Check out the new design

Prijevod značenja časnog Kur'ana - Prijevod na svahili jezik - Prevodilački centar Ruvvad * - Sadržaj prijevodā


Prijevod značenja Sura: Hud   Ajet:
قَالَ يَٰقَوۡمِ أَرَءَيۡتُمۡ إِن كُنتُ عَلَىٰ بَيِّنَةٖ مِّن رَّبِّي وَءَاتَىٰنِي مِنۡهُ رَحۡمَةٗ فَمَن يَنصُرُنِي مِنَ ٱللَّهِ إِنۡ عَصَيۡتُهُۥۖ فَمَا تَزِيدُونَنِي غَيۡرَ تَخۡسِيرٖ
Akasema: Enyi kaumu yangu! Mwaonaje ikiwa ninao ushahidi ulio wazi kutoka kwa Mola wangu Mlezi, naye akawa amenipa rehema kutoka kwake, je, ni nani atakayeninusuru kutokana na Mwenyezi Mungu nikimuasi? Basi nyinyi hamnizidishii isipokuwa kuhasirika tu.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَيَٰقَوۡمِ هَٰذِهِۦ نَاقَةُ ٱللَّهِ لَكُمۡ ءَايَةٗۖ فَذَرُوهَا تَأۡكُلۡ فِيٓ أَرۡضِ ٱللَّهِۖ وَلَا تَمَسُّوهَا بِسُوٓءٖ فَيَأۡخُذَكُمۡ عَذَابٞ قَرِيبٞ
Na enyi kaumu yangu! Huyu ni ngamia wa Mwenyezi Mungu kama Ishara kwenu. Basi mwacheni ale katika ardhi ya Mwenyezi Mungu, wala msimguse kwa ubaya, ikaja kuwaangamiza adhabu iliyo karibu.
Tefsiri na arapskom jeziku:
فَعَقَرُوهَا فَقَالَ تَمَتَّعُواْ فِي دَارِكُمۡ ثَلَٰثَةَ أَيَّامٖۖ ذَٰلِكَ وَعۡدٌ غَيۡرُ مَكۡذُوبٖ
Lakini wakamchinja. Basi (Saleh) akasema: Stareheni katika makazi yenu muda wa siku tatu. Hiyo ni ahadi isiyokuwa ya uongo.
Tefsiri na arapskom jeziku:
فَلَمَّا جَآءَ أَمۡرُنَا نَجَّيۡنَا صَٰلِحٗا وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ مَعَهُۥ بِرَحۡمَةٖ مِّنَّا وَمِنۡ خِزۡيِ يَوۡمِئِذٍۚ إِنَّ رَبَّكَ هُوَ ٱلۡقَوِيُّ ٱلۡعَزِيزُ
Basi ilipokuja amri yetu, tulimwokoa sawasawa Saleh na wale walioamini pamoja naye kwa rehema yetu kutokana na hizaya ya siku ile. Hakika Mola wako Mlezi ndiye Mwenye nguvu, Mtukufu.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَأَخَذَ ٱلَّذِينَ ظَلَمُواْ ٱلصَّيۡحَةُ فَأَصۡبَحُواْ فِي دِيَٰرِهِمۡ جَٰثِمِينَ
Na ukelele uliwaangamiza wale waliodhulumu, basi wakaishia majumbani mwao wamekufa kifudifudi!
Tefsiri na arapskom jeziku:
كَأَن لَّمۡ يَغۡنَوۡاْ فِيهَآۗ أَلَآ إِنَّ ثَمُودَاْ كَفَرُواْ رَبَّهُمۡۗ أَلَا بُعۡدٗا لِّثَمُودَ
Kama kwamba hawakuishi kwa ustawi huko. Hebu zingatieni! Hakika kina Thamud walimkufuru Mola wao Mlezi. Hebu zingatieni! Thamud walipotelea mbali!
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَلَقَدۡ جَآءَتۡ رُسُلُنَآ إِبۡرَٰهِيمَ بِٱلۡبُشۡرَىٰ قَالُواْ سَلَٰمٗاۖ قَالَ سَلَٰمٞۖ فَمَا لَبِثَ أَن جَآءَ بِعِجۡلٍ حَنِيذٖ
Na hakika wajumbe wetu walimjia Ibrahim kwa bishara njema, wakasema, "Salama!" Naye akasema, "Salama!" Kisha hakukaa isipokuwa mara hiyo akaja na ndama wa kuchoma.
Tefsiri na arapskom jeziku:
فَلَمَّا رَءَآ أَيۡدِيَهُمۡ لَا تَصِلُ إِلَيۡهِ نَكِرَهُمۡ وَأَوۡجَسَ مِنۡهُمۡ خِيفَةٗۚ قَالُواْ لَا تَخَفۡ إِنَّآ أُرۡسِلۡنَآ إِلَىٰ قَوۡمِ لُوطٖ
Basi alipoiona mikono yao haimfikii, akawatilia shaka, na akawahofu. Wakasema, "Usihofu! Hakika sisi tumetumwa kwa kaumu ya Lut."
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَٱمۡرَأَتُهُۥ قَآئِمَةٞ فَضَحِكَتۡ فَبَشَّرۡنَٰهَا بِإِسۡحَٰقَ وَمِن وَرَآءِ إِسۡحَٰقَ يَعۡقُوبَ
Na mkewe alikuwa amesimama wima, akacheka. Basi tukambashiria kuhusu (kuzaliwa kwa) Is-haq, na baada ya Is-haq Yaaqub.
Tefsiri na arapskom jeziku:
 
Prijevod značenja Sura: Hud
Indeks sura Broj stranice
 
Prijevod značenja časnog Kur'ana - Prijevod na svahili jezik - Prevodilački centar Ruvvad - Sadržaj prijevodā

Prevod: Prevodilački centar Ruvvad u saradnji sa Udruženjem za poziv u Rabwi i Udruženjem za pružanje islamskog sadržaja na jezicima.

Zatvaranje