisha kuvueni na kuzama na akakufikisheni nchi kavu, mnaacha Tawhid, kumuabudu Mwenyezi Mungu Mmoja, na mnakufuru neema. Ndio mtindo wa binaadamu daima kukataa neema.
Je! Mmeaminisha ya kuwa hatakudidimizeni upande wowote katika nchi kavu, au kwamba hatakuleteeni tufani la kokoto? Kisha msipate wa kumtegemea.
Na hapo tukisha kuvueni mkafika nchi kavu, kwani ndio mmeaminisha kuwa basi haikupateni adhabu ya Mwenyezi Mungu? Hasha! Akitaka anaweza akaipindua ardhi ikakuteketezeni chini yake. Na akitaka atakupelekeeni upepo mkali ukutupieni kokoto na mawe, na wala msipate wa kukulindeni na yanayo kupateni.
Au mmeaminisha ya kuwa hatakurudisheni humo mara nyengine na kukupelekeeni kimbunga cha upepo akakuzamisheni kwa mlivyo kufuru, na kisha msipate wa kukunusuruni nasi.
Au nyinyi mmeaminisha kuwa Mola wenu Mlezi hatakurejesheni tena baharini, na akuleteeni tufani la upepo livunjilie mbali hicho chombo chenu? Akakuzamisheni kwa sababu ya kuto thamini neema yake pale alipo kuokoeni mara ya kwanza? Tena hapo hamtapata wa kukuteteeni kwetu kwa tuliyo kufanyieni ili mpate kusalimika.
Na hakika tumewatukuza wanaadamu, na tumewapa vya kupanda nchi kavu na baharini, na tumewaruzuku vitu vizuri vizuri, na tumewafadhilisha kwa fadhila kubwa kuliko wengi miongoni mwa tulio waumba.
Na hakika Sisi tumewatukuza wana wa Adam kwa kuwapa umbo zuri lilio nyooka, na matamshi, na uwezo wa kukhiari mambo. Na tukawapa hishima na utukufu pindi wakit'ii. Na tukawapakia nchi kavu juu ya wanyama, na baharini katika marikebu, na tukawaruzuku vitu vitamu, na tukawafadhilisha fadhila kubwa kuliko viumbe vingi kwa kuwapa akili na kuweza kufikiri.
Siku tutapo waita kila kikundi cha watu kwa mujibu wa wakifuatacho - basi atakaye pewa kitabu chake kwa mkono wake wa kulia, basi hao watasoma kitabu chao wala hawatadhulumiwa hata chembe.
Ewe Nabii! Waambie watu wako: Siku tutapo waita kila kikundi kwa alama zao wanazo zijua, au mwongozi wao wanaye mfuata, au Nabii, au Kitabu wakaambiwa: Enyi watu wa Musa! Au Enyi watu wa Qur'ani! Na kadhaalika, ili wapokee vitabu vya a'mali zao. Basi atakaye pokea kitabu cha a'mali zake kwa mkono wake wa kulia, na hao ndio wenye bahati njema, hao watasoma kitabu chao kwa furaha. Na wala hawatapunguziwa katika ujira wao duni ya kitu.
Na aliye kuwa hapa kipofu, basi atakuwa kipofu Akhera, na atakuwa aliye ipotea zaidi Njia.
Ama yule wa kikundi kingine yatamhuzunisha atayo yaona. Na atazibiwa njia za kuokoka. Na atakuwa kipofu asione pa kuepuka adhabu yake, kama alivyo kuwa duniani kipofu haioni Njia ya Haki na Uwongofu! Na anaye kuwa duniani kipofu (wa moyo) basi Akhera ni kipofu zaidi, na yu mbali zaidi na Njia ya Kheri.
Na hakika walikaribia kukushawishi uache tuliyo kufunulia ili utuzulie mengineyo. Na hapo ndio wangeli kufanya rafiki.
Hakika washirikina wanatafuta kila njia wakuachishe Qur'ani utafute miujiza myengineyo, ili uwe kama uliye tuzulia Sisi uwongo. Na hapo ndio watakufanya uwe rafiki yao! Na hila hizi zimekaririwa na zimekuwa nyingi. Na kwa hivyo ungeli karibia kuyafuata wayatakayo, ila kwa kuwa wewe ni Mtume wetu uliye muaminifu, hayakuwa hayo.
Na lau kuwa hatukukuweka imara ungeli karibia kuwaelekea kidogo.
Upole wetu umekugubika wewe, tukakulinda usiwakubalie matakwa yao, na tukakupa nguvu usimame juu ya Haki. Na lau kuwa si hayo ungeli karibia kuwakubalia kwa tamaa ya kuwa huenda ikafika siku imani yao ikakamilika baadae wakisha anza kuingia katika Uislamu.
Hapo basi bila ya shaka tungeli kuonjesha adhabu mardufu ya uhai, na adhabu mardufu ya kifo. Kisha usinge pata mtu wa kukunusuru nasi.
Na lau ungeli karibia kuwaelekea hao, basi tungeli kukusanyia adhabu za duniani tukazifanya mardufu, na adhabu za Akhera nazo tukaziongeza mara mbili vile vile. Na wala usingeli pata yeyote wa kukunusuru na adhabu. Lakini hayo hayawi kabisa, hayawezi kumfikilia Mtume wetu Muaminifu.
Contents of the translations can be downloaded and re-published, with the following terms and conditions:
1. No modification, addition, or deletion of the content.
2. Clearly referring to the publisher and the source (QuranEnc.com).
3. Mentioning the version number when re-publishing the translation.
4. Keeping the transcript information inside the document.
5. Notifying the source (QuranEnc.com) of any note on the translation.
6. Updating the translation according to the latest version issued from the source (QuranEnc.com).
7. Inappropriate advertisements must not be included when displaying translations of the meanings of the Noble Quran.
অনুসন্ধানৰ ফলাফল:
API specs
Endpoints:
Sura translation
GET / https://quranenc.com/api/v1/translation/sura/{translation_key}/{sura_number} description: get the specified translation (by its translation_key) for the speicified sura (by its number)
Parameters: translation_key: (the key of the currently selected translation) sura_number: [1-114] (Sura number in the mosshaf which should be between 1 and 114)
Returns:
json object containing array of objects, each object contains the "sura", "aya", "translation" and "footnotes".
GET / https://quranenc.com/api/v1/translation/aya/{translation_key}/{sura_number}/{aya_number} description: get the specified translation (by its translation_key) for the speicified aya (by its number sura_number and aya_number)
Parameters: translation_key: (the key of the currently selected translation) sura_number: [1-114] (Sura number in the mosshaf which should be between 1 and 114) aya_number: [1-...] (Aya number in the sura)
Returns:
json object containing the "sura", "aya", "translation" and "footnotes".