Prijevod značenja časnog Kur'ana - الترجمة السواحلية - علي محسن البرواني * - Sadržaj prijevodā

XML CSV Excel API
Please review the Terms and Policies

Prijevod značenja Ajet: (75) Sura: Sura en-Nahl
۞ ضَرَبَ ٱللَّهُ مَثَلًا عَبۡدٗا مَّمۡلُوكٗا لَّا يَقۡدِرُ عَلَىٰ شَيۡءٖ وَمَن رَّزَقۡنَٰهُ مِنَّا رِزۡقًا حَسَنٗا فَهُوَ يُنفِقُ مِنۡهُ سِرّٗا وَجَهۡرًاۖ هَلۡ يَسۡتَوُۥنَۚ ٱلۡحَمۡدُ لِلَّهِۚ بَلۡ أَكۡثَرُهُمۡ لَا يَعۡلَمُونَ
Mwenyezi Mungu anapiga mfano wa mtumwa aliye milikiwa, asiyeweza kitu, na mwingine tuliye mruzuku riziki njema inayo toka kwetu,naye akawa anatoa katika riziki hiyo kwa siri na dhaahiri. Je, hao watakuwa sawa? Alhamdu Lillahi! Kuhimidiwa kote ni kwa Mwenyezi Mungu.Lakini wengi wao hawajui.
* Mwenyezi Mungu amepiga mfano kufahamisha ufisadi walio nao washirikina. Mtumwa aliye milikiwa kama mtumwa mamluki, hanalo aliwezalo kulitenda; na muungwana anaye ruzukiwa na Mwenyezi Mungu riziki ya halali, naye anatoa katika hiyo riziki kwa siri na dhaahiri! Je, ni sawa watumwa wasio weza kitu, na waungwana wenye nacho na wanatumia walicho nacho? Hakika Mwenyezi Mungu anamiliki kila kitu, na anafanya katika ufalme wake kama apendavyo. Na asiye kuwa Yeye hamiliki chochote. Basi huyo hastahiki kuabudiwa na kuhimidiwa. Sifa zote ni haki ya Mwenyezi Mungu peke yake. Yeye ndiye Mwenye Utukufu peke yake, kwani kila kheri inatoka kwake, na kila zuri linarejea kwake. Wala hawatendi hao wanayo yatenda kwa kujua, bali wanatenda kwa kuwafuata wakubwa zao. Bali wengi wao hawajui, na wanaziambatisha neema za Mwenyezi Mungu kwa wengineo, na wanawaabudu hao badala yake!
Tefsiri na arapskom jeziku:
 
Prijevod značenja Ajet: (75) Sura: Sura en-Nahl
Indeks sura Broj stranice
 
Prijevod značenja časnog Kur'ana - الترجمة السواحلية - علي محسن البرواني - Sadržaj prijevodā

ترجمة معاني القرآن الكريم إلى اللغة السواحلية، ترجمها علي محسن البرواني.

Zatvaranje