আল-কোৰআনুল কাৰীমৰ অৰ্থানুবাদ - ছাৱাহিলী অনুবাদ- আলী মুহছিন আল-বিৰৱানী * - অনুবাদসমূহৰ সূচীপত্ৰ

XML CSV Excel API
Please review the Terms and Policies

অৰ্থানুবাদ ছুৰা: ছুৰা আল-মুতাফ্ফিফীন   আয়াত:

Surat Al-Mutaffifin

وَيۡلٞ لِّلۡمُطَفِّفِينَ
Ole wao hao wapunjao!
Wataangamia wanao punja,
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
ٱلَّذِينَ إِذَا ٱكۡتَالُواْ عَلَى ٱلنَّاسِ يَسۡتَوۡفُونَ
Ambao wanapo jipimia kwa watu hudai watimiziwe.
Ambao wakijipimia wenyewe kwa watu hujitwalia ya kutosha na kuzidi,
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
وَإِذَا كَالُوهُمۡ أَو وَّزَنُوهُمۡ يُخۡسِرُونَ
Na wao wanapo wapimia watu kwa kipimo au mizani hupunguza.
Na wakiwapimia watu kwa vipimo au mizani huwapunguzia haki yao wanayo stahiki, kwa dhulma!
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
أَلَا يَظُنُّ أُوْلَٰٓئِكَ أَنَّهُم مَّبۡعُوثُونَ
Kwani hawadhani hao kwamba watafufuliwa .
Hivyo haiwapitikii katika akili zao hawa wanao punja wenzao kwamba watakuja fufuliwa,
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
لِيَوۡمٍ عَظِيمٖ
Katika Siku iliyo kuu!
Katika siku ya vitisho vikuu?
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
يَوۡمَ يَقُومُ ٱلنَّاسُ لِرَبِّ ٱلۡعَٰلَمِينَ
Siku watapo msimamia watu Mola Mlezi wa walimwengu wote?
Siku watapo simama watu kwa amri ya Mola Mlezi wa walimwengu wote na hukumu yake?
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
كَلَّآ إِنَّ كِتَٰبَ ٱلۡفُجَّارِ لَفِي سِجِّينٖ
Hasha! Hakika maandiko ya wakosefu bila ya shaka yamo katika Sijjin.
Wacheni kupunja, na kughafilika na kufufuliwa! Kwani hakika waliyo andikiwa wakosefu katika a'mali zao mbovu, bila ya shaka yamo katika Sijjin.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا سِجِّينٞ
Unajua nini Sijjin?
Na nini kitakujuvya nini hiyo Sijjin?
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
كِتَٰبٞ مَّرۡقُومٞ
Kitabu kilicho andikwa.
Hicho ni Kitabu kilicho pigwa mistari baina ya maandishi yake.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
وَيۡلٞ يَوۡمَئِذٖ لِّلۡمُكَذِّبِينَ
Ole wao siku hiyo kwa wanao kadhibisha!
Wataangamia wanao kadhibisha siku itapo kuwa kufufuliwa na kuhisabiwa.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
ٱلَّذِينَ يُكَذِّبُونَ بِيَوۡمِ ٱلدِّينِ
Ambao wanaikadhibisha Siku ya Malipo.
Ambao wanaikanusha Siku ya Malipo.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
وَمَا يُكَذِّبُ بِهِۦٓ إِلَّا كُلُّ مُعۡتَدٍ أَثِيمٍ
Wala haikadhibishi ila kila mwenye kuruka mipaka, mwenye dhambi.
Na wala haikanushi Siku ya Malipo ila kila mwenye kupindukia mipaka mwingi wa madhambi.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
إِذَا تُتۡلَىٰ عَلَيۡهِ ءَايَٰتُنَا قَالَ أَسَٰطِيرُ ٱلۡأَوَّلِينَ
Anapo somewa Aya zetu husema: Ni visa vya watu wa kale!
Na akisomewa Aya za Mwenyezi Mungu zenye kutaja kuwepo malipo husema: Huo ni uwongo wa walio tangulia!
