Check out the new design

Prijevod značenja časnog Kur'ana - Prijevod na svahili jezik - Prevodilački centar Ruvvad * - Sadržaj prijevodā


Prijevod značenja Sura: El-Furkan   Ajet:
وَمَآ أَرۡسَلۡنَٰكَ إِلَّا مُبَشِّرٗا وَنَذِيرٗا
Nasi hatukukutuma isipokuwa uwe Mbashiri na Mwonyaji.
Tefsiri na arapskom jeziku:
قُلۡ مَآ أَسۡـَٔلُكُمۡ عَلَيۡهِ مِنۡ أَجۡرٍ إِلَّا مَن شَآءَ أَن يَتَّخِذَ إِلَىٰ رَبِّهِۦ سَبِيلٗا
Sema: Sikuwaomba ujira wowote juu yake; isipokuwa atakaye na ashike njia iendayo kwa Mola wake Mlezi.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَتَوَكَّلۡ عَلَى ٱلۡحَيِّ ٱلَّذِي لَا يَمُوتُ وَسَبِّحۡ بِحَمۡدِهِۦۚ وَكَفَىٰ بِهِۦ بِذُنُوبِ عِبَادِهِۦ خَبِيرًا
Na mtegemee aliye Hai, ambaye hafi. Na umtakase kwa sifa zake. Naye anatosha kuwa ndiye Mwenye habari zote za dhambi za waja wake.
Tefsiri na arapskom jeziku:
ٱلَّذِي خَلَقَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ وَمَا بَيۡنَهُمَا فِي سِتَّةِ أَيَّامٖ ثُمَّ ٱسۡتَوَىٰ عَلَى ٱلۡعَرۡشِۖ ٱلرَّحۡمَٰنُ فَسۡـَٔلۡ بِهِۦ خَبِيرٗا
Ambaye aliziumba mbingu na ardhi, na vilivyo ndani yake kwa siku sita. Kisha akainuka juu ya 'Arshi, Arrahman (Mwingi wa rehema)! Uliza habari zake kwa wamjuaye.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَإِذَا قِيلَ لَهُمُ ٱسۡجُدُواْۤ لِلرَّحۡمَٰنِ قَالُواْ وَمَا ٱلرَّحۡمَٰنُ أَنَسۡجُدُ لِمَا تَأۡمُرُنَا وَزَادَهُمۡ نُفُورٗا۩
Na wanapoambiwa: Msujudieni Arrahman (Mwingi wa rehema!) Wao husema: Ni nani Arrahman (Mwingi wa rehema)? Je, tumsujudie unayetuamrisha wewe tu? Na huwazidishia kujitenga mbali.
Tefsiri na arapskom jeziku:
تَبَارَكَ ٱلَّذِي جَعَلَ فِي ٱلسَّمَآءِ بُرُوجٗا وَجَعَلَ فِيهَا سِرَٰجٗا وَقَمَرٗا مُّنِيرٗا
Ni Mwenye baraka nyingi yule aliyezijalia nyota mbinguni, na akajalia humo taa na mwezi unaong'ara.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَهُوَ ٱلَّذِي جَعَلَ ٱلَّيۡلَ وَٱلنَّهَارَ خِلۡفَةٗ لِّمَنۡ أَرَادَ أَن يَذَّكَّرَ أَوۡ أَرَادَ شُكُورٗا
Naye ndiye aliyefanya usiku na mchana kufuatana kwa nafuu ya yule anayetaka kukumbuka, au anayetaka kushukuru.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَعِبَادُ ٱلرَّحۡمَٰنِ ٱلَّذِينَ يَمۡشُونَ عَلَى ٱلۡأَرۡضِ هَوۡنٗا وَإِذَا خَاطَبَهُمُ ٱلۡجَٰهِلُونَ قَالُواْ سَلَٰمٗا
Na waja wa Arrahman (Mwingi wa rehema) ni wale wanaotembea ulimwenguni kwa staha, na wajinga wakiwasemeza, hujibu: Salama!
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَٱلَّذِينَ يَبِيتُونَ لِرَبِّهِمۡ سُجَّدٗا وَقِيَٰمٗا
Na wale wanaokesha kwa ajili ya Mola wao Mlezi kwa kusujudu na kusimama.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَٱلَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَا ٱصۡرِفۡ عَنَّا عَذَابَ جَهَنَّمَۖ إِنَّ عَذَابَهَا كَانَ غَرَامًا
Na wale wanaosema: Mola wetu Mlezi! Tuondolee adhabu ya Jahannamu. Hakika adhabu yake ikimpata mtu haimwachi.
Tefsiri na arapskom jeziku:
إِنَّهَا سَآءَتۡ مُسۡتَقَرّٗا وَمُقَامٗا
Hakika hiyo ni kituo na makao mabaya.
Tefsiri na arapskom jeziku:
وَٱلَّذِينَ إِذَآ أَنفَقُواْ لَمۡ يُسۡرِفُواْ وَلَمۡ يَقۡتُرُواْ وَكَانَ بَيۡنَ ذَٰلِكَ قَوَامٗا
Na wale ambao wanapotoa matumizi, hawatumii kwa fujo wala hawafanyi ubahili, bali wanakuwa katikati baina ya hayo.
Tefsiri na arapskom jeziku:
 
Prijevod značenja Sura: El-Furkan
Indeks sura Broj stranice
 
Prijevod značenja časnog Kur'ana - Prijevod na svahili jezik - Prevodilački centar Ruvvad - Sadržaj prijevodā

Prevod: Prevodilački centar Ruvvad u saradnji sa Udruženjem za poziv u Rabwi i Udruženjem za pružanje islamskog sadržaja na jezicima.

Zatvaranje