Check out the new design

Prijevod značenja časnog Kur'ana - Prijevod na svahili jezik - Prevodilački centar Ruvvad * - Sadržaj prijevodā


Prijevod značenja Sura: En-Nahl   Ajet:
وَمَآ أَرۡسَلۡنَا مِن قَبۡلِكَ إِلَّا رِجَالٗا نُّوحِيٓ إِلَيۡهِمۡۖ فَسۡـَٔلُوٓاْ أَهۡلَ ٱلذِّكۡرِ إِن كُنتُمۡ لَا تَعۡلَمُونَ
Nasi hatukuwatuma kabla yako isipokuwa watu wanaume tuliowapa Wahyi (Ufunuo). Basi waulizeni wenye ukumbusho kama nyinyi hamjui.
Tefsiri na arapskom jeziku:
بِٱلۡبَيِّنَٰتِ وَٱلزُّبُرِۗ وَأَنزَلۡنَآ إِلَيۡكَ ٱلذِّكۡرَ لِتُبَيِّنَ لِلنَّاسِ مَا نُزِّلَ إِلَيۡهِمۡ وَلَعَلَّهُمۡ يَتَفَكَّرُونَ
Kwa Ishara wazi na Vitabu. Nasi tumekuteremshia wewe Ukumbusho ili uwabainishie watu yale yaliyoteremshwa kwao, ili wapate kutafakari.
Tefsiri na arapskom jeziku:
أَفَأَمِنَ ٱلَّذِينَ مَكَرُواْ ٱلسَّيِّـَٔاتِ أَن يَخۡسِفَ ٱللَّهُ بِهِمُ ٱلۡأَرۡضَ أَوۡ يَأۡتِيَهُمُ ٱلۡعَذَابُ مِنۡ حَيۡثُ لَا يَشۡعُرُونَ
Je wana amani wale wanaopanga njama mbaya kwamba Mwenyezi Mungu hatawadidimiza katika ardhi, na haitawafikia adhabu kutoka wasipohisi?
Tefsiri na arapskom jeziku:
أَوۡ يَأۡخُذَهُمۡ فِي تَقَلُّبِهِمۡ فَمَا هُم بِمُعۡجِزِينَ
Au hatawashika katika harakati zao, na wala hawatamshinda?
Tefsiri na arapskom jeziku:
أَوۡ يَأۡخُذَهُمۡ عَلَىٰ تَخَوُّفٖ فَإِنَّ رَبَّكُمۡ لَرَءُوفٞ رَّحِيمٌ
Au hatawashika huku wana hofu? Hakika Mola wenu Mlezi ni Mwenye huruma kubwa, Mwingi wa kurehemu.
Tefsiri na arapskom jeziku:
أَوَلَمۡ يَرَوۡاْ إِلَىٰ مَا خَلَقَ ٱللَّهُ مِن شَيۡءٖ يَتَفَيَّؤُاْ ظِلَٰلُهُۥ عَنِ ٱلۡيَمِينِ وَٱلشَّمَآئِلِ سُجَّدٗا لِّلَّهِ وَهُمۡ دَٰخِرُونَ
Je, hawavioni vitu alivyoviumba Mwenyezi Mungu, vivuli vyao vinaelekea kushotoni na kuliani, kumsujudia Mwenyezi Mungu na vikinyenyekea?
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَلِلَّهِۤ يَسۡجُدُۤ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِ مِن دَآبَّةٖ وَٱلۡمَلَٰٓئِكَةُ وَهُمۡ لَا يَسۡتَكۡبِرُونَ
Na vinamsujudia Mwenyezi Mungu vyote vilivyomo katika mbingu na katika ardhi, miongoni mwa wanyama mpaka Malaika na wala havitakabari.
Tefsiri na arapskom jeziku:
يَخَافُونَ رَبَّهُم مِّن فَوۡقِهِمۡ وَيَفۡعَلُونَ مَا يُؤۡمَرُونَ۩
Vinamhofu Mola wao Mlezi aliye juu yao, na vinafanya vinavyoamrishwa.
Tefsiri na arapskom jeziku:
۞ وَقَالَ ٱللَّهُ لَا تَتَّخِذُوٓاْ إِلَٰهَيۡنِ ٱثۡنَيۡنِۖ إِنَّمَا هُوَ إِلَٰهٞ وَٰحِدٞ فَإِيَّٰيَ فَٱرۡهَبُونِ
Na Mwenyezi Mungu amesema: Msijifanyie miungu wawili! Hakika Yeye ndiye Mungu Mmoja tu. Basi niogopeni Mimi tu!
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَلَهُۥ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَلَهُ ٱلدِّينُ وَاصِبًاۚ أَفَغَيۡرَ ٱللَّهِ تَتَّقُونَ
Na ni vyake Yeye vilivyomo katika mbingu na ardhi. Na Dini ni yake Yeye daima. Je, mnamcha mwingine asiyekuwa Mwenyezi Mungu?
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَمَا بِكُم مِّن نِّعۡمَةٖ فَمِنَ ٱللَّهِۖ ثُمَّ إِذَا مَسَّكُمُ ٱلضُّرُّ فَإِلَيۡهِ تَجۡـَٔرُونَ
Na neema yoyote mliyo nayo inatoka kwa Mwenyezi Mungu. Kisha yakiwagusa madhara, mnamyayatikia Yeye.
Tefsiri na arapskom jeziku:
ثُمَّ إِذَا كَشَفَ ٱلضُّرَّ عَنكُمۡ إِذَا فَرِيقٞ مِّنكُم بِرَبِّهِمۡ يُشۡرِكُونَ
Na anapowaondoshea madhara hayo, mara kundi moja miongoni mwenu linamshirikisha Mola wao Mlezi.
Tefsiri na arapskom jeziku:
 
Prijevod značenja Sura: En-Nahl
Indeks sura Broj stranice
 
Prijevod značenja časnog Kur'ana - Prijevod na svahili jezik - Prevodilački centar Ruvvad - Sadržaj prijevodā

Prevod: Prevodilački centar Ruvvad u saradnji sa Udruženjem za poziv u Rabwi i Udruženjem za pružanje islamskog sadržaja na jezicima.

Zatvaranje