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
كَلَّاۖ بَلۡۜ رَانَ عَلَىٰ قُلُوبِهِم مَّا كَانُواْ يَكۡسِبُونَ
Hasha! Bali yametia kutu juu ya nyoyo zao hao walio kuwa wakiyachuma.
Ewe uliye kiuka mipaka! Wacha kauli hiyo potovu. Bali nyoyo za wenye kupindukia mipaka imegubikwa na ukafiri na maasi waliyo yatenda.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
كَلَّآ إِنَّهُمۡ عَن رَّبِّهِمۡ يَوۡمَئِذٖ لَّمَحۡجُوبُونَ
Hasha! Hakika hao siku hiyo bila ya shaka watazuiliwa na neema za Mola wao Mlezi.
Hakika ni kweli kuwa hao wanao kadhibisha watazuiliwa siku hiyo rehema ya Mwenyezi Mungu kwa sababu ya maasi waliyo yachuma.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
ثُمَّ إِنَّهُمۡ لَصَالُواْ ٱلۡجَحِيمِ
Kisha wataingia Motoni!
Kisha hakika hao bila ya shaka wataingia Motoni.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
ثُمَّ يُقَالُ هَٰذَا ٱلَّذِي كُنتُم بِهِۦ تُكَذِّبُونَ
Kisha waambiwe: Haya ndiyo mliyo kuwa mkiyakadhabisha.
Kisha wataambiwa kwa kuwakebehi: Hii basi ndiyo adhabu inayo kuteremkieni ambayo mlikuwa mkiikanusha duniani!
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
كَلَّآ إِنَّ كِتَٰبَ ٱلۡأَبۡرَارِ لَفِي عِلِّيِّينَ
Hasha! Hakika maandiko ya watu wema bila ya shaka yamo katika I'liyyin.
Ni hakika kuwa vitendo vya watu wema bila ya shaka vimeandikwa katika I'liyyin.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
وَمَآ أَدۡرَىٰكَ مَا عِلِّيُّونَ
Na nini kitakacho kujuvya nini I'liyyin?
Na nini cha kukujuvya nini I'liyyin?
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
كِتَٰبٞ مَّرۡقُومٞ
Kitabu kilicho andikwa.
Hicho ni Kitabu kilicho andikwa wazi maandishi yake,
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
يَشۡهَدُهُ ٱلۡمُقَرَّبُونَ
Wanakishuhudia walio karibishwa.
Wanakihudhurisha na kukihifadhi Malaika walio kurubishwa.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
إِنَّ ٱلۡأَبۡرَارَ لَفِي نَعِيمٍ
Hakika watu wema bila ya shaka watakuwa katika neema.
Hakika watu wema bila ya shaka watakuwa katika neema za Peponi,
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
عَلَى ٱلۡأَرَآئِكِ يَنظُرُونَ
Wakae juu ya viti vya enzi wakiangalia.
Juu ya viti vya enzi, wakiziangalia neema na ukarimu alio wakirimu Mwenyezi Mungu.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
تَعۡرِفُ فِي وُجُوهِهِمۡ نَضۡرَةَ ٱلنَّعِيمِ
Utatambua katika nyuso zao mng'aro wa neema,
Utaona katika nyuso zao uchangamfu na mng'aro wa neema.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
يُسۡقَوۡنَ مِن رَّحِيقٖ مَّخۡتُومٍ
Watanyweshwa kinywaji safi kiliyo tiwa muhuri,
Wakinyweshwa kinywaji safi kilicho hifadhiwa;
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
خِتَٰمُهُۥ مِسۡكٞۚ وَفِي ذَٰلِكَ فَلۡيَتَنَافَسِ ٱلۡمُتَنَٰفِسُونَ
Muhuri wake ni miski. Na katika hayo washindanie wenye kushindana.
Kuhifadhiwa huko hakukuzidisha ila uzuri wake. Na kupata neema hizo, basi, na washindanie wanao shindana.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
وَمِزَاجُهُۥ مِن تَسۡنِيمٍ
Na mchanganyiko wake ni Tasniim,
Cha kuchanganyia kinywaji hicho ni maji ya Tasniim ya Peponi,
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
عَيۡنٗا يَشۡرَبُ بِهَا ٱلۡمُقَرَّبُونَ
Chemchem watakayo inywa walio kurubishwa.
Nayo ni chemchem wanao inywa walio kurubishwa si wengineo, katika watu wa Peponi.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
إِنَّ ٱلَّذِينَ أَجۡرَمُواْ كَانُواْ مِنَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ يَضۡحَكُونَ
Kwa hakika wale walio kuwa wakosefu walikuwa wakiwacheka walio amini.
Wale walio kuwa wakibeba madhambi kuipingia Dini walikuwa wakiwacheka kuwakejeli Waumini duniani.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
وَإِذَا مَرُّواْ بِهِمۡ يَتَغَامَزُونَ
 Na wanapo pita karibu yao wakikonyezana.
Na wakipita Waumini mbele yao basi wao hukonyezana kwa kuwabeza.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
وَإِذَا ٱنقَلَبُوٓاْ إِلَىٰٓ أَهۡلِهِمُ ٱنقَلَبُواْ فَكِهِينَ
Na wanapo rudi kwa watu wao hurudi nao wamefurahi.
Na hao wakosefu wakirejea kwa ahali zao hurejea kwa furaha na kuona ladha kwa vile kuwakejeli Waumini.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
وَإِذَا رَأَوۡهُمۡ قَالُوٓاْ إِنَّ هَٰٓؤُلَآءِ لَضَآلُّونَ
Na wanapo waona husema: Hakika hawa ndio khasa walio potea.
Na wakiwaona Waumini husema: Ama hakika hawa wamepotea kweli kwa kumuamini Muhammad.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
وَمَآ أُرۡسِلُواْ عَلَيۡهِمۡ حَٰفِظِينَ
Na wao hawakutumwa wawe walinzi juu yao.
Wala hao wakosefu hawakutumwa wawe wa kuwahukumu Waumini kwa kuwaongoza au kuwapoteza, wala kuwa ni walinzi wa vitendo vyao.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
فَٱلۡيَوۡمَ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ مِنَ ٱلۡكُفَّارِ يَضۡحَكُونَ
Basi leo walio amini ndio watawacheka makafiri,
Basi Siku ya Malipo walio amini watakuwa ndio wa kuwacheka hao makafiri kwa kuwalipizia kile kicheko chao na kejeli yao ya duniani.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
عَلَى ٱلۡأَرَآئِكِ يَنظُرُونَ
Nao wako juu ya viti vya enzi wakiangalia.
Ilhali wako juu ya vitanda na matakia watakuwa Waumini wakiziangalia neema za Mwenyezi Mungu alizo wapa.
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
هَلۡ ثُوِّبَ ٱلۡكُفَّارُ مَا كَانُواْ يَفۡعَلُونَ
Je! makafiri wamelipwa malipo ya yale waliyo kuwa wakiyatenda?
Je! Makafiri watalipwa huko Akhera kwa waliyo yatenda duniani?
আৰবী তাফছীৰসমূহ:
 
অৰ্থানুবাদ ছুৰা: ছুৰা আল-মুতাফ্ফিফীন
ছুৰাৰ তালিকা পৃষ্ঠা নং
 
আল-কোৰআনুল কাৰীমৰ অৰ্থানুবাদ - ছাৱাহিলী অনুবাদ- আলী মুহছিন আল-বিৰৱানী - অনুবাদসমূহৰ সূচীপত্ৰ

ছাৱাহিলী ভাষাত কোৰআনুল কাৰীমৰ অৰ্থানুবাদ- অনুবাদ কৰিছে মুহছিন আল-বিৰৱানী

বন্ধ